Uhalisia wa Vitu na Sayansi Baina ya Kuthibitisha na Kukanusha
Question
Kuna Watu wengi wanaoukanusha uhalisia wa Vitu na Sayansi au wanajadili ili kuthibitisha. Je, Ni upi msimamo wa fikra za Kiislamu katika Suala Hili?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Katika Misingi ambayo Ahlu Sunna (Watu wa Sunna) wamekubaliana juu ya Kanuni zake, na wakawakosoa wale waliowapinga, ni suala la kuthibitisha uhalisia na Sayansi. hakika Ahlu Sunna wamekubaliana katika kuthibitisha Sayansi na maana zilizopo za Wanachuoni, na wakawakosoa wale wote wanaokanusha Sayansi na dalili zake zote. Na miongoni mwao ni kundi la Sophistis ambalo lilikanusha Sayansi na uhalisia wa mambo yote, na vilevile kundi lingine la wale ambao walitilia shaka uwepo wa Uhalisia, na pia wale ambao wanaona kwamba Uhalisia wa vitu uko chini ya imani, na wakasahihisha imani zote licha ya kutofautiana na kupingana kati yao.
Ahlu Sunna wanaona kwamba Watu wa Rai hizi tatu wako makosani na wanapinga mambo ya yaliyo wajibu kiakili. Na Ahlu Sunna Waljamaa wanaona kwamba Sayansi za Watu ziko aina tatu: Sayansi ya Kimaumbile, Sayansi ya Kihisia , na Sayansi kwa njia ya kusaka dalili, na kwa hivyo kila mwenye kuzipinga Sayansi za Kimaumbile na Kihisia zinazotokana na viungo vitano vya Hisia, au akakana Sayansi za Kinadharia zitokanazo na kutizama na usakaji wa dalili, basi huyo ni mkaidi tu. Na hakika mfano wa Kauli hizo zinaweza kumpelekea msemaji wake katika kuamini Ukale wa Ulimwengu na kumkana Muumba au kuzikana Dini zote.
Na Wanachuoni wa Ahlu Sunna Waljamaa wanasisitizia umuhimu wa kutumia Hisia tano na yanayopatikana kutokana nazo, na viungo vyake navyo ni Macho kwa ajili ya kuviona vitu vinavyoonekana, Masikio kwa ajili ya kusikilizia vinavyosikika, na Ulimi kwa ajili ya kuonjea ladha kwa vinavyoonjeka ambavyo vinalika, na Pua kwa ajili ya kunusia vinavyonusika, na Hisia ya kugusa ili kuhisi vinavyogusika kama vile Joto, Baridi, Unyevunyevu, Ukavu, Ulaini, Ugumu na kadhalika. Kwa hiyo vyote vinavyohisika kupitia viungo hivyo vina maana ya viungo vinavyoitwa Hisia hivyo, na kwa kuvitumia hivyo viungo vya mwili, Kundi la Jabaai katika Muutazila limepotosha lilipoona ya kwamba kudiriki kitu sio onesho, na hakuna maana na kwamba si chochote isipokuwa kinachodirikiwa.
Na kwa upande mwingine hakika Ahlu Sunna wanazichukua Hadithi hizi, na wanaziona kwamba Hadithi Mutawaatir ni njia ya kuelekea kwenye elimu ya Msingi kwa kusihi Mapokezi yake kama vile kujua kwetu Mitume, na wameweka masharti katika Hadithi za Aahaad kusihi kwa Isnadi yake na Matini zake zisiwe haziwezekani kiakili, na kwa hivyo huwajibisha kuzifanyia kazi bila ya kuzijua, na huwa katika daraja ya Ushahidi wa Waadilifu mbele ya Kiongozi, katika kuwajibisha kwake kwa Uwazi wake, hata kama ukweli unaofichwa haukuonekana. Na kwazo, Wanachuoni wa Fiqhi wamethibitisha Matawi mengi ya Hukumu mbalimbali za Kisheria katika Ibada, Miamala, na vilevile milango mingine ya Halali na Haramu. Na baina ya Hadithi zenye mapokezi yenye Mlolongo Wa Wapokezi na yale ya Mpokezi ya mmoja mmoja kuna kiwango cha kati ambacho ni Hadithi Mustafiidhu, nayo inashirikiana na Mutawaatir katika kuwajibisha Kujua na Kufanyia kazi, lakini Hadithi ya aina hiyo inatofautiana nayo kwa upande wa kwamba Elimu yake Halisi inakuwa ni yenye kupatikana kwa kuitafuta Kinadharia wakati ambapo Elimu itokanayo na Mutawaatir inakuwa ni ya lazima isiyochomoka Kinadharia.
Na Hadithi Mustafiidhu ziko aina mbalimbali:
Miongoni mwake ni habari za Mitume ndani ya nafsi zao, na pia maelezo ya aliyemwambia Mtume S.A.W, kwa ukweli wake, na miongoni mwake ni Maelezo yaliyoenea kwa baadhi ya Watu, yanapotolewa kwa kuwepo watu wengi haijuzu kwa watu hao kuhusishwa na uongo na wakadaiwa kutokea kwa yale aliyoyasema kwa kuwepo kwao, na ikiwa hakuna yeyote miongoni mwao aliyeyakanusha basi itakuwa imejulikana ukweli wake.
Na katika Kitengo hiki tumejua Muujiza wa Mtume Wetu S.A.W, katika Tasbihi ya vijiwe katika mkono wake, na kuwashibisha Watu wengi kwa chakula kidogo, na miujiza mingine mingi ambayo elimu imefahamisha, isipokuwa Qur`ani Tukufu ni Muujiza Mkubwa wa Uislamu kwani Muujiza huu umethibiti kwa Mfululizo wa Mapokezi ya wengi ambao ni lazima kuamini.
Na miongoni mwa Hadithi Mustafiidh: ni Hadithi Mustafiidh zilizo baina ya Maimamu wakubwa wa Hadithi na Fiqhi ambao walikubaliana kusihi kwake, mfano wa Hadithi ya kuthibitisha Maombezi ya Mtume S.A.W, na Hadithi za kuja kwa Mahdi, na Masihi Dajali, na Hadithi za Adhabu ya Kaburini, Kuhesabiwa, Mto wa Haudhi, Mizani, na Kumwona Mwenyezi Mungu Mtukufu na mfano wa hayo miongoni mwa mambo ya Akhera.
Na katika Hadithi Mustafiidh: Hadithi Mustafiidh katika Hukumu nyingi za Kifiqhi kama vile Kiwango cha Zaka na Kufuta juu ya Khofu mbili na Adhabu ya Kunywa pombe, na Kumpiga mtu Mawe, na Kuritadi, na mfano wa hizo ambazo Wanachuoni wa Fiqhi walikubaliana kuzichukua Hadithi zake na kuzifanyia kazi ipasavyo, na kwa ajili hiyo, Ahlu Sunna wamethibitisha Uwepo wa kosa kubwa lililotokea kwa wale waliozikana Hadithi Mustafiidh.
Na katika waliyokubaliana Ahlu Sunna katika Mlango huu ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amewakalifisha waja wake wamjue na akawaamrisha jambo hili, na kwamba Yeye amewaamrisha Kumjua Mtume wake na Kitabu chake, na Kuyafanyia kazi yaliyomo kwenye Kitabu na katika Sunna miongoni mwa dalili mbalimbali, na kwa hivyo wao wamemkana yule anayeona kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hakumkalifisha Mtu yeyote Kumjua Yeye kama yaonavyo baadhi ya Makundi, kama ilivyo kwa baadhi ya Kadariyya na Raafidhwa.
Na Ahlu Sunna Wote wamekubaliana kwamba kila elimu ni faida ya Kinadharia, inajuzu Mwenyezi Mungu Mtukufu atujaalie tulazimike kidharura kuijua vilivyo, kinyume na wale Wanaodhani miongoni mwa Muutazila kwamba Kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyetukuka katika Akhera yanapatikana kwa kujifunza bila ya kulazimika kumjua Yeye.
Na Ahlu Sunna wote kwa pamoja wanaona kwamba Misingi ya Hukumu ya Sheria ya Kiislamu ni: Qur`ani Tukufu, Sunna za Mtume S.A.W, na Ijmai ya Umma, na Ahlu Sunna wamemkana vikali kila mwenye kwenda kinyume na kutumika kwa Hoja ya Sunna Tukufu au Kutumika kwa Hoja ya Ijmai.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Rejeo: Profesa: Abdulrahmaan Al Abd, Masomo katika Fikra za Kiislamu, Maktabat Al Anglu Al Masriyah, Kairo, 1977, Ku. 22-24