Kumuita Mtoto kwa Jina la: “Basmall...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumuita Mtoto kwa Jina la: “Basmallah”.

Question

 Tumepitia barua iliyopokelewa na Shaikh Muhammad Zaky Badary “Katibu Mkuu wa Jopo la utafiti wa mambo ya Kiislamu, ya tarehe: 14/01/2014 iliyosajiliwa kwa Fatwa nambari 17 ya mwaka 2014 kuhusu ombi lililofikishwa kwake Katibu kutoka kwa Mwl: Sharif Muhammad Bahiyudeen kuhusu: Kupewa jina mtoto aliyezaliwa la Basmallah.
Kwa heshima ifikishwe Ofisi ya Mufti wa Misri kutokana na azimio la tume ya utafiti wa kifiqhi kwenye Jopo la utafiti wa mambo ya Kiislamu kwa kikao chake cha tano awamu ya hamsini ambacho kilikaliwa siku ya jumatano mwezi 7 mfungo sita 1435H sawa na tarehe 8 Januari 2014.
Mwenye barua hiyo maneno yake yamekusanya mambo mengi ambayo ameona kuwa yanaonesha uharamu wa kumwita mtoto kwa jina hilo, kwa namna alivyofupisha:
Kwanza: Basmallah ni maalumu kwa Mwenyezi Mungu ambao haufai kushiriki Mungu na kiumbe chake chochote.
Pili: Basmallah ni sehemu isiyotengana na Qur1ani.
Tatu: Kuita mtoto kwa jina hili hufuta utukufu unaohitajika wa Basmallah.
Nne: Kuita mtoto wa kike kwa jina hilo ni ukiukaji katika majina mazuri ya Mwenyezi Mungu.
Tano: Ni kuwa Basmallah inakusanya jina la Mwenyezi Mungu na jina la Rahman, na yote hayo mawili ni haramu kumwita mtu, hivyo ni haramu kuita kwa majina hayo.
Sita: Mtoto wa kike mwenye kuitwa kwa jina hilo atakuwa anaweza kufikwa na hali ya kutukanwa au kudharauliwa na mfano wa hayo.
Saba: Watu wanapinga kuita kwa jina hilo pindi watakapo fahamu maana yake, na kinachopingwa na watu basi hiko ni kibaya.
Nane: Kuitwa jina hilo ni miongoni mwa uovu ulioharamishwa kwa kauli yake Mola Mtukufu: {Na anakuhalalishieni vilivyo vizuri na kukuharamishieni vilivyo vichafu} [AL AARAF: 157].
Tisa: Kumwita kwa jina la: “Basmallah” ni miongoni mwa uzushi unaopingwa.

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka siku ya malipo
Jina kwa upande wa lugha: Ni lenye kufahamisha mwenye kuitwa, nalo kwa watu wa Basra: Linatokana na maana ya juu ni kwa sababu humuinua juu mwenye kuitwa na kumuonesha, kwa watu wa Kuufah: Hutokana na maana ya kufundisha alama, ni kwa sababu lenyewe ni alama kwa mwenye kuitwa. Angalia: Kitabu cha Risala Al-Kubra cha sheikh Saban ukurasa wa 22, 25, 26 chapa ya Kituo cha uchapishaji cha Kheiria chapa ya kwanza ya mwaka 1325.
Na kuita ni chanzo cha kitenza ameita. Na ameita hivi: Amempa jina, fulani ameitwa Zeydi, na ameitwa kwa jina la Zeydi kwa maana nimemwita mfano wake, naye ameitwa fulani pindi linapokubaliana jina lake na jina la fulani. Angalia kitabu cha [Mukhtar As-Sahah cha Imamu Ar-Razy uk. 155, chapa ya Maktaba Al-Asriyah, na kamusi ya kati na kati ya Jopo la wataalamu wa lugha ya Kiarabu nchini Misri uk. 452 chapa ya Maktabat Ash-Shuruok].
Kumwita jina ni kumkirimu mtoto aliyezaliwa, kwa sababu atafahamika kwa kuitwa jina na kutafautishwa na mwingine, hivyo jina ni lenye kuhitajika Kisharia kwa kauli yake Mola Mtukufu: {Kwa hakika tumemkirimu mwanadamu} [AL ISRAA]. Ameelezea Ibn Hazmi makubaliano ya Wanachuoni juu ya ulazima wake akasema kwenye kitabu chake cha [Maratib Al-Ijmaa ukurasa wa 154 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Elmiyah]: “Wanachuoni wamekubaliana kuwa kupewa jina mwanamme na mwanamke ni jambo la lazima”.
Sharia imependezesha kutumika majina mazuri, imepokelewa na Imamu Abu Daud katika Sunan yake kutoka kwa Abi Dardai R.A amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W: “Hakika siku ya kiyama mtaitwa kwa majina yenu na majina ya baba zenu hivyo peaneni majina mazuri”.
Asili ni kwamba inafaa kuita kwa jina lolote isipokuwa yale majina yaliyokatazwa, ni haramu kuita kwa majina yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, vile vile ni haramu kumuita jina maalumu la Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama vile jina la Rahman na Qudduus, au kuita jina lisiloendana isipokuwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kama vile mmiliki wa wamiliki, sultani wa masultani na hakimu wa mahakimu. Imepokelewa na Imamu Bukhari kutoka kwa Abi Hurairah R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Majina dhalili zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya kiyama ni mtu kujiita mmiliki wa wamiliki”.
Imamu Waliyyudeen Al-Iraaqy amesema katika kitabu cha [Twarhu Tathreeb 2/152 chapa ya Dar Ihyaau Al-Kutubi Al-Arabiyah] wakati wa kusherehesha Hadithi iliyopita: “Ndani yake kuna uharamu wa kuita kwa jina hili, ni sawa sawa limekuwa hilo jina kwa lugha ya Kiarabu au lugha ya kigeni, kwa utaratibu wa ahadi hii ya adhabu kali, na dalili yake ni kuwa hasira za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mwenye kuitwa kwa majina haya ni kali zaidi kuliko mwingine yeyote….na inakutana na hilo kuita kwa majina maalumu ya Mwenyezi Mungu kama vile Ar-Rahman, Al-Quddus, Al-Muhaimin, Muumba wa viumbe na mfano wake”.
Inachukiza kuita kwa majina ambayo ndani yake kuna ubaya au utakaso wa nafsi, kwani imepokelewa na Imamu Muslim kutoka kwa Ibn Omar R.A. kuwa Mtume S.A.W. alibadili jina la Aasiyah na akasema: “Wewe ni Jamilah”.
Imepokelewa na Imamu Bukhari kutoka kwa Abi Huraira R.A. kuwa Zainabu jina lake lilikuwa ni Barrah, hivyo Mtume S.A.W. akamwita jina la Zainabu.
Imepokelewa na Imamu Muslim kutoka kwa Samrah Ibn Jandab R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Usimpe jina mtoto wako la Yasara wala Riyaha wala Najiha wala Aflaha”.
Imamu An-Nawawiy amesema katika kitabu cha [Sharhu Muslim 14/119 chapa ya Dar Ihyaa Turaath Al-Arabiy]: “Amesema mwenzetu: Inachukiza kumuita kwa majina haya yaliyotajwa katika Hadithi, na yanayobeba maana yake, wala haihusishi uchukizo peke yake, ni uchukizo wa kuepushwa na upungufu, sababu ya kuchukiza ni iliyoelezewa na Mtume S.A.W.: “Je anapata dhambi? Anasema hapana”, imechukizwa kwa ubaya wa jibu, na huenda baadhi ya watu wameingia sehemu ya majina hayo”.
Na amesema katika sherehe ya kitabu cha [Al-Muhadhibu 8/418 chapa ya Al-Muniiriyah]: “Yanachukiza majina mabaya, kwa Hadithi ya Samrah ambayo imetajwa na mtunzi, na zimekuja Hadithi nyingi katika vitabu sahihi kwa maana yake, miongoni mwa majina mabaya: Harbu, Murrah, Kalbu, Jaryi, Asayah, Mughriyah, Shaitan, Shihab, Dhwalim, Himar na yanayofanana na hayo, majina yote haya huitwa watu, na mengine yaliyotajwa katika Hadithi ya Samarah nayo ni: Bashar, Riyah, Naafii, Najaah, Najih, Baraka, Aflaha, Mubarak na mfano wake. Mwenyezi Mungu ndiyo Mwenye kujua zaidi”.
Imamu Al-Khatwabiy amesema katika kitabu cha [Maalim As-Sunan 4/128 chapa ya Al-Elmiyah – Halabu]: Mtume S.A.W. amebaini maana ya hayo, na akataja sababu ambayo kwa ajili hiyo imekatazwa kumuita mtu, na sababu hiyo ni kuwa wao walikuwa wanakusudia kwa majina haya na yanayobeba maana zake ima kujibariki nayo, au kujipa matumaini kwa uzuri wa matamshi yake, akawatahadharisha kufanya hivyo huenda yakawageukia yale waliyoyakusudia katika majina haya na kuwa kinyume, na hilo pale walipouliza wakasema: Kuna dhambi kuita Yasara? Kuna dhambi kuita Riyaha? Pindi paliposemwa: Wala musiyakatie tamaa na kudhamiria uzito kwenye wepesi, akawakataza kwa sababu ambayo inawaletea dhana mbaya kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwaletea ugumu kwenye kheri zake”.
Ama neno “Basmalah” ni ufupi wa maneno: Bismillah Ar-Rahman Ar-Rahim, aina hii ya ufupishaji huitwa kwa Wanachuoni wa lugha “Sifa” na sifa ni njia ya Waarabu katika kufupisha maneno, wametumia sana sifa katika maneno yao, wakiwa wanataka wepesi wa kuelezea na kufupisha, na mfano wa hilo pia: “Haukala” katika jumla ya: Laa haula wala kuwwata illa billah, kwa dalili ya utamkaji wake, vile vile neno “Haiala” ikiwa ni kauli ya muadhini ya kusema: Hayya alaa Sala, Hayya alaal-Falaah, na neno “Sabhala” kwenye kauli ya: Subhanallah, na neno hailala kwenye kauli ya: Laa ilaaha illal-laah, na neno hasbala kwenye kauli ya: Hasbiyallah, na neno twalbaka kwenye kauli ya msemaji: Mwenyezi Mungu akupe umri mrefu, angalia kitabu cha [Al-Muz’har] katika elimu za lugha na aina zake cha Imamu Suyutwiy [1.382, 373, chapa ya Dar Al-Kutubi Al-EIlmiyah], kitabu cha mambo ya sifa na maelezo ya uhalisia wake na ufipisho wake wa kanuni zake cha Shaikh Mahmoud Shukry Al-Aalusiy ukurasa wa 28: 48.
Amesema Abu Mansour Thaalaby katika kitabu cha [Fiqhi lugha ukurasa wa 269 chapa ya Ihyaau Turaath Al-Arabiy]: “Waarabu husifu maneno mawili na matatu kwenye neno moja, nayo ni jinsi ya ufupishaji, kama vile kauli yao: Abshamiyy, ikiwa ni kunasibishwa na Abdu Shams. Khalil asema: Nina mwambia na machozi yakishuka – hivi hukuhuzunika na sauti ya muitaji kwenye Sala.
Mwanachuoni Sabani amesema kwenye kitabu cha [Risalatul-Kubraa juu ya basmalah ukurasa wa 62 chapa ya Al-Khairiyah]: “Mara nyingi hutumika neno basmala kwa kusudio la Bismillah Ar-Rahman Ar-Rahim, nao ndiyo msamiati wake kwa maelezo ya Ibn Hisham ambapo amesema: Neno Basmalhah kilugha ni kauli ya: Basmallah, na kimsamiati ni: Bismillah Rahman Rahim”.
Lakini pia imesemwa kuwa ni neno lililoletwa, halijasikika kwa Waarabu wafasihi wa lugha, lakini si sahihi kwani imethibitishwa na Maimamu wengi wa lugha kama vile Ibn Sikkiitu na Matwrazy na kutumika na Waarabu wafasihi.
Ama kuita kwa jina la Basmallah inafaa hakuna uharamu, kwa sababu hakuna dalili ya uharamu, lakini haipendizi na wala haitakiwi, na hilo ni kutokana na katazo lililopokelewa kuita baadhi ya majina ambayo huleta ukatishaji matumaini kupingwa kwake – kama ilivyoelezewa – hakuna shaka kuwa ikiwa itaulizwa: Je hapa kuna basmallah? Itasemwa hapana hapa hakuna basmallah, hiyo inakuwa ni kupinga jambo la kujibariki nalo, hilo ndio linalokusanya makatazo yaliyopo kwenye Hadithi.
Vile vile watu katika zama hizi wanaweza leta dharau kwenye jina hili pamoja na uwepo maana ya utukufu wa Mwenyezi Mungu kisha akatukanwa mwenye kuitwa kwa jina hilo ikiwa ni katika njia ya kutiwa adabu, ndipo mwenendo wa Omar Ibn Khattab R.A ulikuwa ni kuchukiza kuita kwa majina ya Manabii ili kuepusha jina takatifu kupatwa na hali ya dharau kupitia kauli za watu bila ya kukusudia hilo.
Imepokelewa na Ibn Aby Shaibah katika kitabu chake [5/262 chapa ya maktaba Rushdi – Riyadh] kutoka kwa Abi Al-Aaliyah amesema – pindi alipoulizwa kitu – “Munafanya makosa kwenye hilo, mnawapa watoto wenu majina ya Manabii kisha munawalaani”.
Imamu Al-Baghwy amesema kwenye kitabu cha [Sharhu Sunna 12/335 chapa ya Al-Maktabu Al-Islaamiy]: “Imepokelewa kutoka kwa Umar alikuwa anachukia kuita kwa jina la Nabii na Malaika, pakasemwa: Anachukia hilo ni kulaani au kutukana kwa jina lake.
Mwanachuoni Ibn Qayyim amesema katika kitabu cha [Tuhfatu Al-Mauduud ukurasa wa 128 chapa ya Maktaba Dar Al-Bayan – Damascus]: “Mwenye kauli hii – kwa maana ya kuchukia kuita kwa majina ya Manabii – amekusudia kulinda majina yao kutumika vibaya, na uwezo wa kutolewa maneno mabaya wakati wa hasira”.
Ama shaka ambayo anayoielezea muulizaji akidhania kuwa ina maanisha uharamu, uwazi wa maelezo ni kama yafuatayo:
Kwanza: Neno basmallah ni maalumu la Mwenyezi Mungu ambalo halifai kumshirikisha Mungu kwenye neno hilo na yeyote katika viumbe vyake.
Jibu: Ni kuwa basmallah si katika umaalumu wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ni kauli ya Bismillah Ar-Rahman Ar-Rahim – na maelezo yametangulia katika kuelezea maana yake – basmallah si jina lake Mwenyezi Mungu, na kutofahamika tafauti hii kupo wazi, na kuchanganya kati ya jina la Mwenyezi Mungu na uwepo wa jambo linalokadiriwa linalotokana na herufi ya Ba katika kauli ya msemaji: Basmallah hivyo huonekana maana ya basmallah na inakuwa kama: Ninaanza kwa jina la Mungu au kuanza kwa jina la Mungu, hiyo ndio asili na msingi wa tatizo kwa muulizaji.
Pili: Basmallah ni sehemu isiyojitenga na Qur`ani.
Jibu: Ni kuwa basmallah inaweza kuwa Qur`ani na inaweza pia kuwa si Qur`ani, kwa mfano kauli ya msemaji: “Bismillah Ar-Rahman Ar-Rahim” katika Suratul-Fatiha ni Qur`ani, ama nje yake ikiwa hakuna kusudio na nia ya kuwa Qur`ani basi inakuwa si Qur`ani, na kama sio hivyo basi ingekuwa ni haramu kwa kila mwenye janaba au hedhi kutamka hata kwa kutaja tu, kwa sababu ni haramu kwa watu hao wawili kusoma Qur`ani, kutokana na yaliyopokewa na Ibn Maja kutoka kwa Ibn Omar R.A kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Asisome mwenye janaba na mwenye hedhi kitu chochote katika Qurani” lakini si haramu kwao katika hilo kwa makubaliano ya Wanachuoni. Imamu An-Nawawiy amesema katika kitabu cha [Tibyaan fii aadabi hamlati Al-Quran ukurasa wa 73, 74 chapa ya Dar Ibn Hazmi]: “Ama mwenye hedhi na mwenye janaba ni haramu kwao kusuma Qur`ani, ni sawa sawa Aya au chini ya Aya, na inafaa kwao kuipitisha Qur`ani ndani ya mioyo yao pasi ya kutamka, na inafaa kwao kuangalia kwenye Msahafu na kupitisha kwenye moyo, wamekubaliana Waislamu kuwa inafaa kuleta tasbihi tahlil tahmiid takbiir na kumsalia Mtume S.A.W. ikiwa watasema kumwambia mtu kwa mfano: “Chukua Kitabu kwa nguvu” na hawakukusudia Qur`ani basi inafaa, vile vile yanayofanana na hayo, na inafaa kwao kusema wakati wa kutokea tatizo hasa hali ya kifo: “Innaa lillah wainnaa ilayhi raajiun” ikiwa hawatakusudia Qur`ani, wamesema wenzetu: Inafaa wao kusema wakati wa kupanda mnyama: “Subhana lladhiy sakhkhara lanaa haadhaa wamaakunna lau Muqriniin” na wakati wa kuomba duwa inafaa kusema: “Rabbanaa Aatina fiddun’ya hasana, wafil-Aakhiratu hasana wakinaa adhaaba nnaar” ikiwa hawatakusudia Qur`ani, amesema Imamu Al-Haramain: Pindi anaposema mwenye janaba: “Bismillah wal-hamdulillah” ikiwa amekusudia Qur`ani atakuwa amefanya maasi, ikiwa amekusudia utajo au hakukusudia kitu chochote hatopata dhambi”. Hapa kutaja basmallah katika hali ya kutokusudia Qur`ani hakuambatanishwi na sababu zilizotajwa.
Kisha si kila kilichokuja ndani ya Qur`ani hakifai kutajwa kwa mfano jina Ahmad Isa Yahya zakaria Luqman Maryamu Aalaa Bushraa na mengineyo katika majina na maneno ambao yamekuja na kutajwa ndani ya Qur`ani, hakuna uharamu katika kuyataja pamoja na kuwepo ndani ya Qur`ani.
Tatu: Kuitwa kwa jina hili kunafuta utukufu unaopaswa wa basmallah.
Jibu: Muulizaji ametaja pingamizi hili, lakini hakuweka wazi upande wa kufuta utukufu uliotajwa.
Nne: Kumuitia mtoto wa kike kwa jina hilo ni ukiukaji katika majina mazuri ya Mwenyezi Mungu.
Jibu: Hili si sahihi kwa sababu ukiukaji katika majina ya Mwenyezi Mungu ni kumuita Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa jina lisilopokelewa, au majina yaliyo na maana chafu au kupinga kitu kilichothibiti kwake katika majina yake.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo. Na waacheni wale wanao haribu utakatifu wa majina yake. Hao watakuja lipwa waliyo kuwa wakiyatenda} [AL-A'ARAF: 180]
Amesema Mwanachuoni Abu Suud katika tafasiri yake wakati wa kufasiri Aya Tukufu, kuharibu utukufu wa majina yake, ni kule kwenda kinyume na makusudio kama vile kuacha kuiendea haki na kwenda kwenye batili, ima kwa kumuita Mola Mtukufu kwa kile asichokuwa nacho au kwa kile kitakachochukuliwa kwa maana chafu.
Na amesema Mwanachuoni Ibn Ashuur katika cha [Tfasiri yake ya Tahrir wa tanwiir 9/189 chapa ya Dar Tuunisia]: “Na maana ya kuharibu utukufu wa majina ya Mwenyezi Mungu ni kuyafanya sura katika sura za kukufuru, na hilo ni kwa kupinga kuitwa Mwenyezi Mungu kwa majina yenye kuonesha sifa thabiti kwake, Naye ndiyo anayestahiki ukamilifu wa maana ya sifa hizo, wao wamepinga Rahman kama ilivyotangulia, na wakafanya kuitwa kwake ndani ya Qur`ani njia ya uovu, na kusingiziwa Mtume S.A.W kuwa ana miungu mingi, hakuna uzushi mkubwa kama huu, ni kweli kabisa kuitwa uharibifu kwa sababu ukiukaji wa haki kwa kukusudia kujikuza na uhasidi”.
Na kuita kwa jina la Basmallah hakuna uhusiano wa kuita jina lisilopokelewa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kuita kinachodhani kuwa na maana ovu kwa Mola.
Tano: Basmallah inakusanya jina la Mwenyezi Mungu na jina la Rahman, na yote hayo mawili ni haramu kuita hivyo ni haramu kuita majina hayo kwa kila moja peke yake na ni haramu kuita majina hayo kwa pamoja.
Jibu: Kuita kwa jina la basmallah hakuna kinachopelekea kuita kwa jina la Mwenyezi Mungu au jina la Rahman kwa pamoja au kutafautisha kwa sababu basmallah yenyewe sio jina la Mwenyezi Mungu kama ilivyoelezewa.
Sita: Mtoto wa kike mwenye kuitwa kwa jina hilo atakuwa anaweza kufikwa na hali ya kutukanwa au kudharauliwa na mfano wa hayo.
Jibu: Maana hii sio lazima kumuitia huyo aliyetajwa, bali huenda ukawepo uitaji na mwenye kuitwa asipatwe na hali yeyote ya kudharauliwa, na kufanya sababu hii inalazimisha uharamu ni kupanua kizuizi cha kisichoridhiwa, inafanana na kauli ya kuharamisha ujenzi wa makazi kuwa jirani ili watu wasifanye vitendo vya uzinzi kwa sababu ya ujirani, au kuharamisha kilimo cha zabibu ili isije zalishiwa pombe.
Na kilichopitishwa kiasili ni kuzuia wigo wa kusababisha maasi, au kuzuia kuharamisha njia wakati wowote wa kuwa kitendo ni salama kutokana na uharibifu, kwa sababu asili ni kuondoa jukumu la amri, na haya ndiyo madhehebu ya Imamu Shaafi na wengine katika Wanachuoni, mwisho wa jambo ni kuwa sababu hii inaweza kuonesha chukizo, na hili ndiyo tuliokubaliana hapo mwanzo wakati wa maelezo yetu ya kauli inayochukiza, ama uharamu hapana.
Saba: Watu wanapinga kuita kwa jina hilo pale wanapofahamu maana yake, na kinachopingwa na watu hiko ni baya.
Jibu: Ni kuwa kupinga watu kunakuja kwa sababu ya kulipa kwao uelewa na maana yao kuwa jina “Basmallah” lina maana ya jina la Mwenyezi Mungu na kuhuzunishwa na maana hiyo batili.
Kisha kupinga huku lau kungekuwa, basi hakuchukui watu wote, na kudai hivyo ni uwongo, na ama kusema kilichopingwa na watu ni kibaya haiwi isipokuwa upingaji huu ukiwa umefanywa na watu wa elimu, kwa sababu wao ndio ambao wanaozingatiwa kauli zao kukubali kwao na kupinga kwao, hawa ndio wanazingatiwa kwenye makubaliano ya Wanachuoni, na wala sio kuzingatiwa katika kuhusisha watu wakiwemo na wale wajinga, hivyo makubaliano ya Wanachuoni: Ni makubaliano ya wanajitihada katika Umma wa Mtume Muhammad S.A.W baada ya kufa kwake, ikiwa katika jambo miongoni mwa mambo ya zama katika zama. Badru Zarkashy amesema katika kitabu cha Bahri Al-Muhiitwu 6/380 chapa ya Dar Al-Kutuby akielezea: “Makubaliano ya wasio wasomi hakuna mazingatio kwa makubaliano yao wala kutokubaliana kwao”.
Nane: Kuita kwa basmallah ni miongoni mwa maovu haramu kwa kauli ya Mola Mtukufu: {Anawahalalishia vilivyo vizuri na kuwaharamishia vilivyo viovu}[ AL A'ARAF: 157].
Jibu: Dalili hii ni batili na nikuchezea Aya za Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwenye Aya hakuna dalili wala harufu ya dalili juu ya hilo, amesema Imamu Ibn Jarir Twabary katika tafasri yake ya [Jaamii Al-Bayan 13/165, 166 chapa ya Taasisi ya Risalah], wakati wa kutafasiri neno viovu vilivyotajwa katika Aya Tukufu: “Hilo ni pamoja na nyama ya nguruwe uzinifu na waliyokuwa wakihalalisha miongoni mwa vyakula na vinywaji ambavyo Mwenyezi Mungu ameviharamisha, kama alivyonizungumzisha Al-Mathnaa amesema: Ametuambia Abdillah Ibn Saleh amesema: Ameniambia Muawiyah kutoka kwa Ally, kutoka kwa Ibn Abbas: {Na kuwaharamishia vilivyo viovu} nayo ni nyama ya nguruwe riba na waliyokuwa wakihalalisha miongoni mwa yaliyo haramu katika vyakula ambavyo Mwenyezi Mungu ameviharamisha”.
Tisa: Ni kuwa kuita kwa jina la “Basmallah” ni katika uzushi wenye uovu.
Jibu: Ama kuita kilichotajwa ni uzushi ni ndio kwa sababu uzushi kwa upande wa lugha: Ni kilichofanyiwa kazi bila ya kuwepo cha mfano wake kilichopita, kila mwenye kuzusha kitu anakuwa ameleta uzushi. Angalia kitabu cha: [Jamharatu lugha cha Abi Bakri Ibn Dardir 1/298 chapa ya Dar Al-Elmu lil-Malayiin].
Ama kauli kuwa yenyewe ni uovu, wakati huo huo ni madai na wala si dalili, na kitu kuwa ni kiovu kipana zaidi ya kuwa kwake haramu, kwa sababu sifa hizi mbili zinakubaliana kwenye kuchukiza.
Kisha sio kila kilichozushwa ni haramu bali kilichokubalika kwa Wanachuoni ni kuwa uzushi kuna hukumu tano za Kisharia, wakati mwingine uzushi unakuwa ni wa lazima, na wakati mwingine unakuwa ni haramu, na wakati mwingine unakuwa ni Sunna, wakati mwingine unakuwa ni wenye kuchukiza na wakati mwingine huwa ni halali.
Sheikh Ezzudin Ibn Abdusalaam amesema katika kitabu chake cha [Kawaidi Al-Ahkaam 2/204 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Elmiyah]: “Huo uzushi umegawanyika sehemu tano: Uzushi ulio wajibu, uzushi haramu, uzushi ulio Sunna, uzushi unaochukiza na uzushi halali, na njia ya kufahamu hayo: Ni kuingiza uzushi kwenye kanuni za Kisharia, ikiwa utaingia kwenye kanuni za wajibu basi uzushi huo ni wajibu, na ukiingia kwenye kanuni za uharamu basi wenyewe ni haramu, ukiingia kwenye kanuni za Sunna uzushi huo ni Sunna na ukiingia kwenye kanuni za kuchukiza ni uzushi unaochukiza na ukiingia kwenye kanuni za halali basi uzushi huo ni halali”.
Kisha Shaikh anataja mifano ya kila sehemu na anasema: “Uzushi wa wajibu una mifano mingi wa kwanza: Kujishughulisha na somo la Sarufi (Nahwa) ambalo linafundisha kufahamu maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno ya Mtume S.A.W uzushi huo ni wajibu kwa maana ni wa lazima kwa sababu kulinda Sharia ni jambo la lazima wala kuilinda kwake hakuji isipokuwa kwa kuifahamu, na kisichotimiza wajibu mpaka kiwepo hiko, basi hiko kinakuwa ni wajibu. Mfano wa Pili: Kuhifadhi lugha ngeni ndani ya Qur`ani na Sunna. Mfano wa Tatu: Kuandika somo la misingi ya Fiqhi (Usuul Al-Fiqhi). Mfano wa Nne: Maneno katika elimu ya Hadithi ili kupambanua sahihi katika zisizosahihi, na kanuni za Sharia zimeeleza kuwa kuhifadhi Sharia ni jambo la lazima inayotosheleza na wala haiwezi kufanyika kazi ya kulinda Sharia isipokuwa kwa tuliyoelezea.
Uzushi haramu, una mifano mingi miongoni mwake: Ni madhehebu ya Qadriyah, pia madhehebu ya Jibriyah, pia madhehebu ya Marjiah, na pia madhehebu ya Mujsama na kuwajibu watu wa madhehebu haya ni katika uzushi ulio lazima.
Uzushi wa Sunna, mifano yake: Kujenga madaraja kujenga shule kujenga uzio mkubwa wa maji, pia kila jema lisilokuwepo zama za mwanzo, miongoni mwa mifano pia: Swala ya Taraweh, pia maelezo ya undani wa tasawufi, pia maneno katika mijadala kwenye mahafali ili kupata dalili ya masuala ikiwa kusudio ni Mwenyezi Mungu katika hilo.
Uzushi wenye kuchukiza, mfano wake: Kupamba Misikiti na Misahafu.
Uzushi halali mfano wake: Kupeana mikono baada ya Swala ya Alfajiri na Swala ya saa kumi, pia kuongeza ladha kwenye vyakula na vinywaji pia kufanya uzuri kwenye mavazi na makazi, kuvaa kanzu na kupanua mikono ya kanzu, kumekuwa na tafauti baadhi ya hayo, kwani baadhi ya Wanachuoni wamefanya ni katika uzushi wenye kuchukiza, na wengine wamefanya ni katika Sunna zilizofanyiwa kazi zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu na baada yake”.
Kwa ufupi sana:
Ama uwazi wa Hadithi aliyopokea Imamu Muslim kutoka kwa Jabir Ibn Abdillah R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Kila uzushi upotofu” ni kuwa kila uzushi ni wenye dhambi Kisharia, uwazi wake sio kusudio, amesema Imamu An-Nawawiy katika [Sharhu Muslim 7/104] kauli ya Mtume S.A.W: “Kila uzushi ni upotofu” hii jumla maalumu, na dalili ya hili ni pana lakini sio hapa, pia Hadithi iliyopokelewa na Muslim kutoka kwa Jarir Ibn Abdillah R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Mwenye kuzusha katika Uislamu jambo jema kisha likafanyiwa kazi hapo baadaye huandikiwa malipo sawa na aliyefanyia kazi wala hayapungui malipo yao hata kidogo, na mwenye kuanzisha Sunna mbaya katika Uislamu ikafanyiwa kazi hapa baadaye huandikiwa ubaya sawa na wale walioifanyia kazi wala hakipungui chochote kwenye ubaya wao”.
Imamu An-Nawawiy amesema kwenye Sharhu ya Hadithi: “Ndani yake kuna uhimizo wa kuanzisha mambo ya kheiri na kuanzisha Sunna njema na kuchukua tahadhari na uzushi batili na muovu…katika Hadithi hii inahusisha kauli ya Mtume S.A.W: “Kila jipya ni uzushi na kila uzushi ni upotofu” kusudio lake ni mapya yaliyo batili na uzushi mbaya”.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia: Tunaona kuwa mtoto kumpa jina la Basmallah ni jambo linalofaa Kisharia pamoja na kuwemo hali ya kuchukiza, lakini tunapenda kutoa nasaha kwa ndugu muuliza swali; kutovamia asiyoyajua wala kufahamu hakumu za Kisharia na ufafanuzi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu pamoja na Sunna za Mtume S.A.W bila ya kuwa na elimu, kwa sababu yote hayo ni kumsemea Mwenyezi Mungu bila ya kuwa na elimu, ni katika mambo makubwa yaliyo haramu kabisa, kwani Mwenyezi Mungu Anasema: {Sema: Mola Mlezi wangu ameharamisha mambo machafu ya wazi na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asichokiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyoyajua} [AL-A'ARAF: 33]. Na Akasema tena Mola Mtukufu: {Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali, na hichi haramu - mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa} [AN NAHL]: 116.
Vile vile tunampa nasaha kujipamba na adabu za kuuliza swali na kutaka ufafanuzi ikiwa ni pamoja na kuacha kujuajua kuheshimu na kutaka faida, imepokelewa na Abdulrazak katika [Tafasiri yake 3/234 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Elmiyah] kuwa Amiri wa Waumini Ally Ibn Abi Twalib R.A aliulizwa kuhusu tanziko au tatizo akamwambia muulizaji: “Ole wako uliza ili ufahamu wala usiulize kwa ubishi”.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas