Maswali Mapana na athari yake katik...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maswali Mapana na athari yake katika kutatua baadhi ya Matatizo ya Kifikra

Question

 Ni kipi kinachokusudiwa kwa neon Maswali Mapana, na ni ipi atahri ya vidokezo vyake katika kutatua baadhi ya Matatizo ya Kifikra?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hakika sisi tunamaanisha maswali mapana kwa Swali la kwanini baada ya kila jibu la swali lililopita, huku tukihangaikia kwa hilo kufichua ukweli wa vitu, na kutafiti misingi na asili yake.
Kwa hivyo, Nyanja za Elimu ya Tauhidi inayatiba Masuala mbalimbali ya Kifalsafa kwa maana yake iliyozoeleka, kwani ndani yake kuna jibu la tafiti za Uwepo na Ukosekanaji, na kuhusu Maarifa, na kuhsu tafiti za Maadili vilevile. Elimu hii inazungumzia asili ya Uwepo na tabia za vitu na inabainisha Ukweli wakena ulivyo pamoja na asili yake na jinsi ya kufikiri na hatua zake, na inazungumzia Masuala Makubwa kama vile Upwekeshaji katika Haki ya Mwenyezi Mungu na Masuala ya Ujenzi wa Ulimwengu na Utakasaji wa Nafsi, lakini pia kuhusu Sehemu ya Maadili kama vile masuala ya Uadilifu, Tshsiin na Taqbiih (Kukifanya kitu hukumu ya Uzuri na Ubaya) kwa kutumia akili na mengine mengi kama yajulikanavyo.
Na kwa njia yoyote tunaweza kuanzia juu ya (Maswali Mapana) tunajikuta sisi kwa mfano tunapokuwa katika Masuala ya Usuulul Fiqhil Islaamiy na kwa kuufuatili ule mnyororo wake – runahamia katika Nyanja za Elimu ya Tauhidi.
Mwanachuoni wa Usuuli anapozungumza kwa mfano kuhusu sababu ya kuharamishwa pombe: Ni kwanini Mwenyezi Mungu aliiharamisha pombe au kwa sababu ipi Mwenyezi Mungu aliiharamisha Pombe? Jibu lake linakuja kwamba yeye Mwenyezi Mungu aliiharamisha Pombe kwa sababu maalumu ya kuwa na kilevi ndani yake, na hiki ndicho ambacho Wanachuoni wa Usuul wanakiita Sababu ya Hukumu hiyo, kwani hiyo kwa wao: "Ni wasifu ulio wazi unaodhibitika na unakusanya maana inayoendana na Uhsaria wa Hukumu kwa upande wao".
Na jibu hili tunaweza kulipa Sababu ya Kwanza, kasha Mwanachuoni wa Usuuli anauliza: ni kwanini Kilezi kimekuwa Wasifu unaonendana na Uharamishaji? Na anajibu: Ni kwa kuwa Kilezi huondosha akili, na Kuilinda akili ni katika Makusudio Matano MAshuhuri ya Kijukumu, nayo ni: Kuilinda Nafsi, Kuilinda Akili, kuilinda Dini, kuilinda Hesima na kuilinda Mali.
Na tunaweza kulipa jina Jibu hili katika hatua hiyo kama ni Sababu ya Sababu, au Sababu ya pili; kwa sababu ni jibu la Swali la Pili lililozalika kutokana na Swali la kwanza.
Kasha maswali yanapanika kwalo katika sura ya mnyororo na kwa kufuatana na anauliza: Kwanini kuondoka kwa akili kukawa kunahukumia katazo?
Na jibu linakuja kwamba Akili ndiyo inayopelekea kukalifishwa, na kukalifishwa kunakuwa kwa ajili ya kulifikia lengo la Mwenyezi Mungu kutoka kwa Viumbe vyake, na kwa hakika Ufunuo umetuambia ya kwamba lengo la Mwenyezi Mungu kwa Viumbevyake ni kumwabudu yeye Mwenyezi Mungu na kuijenga Duni: anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na sikuwaumba Majini na WAtu isipokuwa waniabudu}( ). Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Yeye ndiye aliyekuumbeni katika ardhi na akakuwekeni humo}( ). Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Mimi nitamweka katika ardhi mfwatizi}( ); Tunajikuta katika ngazi hii miongoni mwa ngazi za majibu ya Maswali Mapana yanayofululiza na tumehama na kuelekea katika Masuala ya Elimu ya Tauhid, na tunaweza kuliita hilo jibu kama sababu ya sababu ya Sababu, au sababu ya tatu.
Na hapa kuna tanabahisho juu ya Uzuri katika mazuri ya maneno ya Wanachuoni wa Fiqhi na wa Usuul ambapo wanazungumzia kuhusu kwamba Hukumu Fulani haina Sababu isipokuwa ipo kwa ajili ya Ibada, na tunakuta Wanachuoni wa Fiqhi wanatofautiana na baadhi yao wanaona kuwa Hukumu Fulani ina sababu, na baadhi yao wanaona kwamba haina sababu bali ni ya kiibada, na tunakuta kwamba wao wanataja sababu ya hukumu, kisha wanarejea na kuipa wasifu wa Ibada, na tunawakuta wao wanasema kwa kuziwekea Hukumu sababu, na kwamba wao wanasema pia ya kwamba hukumu za Mwenyezi Mungu haziwekewi sababu.
Na kwa kuifahamu nadharia ya Maswali mapana Ukinzani unafunguka katika Sura hizi zote; ambapo kushindwa kuleta wasifu wa wazi unaodhibitika juu ya maana inayokubalika kiakili inaendana na Usharia wa Hukumu kwake, kwa namna ambayo katika kujibu Swali hakibakii isipokuwa kwamba Mwenyezi Mungu ameamrisha, na hapana budi kufuata maamrisho yake – huu ni uhalisia wa kuabudu.
Kwa mfano Udhu ( ) kwa Jinsi unavyojulikana, hatuwezi kujibu swali la: Kwanini viungo hivi kwa namna hii na kwa njia yake ambayo ndani yake kuna mpangilio wa mambo yajulikanayo kwa lengo la kufikia kwayo kisichojulikana (nao ni ukweli wa Fikra) ( ), na kutokea hapo, hakika ya Udhu ni suala la kiibada moja kwa moja.
Wakati ambapo Imamu Malik hakuweza kujibuSwali la Kwanini katika suala la kukiosha mara saba Chombo kilicholambwa na Mbwa, moja yake ni kwa mchanga, akaliweka jambo hili katika upande wa Ibada ( )
Na akajibu Shafi kwamba huo ni mpangilio wenye kuonesha ukubwa wa najisi ya mbwa ( ) kwa namna ambayo udenda wake unakuwa najisi kali zaidi kuliko zingine na hakuna jibu lenye maana iingiayo akilini la swali hili jambo ambalo linamaanisha kutimiza Ibada kwa sababu ya pili, kwa maana ya: katika kulijibu swali la pili.
Na tofauti baina ya Wanachuoni wa Fiqhi ni katika kuharakisha jibu kwa kutekeleza Ibada juu ya maswali mapana.
Na tunawaona wakitofautiana katika sababu ya kuharamishwa kwa Riba kwa kiasi cha njia kumi, kisha tunamwona Sheikh Jamal katika Haashiya yake( ) akisisitiza ya kwamba sababu ya kuharamishwa kwa Riba ni ya Kiibada, na kuweka wazi jambo hilo kunakwa kwa kuweka kila jawabu la hatua miongoni mwa hatua za Maswali mapana, na kwa hivyo inadhihirika wazi kwamba tofauti zao katika kuziwekea Hukumu sababu zimekuja kwa mpangilio huu, kwani Hukumu zina sababu katika Majibu ya maswali ya kwanza; kwani yenyewe yanawekewa sababu ya kuabudu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu {anafanya atakalo} ( ), {na wala haulizwi kwa yale ayadanyayo} ( ) katika majibu ya maswali ya hivi mwishoni.
Na bila ya kusema kwamba kuleta kwetu istilahi ya sababu ya kwanza na ya pili na mfano wake hakuna uhusiano wowote na zile zilizotulizana katika Elimu nyingine kama vile Elimu ya Tauhidi na Elimu ya Nahau na kadhali, bali huu ni uitaji unaoendana na maana za fikra ambazo tunataka sisi kuzihamishia kwa msomaji, na ni muhimu katika mfano wa utafiti wetu huu tubainishe ya kwamba Istilahi katika kipindi cha kufikiri inapaswa iwe nyambuliko ambayo tunaitumia kuona fikra kupitia istilahi hiyo bila ya sisi kuangazia istilahi zilizokubalika ili tuweze kuibadilisha, au kuleta neno lolo kuihusu istilahi hiyo, mpaka ikubalike kwa Wanachuoni wote. Na jambo hili katika sifa zake kuanzisha Fikra kwa ajili ya kubuni kwa kufuata misingi yake, na hilki ni jambo tulilolikosa kwa kukosa kwetu sifa maalumu za zama za Kujitahidi Mwanzoni.
Na vilevile kutokana na jambo hili, zinakuja tafiti za kufafanua akili, Uwajibishaji na je kitendo kina sifa zake chenyewe, na je amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu inabebesha jukumu kwa utashi wake? Na kuna tofauti gani baina ya Utashi wa Kisharia na Kilimwengu? Na je inafaa kubebesha majukumu yasiyobebeka? Na je, inafaa kufungamanisha Amri na Kisichokuwepo? Na je huku ya zamani inafungamana na tukio? Na je amri ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake yanakuwa kwa sababu na hekima fulani? Na je sababu za Kisharia zina maana ya Mtumaji na Mlinganiaji? Na je, kila mwenyekujitahidi anapatia?
Ns je, Mtume S.A.W, anajitahidi? Na je, Hukumu ya Mwenyezi Mungu inaongezeka idadi yake kwa kuongezeka watu na jitihada zao? Na je, dalili zinaendana na zinakuwa sawa? Na mengine mengi yasiyokuwa hayo katika yale Mwanachuoni wa Usuul anayoyatafiti kama utafiti wa Kiusuul, na anahitaji Falsafa ya Kiislamu mahitaji ya kimsingi.
Na hebu tuzichukue katika maudhui hizi mfano, nao ni: Suala la Mtume S.A.W, kujitahidi, linaonekana limeibuka katika Fikra za Kiusuli kwa mujibu wa yaliyoibuliwa katika Falsafa ya Arestoto ya kwamba Mwanadamu anapokuwa na njia mbili mbele yake, moja ni ya kukata shauri na nyingine ni ya kukisia katika kujiatia maelezo fulani, je, inafaa kwake apite katika njia ya kukisia pamoja na kuwa kwake na uwezo wa kupita njia ya kukata shauri?
Kisha masuala haya yakawa katika Usuul, na huko likaibuka swali kuhusu kujuzu kujitahidi kwa Mitume na kutojuzu kujitahidi kwao; kwani Mtume anaweza kupokea hukumu kupitia Ufunuo au Wahyi, nao ni Mkato wa Shauri, na anaweza kuifikia hukumu kwa kuigundua na hii ni njia ya kukisia, na kutokana na suala hili, pakazalika suala jingine jipya ambalo nalo ni kwamba yeye Mtume S.A.W, je, anaweza kukosea katika kujitahidi? Na Jamhuri ya Wanachuoni ikachagua ya kwamba, Mtume hakosei mpaka Bin Sabkiy akasema katika kitabu chake cha Al-Ihbaaj ( ); ((na mimi ninakiepusha kitabu changu kwa kusimulia ndani yake kauli kinyume na kauli hii))
Wakati ambapo Ibnul Haajib ( ) amechagua kinyume na hivyo kwa sharti la kutoipitisha, na akajaali kukupitishwa kwake au kunyamaziwa ni hukumu ya kusihi kwake.
Hakika haya Maswali Mapana kama tulivyoyasherehesha, yanabainisha vyanzo vya elimu yoyote na yanaonesha pia uhusiano wa Elimu hiyo na Elimu zingine, na pameamuliwa kwa Wanachuoni wa Usuli kwamba Usuulul Fqhi ni Elimu inayotokana na Elimu tatu ambazo ni: Elimu ya Tauhidi, Elimu ya Lugha, na Fiqhi ya Kiislamu, na hii inamaanisha ya kwamba upanuzi wa Maswali Mapana unarejeshwa katika moja ya Elimu hizi tatu wakati wa kuyapitisha kwake. Na hivi ndivyo inavyowezekana kupitia nadharia ya Maswali Mapana kutatua matatizo mengi ya Fikra ambazo zinamwelekea Mwanadamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Vyanzo na MArejeleo
1) Al-Ibhaaj liaali Sabkiy (Takiyu Din Ali bin Abdil Kaafiy Sabkiy Shaafiiyu, alifariki mwaka wa 756h, na mwanae Taaju Diin Abdul Wahaab bin Ali Shaafiy, aliyefariki mwaka wa 771), kilichohakikiwa na Dr Shaabani Ismaili, chapa ya Vitivo vya Awali vya Azhar, Mwaka wa 1401/1981.
2) Al-Ihkaamu Fii Usuulil Ahkaam, cha Aamidiy (Seifu Diin Abi Hasan Ali bin Abi Ali bin Muhammad Shaafiiyu, aliyefariki mwaka wa 631h.
3) Albahrul Muhiitw, cha Zarkashiy (Badru Diin Muhammd bin Mahaadir bin Abdillah Shaafiiy, aliyefariki mwaka 794h), Daarul Kutubiy, ch.1 mwaka wa 1414/1994. Na ch. Wizara ya Mambo ya Wakfu ya Kuweit, ch.1 mwaka wa 1419/1988.
4)Bayaanul Mukhtaswar, Cha Aswfahaaniy (Shamsu Diin Mahmuud bin Abdil Rahmani Shaafiiy, aliyefariki wwaka wa 749h), Uhakiki wa Dkt Muhammad Mudhhir Bakaa, ch. Chuo chha Ummul Quraa, Makatul Mukarramah, ch. 1 mwaka wa 1406/1986.
5) Atabswirah cha Shairaaziy (Abuu Ishaaka Ibrahim bin Ali Shaafiiy, aliyefariki mwaka wa 476h), Uhakiki wa Muhammad Hitu, Daarul Fikri Damascus, 1400h/1980.
6) Haashiyatul Jumal (Suleiman bin Amru bin Mansouril Ajiiliy Azhariy Shafii, aliyefariki mwaka wa 1204h) juu ya Sharhul Manhaj cha Sheikhul Islaam Zakariyyahl Answaary (Abu Yahyaa Zakariyya bin Muhammd bin Ahmad bin Zakariyyal Answaariy Saniikiiy Maswriyu Shaafii, aliyefaariki mwaka wa 926h) ch. Atijaariyatul Kubraa, 1375h
7) Mungnil Muhtaaj, Sharhul Minhaaj, cha Khatwiibu Sharbiiniy (Shamsu Diin Muhammd bin Ahmadl Qaahiriy, aliyefariki mwaka mwa 977h), chapa ya Mustafal Halabiy, 1377/1958.
8)Muntahaa Sauli wal Aml Fii Ilmil Usuuli wal Jadal, cha Ibnul Haajib (Abuu Amru Othmaan bin Omar Nahwiy Maalikiy aliyefariki 646h) chapa ya Alsaada, 1326h.
9) Mawaahibul Jaliil fii Sharhi Mukhtaswari Khaliil, cha Hatwaab (Muhammd bin Muhamma bin Abdil Rahman Raiiniy, aliyefariki mwaka wa 954h), Maktabatu Najaah, Libya, ch. Ya kwanza, dt.
Chanzo: Usuulul Fiqhi wa alaaqatuhu bil Falsafatil Islaamiyah. Cha Mheshimiwa Mufti wa Misri, Profesa Ali Juma.

Share this:

Related Fatwas