Maadili kwa Wanafikra wa Kiislamu - Mtazamo wa Kihistoria
Question
Je, wanafikra wa Kiislamu wanajali kwa kiasi gani kipengele cha maadili?
Answer
Sifa zote njema ni za Allah pekee, na swala na salaam ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya jamaa zake na maswahaba zake, na juu ya wale wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
1) Ni kwamba maadili yalikuwa na yanaendelea kuwa suala muhimu kwa Waislamu kwa kila aina ya sayansi na utaalamu, na hii inaoneshwa - kama anavyosema Prof. Dk. Abdel Hamid Madkour, Profesa na Mkuu wa zamani wa Idara ya Falsafa ya Kiislamu katika Kitivo cha Dar Al Uloom- kwamba kuna umuhimu mkubwa wa maadili katika tanzu mbalimbali za utamaduni wa Kiarabu na Kiislamu, na hili lilidhihirika katika vitabu vya fasihi, katika mashairi ya washairi, na mifano ya waandishi, kama ilivyokuwa dhahiri kwa wanahistoria na wasimulizi wa habari ambao walikuwa wakizungumzia maadili kila inapojitokeza haja ya kufanya hivyo, na hili pia lilionekana katika vitabu vya baadhi ya Masufi ambao walitilia maanani kipengele hiki kwa uwazi kabisa, kama vile, Al-Harith Al-Muhasabiy na Al-Hakim Al-Tirmidhiy.
2) Wanazuoni wa Fiqhi pia walishughulikia maadili, kwani utungaji wa sheria, kama Ibn Rushd anavyosema, unahitaji wema wa kiutendaji. Imam Malik, akiwa kama mmoja wa Wanazuoni wa Fiqhi, aliweza kutatua matatizo kadhaa ya kimaadili kwa kutumia mojawapo ya vyanzo vya kisheria vilivyotumiwa na baadhi ya Wanazuoni wa Fiqhi katika Misingi ya Fiqhi, ambayo ndiyo ni Msingi wa “Maslahi yanayokusudiwa katika Sheria.”
3) Pia miongoni mwa Misingi ya Kifiqhi na ya Kisheria ambayo ilitegemewa na Wanazuoni wa Fiqhi ni (hakuna madhara wala kudhuru), na ni Msingi unaojulikana sana katika Sheria, ambao unakusudiwa kutilia maanani kipengele cha maadili katika kutangamana na wengine, ili tu isiwaletee madhara, na hii inatumika katika misingi mingine, kama msingi wa (Mambo yote yanazingatiwa kwa makusudio yake), ambao unahusika na kuzungumzia nia, ambayo ni kiini cha kitendo cha maadili, na msingi wa (madhara yanaendelea kuwa ni madhara). Walichoshughulikia pia ni: Mada ya kulazimishwa, ambayo inahusiana sana na utashi, ambao ni moja ya vipengele vya vitendo vya kimaadili.
4) Miongoni mwa mambo yanayodhihirisha hamu ya wanachuoni wa Sheria katika maadili ni kuafikiana kwa umma juu ya kukataza hila ambazo baadhi ya watu huzifuata ili wasitekeleze baadhi ya faradhi za kisheria, kwa sababu ya uovu unaotokana na kuzifuata hila hizo.
5) Pia inadhihirika kuwa wanazuoni wa Hadithi Tukufu wanashughulikia maadili, kwani Hadithi Tukufu ni rekodi ya maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., vitendo vyake, riwaya zake na sifa zake, naye Mtume S.A.W., ndiye kigezo chema, kwani yeye ni mwenye kufikisha uwongofu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana} [AL AHZAAB: 21]. Ndio maana tunapata Hadithi nyingi zinazozungumzia kipengele cha kimaadili katika Sunnah. Kwa mfano, tunapata majina kama vile Kitabu cha Wema, Kitabu cha Adabu, na Al-Raqaq. Wanazuoni Wengi pia waliandika vitabu vinavyojitegemea vinavyohusu kipengele cha kimaadili katika Sunnah kama vile Adabu ya pekee ya Al-Bukhariy, na vitabu mbalimbali vya kuupa nyongo Ulimwengu, vile vile tumekuta kwamba baadhi yao walilitunza sana suala hilo, kama vile, Ibn. Abi Al-Dunia katika Risala zake, Al-Kharaitiy, Abu Abd Al-Rahman Al-Sulamiy, Abu Bakr Al-Ajriy na wengine miongoni mwa Wanaohifadhi Hadithi ambao walishughulikia kuelezea kipengele cha maadili katika Sunnah tukufu. Pia umuhimu wa maadili ulionekana katika vitabu vya Insaiklopidia ambavyo vinajumuisha mada mbalimbali katika fasihi, siasa na historia, kama vile kitabu cha Ibn Qutayba [Uyun Al-Akhbar], ambacho kilibainisha sehemu katika kitabu chake kiitwacho “Kitabu cha Tabia na Tabia zinazokemewa.”
6) Mwenendo huu wa jumla hujali maadili kama wanavyuoni wa Kiislamu wanavyoyashughulikia Maadili ambayo yanapasa kusifiwa na wanachuoni na watu wa hadhi katika jamii bila ya kujali utaalamu wao na nyadhifa zao. Haya ni pamoja na yale yaliyoyaandikwa na Abu Bakr Al-Ajriy juu ya maadili ya wanachuoni, Al-Mawardii kuhusu ushauri wa wafalme, na yale yaliyoandikwa na wengine juu ya Adabu ya Kadhi, Al-Khatib Al-Bughdadii juu ya Mwanazuoni wa Fiqhi, na Maadili ya Msimuaji na Adabu za Msikilizaji, Al-Nawawiy juu ya Adabu ya wanaohifadhi Qur’ani, Adabu ya Mufti na Mtoa Fatwa, Ibn Qutayba juu ya Adabu ya Mwandishi, na yaliyoyaandikwa na Al-Qalqashandiy kuhusu hili katika Subh Al-Asha, na Abu Bakr Ar-Razi, mwanafalsafa, alitoa kitabu chake cha At-Tib Ar-Rawhaniy na baadhi ya barua zake kuzungumzia Maadili.
7) Inaweza kusemwa kuwa kuzungumzia maadili ya wanachuoni kumekuwa ni mila na desturi inayofuatwa na wanazuoni wa Kiislamu ambao hutenga vitabu au sura zinazojitegemea katika vitabu vyao kabla ya kuzungumzia masuala ya elimu, na kupendezwa huku na Maadili ni moja wapo ya mambo yaliyoingia kwenye nyanja zingine za Utamaduni wa Kiislamu, ambayo ilikuwa ikikamilishwa polepole tangu mwanzo wa harakati za Uandishi, kisha hatua hii ilifuatiwa na harakati ya Utunzi na Tafsiri kutoka katika lugha zingine kwenda katika lugha ya Kiarabu, na Waislamu hawakuona ubaya wowote wa kuzihamishia Elimu mbalimbali kwenye lugha yao kwa kuona kuwa hakuna ukiukaji wowote wa msemo walio nao wa Maadili ya Kidini.
8) Zaidi ya hayo, tutakuta mielekeo iliyo wazi ya kimaadili miongoni mwa wanachuoni, wakiwa ni watu wa Sunni kama vile Ash'ariyah au wengineo kama vile Muutazila, pia tutapata nia ya wazi ya kimaadili miongoni mwa Masufi wa Kiislamu, na miongoni mwa Wanafalsafa wa Kiislamu, ingawa hawa wa mwisho (Wanafalsafa wa Kiislamu) wanachukuliwa kuwa ni upanuzi na Mwendelezo wa urithi wa Falsafa na Maadili ya Kigiriki, lakini kazi zao hazikuwa bila nyongeza ambazo waliziongeza kwenye fikira za kimaadili za Kigiriki zilizowafikia, kwa mfano, Al-Farabiy alipoandika kuhusu maadili wakati fulani anakubaliana na Plato, na wakati mwingine anaafikiana na Aristotle, na mara ya nyingine anaelekea wazi wazi katika kuupa nyongo Ulimwengu katika mawazo yake ya kimaadili.
9) Kuhusu Masufi wa Kiislamu, tutakuta kwamba nao walikuwa na nadharia zilizo wazi za kimaadili, katika uwanja huu wametoa jambo muhimu zaidi ambalo Waislamu waliliwasilisha. Inawezekana kuona mwelekeo wa wazi wa kimaadili miongoni mwa wale walioufafanua Usufi kuwa ni “Tabia njema, kwa hiyo yeyote anayekuzidishia tabia njema atakuzidishia usafi.” Inaweza kusemwa kwamba kushughulikia Masufi kwa maadili kulikuwa ni kwa kina kwa kila kipengele cha Usufi, hali ambayo ni maarufu katika hatua zake. Kwa hiyo, ilikuwa ni lazima kusifiwa kwa sifa ile maadili ya kimungu, ambayo yanawakilishwa katika majina mazuri ya Mwenyezi Mungu, na ambayo watu wanapaswa kuyakubali au kuyahusianisha nayo kulingana na kila jina miongoni mwa majina hayo. Hivyo, wakafanya kuiga tabia ya Mtume S.A.W. ni lengo lao, kwa sababu Mtume S.W.A., ndiye mfano wa juu kabisa wa ukamilifu wa kibinadamu.
10) Kupitia mazungumzo ya Masufi kuhusu kupambana na nafsi inadhihirika kwamba wao wanashughulikia sana na maadili ambayo ni uti wa mgongo wa maisha ya kisufi na msingi wa ujenzi wake. Mapambano haya yanahitaji kupinga matamanio ya nafsi na kuyakabili matamanio yake, ili yasiwe pazia baina ya mja na Mola wake, na hapana shaka kuwa mapambano haya yanajumuisha malengo ya wazi ya kimaadili, kwa sababu yanataka kuiondoa nafsi maovu ya maadili na kisha kusifiwa kwa maadili mema badala ya maadili mabaya yaliyowaondoa, na Masufi wanaeleza mambo mawili hayo kwa kujinyima na kujipamba, na kwa kujinyima maana yake ni kuacha tabia mbaya, na kujipamba tabia njema.
11) Mwenendo wa wazi wa kimaadili wa Masufi pia unadhihirika katika mazungumzo yao kuhusu maqamat, ambalo ni elimu ya maadili ya Kisufi, na Masufi wameona jukumu lao muhimu katika kuboresha maadili ya mwanadamu, ili katika kila kituo kinachopatikana anaondoshwa na maovu mengi. Yeyote anayejipamba kwa kujinyima moyo ataondokana na kuipenda dunia na kuitamani, na yeyote anayejipamba kwa kumtegemea Allah ataondokana na wasiwasi na kukosa kumtegemea Mwenyezi Mungu, na yeyote anayejipamba kwa kumcha Mungu ataondoa uvivu na kughafilika katika utiifu na kutenda madhambi mbalimbali. Kwa hivyo, maqamat ni njia ya kumtambulisha mtu kwa maadili mengi ambayo yametokana na maadili ya Sheria.
12) Iwapo tuliyoyawasilisha hadi sasa yanazingatia nafsi katika uhusiano wake na Mungu, basi Masufi nao wanachunga maadili wanayopaswa kuyapata katika uhusiano wao na watu wengine katika jamii Masufi walizingira maisha yao katika jamii kwa uzio wa maadili yenye hadhi ya hali ya juu. Sufi wa kweli anaishi katika maisha na moyo usiojua ubaya wala uadui. Ni mwenye moyo mzuri kwa Waislamu wote. Kwa hiyo, wao hawaathiriwi na shari kwa upande wake wa Sufi, kwani yeye habishani nao katika mambo yanayowahughulisha, na ikiwa Sufi wa kweli hatamuudhi mtu, basi hatosheki na hilo, bali zaidi ya hayo anavumilia madhara ya wengine, na anasamehe hali ya kuwa uwezo wa kulipiza kisasi, na ni bora kuliko misukumo yake mwenyewe, na kwa hiyo ilikuwa ni kawaida kwa Sufi kuwa chemchemi ya usalama na mahali pa amani katikati ya jamii. Usufi ulitoa mifano ya ubinafsi ambao ulifunua urafiki wa dhati na upendo safi, pamoja na kufunua roho na dhamiri iliyo macho na hai. Hivyo, maisha ya kweli ya Usufi yanachanganyika na maadili katika hatua zake zote, na katika nyanja zake zote.
13) Sifa ya maadili ya Kiislamu ambayo Masufi wa Kiislamu walituletea ni kwamba si fadhila za kubahatisha za kinadharia kama zile zinazotolewa na wanafalsafa, bali ni maadili ya kivitendo ambayo yanaweza kutumika. Kwa hivyo, ni wazi kutokana na mazungumzo ya Masufi kuhusu maadili kwamba wanaamini katika uwezekano wa kubadili maadili na kuyapata, na kama si hivyo, kujitahidi kusingekuwa na maana yoyote.
14) Masufi wa Kiislamu walizingatia sana nia, kwani nia ndio asili na roho ya kitendo cha maadili, na shauku yao katika nia huanzia mwanzo wa kitendo, kwani wanamtaka mtu achunguze nia yake daima. Kupendezwa kwao na nia kunatokana na ukweli kwamba kuna vitendo vya karibu ambavyo nia pekee ndiyo hutofautisha baina yake, vile vile, nia inageuza kitendo kuwa utiifu, na kitendo hicho kinaokolewa na maafa ya nafsi iliyojengwa upya. Kwa hivyo hamu yao ya mara kwa mara ya kuibua nia kila wakati, na hamu hii kwa ajili ya nia ilikuwa na athari katika hamu yao kwa uchunguzi wa kisaikolojia, ambao hauna kina kidogo wala mengi ya yale yaliyowasilishwa na utafiti wa kisasa unaohusiana na uchanganuzi wa kisaikolojia, hata kama njia husika zilitofautiana, na malengo yalitofautiana pia.
15) Masufi wa Kiislamu, katika mazungumzo yao kuhusu maadili, waliunganisha kile kinachoweza kuitwa upande chanya unaohusiana na wema na kupata kwao, na upande mbaya unaohusiana na maovu na kupambana nayo. Kipengele chanya kinaonekana katika mazungumzo yao juu ya vituo vya njia, kama vile subira, shukrani, kuridhika, upendo na kadhalika, na kupendezwa na kipengele cha pili huonekana katika maneno yao juu ya makosa na magonjwa ya nafsi, ambayo yanazuia kutoka na kuufikia ukamilifu wa maadili, kama vile husuda, majivuno, na ubatili.
16) Pamoja na hamu yao kwa upande wa utendaji, pia walitilia maanani upande wa kimaadili wa kinadharia, kwa hiyo kazi yao ya kimaadili ilitanguliwa na mtazamo, na tabia zao ziliegemezwa kwenye fikra, hivyo walichanganya mwelekeo wa kivitendo na mazingatio ya kimawazo, na upande wa kinadharia unaowakilishwa na mbinu za tabia zilizotengenezwa na masheikh wa Kisufi, ambazo ni matunda ya Elimu na Fikra, na uteuzi wa vipengele vya misingi, hatua na masharti, ambayo yote yanatafuta kufikia malengo yanayotakiwa kutokana na tabia, Kisha kipengele cha kinadharia kinakuwa wazi katika yale yaliyoonekana kwao kutokana na mafundisho ya utambuzi ambayo yanaelezea uzoefu wao, kufafanua hali zao na tabia zao, na kuanzisha nadharia ambazo haziishii kwenye mipaka ya uzoefu mdogo, lakini zinaenea hadi kwenye nadharia za jumla za kuwepo na ujuzi, na kwa upande wa elimu tunawakuta wanazungumzia njia zake, tabia na masharti yake, na uhusiano wake na vyanzo vingine vya elimu, kwa njia ambayo inakaribia – kutokana na mtazamo wa kimbinu – maneno ya wanafalsafa, hata kama njia ni tofauti na matokeo na safu zinatofautishwa.
17) Na vivyo hivyo yanakuja mazungumzo yao juu ya maadili, kwani ni kitendo kilichotanguliwa na mtazamo, na tabia inayoegemezwa kwenye fikra, na Masufi walikuwa wakifananisha kazi ya sheikh au mwalimu mlezi na kazi ya daktari, ambaye si sahihi kwake kutibu wagonjwa bila ujuzi, basi anatakiwa kuangalia matibabu kwa hali ya mwili na hali ya wakati, ugonjwa, umri na hali nyingine, na njia sahihi ya matibabu.
18) Hapana shaka kwamba Usufi wa Kiislamu ni mpana kiupeo, mpana kinyanja, unaenea katika suala la wakati, mahali, madhehebu na bendera, na ni vigumu kuufahamu kwa dharura hii, tulichowasilisha si chochote zaidi ya maoni ya mwelekeo wao wa kimaadili.
19) Hatimaye, Maadili ya Usufi yameelezewa na baadhi ya watafiti kuwa yana sifa ya kutokubalika kabisa, na kwa kuzingatia hayo yaliyotangulia inakuwa wazi kwamba rai hii haiwezi kukubaliwa hata kidogo.
20) Kwa kuzingatia hili, inawezekana kukosoa mwelekeo ambao baadhi ya watafiti wameuchukulia kwamba hakuna mafundisho ya kweli ya kimaadili katika fikra ya Kiislamu, na kwa kweli, mwelekeo huu unaweza kutafsiriwa kuwa unatokana na wazo lisilo sahihi ambalo ni kuyatazama matokeo ya fikra ya Kiislamu kupitia Falsafa ya Kigiriki, ili isitambuliwe kwa matokeo haya, isipokuwa inakuja kwa muundo ule ule ambao tafiti hizi zilionekana kwa Wagiriki, na katika hili kuna kutia chumvi katika kuthamini jukumu la Kigiriki, na hatuna maana ya kuwadharau, au kupuuza mchango waliochangia katika uwanja wa masomo ya maadili na falsafa, lakini tungependa tu kuashiria kwamba katika kutia chumvi huko ni kuhukumu maendeleo yote ya kibinadamu kwa vigezo vya mawazo ya Kigiriki pekee, na hasa kwa kuwa wazo hili halikuzingatia kipengele cha kidini kwa uwazi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
Rejea: A / Dr. Abdel Hamid Madkour, Dirasaat Fii Elim Al-Akhlaaq, Kairo: Dar Al-Hani, 1426 AH / 2005 AD, (uk. 127-178) kwa ufupi.