Amani kama ni Msingi Miongoni mwa M...

Egypt's Dar Al-Ifta

Amani kama ni Msingi Miongoni mwa Misingi ya Kusongea Mbele katika Uislamu

Question

 Ni Nini Umuhimu wa Amani katika Uislamu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hapana Shaka yoyote kwamba Amani na Usalama wa Kimataifa kwa upande mmoja, na Kusonga mbele Kijamii na kukuza uchumi kwa upande mwingine – ni mambo yenye mfungamano mkubwa unaoathiri kila upande, na kinyume chake pia ni kwamba matumizi ya nguvu na Vita vina athari mbaya katika mwelekeo wa Kusonga mbele Kimaendeleo, na Maisha Mazuri ya jamii ya Kiislamu.
Na ili maana hizi ziwe wazi, tunaweza kuzitolea hukumu ya kuzikataa au kuzikubali, lazima kwanza tutaje maana ya maneno haya kwa lugha ya Kiarabu, ili yatuchoree picha kamili ya kweli ya Matamshi haya akilini, ili tupate nafasi ya kuyahukumu kwani kukitolea Hukumu kitu ni Sehemu ya kuleta taswira yake.
Basi Amani katika Kiarabu ni Usalama, na Usalamu ni jina miongoni mwa majina mazuri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Amani katika asili ni Usalama, Na kutoka huko Pepo inaitwa: Daru Salaam, kwani Pepo ni nyumba ya Amani isiyo na Mabaya. Na anasema Zajaaj: Pepo imeitwa hivyo kwa sababu ni Nyumba ya Amani ya kudumu isiyokatika au kwisha nayo ni Nyumba ya Kusalimika na Umauti, Uzee, na Magonjwa. Na Mwenye Afya Njema ni kama vile amekuwa na furaha ya Pepo kwa Amani yake.
Neno Vita Kilugha: Ni kinyume cha Amani. Na Upole katika lugha ya Kiarabu ni: Kinyume na Matumizi ya Nguvu. Na rafiki ni mswahibu kama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wapamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongonimwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!} [AN NISAA 69]. Matumizi ya nguvu Kilugha ni: Kinyume cha Upole.
Hizi ndizo maana za Maneno haya Manne: Amani, Upole, Vita, na Matumizi ya Nguvu, ambayo Maudhui ya Makala yetu itayazungumzia kwa kina kuhusu athari nzuri za Amani na Upole katika kusonga mbele kwa Jamii za Kiislamu, na pia Athari mbaya za vita na matumizi ya nguvu dhidi ya mwelekeo wa Wananchi wa Kiislamu katika kusonga mbele Kimaendeleo cha kiutamduni.
Hakuna shaka kwamba Uislamu uliagiza kwa kuimarisha ardhi, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na kina Thamud tuliwapelekea ndugu yao Saleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi}. [HUUD 61]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amejaalia kutekeleza Nyadhifa na Kazi mbalimbali wanazozihitaji watu katika maisha yao miongoni mwa yale yenye Hukumu ya Faradhi, na hakuyajaalia kuwa na Hukumu ya Halali au Yenye kukokotezwa, na wanachuoni wamekubaliana wote kwamba mgonjwa wa jamii ya Kiislamu, ikiwa hajapata Mganga wa kumtibu, basi Dhambi na Adhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu zitaifikia Jamii yote.
Na vilevile katika nyanja za Biashara na Viwanda, na kila kinacholeta utulivu katika Maisha ya Jamii ya Kiislamu, ni kufika katika viwango vya juu vya utoaji huduma za Jamii katika nyanja zote za maisha, kama vile kufikia viwango vya juu katika huduma za afya na mwili wake, na pia viwango vya juu katika Elimu, na viwango vya juu katika Usafirishaji na Mawasiliano, Kutosheleza maji ya kunywa, na mengineyo miongoni mwa mahitaji ya msingi, na hapana Shaka yoyote kwamba kufanya juhudi za kutosheleza huduma hizi kwa ajili ya kuihudumia jamii ni jambo la kulipwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu na ni jambo zuri la kusifiwa na viumbe vyote.
Na Ustaarabu wa Kiislamu umechangia kwa kiasi kikubwa cha kutosha katika kuleta maendeleo ya nyanja mbalimbali za Elimu, Tiba, na Mafanikio yaliyopatikana katika Ulimwengu wa kale na wa Kisasa, na Umma haukuachwa nyuma katika kwenda sambamba na Ustaarabu katika nyanja mbalimbali isipokuwa kwa sababu za vita vilivyoanzishwa dhidi yake na mkoloni mwenye tamaa za mali za umma, na maliasili zake, na mchakato wa kunufaika nazo kwa Viongozi wa Mwamko Mpya Nchini Ufaransa.
Na kuanzia hapo tunatambua kwamba Uislamu umehimiza juu ya Amani na Usalama, na Athari zake zenye umuhimu wa hali ya juu kwa Utulivu wa Maisha ya Watu na maendeleo yao kwenye nyanja zote, na ili tuelewe upeo wa athari za Usalama na Amani juu ya Maendeleo ya Mataifa, tunapaswa kutupia macho juu ya athari angamizi za vita dhidi ya Wananchi na Maendeleo yao Kusonga kwao mbele.
Kama isemwavyo: Kinyume hudhihirishwa uzuri wake na Kinyume, na hakika moja ya misingi ya awali ya Maendeleo ya Umma ni kutengemaa kwa Jamii kiafya na kimwili ili kutekeleza Nyadhifa zao, kwani tunapotambua kwamba vita na vikwazo vya kiuchumi vina athari mbaya mno kwa afya ya Mataifa na Uzima wake.
Kutokana na tafiti zilizofanyika, imedhihirika kwamba matukio haya yamesababisha vifo na ulemavu kuliko yale yaliyosababishwa na ugonjwa wowote miongoni mwa magonjwa makuu. Vita vimeziangamiza Jamii na Familia, na mara nyingi vilikuwa ni sababu kuu ya kusita kwa maendeleo ya msuko wa Kijamii na Kiuchumi katika Mataifa.
Athari za Vita na Vikwazo vya Kiuchumi zimesababisha kuleta madhara makubwa sana ya kimwili na kinafsi yenye athari za kudumu kwa watoto na wakubwa, na kupungua kwa mtaji wa mali na nguvu Kazi. Vilevile vikwazo vya Kiuchumi dhidi ya Mataifa vilikuwa na athari mbaya za kiafya, na mara nyingi vilizorotesha utendaji wa sekta ya Afya.
Vita Vikuu vya Dunia vya Kwanza vikipoteza Maisha ya Watu milioni 30, wakati ambapo Vita Vikuu vya Dunia vya Pili vilipoteza maisha ya watu milioni 54.8, ukiongezea na mateso makubwa ya kibinadamu na maelfu ya mabilioni ya hasara ya vitu mbalimbali na Dunia nzima kujihusisha kwa njia moja au nyingine na Vita hivyo na Mapinduzi na Ukosefu wa utulivu, na baadhi ya nchi bado zinaendelea kutawaliwa kikoloni mpaka sasa mazingira yetu kama vile Palestina, Iraki, na kama ilivyo katika Jamuhuri ya Sovieti ya zamani, na Yugoslavia na Afghanistan na nyinginezo nyingi.
Hakika Vita vinaangamiza maisha na uchumi unaporomoka, na vilevile huzuia matarajio ya kibinadamu katika kujiletea maisha ya furaha kwenye mazingira salama, ukiongezea na uchafuzi wa mazingira na kiasi kikubwa cha matumizi ya rasilimali ambazo lazima zitumike katika kuupiga vita umasikini na kuleta maendeleo endelevu.
Na kuhusu athari za Uchafuzi umetokea na hakuna ubaya wowote kuusema, kwani katika Nchi ya Marekani, kuna maeneo 21401 yaliyochafuliwa kwa kiwango kikubwa mno ukiwemo uchafuzi kwa mionzi mikali iliyosababishwa na ulipuaji wa mabomu 1800 ya nyukilia katika maeneo mbalimbali Ulimwenguni katika hatua za majaribio, robo ya mabomu hayo yalilipuliwa angani. Na uzalishaji wa Silaha unazalisha asilimia 95 ya uchafu wa maada zenye kiwango kikubwa cha sumu na asilimia 78 ya maada zenye mionzi mikali ya kati na ya chini yenye sumu kwa maana ya: kiwango kinacholingana na trilioni 1.4 za sarafu ya Kori, na hii ni sawa na mara 28 ya ongezeko la mionzi iliyosababishwa na Ajali ya Chernobyl ni sawa na sarafu ya Kori (milioni 50).
Na yote haya yanatokea katika mazingira ya kawaida ya Mafunzo bila ya Kutokea vita, na tuangalie kidogo Urithi tulioachiwa na Vita Baridi: Mabilioni ya fedha yalitumika katika Mashindano ya kumiliki silaha, na Mabilioni mengine lazima yatumike katika Uteketezaji wa Silaha hizi hatari zilizozidi, kiwango kikubwa cha mabaki hatari ya kivita ambayo lazima sumu yake iteketezwe kisha nayo pia yateketezwe.
Na kuna maeneo mengi mno yasiyohesabika ambayo udongo na maji yake vimechafuliwa kwa sumu yanasubiri kuandaliwa na kusafishwa, na mrundikano wa silaha zilizozidi za kizamani zinakongolewa kwa njia inayokubalika (salama) kwa mfano Nchini Ujerumani pekee Kiasi cha mzigo wa silaha 5000 zilizoteketezwa na majeshi ya Urusi na Marekani na Jeshi la Ujerumani ya Mashariki ya zamani, kiwango cha fedha cha kuziteketeza silaha hizo kinakadiriwa Mark trilioni moja.
Hakika Vita zimeacha hasara kubwa mno ya Maisha ya Watu na mateso makubwa kwa waliojeruhiwa na waliosababishiwa ulemavu, pamoja na kupungua kwa maadili Mema, na kuongezeka kwa Uvurugaji wa Imani na Maadili, na athari hasi kwa watu na mazingira inapindukia kwa kiasi kikubwa mno faida alizozipata mshindi wa Vita.
Yote haya na mengine mengi yanatufanya tuwe na uhakika kamili ya kwamba – sisi Waislamu na Ulimwengu unaotuzunguka – tuna haja kuu ya kuwa na Amani na Usalama zaidi kuliko wakati wowote mwingine, kwani hakuna njia nyingine yoyote ya kuleta Maendeleo yanayotakiwa na ambayo ndio lengo la Serikali zote Ulimwenguni, isipokuwa kwa njia ya Amani, na kwamba athari za Vita moja tu zinatosha kuuchelewesha Umma mamia ya miaka, ukiongezea na kusimama kwa umma bila ya kusonga mbele katika hiyo miaka yote.
Vita na Gomvi tangu zamani, Ufisadi na Umwagaji damu, vilikuwa ni sababu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu, na hii ilikuwa Kazi ya Msingi ya Dini zote za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Dini hizo zilifanya kazi ya kumwokoa Mwanadamu na Kiza cha ujinga, na kuingiza Imani na Utulivu katika nyoyo za Watu, kutokana na mafundisho yake na mwenendo wa Waumini, Kwa kuwa Dini ina athari kubwa kwa Mwenendo na Fikra pamoja na Hisia, Athari hii imeonekana wazi katika Urithi wa Kiislamu kama ambavyo inaweza kuonekana pia kupitia kuathirika kwa Kiwango kikubwa sana cha maisha ya kila siku ya Waislamu. Kwani Uislamu ni Mfumo wa Maisha na Ahadi ya Utukuzo na ni Mfumo wa Kanuni unayoyagusa maisha ya mwislamu kwa pande zake zote.
Uislamu Mtukufu umekiwa kwa Watu ili uwatoe katika Udikteta na Ujeuri, na kuwashika mkono watu na kuwapeleka katika Uadilifu na Usalama, sio kuwatupia katika mapotevu ya Mabavu na Matumizi ya Nguvu ambayo hakuna anachokipata kutokana nayo isipokuwa Maafa na Mateso. Na wito wa Dini ya Kiislamu kwa ajili ya Usalama na Amani vya Kimataifa uko wazi. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwawalimwengu wote} [AL ANBIYAAI 107]
Na katika ubainishaji huu wa Qur’ani Tukufu yenye Maana pevu, aliyoiweka Mwenyezi Mungu Mtukufu, Maana ya kuhabarisha, hii Habari iliyopambika kwa Mbinu maalumu Zuifu na Fupishi, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anazuia kila malengo yanayokisiwa. Wenye shaka kwamba yeye S.A.W alitumwa kwa ajili yake, na Mtu yeyote atakayedhani kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimtuma Mtume S.A.W, kwa ajili ya kuua watu au kupora ardhi na mali, au kwa ajili ya umwagaji damu – Mwenyezi Mungu Mtukufu amemuepusha na kumkinga – basi mtu huyu atakuwa na dhana potovu na hatafanikiwa huo uovu mchafu anaoutarajiwa anaposoma aya hiyo.
Bali kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ameagiza kwa Amani na kuingia ndani yake kwa njia wazi katika kitabu chake kitukufu: {Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwaukamilifu, wala msifuate nyayo za She'tani; hakikayeye kwenu ni adui aliye wazi} [AL BAQARAH 208]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua} [AL ANFAAL 61].
Na katika Sunna vilevile Wito wa Uislamu kwa ajili ya Amani uko wazi. Kutoka kwa Ammaar R.A. kwamba Mtume S.A.W., amesema: “Mambo Matatu ambaye aliyakusanya, basi ameikusanya Imani: Kutoa huku ukiwa na Shida. Kujifanyia Uadilifu na Kueneza Amani Ulimwenguni” .
Na kuenea kwa maneno ya kwamba Uislamu umeenea kwa Upanga, na kwamba Uislamu unalingania vita na Vurugu, na inatosha kujibu hali hii kwa kuangalia na kulinganisha Uadilifu na Utoaji wa haki sawa alioamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutochanganya mambo, na Kuusaka ukweli kama ulivyo, na kutowazulia mambo wengine. Ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema katika kitabu chake tukufu: {Enyi Watu wa Kitabu! Mbona kweli mnaivisha uwongo,na kweli mnaificha na hali mnajua?} [AAL IMRAAN 71].
Na kwa kulinganisha unyama wa kivita uliotajwa, Umwagaji damu na Uharibifu mkubwa, na Uangamizaji wa Nchi na Watu kutokana na Vita vya Maadui – tunakuta kwamba Sira ya Mtume Mteule S.A.W, ni safi haina tuhuma hizo bali hatua zake za Kijeshi zilifikia vita zinazokaribia themanini, ndogo na kubwa, na zote zilikuwa kwa sababu ya kuondosha dhuluma na ukandamizaji na kujibu mashambulizi ya adui, na haikutokea vita hasa katika hatua hizi zote isipokuwa katika maeneo saba tu katika Sira yake Mtume S.A.W, alipokuwa analingania Uislamu.
Na utakuta matokeo ya kushangaza katika maeneo hayo, na miongoni mwake: Wapiganaji wote walikuwa wanatokea kabila la Mudhwar, watoto wa Baba yake Mdogo S.A.W., na hakuna yoyote aliyepigana naye akitokea katika kabila la Rabiia au Kahtwaani, na kwamba idadi ya Waislamu waliokufa vitani ni 139, na Washirikina 112, na wote kwa ujumla ni 251, na hii ni idadi ya vifo vinavyosababishwa na ajali za magari katika mji wenye ukubwa wa kati kwa mwaka mzima, na kwa hivyo, Idadi ya vifo katika hatua zote hiyo themanini ni 3.5 ya watu.
Hili ni jambo la kuchekesha pamoja na jinsi Waarabu walivyoumbwa na nguvu pamoja na ukaidi katika vita iwe hiyo ndio sababu ya kuingia kwao Uislamu na kubadilisha Dini yao; jambo ambalo linathibitisha kwamba Uislamu ulienea baada ya hayo kwa njia ya kawaida haihusiani na Upanga au Kulazimisha, bali ni kwa Kuishi kwa familia baina ya Waislamu na Wasiokuwa Waislamu, na kwa njia ya Uhamiaji ulioandaliwa kutoka ndani ya Eneo la Hijazi (Makah na Madina) na kusambaa Duniani kote.
Na zipo hakika kuhusu ueneaji huo endapo inabainika kwamba katika miaka mia ya kwanza kutoka Hijrah, kiwango cha ueneaji wa Uislamu kilikuwa nje ya Ghuba ya Kiarabu kama ifuatayo: Katika Uajemi kiwango cha ueneaji wa waislamu ndani yake kilikuwa asilimia tano, na katika Iraq asilimia tatu, na katika Sirya asili mia mbili, na katika Misri asilimia mbili, na katika Andalosi asilimia chache ya moja,
Ama miaka ambayo kiwango cha ueneaji wa waislamu kilifika asilimia 25 kutoka wakazi nchini ni kama ifuatayo: Uajemi mwaka wa 185 kutoka Hijra, Iraq katika mwaka wa 225 kutoka Hijra, Sirya katika mwaka wa 275 kutoka Hojra, Misri katika mwaka wa 275 kutoka Hijra, Andalosi katika mwaka wa 295 kutoka Hijra.
Na miaka ambayo kiwango cha ueneaji wa waislamu kilifika asilimia 50 kutoka wakazi nchini ni kama ifuatayo: Uajemi mwaka wa 235 kutoka Hijra, Iraq katika mwaka wa 280 kutoka Hijra, Sirya katika mwaka wa 330 kutoka Hojra, Misri katika mwaka wa 330 kutoka Hijra, Andalosi katika mwaka wa 355 kutoka Hijra.
Ama miaka ambayo kiwango cha ueneaji wa Waislamu kilifika asilimia 75 kutoka wakazi nchini ni kama ifuatayo: Uajemi mwaka wa 280 kutoka Hijra, Iraq katika mwaka wa 320 kutoka Hijra, Sirya katika mwaka wa 385 kutoka Hojra, Misri katika mwaka wa 358 kutoka Hijra, Andalusia katika mwaka wa 400 kutoka Hijra.
Vilevile utagundua kwamba Ueneaji huo wa Uislamu umekuwa pia na sifa za kipekee, na miongoni mwazo: Kutoyaangamiza Mataifa, na kuwatendea watumwa wema ulio juu kihadhi baada ya kuwasomesha na kuwafundisha kazi na kuwapatia majukumu ya Uongozi katika kipindi kilichojulikana katika Historia ya Uislamu kama Kipindi cha Mamaaliik, na kubakisha mfumo wa Dini nyingi za Uyahudi, Ukristo, na Umajusi ambapo tunakuta Uhundukia upo kama ulivyokuwa hapo zamani na Dini za Kusini Mashariki ya Asia vilevile.
Na kupitisha Uhuru wa kufikiri na usikuzoeleka kwamba wao waliweka Mahakama na Ukaguzi wa yeyote katika Wenye Maoni Kinyume na yao, vilevile palikuwepo Uadilifu katika kugawa utajiri wa nchi ambazo ziliingia katika Uislamu, na hakika Eneo la Hijazi ambalo ni chanzo Kikuu cha Ulinganiaji wa Kiislamu liliendelea kuwa masikini mpaka ulipokuja ugunduzi wa petroli katika hizi zama za kisasa.
Wengi wasio Waislamu wameushuhudia Ukweli huu katika zama hizi mpya, kwa mfano Mwanafikra “Lord Hedly: anashangazwa na jinsi Mtume S.A.W, anavyowafanyia Mateka wa Kishirikina katika vita Kuu ya Badri, akigundua ndani yake uwepo wa kilele cha Maadili Mema ya Usamehevu na Mtangamano mwema wa Ukarimu.
Kisha anajiuliza “Je hii haimaanishi kwamba Muhammad hakuwa na wasifu wa roho ngumu na kiu ya damu, kama wasemavyo wagomvi wake? Bali daima alikuwa anajitahidi kuzuia umwagikaji wa damu kiasi awezavyo, na Ghuba ya Kiarabu yote ilikuwa chini yake, na akatembelewa na ujumbe wa Najraani kutoka Yemeni ukiongozwa na Padri, na hajawahi kujaribu kuwalazimisha waingie katika Uislamu, kwani hakuna kulazimishana katika Dini, bali aliwawekea Usalama wa mali zao na maisha yao, na akaamrisha wasisumbuliwe na yoyote juu ya Imani zao na Ibada zao za Kidini.
Mwanafalsafa wa Kifaransa (Walter) anasema: Hakika Sunna zote alizokuja nazo Mtume Muhammad S.A.W, zilikuwa zote za kuushinda moyo na kuufundisha, na Uzuri wake uliifanya Dini ya Uislamu ipendwe mno na kutukuzwa kwa kiwango kikubwa, na kwa ajili hii, watu wengi wa Mataifa mbalimbali walisilimu, wakiwemo Waafrika walio katikati ya Afrika, na wakazi wa Visiwa vya Bahari ya Hindi.
Kwa upande wa Msomi wa Kimarekani (Michael Hart) yeye anayarejesha mafanikio ya Mtume S.A.W, katika usambazaji wa Ulinganiaji wake na kasi ya kuenea kwa Uislamu Duniani inarejea katika Usamehevu wa Dini hii na Ubora wa Maadili ya Mtume S.A.W, ambaye Mwenyezi Mungu Mtukufu alimchagua aongoze Watu Mia moja miongoni mwa Watu Mashuhuri walioacha ya wazi Ulimwengu katika Historia ya Binadamu, na anasema: “Hakika Muhammad ndiye Mtu pekee katika Historia ambaye alifanikiwa bila kikomo katika nyanja za Dini na za Kilimwengu, na akaja kuwa Kiongozi wa Kisiasa na Kijeshi.
Na huyu hapa Thomas Karliel anasema katika kitabu chake cha “Mashujaa na Kuabudu Ushindani” anasema: "Hakika kumtuhumu Bwana Wetu Muhammad" kwamba aliutumia upanga katika kuwalazimisha watu waukubali wito wake ni jambo lisilo na maana yoyote na halieleweki kabisa; kwani si katika yanayojuzu kiakili mtu mmoja autumie upanga wake kwa ajili ya kuangamiza watu, au wamkubali yeye, na watakapomwamini wale wenye uwezo wa kupigana vita na maadui zao, hakika walimwamini kwa kumtii na Kumwamini kweli na wakapigwa vita na wengine kabla ya wao kuwa na uwezo wa kupigana nao.
Na Mwandishi wa Historia wa Ufaransa Ghostaf Lorbon, katika Kitabu chake cha Ustaarabu wa Kiarabu – akizungumzia siri ya kuenea kwa Uislamu katika zama zake na katika zama za Funguzi zilizokuja baadaye, anasema: “Historia imethibitisha kwamba Dini hazilazimishwi kwa nguvu… na Qur’ani haikuenea kwa Upanga, bali ilienea kwa Ulinganiaji pekee, na kwa Ulinganiaji huo watu wengi waliingia katika Dini wakiwa wamewazidi Waarabu kwa nguvu kama vile Waturuki na Wamongolia.
Na katika kuenea kwake, Qur'ani ilifika mpaka India ambako waarabu hawakuwemo isipokuwa kama wapita njia tu jambo ambalo liliongeza idadi ya Waislamu na kufikia milioni hamsini ndani yake”. Na kwa kumalizia tunasisitizia Unyeti wa Amani na Usalama kama Msingi muhimu miongoni mwa Misingi ya kuleta Maendeleo katika Jamii za Kiislamu.
Na katika hitimisho tunatarajia kuwa tumewafikishwa katika kuionesha fikra hii, na vilevile kuondosha Shubha ya kukinzana baina ya Uislamu, Amani na Usalama, au Shubha ya kuenea kwa Uislamu kwa Upanga.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu na kwa Mtume wake S.A.W, twaomba kupitia yeye, Mwenyezi Mungu ayajaaliye masiku yetu yote yawe amani na salama, na Waislamu wasonge mbele katika kila nyanja za maisha, na mwisho wa Maombi yetu tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa viumbe vyote.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Rejesho: Kitabu cha: [Sematu Al Aswer] kwa Mheshimiwa Mkuu Mufti wa Misri Dkt. Ali Juma

Share this:

Related Fatwas