Kutumia Jina la Familia ya Mlezi kw...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutumia Jina la Familia ya Mlezi kwa Asiyefahamika Kizazi chake

Question

 Je, kwa upande wa Sheria inafaa kwa mlezi wa mtoto yatima au asiyefahamika kizazi chake kupewa jina la famili ya mlezi wake?

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, Sala na salamu zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W. pamoja na Watu wake Masahaba zake na wale wenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Kiyama, na baada ya utangulizi:
Kwa upande wa Sheria inafaa kwa mlezi wa mtoto yatima au asiyefahamika kizazi chake kupewa jina la famili ya mlezi wake, ni sawa katika hilo mlezi akiwa ni mwanamume au mwanamke huongezwa katika jina la mwisho kwa maana ya jina la mwisho la mtoto yatima jina la familia ya mlezi, ambapo mwisho anakuwa ni sehemu ya familia hiyo bila kuchafua au kugushi kuwa ni mtoto wake au binti yake wa damu, ili asijeingia kwenye wigo wa mtoto wa kuzaa jambo lililo haramu Kisheria, bali uongezaji huo wa jina la mwisho la mtoto yatima au asiyefahamika kizazi chake ni kama mfano wa usimamizi ambao ulikuwepo hapo zamani kati ya makabila ya Kiarabu, katika hilo hakuna chochote katika ubini ulio haramu katika Sheria, kwani ubini: Ni kumuongeza mtoto mwingine, na kumuingiza sehemu ya mtoto wake katika mirathi na nasaba na kukaa pamoja na watoto wa kike wa familia yake kwa kuwa ni maharimu yao, na yasiyokuwa hayo miongoni mwa yale yaliyokuwa yameenea sana katika zama za ujinga na wakati wa mwanzo wa Uislamu kisha Uislamu ukaharamisha hilo ikiwa ni kuchunga kutochanganya nasaba.
Ama kunasibika kwa mlezi jambo hilo halina athari yoyote katika athari za ubini ulio haramu Kisheria, bali hilo ni mfano wa yale yaliyokuwa yanatokea kwa Wanachuoni na wasimulizi wanaonasibishwa kwa wasiokuwa kabila lao, kwani ulitumika unasaba kila mmoja miongoni mwao kwa kiwango ambacho mtu anadhani kwa aliyenasibishiwa naye ni mtoto wa kuzaliwa naye, kwa maana miongoni mwa mtoto wa damu.
Unasaba unapotoka kuwa si asili ya mtu basi hilo linakuwa ima:
1- Kuacha huru mtumwa na hiyo ndio mara nyingi sana, mfano: Baba Bakhtariy Twaiy, jina lake ni Saidi Ibn Feiruzi, ni bwana wa Twaiy, kwa sababu bwana wake ni kutoka Twaiy kisha akamuacha huru.
2- Kiapo cha uaminifu ambacho asili yake ni makubaliano ya kusaidia mfano: Imamu Maliki Ibn Anas As’bahiy Taimiy, jina la As’bahiy ni asili na jina la Taimiy la kiapo cha uaminifu, na hilo ni kwa sababu watu wake ni “As’buh” waaminifu kwa Taim Kuraishi kwa kiapo.
Uislamu uliondoa usimamizi wa kiapo cha uaminifu kutokana na yaliyokuwepo wakati wa zama za ujinga ikiwa ni pamoja na fitina na mauaji kati ya makabila au mashambulizi pasina kuzuia dhuluma wala kuunganisha undugu.
3- Uaminifu wa urafiki kwa ufanyaji kazi au mafunzo mfano: Miqsam aliyetajwa ni mtumwa wa Ibn Abbas kwa kuwa naye kwake karibu, au kama vile Malik Ibn Anas pia kwani ilisemwa: Amenasibishwa na Taim kwa kuwa ni babu yake Malik Ibn Abi Aamir alikuwa ni mfanya kazi wa Talhah Ibn Ubaidillah pale Talhah alipotofautiana katika biashara.
4- Kunyonya, kama vile Abdillah Ibn Saady Sahabiy, An-Nawawy amesema katika kutumia majina mazuri na lugha: “Ameitwa kwa jina la baba yake Saady kwa sababu alinyonya upande wa Ibn Saad Bany Bakr”( ).
5- Uaminifu wa dini na Uislamu mfano: Muhammad Ibn Ismail Al-Bukhari Al-Juufy, kwa sabau babu yake Mughirah alikuwa ni majusi akasilimu kupitia Al-yaman Ibn Akhnas Al-Jufy na kunasibishwa kwake.
6- Ofisi kuu, kwa maana ya jina lake limeandikwa kwenye moja ya Ofisi na kunasibishwa na watu wa hiyo Ofisi, kama vile Laith Ibn Said Ibn Abdulrahman Al-Fahmy, akanasibishwa na Al-Fahmy kwa sababu jina lake limo kwenye taasisi ya fedha chini ya Kinanah Ibn Fahmi, na watu wa nyumbani kwake wanasema: Sisi ni wa Fursi ni katika watu wa As’bahan, kwa maana asili yake ni kutoka As’bahan lakini amenasibishwa na Fahmi kwa sababu jina lake limo kwenye ofisi ya Fahmi( ).
Huenda unasaba ukapanuka zaidi ambapo hunasibishwa kwenye kabila au ukoo yule mwenye kuwa mtumwa wa ukoo mfano wa: Saidi Ibn Yasaar Abil-Habab Al-Hashimiy, kwa kuwa kwake mtumwa wa Shaqran mtumishi wa Mtume S.A.W. hivyo akanasibishwa na ukoo wa Baniy Hashim( ).
Kwa upande wa kinyume na asili kwenye mifano iliyopita haiendani na makatazo ya Kisheria ambayo yamo kwenye ubini, vilevile hali kwa upande wa mtoto kwa mlezi wake, kwa sababu makusudio kwenye huu unasaba ni ibara tu ya kuongeza jina na wala si ukweli halisi.
Na upande wa mtoto kwa mlezi wake hufikiwa masilahi mengi kwa mtoto, kwani hilo huongeza kwenye maisha ya mtoto hali ya utulivu na matumaini, kwani anapata haki sawa na haki za watoto wa Kisheria, anakuwa na baba pamoja na mama mbele za watu katika hatua mbalimbali za makuzi yake na hata wakati wa kuoa kwake, hilo pamoja na kulinda hukumu za Kisheria za uharamu wa ubini na yanayoendana na hayo miongoni mwa athari za Kisheria.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

 

Share this:

Related Fatwas