Mawazo ya Kiislamu Kati ya Kuenea n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mawazo ya Kiislamu Kati ya Kuenea na Kutoenea

Question

 Ni vipi kuenea na kutoenea kwa mawazo ya Kiislamu?

Answer

 Sifa zote njema ni za Allah pekee, na swala na salamu ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya jamaa zake na maswahaba zake, na juu ya wale wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Moja ya asili ya vitu ni kwamba harakati za kimawazo zilizo katika hatua ya baadaye ambayo ni tajiri kuliko harakati za kimawazo katika hatua iliyotangulia, na nadharia hii inathibitishwa kama njia ya maisha ya umma itakuwa ya kisiasa, kiuchumi na kistaarabu inayoyaelekea maendeleo. Ikiwa harakati za kimawazo zinairejea awamu ya baadaye zaidi kuliko awamu iliyopita pamoja na mtiririko muafaka mwingine wa maisha katika mwelekeo wake wa juu, basi lazima kuwe na msingi mbaya ambao ulisababisha mabadiliko haya.
Mzingativu wa harakati za mawazo wa Kiislamu anatishwa na kile anachokiona kutokana na kutoenea kwa mawazo hayo bila haki, pamoja na kupatikana kwa uwezo wa kimawazo, kisayansi na kiufundi katika kiwango ambacho hakikupatikana katika awamu zilizopita.
Nyuma ya jambo hili lazima kuwe na mambo ya kurudisha nyuma ambayo yanazuia maendeleo ya fikra na kuzuia uzinduzi wake. Mawazo ya Kiislamu mara nyingi huonekana kuwa mawazo ya kuridhika na kujiuzulu, mawazo ambayo hayatafuti harakati za bidii au harakati za kuhangaisha, au ni mawazo yasiyoshikiliwa na hukumu zake za mwisho, na hayawezi kudumisha mazungumzo pamoja na mwingine. Wakati mawazo ya Kiislamu lazima yaweze kuziibua chemchemi za kielimu, dhana za mizizi, na kutamani nadharia..
Inaonekana kati ya waanzilishi wa mawazo ya Kiislamu ya kisasa kwamba kila mmoja wao alikuwa sauti ambayo yeye mwenyewe hataki kuwa sauti iliyokaririwa, au mwangwi wa sauti moja au inayorudiwa rudiwa, na kwa hamu hii wote waliweza kuunda mzunguko kamili unaoongoza kuanzia mwanzo hadi mwisho. Vivyo hivyo, ndivyo mawazo ya Kiislamu yanavyopaswa kuwa katika wakati huu. Mawazo ya Kiislamu katika harakati zake lazima yawe na sifa ya ujumuishaji na mawasiliano, ili isibaki kuwa majaribio ya binafsi tu.
Marejeleo: Fi Al-Fikr Al-Islami Minal Wajahtil Adabiyaah, na Dk. Muhammad Ahmad Al-Azab, Cairo: Baraza Kuu la Utamaduni, 1983 BK, (uk. 114-121).

Share this:

Related Fatwas