Utamaduni wa Kupiga Makelele na Uta...

Egypt's Dar Al-Ifta

Utamaduni wa Kupiga Makelele na Utamaduni wa Kuzingatia.

Question

 Nini kusudio la Utamaduni wa kupiga makelele na Utamaduni wa kuzingatia? Na athari zake katika mawazo ya Muislamu wa Kisasa?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Sisi kwanza kabisa tuko pamoja na Utamaduni wa Kuzingatia na tuko dhidi ya Utamaduni wa Kupiga Makelele, kwani Utamaduni wa Kupiga Makelele hujenga Akili tete isioweza kufikiri, na kwa kawaida uchangamfu hutangulia kufikiri. Na kutangulia uchangamfu mbele ya kufikiri ni moja ya alama Kuu katika kuathiri Staarabu, Sanaa, mafunzo na Maisha. Na Abdulrahman Yahaya (ambaye anaitwa Reneh Jinu kabla ya kusilimu) katika kitabu chake kutokana na Ustaarabu wa kisasa, ni moja ya alama ambazo zimemwua binadamu mbele ya nafsi yake, ama dalili ya hayo katika Qur'ani Tukufu na Sunna ya Mtume S.A.W. tutataja katika yafuatayo:
1- Mwenyezi Mungu Mtukufu anasimulia hali ya Iblisi ambaye ni sura ya shari na uovu na anasema: {Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali na wana, na waahidi. Na Shet'ani hawapi ahadi ila ya udanganyifu} [Al-ISRAA 64]. Njia za Ibilisi huanza kwa Sauti ya kelele kisha kelele hupata nguvu nayo ni katika kukusanya, kisha kelele hupata nguvu tena kwa kushirikiana mpaka kelele ikawa sehemu ya maisha yetu ya kila siku, nayo ni hali inayopoteza sehemu kubwa ya kufikiri, kuzingatia na kuweka akilini, na hupoteza sehemu kubwa ya raha na Utulivu wa moyo.
Kama hizi ni miongoni mwa njia za Ibilisi – sura ya Shari ya Uovu – basi hakika huo ni ukweli wa mambo, na huo ni mfumo wa kushawishi kwenda kinyume na Haki. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika haki ya Washirikina: {Na walio kufuru walisema: Msiisikilize Qur'ani hii, na timueni zogo, huenda mkashinda [FUSSILAT 26]. kuzuia usikivu wa Qur`ani inayotuamrisha kuzingatia na kufikiri na kutia akilini, na kufanya mambo ya Kipuuzi mbele yake, na kunyanyua Sauti inaposomwa Qur`ani Tukufu – inadhihirisha tofauti baina ya tamaduni mbili. Mwenyezi Mungu Mtukufu anaesma: {Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi}. [AN NISAA 82] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Je! Hawaizingatii hii Qur'ani? Au kwenye nyoyo zao zipo kufuli?} [MOHAMMAD 24}, Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili}. [SWAAD 29]
Halafu Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika kusifu kwake kwa hali ya waumini wenye kusadikika: {Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure, Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto}, [AAL IMRAAN 191]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amejaalia kusikia na kusikilizia Qur'ani ni sehemu kutoka ulingano mwema.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Wamenunua thamani ndogo kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakazuilia watu na Njia yake. Hakika hao ni maovu waliyo kuwa wakiyatenda} [ATAWBAH 9]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Basi Shetani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu hakukukatazeni mti huu ila msije mkawa Malaika, au msije mkawa katika wanao ishi milele} [AL AARAF 20].
2- Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu anakujaalia kunyanyua Sauti na kupiga kelele kuwa nje ya mipaka ya adabu kwa watu wote Qur’ani inazungumzia nyasia za Luqmani kwa Mwanaye huku akimpa mawaidha: {Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda} [ LUQMAAN 19].
Na Adabu hii inageuka na kuwa mafunzo makuu yanayokusanywa kuangalia na kuwatendea wema watu wote, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!. Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipo kuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo} [AT TAWBAH 30-31].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni} [AL ISRAA 24]. Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Usivitumbulie macho yako vitu tulivyo waneemesha makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini} [AL HIJR 88]. Halafu inageuka kwa mpango wa maisha, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea} [AAL IMRAAN 159].
3- Na inawaamrisha katika Umaalumu wa Mtume S.A.W. kutopigia Makelele. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Kwa hakika wanao teremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa uchamngu. Hao watakuwa na maghfira na ujira mkubwa (3). Hakika hao wanao kuita nawe uko nyuma ya vyumba,wengi wao hawana akili (4). Na lau wao wangeli ngojea mpaka uwatokee ingelikuwa kheri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira,Mwenye kurehemu(5)} [AL HUJURAAT 3-5].
4- Na Tamaduni mbili zilisambaa kwa Swala, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na haikuwa ibada yao kwenye hiyo Nyumba (Al Kaaba) ila ni kupiga miunzi na makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru} [AL NFAAL 35]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, nasimameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea)} [AL BAQARAH 238].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:{Sema: Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Wala usitangaze Sala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati ya hizo} [AL ISRAA 110]. Na Mtume S.A.W. aliwaambia Maswahaba wake waliponyanyua Sauti zao kwa Dua: “Jisikilizesheni nyinyi wenyewe, kwani hakika mnaemwomba sio kiziwi wala asiyekuwepo, hakika mambo yalivyo, mnamwomba Msikivu na Mwenye kuona.
5- Na Mtume S.A.W. alipenda sauti nzuri, kwa hiyo alimwamuru Bilal atoe Adhana, na akamwambia Abdullahi Bin Zaid, aliyekuwa akiona njozi ya Adhana alisema: " Alipoamrisha kupulizwa pembe atakayoitumia kwa ajili ya Watu ili wakusanyike kwa ajili ya Swala, mtu mmoja alipitia kwangu nikiwa nimelala na alikuwa amebeba pembe mkononi mwake nikasema: Ewe Mja wa Mwenyezi Mungu, unauza mapembe? Akasema: unataka kufanyia nini? Nikasema: tunawaitia watu Wakasali. Akasema: Je nikuelekeze jambo zuri zaidi kuliko ya hilo? Nikasema: Ndio. Akasema: Unasema: Allaahu Akbar, akayasema maneno hayo mara nne bila ya kurejea rejea. Akasema: kisha akasogea mbali kiasi na akasema: Utasema pindi utakaposimama kwa ajili ya Swala: akaitaja Iqaama pekee mara moja moja kisha akakariri mara mbili Qad qaamat Swalaatu. Nilipoamka nikamwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, na nikamweleza nilichokiona, na akasema: Hakika hiyo ni ndoto ya Kweli inshaallah basi nyanyuka wewe na Bilali na umsomee hayo, uliyoyaona na kisha atoe Adhana kwa maneno hayo kwani hakika yeye ana sauti kali zaidi yako, basi nilisimama pamoja na Bilal, ninasoma na yeye anatoa adhana. Akasema: Omar Bin Al Khatwaab akasikiliza adhana naye katika nyumba yake, basi akatoka kuvuta kanzu yake na akisema; Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, naapa kwa Mola wako aliyekutuma kwa haki, mimi nimeona ndoto kama hiyo basi akasema: Namshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na Abu Mahdhura alimchukua muadhini katika Makka, naye ni Aus Bin Maier Bin Ludhaan Bin Rabiah Bin Saad Bin Jomah, na inasemakana kuwa jina lake ni Samir Bin Omair Bin Ludhaan Bin Wahb Bin Saad Bin Jomah, na mama yake kutoka Khuzaah, Adhahabiy anasema juu yake: " Alikuwa na Sauti kali na nzuri kuliko watu Wote. Na kilipokelewa Kisa cha Adhana yake kutoka kwake na Majaribio ya Mtume S.A.W, ya Sauti za Watu mbalimbali ambapo alisema: Mtume aliporejea kutoka Hunaini, nilitoka pamoja na watu tisa kutoka Makkah tunawataka, nikawasikia wakiadhini kwa ajili ya Swala, nasi tukasimama huku tukiadhini kama tunafanya mchezo. Mtume S.A.W, akasema: Nimesikia kwa hakika katika hao Adhana ya mtu mwenye Sauti nzuri. Akatuita kisha akawa anaadhini mmoja mmoja na mimi nilikuwa wa mwisho wao. Na akasema pindi nilipoadhini: Njoo hapa! Basi akanikaza baina ya mikono yake, na akapungusa uso wangu, na akaomba Baraka mara tatu, kisha akasema: Nenda na uadhine kwanye Nyumba ya Haramu".
Na Mtume S.A.W., alikuwa akisema: "Mtu yeyote atakayependezwa na Usomaji wa Qur'ani Tukufu kama ilivyoteremshwa basi aisome mbele ya Ibnu Ummi Abd". Na alimwambia Hassani Bin Thaabit pindi alipoyasikia Mashairi yake yanayounusuru Uislamu: Hakika Roho mtakatifu yuko pamoja nawe.
Na akasikia Kaab Bin Zohair katika shairi lake ambalo alilianzishia kwa kauli yake:
Suadu amebayana na moyo wangu leo umezubaa,
Nimekuwa baada ya hilo kama mateka mfungwa asiye na cha kumkombolea.
Na hakuwa Suadu, asubuhi na mapema walipoondoka
Kama Paa na sauti nzuri, huku ncha za macho yake zikiwa na wanja
Je, mpaka hapa tulipo, tuna sisi Usaili Wetu mpaka tukahukumumia hali yetu ya Kitamaduni ili tuone upande wowote tunaouelemea au tunataka tuwe, tuelekee upande wa utamaduni wa kupiga makelele? Au tuelekee upande wa utamaduni wa Kuzingatia akilini? Na je, inafaa tujenge kigezo kinachotokana na haya yote kwa ajili ya Uchanganuzi wa kifasihi na kiufundi hututoa katika upotevu au hutupeleka sisi katika Eneo la usalama?
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Rejeo ni: Kitabu cha; [Semaatu Al Aswer, kwa mheshimiwa mkuu Mufti wa Misri Sheikh Al Jumaa.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas