Uzushi Juu ya Nchi

Egypt's Dar Al-Ifta

Uzushi Juu ya Nchi

Question

Hivi sasa ndani ya jamii ya Misri kumeibuka baadhi ya vitendo ambavyo havijawahi kuwepo kabla ya hapo, ambapo baadhi ya watu wanafanya kazi ya kutekeleza kile wanachokidai kuwa ni mipaka ya Kisharia au adhabu dhidi ya wengine kwa madai kuwepo ukiukaji wa Sharia unaofanywa na hao wengine.
Pia kuna wanaotoa wito kuwa sehemu ya wananchi wateremke mitaani ili kulinda taasisi za umma badala ya kulindwa na vikosi maalumu. Nini hukumu ya Kisharia katika sura hizi mbili?
 

Answer

Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume wetu Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Maswahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka siku ya malipo.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amewajibisha kwa Waislamu kuwepo msimamizi mkuu wa mambo yao na kuchukuwa hatua mbalimbali zenye maslahi ya nchi na wananchi, na hili ni sehemu ya makubaliano ya Wanachuoni hakuna tafauti yeyote. Mwanachuoni Ibn Hajar Al-Haitimy amesema katika kitabu cha: [Sawaaiki Al-Muhrikah 1/25 chapa ya Taasisi ya Risala]: “Fahamu pia Maswahaba R.A wamekubaliana kuwa Imamu kuchukuwa nafasi ya uongozi baada ya kumalizika kwa muda wa Mtume ni jambo la lazima, bali wamelifanya ni lenye uwajibu muhimu zaidi”.
Kabla yake alisema hoja ya Uislamu Imamu Al-Ghazaly katika kitabu chake: [Al-Iqtiswad fiil Iitikaad ukurasa wa 202 chapa ya Al-Hikma]: “Mamlaka ni jambo muhimu katika mfumo wa dunia, na mfumo wa dunia ni muhimu katika mfumo wa dini, na mfumo wa dini ni muhimu katika kufanikiwa kupata furaha siku ya mwisho, makusudio ya moja kwa moja ni Manabii, imekuwa kushika nafasi ya utawala kwa Imamu ni katika mambo muhimu ya Sharia ambayo hakuna njia ya kuiacha”.
Sharia Takatifu imepangilia kwa usimamizi wa mambo ya Waislamu mazingatio kadhaa ili aweze kusimamia aliyopewa usimamizi ikiwa ni katika majukumu hatari na makubwa, na pia ikafanya kuvamia mtu mwingine na kuchukuwa kitu kwenye umaalumu huu wa Imamu au kumzonga ni katika jumla ya mambo yaliyokatazwa Kisharia ambayo yanapaswa kuzuiwa ili kuepusha kuenea fujo na ili kufanya kazi mfumo mkuu, na kufikiwa usalama wa kijamii unaohitajika.
Wanachuoni Waislamu wameelezea mwenye kugombana na mtawala katika yale aliyokuwa nayo basi huo ni uadui kwa mtawala.
Na uadui kwa kumfanyia mtawala ni jambo lenye kuzuiliwa na haramu, kwa sababu ni kufanya uadui dhidi ya haki yake kwa kumzonga kwenye aliyonayo, na ni kushambulia utashi wa umma ambao unawakilishwa na mtawala wao katika kusimamia mambo.
Al-Imamu Shamsi Diin anasema katika kitabu cha: [Badaai As-Siliku fii twabaai Al-Maliki 2/45 chapa ya Wizara ya habari ya Iraqi] – katika kuelezea ukiukaji ambao unapaswa kuepukwa katika haki za wasimamizi wa mambo - Ukiukaji wa tatu: Kumfanyiwa uadui kwa maana ya mtawala kwa kupinga mamla aliyopewa, na katika uharibifu mkubwa ni kubadilisha maovu kwa kiwango ambacho hakikubaliani isipokuwa kwa mtawala, imeelezwa kuwa miongoni mwa siasa ni pamoja na kuchukuwa haraka mikononi mwa mwenye kutamani hilo na kuondoa misingi ya kujionesha”.
Ujumla wa mambo na umaalumu ambao haupo isipokuwa kwa mtawala au mwenye kukaimu nafasi yake: Kusimamia mipaka na kuteleza adhabu, hilo Sharia imetoa usimamizi kwa Maimamu na Watawala ili isitokee fitina ya ukandamizaji.
Ibn Zanjawih amepokea katika kitabu cha [Al-Amwali” 3/1152 chapa ya Kituo cha Mfalme Faisal cha utafiti wa na sayansi ya Kiislamu nchini Saudi Arabia], kutoka kwa Muslimu Ibn Yasar kutoka kwa Abdillah mmoja wa Swahaba wa Mtume S.A.W amesema Muslimu: Ibn Omar alikuwa anatuamrisha kuchukuwa kwake akasema: “Ni Mwanchuoni basi chukuweni kwake” nikamsikia anasema: “Zaka utekelezaji wa adhabu ngawira na swala ya Ijumaa ni jukumu la Mtawala”.
Ibn Aby Shaibah amepokea kwenye kitabu cha: [Al-Muswannif” 5/506 chapa ya Dar Al-Fikri kus], kutoka kwa Al-Hassan amesema: “Mambo manne yanamuhusu Mtawala: Zaka, Swala, Adhabu na Hukumu”.
Kutoka kwa Ibn Mahiriz amesema: “Swala ya Ijumaa, Adhabu, Ngawira na jukumu la Mtawala”.
Kutoka kwa Atwaa Al-Khurasan amesema: “Kwa Mtawala kunapaswa zaka ijumaa na adhabu”.
Haya ndio yaliyoelezewa na Maimamu wa dini na Wanachuoni wa mila wa madhehebu mbalimbali.
Kwa upande wa Imamu Abu Hanifa: Imamu Sarkhasiy amesema katika kitabu cha Sherhu Sairi Al-Kabiir” 5/ 1938 chapa ya shirika la Mashariki la matangazo: “Utekelezaji wa adhabu ni jukumu la Mtawala”.
Mwanachuoni Al-Kasanyi amesema katika kitabu cha [Badaii Swanaii” 7/57, 58 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Ilmiyah]: “Ama masharti ya kutekeleza – kwa maana ya adhabu – miongoni mwa masharti hayo ni yanakusanya adhabu zote, na mengine yanahusu baadhi pasina mengine, ama ambayo yanakusanya adhabu zote ni mtawala, naye ni kuwa mwenye kutekeleza adhabu awe ni Imamu au anaye kaimu nafasi yake…na maelezo ya hilo:
Ni kuwa mamlaka ya kutekeleza adhabu yanathibiti kwa Imamu kwa ajili ya maslahi ya waja – nayo ni kulinda nafsi zao mali zao na heshima zao -…..na Imamu ni mwenye uwezo wa kutekeleza kwa nafasi yake na kufuatwa kwake na wananchi kwa nguvu na kulazimishwa, bila ya kuhofia matakwa ya wahalifu na wafuasi wao kwa kutokuwepo kwa upingaji kati yao na Imamu, na tuhuma za kuegemea na kupendelea katika kutekeleza adhabu ni zenye kutawanyika kwake, kwani hutekelezwa kwa sura yake na kufikia lengo kwa yakini la Sharia ya utawala…. Jukumu la Imamu la kutelekeza adhabu kwa sababu hawezi kutelekeza yote yeye mwenyewe, kwa kuwa sababu za ulazima wake zinapatikana katika nchi za Kiislamu, wala haiwezekani kuziendea na kuzifikisha sehemu ya Imamu ni uzito mkubwa, ikiwa haitofaa kutawala basi utekelezaji adhabu utasimama, na hili halifai, na kwa hili alikuwa Mtume S.A.W akiwafanya Makhalifa watekelezaji wa hukumu na kutekeleza adhabu’.
Kwa upande wa Imamu Maliki: Imamu Al-Kutuby amesema katika tafasiri yake [2/245, 246 chapa ya Al-Kutubi Al-Misrihah]: “Hakuna tafauti kuwa utekelezaji wa kisasi katika kuuwa hufanywa na watu wenye mamlaka, wamelazimishwa kutekeleza adhabu za kisasi pamoja na adhabu zingine, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaambia Waumini wote kutekeleza kisasi, kisha Waumini wote wasijiandae kwenye kutekeleza hukumu ya kisasi bali Mtawala akasimama nafasi yao katika kutekeleza hukumu hiyo na adhabu zingine”.
Imamu Ibn Rushdi amesema katika kitabu cha [Bidayatul-Mujtahidi 4/228 chapa ya Dar Al-Hadithi]: “Ama mwenye kutekeleza adhabu – kwa maana ya adhabu ya kunywa ulevi – wamekubaliana kuwa Imamu ndio mtekelezaji wa hilo, vile vile katika adhabu zingine zilizobakia”.
Na amesema katika kitabu cha [Mukhtasar Khalil na sherehe yake cha Ahmad Dardiir 4/239]: “Muuaji wa makusudi na kwa uadui basi ni mwenye kuzuiliwa kuuwa bila ya haki, ama kwa upande wa mwenye haki ya kuuwa – naye ni msimamizi wa aliyeuliwa – si mwenye kuzuiliwa, lakini ikiwa atauwa muuaji bila ya ruhusa ya Imamu au makamu wake basi hutiwa adabu kwa kumkiuka kwake Imamu”.
Kwa upande wa Imamu Shafi: Imamu Al-Umraniy amesema katika kitabu cha [Al-bayan 12/376 chapa ya Dar Al-Minhaj]: “Inapowajibika adhabu kwa mzinifu au mwizi au mnywa pombe huru na si mtumwa haufanyiki utekelezaji wake isipokuwa hutekelezwa na Imamu au yule aliyepewa uwakilishi wa usimamizi na Imamu, kwa sababu adhabu katika zama za Mtume S.A.W na katika zama za Maswahaba waongofu R.A hazikutekelezwa isipokuwa kwa ruhusa yao, na kwa kuwa utekelezaji wake hauhitaji mtazamo na jitihada hivyo haifai kutekeleza isipokuwa na Imamu au kaimu wake”.
Imamu Abu Is-haqa Shiirazy amesema katika kitabu cha [Al-Muhadhibu 3/191 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Elmiyah]: “Wala haifai kutekeleza kisasi isipokuwa na Mtawala kwa sababu haihitaji jitihada, ikiwa itatekelezwa si na mtawala ataadhibiwa mtekelezaji kwa mtazamo wa mtawala kwa sababu atakuwa amemkiuka mtawala”.
Kwa upande Imamu Hambal: Imamu Ibn Muflih amesema katika kitabu cha [Al-Furuui 6/53 chapa ya Aalam Al-Kutub]: “Ni haramu kutekelezwa adhabu isipokuwa kwa Imamu au kaimu wake”.
Na imekuja katika kitabu cha [Matwalibu Uli Nuha katika sherehe ya Ghayatul-Minhaj 6/159 chapa ya Al-Maktabi Al-Islamy cha Shaikh Ruhaibany]: “Kutekelewa kwake kwa maana ya adhabu ni kwa Imamu au kaimu wake – kwa maana ni sawa sawa imekuwa adhabu ya uzinifu au kwa upande wa mwanadamu kama vile adhabu ya kutukana watu wema – kwa sababu adhabu hizo hazihitaji jitihada, ikawajibishwa uwakilishaji kwa wawakilishi wa Mwenyezi Mungu katika waja wake, kwa sababu Mtume S.A.W alikuwa anatekeleza adhabu katika maisha yake na vile vile Makhalifa waongofu baada yake, na kaimu wa Imamu anasimama nafasi ya Imamu mwenyewe kwa kauli ya Mtume S.A.W: “Nenda ewe Unais kwa huyu mwanamke, ikiwa atakiri basi mpige mawe, akakiri na akampiga mawe”, pia Mtume aliamuamrisha Maizi kutekeleza adhabu kupiga mawe na wala yeye mwenyewe Mtume hakuhudhuria, na alimwambi pia Sarik: “Nendeni naye na mkateni shingo”.
Na tunasema pia kutekeleza adhabu katika zama za sasa chini ya uwepo wa taasisi ya dola basi hupewa sehemu maalumu huegemewa kwa kila kinachoitwa serikali ya utendaji, na upande huu hauwezi kuteleleza adhabu yeyote isipokuwa amri ije kutoka upande husika wa mamlaka ya kimahakama, ambayo inajukumu la kuangalia tukio kwa undani zaidi, na kukamilisha dalili za tukio ikiwa ni pamoja na kuzungumza mashahidi, na kuangalia sababu na mazingira yanayozunguka tukio, kisha ndio hutolewa hukumu adhabu maalumu sawa na jinai lenyewe, na upande huu kwa nafasi yake huwezi kutekeleza adhabu isiyotajwa na sheria inayofanya kazi nchini, na upande unaofanya kazi ya kutengeneza sheria hizo ni mamlaka ya kutunga sheria, na kila upande katika pande hizi tatu huzingatiwa ndio wasimamizi wa mambo ya nchi kwa maana ya ndio tawala za nchi, amesema Mwanachuoni Ibn Ashur katika kitabu cha Tahrir wa Tanwiir 5/97, 98 chapa ya Dar Tunisa – wakati wa kutafsiri kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wale wenye mamlaka kwenu} [AN NISAA: 59]: “Watu wenye mamlaka katika umma ni wale ambao watu wamewapa usimamizi wa mambo wa mambo yao na wanawategemea kwenye hilo, hivyo amri inakuwa ni maalumu kwao…hivyo wasimamizi wa mamlaka hapa ni kuanzia wale walioandaliwa na Mtume S.A.W kuanzia Makhalifa mpaka wasimamizi wengine na kuanzia viongozi wa kijeshi na Wanachuoni Maswahaba na wanajitihada mpaka kufika kwa watu wa elimu ndani ya zama za mwisho, wenye mamlaka ni wale ambao huitwa pia watu wa ufumbuzi na makubaliano”.
Hivyo basi baadhi ya watu hivi sasa kutekeleza adhabu wao wenyewe dhidi ya baadhi yao kwa uhalifu au katika kuamrisha mema kwa kufanya uadui ni kukiuka wasimamizi wa pande hizi tatu zenye mamlaka, kwani anaweza kuadhibu muhalifu kinyume na sheria, na kabla ya hapo huingia katika tuhuma kupitia hawa wafitinifu bila ya kufanyika uchunguzi wa kina au kujitetea, au huenda akaingia kwenye tuhuma kinyume na kustahiki tuhuma hizo, ambapo anaweza kuwa amefanya jambo halali lakini mwingine anaona au anadhani – kwa ujinga wake na kutofanya uchunguzi wa kina kinyume na inavyofanyika na watu wenye elimu – kuwa si jambo la kisheria, kisha inakuja adhabu baada ya hapo kutoka kwa watu wasio kuwa na weledi wa jambo hilo, yote haya mwisho kabisa hupelekea jamii kuingia kwenye fujo na mpasuko katika mfumo mkuu, kuongezea pia kuharibu sura ya Uislamu, na chuki kwenye makusudio ya kazi ya ulinganiaji wa Uislamu kupingwa mbele ya walimwengu.
Ama kulinda asasi za umma yenyewe kwa asili ni jukumu la jeshi la polisi au jeshi la taifa – kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosimamia hilo – si jambo lenye kuachwa tu kwa watu wajifanyie wenyewe, na hilo ni kwa sababu jukumu la ulinzi linahitaji ujuzi maalumu, pamoja na kuchunga hatua za utishiaji na mengine katika yale wanayoyafahamu hawa na kuchukulia mafunzo yake, nayo inafanana na yaliyozungumzwa na Wanachuoni ya kumuondoa mhalifu ambapo haikimbiliwi kwa mtumia nguvu zaidi katika kuondoa pamoja na uwepo wa uwezekano wa kwenda kwa aliyechini zaidi, masharti haya na uzoefu huu kutekelezwa na baadhi ya watu kunapingana, kama vile utekelezaji huu unahitaji chombo na silaha ya kutumika kwenye ulinzi, na hili ni katika lisiloruhususiwa na sheria isipokuwa katika hali maalumu kwa watu maalimu, hupewa hawa watu kibali au leseni rasmi kumiliki silaha maalumu, kwani ikiwa jukumu hili litaachwa kusimamiwa na baadhi tu ya watu hakutakuwa na amani kwa mwenye kutaka kutekeleza ubaya bila ya kukusudia kheir, hivyo huchanganywa kati ya kamba na manate, wala haifahamiki nani muhalifu, kisha mambo hubadilika kutoka wajibu unaofanywa na vikosi maalumu vya ulinzi kwa kufuata misingi iliyojengwa na kuimarishwa na kuwa mivutano inayoonguza na mapigano ya kijinga kati ya wananchi wa nchi moja, jambo ambalo husimika uadui na chuki kati yao, wakati mwingine damu humwagwa bila ya sababu za Kisharia.
Hivyo Kisharia hakuna ruhusa kwa kikundi cha watu kujitokeza kwa haraka wao wenyewe kusimamia jukumu la ulinzi uliotajwa madamu tu vyombo husika vya nchi vipo kwa kazi za kuzuia uadui dhidi ya maeneo ya umma, kinyume na hivyo basi itakuwa ni ukiukaji wa yale waliyoyafanya, isipokuwa ni kwa kuvitumia vyombo hivi vya ulinzi chini ya ufuatiliaji na usimamizi kupitia kamati za kirai kwa mfano, hapo hilo linafaa, kwa sharti la kuwajibika kila mmoja na nafasi inayotakiwa kwake kuchukuliwa bila ya kuvuka mpaka wa mwingine.
Vile vile ikiwa sehemu imekosa watu wa kuilinda na kutokea vitendo vya uporaji na mfano wake basi wakati huo inafaa kwa watu kuunda kamati za kiraia za ulinzi wa maeneo ya umma na taasisi kwa ujumla, ikiwa kamati hiyo ina uwezo wa kufanya hilo bila ya kufanyika ubaya miongoni mwao au uharibifu.
Asili yake ni Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhary kutoka kwa Anas Ibn Maliki R.A amesema: “Mtume S.A.W alitoa amri Zaidi kubeba bendera kisha akashambuliwa na bendera ikachukuliwa na Jafar naye pia akashambuliwa, kisha ikachukuliwa na Abdillah Ibn Rawahah naye pia akashambuliwa, kisha ikachukuliwa na Khalid Ibn Waliid mpaka wakashinda” amesema Al-Mulhibu kwenye kauli ya Mtume S.A.W: “Kisha akachukuwa Khalidi Ibn Waliid mpaka wakapata ushindi” ndani yake kuna aina ya Sharia: Kuwa mwenye kuona kasoro kwa Waislamu na akaweza kuiziba ikiwa ana weza kufanya hivyo na akajifahamu yeye mwenyewe kuwa na nguvu na udhubutu” ni kitabu cha sherehe ya sahihi Bukhary cha Ibn Batwal 5/223 chapa ya Maktaba Rushdi.
Na kwa maelezo yaliyotangulia muulizaji anafahamu jibu la kilichoulizwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi


 

Share this:

Related Fatwas