Uhuru wa Maoni na Unavyotumika Viba...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uhuru wa Maoni na Unavyotumika Vibaya – Sura Chafuzi kama Mfano.

Question

Hivi karibuni pamejitokeza Sura zinazomkashifu Mtume wetu, Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. je, huu ni uhuru wa maoni? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ni muhimu tukazungumzia tofauti kati ya Uhuru wa Maoni na Uhuru wa Kujieleza, na uhusiano wake na Msingi wa Demokrasia, na kwa Uislamu.
Sio Dini peke yake tofauti, na Akili tofauti na Historia tofauti, na Utamaduni tofauti, bali pia Uchukuliaji wake nao ni tofauti. Na tunaona kwamba kuna umuhimu mkubwa mno wa kuufungua mlango huu, na sisi tunatoa wito wa kujenga madaraja ya mazungumzo na maelewano kati ya Wanadamu, na kwamba tofauti hizi katika lugha ya mazungumzo na katika Mieleweko mbalimbali zinazingatiwa kuwa ni kizingiti kikumbwa kinachobomoa kila tunachokijenga na kinatupunguzia mwendo kila tunapoanza safari yetu na kinatuvurugia lengo tunalotaka kulifikia.
1- Kitabu cha Demokrasi nchini Marekani, nacho ni katika hazina na Mwandishi Alex Tocqueville na kimetafsiriwa na kuwekewa maelezo na: Mwalimu Amiin Mursii Kindiil, chapa ya Aalamul Kutub, na kilichapishwa mara tatu nay a mwisho ilikuwa mwaka wa 1991, na Ufasiri huu ni wa chapa ya kumi na sita, uliyotayarishwa na kuwekewa maelezo na Andrey Jain na kilibahatika kitabu hiki kutolewa na Dkt Muhsin Mahdii, Mwalimu wa Masomo ya Kiarabu katika chuo Kikuu cha Havard na ni kitabu muhimu mno; mwandishi alikiandika kmwanzoni mwa karne ya kumi na tisa kwa lugha ya kifaransa, na kikachapishwa nchini Marekani mwaka wa 1862 kwa lugha ya Kiingereza, kisha kinaonekana kusambazwa mpaka leo hii; na kwa hivyo ni katika vitabu vya msingi sana vinavyoelezea mizizi ile tunayoitafuta kwa lengo la kuelewa lugha nyingine, na vijenzi vya akili yake, nalo ni jambo la lazima ili kuweza kuchambua Yaliyomo na kuyasoma matukio, na muhimu zaidi katika hayo ni jinsi ya kushughulikia.
Na kitabu hiki kimenikumbusha vile vile vitabu vingi vya msingi ambavyo tunalazimika kuvisoma baada ya sisi kuwa katika kijiji kimoja, au katika bahari moja tunayahisi sote kwa pamoja mawimbi yake sawasawa na kiwango kimoja.
2- Katika kile kitabu anasema: Hakika msingi wa demokrasia ni kuuhangaikia usawa, na hakika jambo hili linasababisha tatizo kubwa linalowaandamana makuhani wa demokrasia na walinganiaji wake pamoja na uhuru na maana yake, kwani kuna uhuru wa maoni na imani, na kuna uhuru wa kujieleza, na kwamba uhuru wa maoni na imani umehifadhiwa kwa kila mtu tangu yaanze madhehebu ya Wafanyabiashara, na maneno ya Adamu Smith: mwache afanye mwache apite, na hakika haya yanahukumia suala hilo, nalo ni lile ambalo hatuoni sisi ubaya wowote katika Dini ya Uislamu, ambayo imeupitisha uhuru katika sura zake nzuri zaidi na ukachelewesha kuhesabiwa kwake hadi siku ya Kiama, na wala sio katika Maisha ya Duniani, anasema Mwenyezi Mungu:{Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye na aamini. Na atakaye na akatae}
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hapana kulazimishana katika Dni. Kwani Uongofu umekwisha pambanuka na upotofu} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mnwenye kumtii Mtume basi ndiyo amemtii Mwenyezi Mungu. Na anayekengeuka, basi sisi hatukukutuma wewe uwe mlinzi wao}.
Ama kwa upande wa uhuru wa kujieleza huo utakatana na Itikadi za wengine kwa upande mmoja, na Usawa kwa upande wa pili, iwapo hili ni tatizo la makuhani wa demokrasia tangu mwanzo wa karne ya kumi na tisa, na cha kushangaza ni kwamba tatizo hili bado lipo na sisi tuko katika karne ya ishirini na moja.
Ingawa wao walipitisha maazuzi ya wazi katika vitabu vyao wakasema: Hakika kuna aina mbili za Uhuru: aina ya kwanza inakataliwa, nayo inauona uhuru wa kujitoa katika vidhibiti vyote, kwa namna ambayo mtu anaweza kufanya kila kitu akitakacho, nalo ni jambo ambalo linaugeuza mkusanyiko wa kibinadamu na kuupeleka katika fujo kubwa isiyofikirika, ukiachana na kuikubali kwake. Na aina ya pili ya Uhuru: inaona kuwa Uhuru ni Uongozi kuwa huru na kujitegemea na Uhuru wa kujieleza kwa namna inayoendana na Jamii, na kufuata vidhibiti vyote ambavyo jamii imekubaliana navyo; kama vile vidhibiti vya kidini, kimaadili na kimila na desturi, mambo ambayo jamii yote kwa ujumla inarekebishana kwayo. Na uhuru kwa mtazamo huu unaelekeza kana kwamba wenyewe ni uso mwingine wa majukumu, na kabla mtu hajajua kwamba yeye ana uhuru anajua kwamba yeye ana majukumu ya uhuru huo na mambo ya kuchagua, kauli na vitendo mbali mbali mbele ya Jamii yake anamoishi.
Na kwa ajili hiyo tunaona ya kwamba uhuru wa mtu ni katika mahitaji ya Jamii ya Kibinadamu kusimama imara, na hasa kwa kuingiliana masilahi na tofauti ya matamanio ya nafsi, na uhuru unaendelea kuwa na maana yenye kikomoinayotofautiana kwa kutofautinana upande ambao unatazamiwa kwayo, hata kama upeo wake utaainishwa na ukapewa wasfu maalumu – wa kisiasa, kiuchumi, au kidini.. na kuendelea – uhuru unaweza kukusudiwa kutoka katika mfungamano maalumu kwa maana ya kisiasa, au uhuru kwa kukusudia lengo maalumu kwa maana ya Jamii.
3- Baada ya gazeti la Dermark kuteleza na kuksambaza matusi yaliyoenezwa dhidi ya Bwana wa Ulimwengu huu, tumeona gazeti la Norway linafanya hivyo hivyo, kasha Ufaransa, kwa madai ya kwamba wanataka kulipima jambo hili, lakini wameliweka kwa njia ya kijinga mno, na sio kwa ile njia aliyoizungumzia Alexstokville, mwenye asili ya Ufaransa katika kitabu chake kilichoashiriwa.
Na hili linatuonesha ya kwamba Utulivu na Unyoofu wa Kufikiri vimeondoshwa kwa wanasiasa waropokaji, nayo ni alama katika alama za Zama hizi, na tunamwomba Mwenyezi Mungu atuhurumie katika hilo.
4- Uhuru wa kujieleza kwa Wanachuoni wa Kiislamu ni Uhuru wa kuwajibika, haijuzu kuvishambulia vitakatifu vya wengine na hata kama hao wengine wanaaudu masanamu. Anasmea Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msiwatukane hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua.}
Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Na waja wa Arrahmani Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea Ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na tulipofunga agano na wana wa Israili: Hamtamwabudu yeyote isipokuwa Mnwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi na jamaa na mayataima na masikini, na semeni na watu kwa wema, na shikeni Sala na toeni Zaka. Kisha mkageuka isipokuwa wachache tu katika nyinyi; na nyinyi mnapuuza.}.
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika katika hayo zipo ishara kwa waaguzi. Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini}.
Na aya hizi lazima ziwe msingi wa kuushughulikia mgogoro huu; kwani ni ishara za Mwenyezi Mungu Mtukufu zenye kinga yake kwa Matamanio, Kuponyoka, Mapungufu na Kuzembea, na sisi tunapaswa kuzizingatia, na tuweze kutoa ndani yake Msingi wa namna ya kuendesha Migogoro yetu.
Na ushahidi ni huu ambapo matukio machungu yametuthibitishia usahihi wa mtazamo wetu wa ulazima wa kutoa Msingi wa kuendesha Migogoro yetu, na hapa tunajionea watu wanaozichoma balozi katika mapinduzi ya kihisia kali yaliyowajibisha kutolewa kwa nyudhuru kutoka kwa baadhi yetu, na katika hili, ongezeko la ukubwa wa suala letu haufichikani, na kuzembea mafanikio yoyote yale kunaweza kupelekea tukawa tumefikia katika hali hiyo ndani ya miezi kadhaa.
Na tuelekee kwa mara nyingine sisi sote tuyavuke haya matukio ya kusikitisha; kwa sababu sisi katika ukweli, tunaangalia Mbele na tunataka kuasisi Idara ya Migogoro inayokusanya jaribio la kutoangukia ndani yake katu, na kuizuia kabla ya kutokea kwake.
1- Kufikiri kimantiki kunatufanya tuisome hali iliyopo na tujaribu kuangalia sababu za mgogoro huu kwa uadilifu, na ninatarajia ya kwamba neno hili la uadilifu halipiti kwa sura ya kupita tu bali ni moja kati ya vinavyoijenga akili ya Mwislamu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndiyo kuwa karibu mno na uchamungu. Hakika Mnweyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda}
2- Na Mtume S.A.W anasema: {Anza na nafsi yako wewe, kisha wale unaowalea}
Na anasema Mtume S.A.W: {Mmoja wenu ataona kibanzi katika jicho la nduguye, na anasahau gogo katika jicho lake} , na sisi tutaanza kwanza kukiona kibanzi katika jicho la mwingine kasha baada ya hapo tunahamia kwenye gogo la mtende ambalo limo kwenye macho yetu.
3- Mitaala ya Elimu ya nchi za Magharibi inaichafua sura ya Uislamu na Waislamu, iwe katika Historia ya Kiislamu, Sharia, Akida, Uhalisia au katika Vyanzo vya Uislamu, kwa sura ambayo inazalisha chuki kwa watoto wadogo wa kimagharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu, na Profesa Abdul Jawaadi – Mwenyezi Mungu amrehemu – akiwa na mjumuiko wa tafiti, alidurusu sura hizo zinazouchafua Uislamu na Waislamu, moja baada ya nyingine na chuo kikuu cha Collin nchini Ujerumani, kikamchapishia miaka ya themanini mpaka mwanzoni mwa miaka ya tisini, nazo mpaka sasa zipo na zinazuzwa masokoni, kasha akazifanyia ufupisho wake kwa lugha ya kiarabu, na utafiti huu wa kielimu unaotokana na uhalisia unaweza kutegemewa katika kuitaka Magharibi na Umoja wa Ulaya ziwajibike kusahihisha Sura ya Uislamu na Waislamu kaitka mitaala ya kielumu ya Magharibi, na vivyo hivyo itafanyika Marekani kasha katika nchi zingine Duniani.
Usahihishaji huu umefanyiwa kazi pevu ya majaribio kadhaa lakini hayakufanikiwa; jambo lililopelekea kuimarisha zaidi sura chafu katika akili za Wamagharibi, nalo ni jambo linalokiuka Mikataba yote ya kimataifa ya Haki za Binadamu na Sheria zote za Kimataifa ambazo zilikwishatulizana juu ya kutombagua mtu kwa rangi, kabila au dini yake, na Uhusiano wake ulisimama juu ya Msingi wa Uhuru wa Akida, Kazi, Kuhama na Uhuru wa kujielezea.
3- Na katika vibanzi vilivyomo machoni mwao ni baadhi ya sheria mbovu ambazo zinawazingira Waislamu katika Itikadi zao au Ibada zao, nay a mwisho yake ni ile iliyotokea Ufaransa kuhusu suala la Hijabu, na lazima wito utolewe wa kusafisha Sheria hizi; kwani zinaenda kinyume na Katiba za nchi hizi, na usafishaji huo uwe kwa njia ya kuchukua hatua za kisheria na za kisiasa katika Nyanja hizi.
4- Na kuhusu hali ya Denmark, maada ya 140 inasema hivi: {Katika hali ya mtu yoyote kuyakejeli au kuyadhihaki hadharani mafunzo au misingi ya mtu yoyote ya kidini inayotambulika rasmi, mtu huyo tatozwa faini au atahukumiwa kifungo kinachoweza kufikia miezi mine}
Vilevile kifungu cha Sheria namaba 266 b kinasema: (Katika hali ya mtu yoyote kusambaza au kutaka kusambaza jumla moja au kauli inayotishia au kuchafua sifa au inalitusi kundi miongoni mwa watu kwa misingi inayogusa asili, rangi, uraia, mizizi ya asili yao, imani zao au uraia wao, tatozwa faini au atafungwa kifungo kinachoweza kufikia miaka miwili)
5- Wakati wa utoaji wa adhabu, sifa ya taasisi iliyosambaza itazingatiwa kama moja ya sababu za kuzua fitina.
6- Kwa hivyo, waislamu wakaipeleka kesi yao kwa mahakimu wa Denmark katika ule mgogoro wa michoro, na Hakimu akakataa kuisikiliiza, na hakika yeye anafanya hivyo kutokana na moja kati ya mambo mawili; la kwanza ni kwa kuwa yeye hautambui Uislamu kama ni Dini, na hilo ni jambo linaloenda kinyume na Hali ya Denmark, au la pili inaweza kuwa anaukana Uadilifu, nalo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Kwa hivyo lizingatie hilo.
7- Na vilevile miongoni mwa vinavyounda kibanzi katika macho yao ni suala la Kuzitenga na Kuziweka pembeni Jamii za Kiislamu, nalo ni kinyume na suala la kuunganishwa kijamii na ni jambo lenye mapana na marefu na linafaa kufanyiwa utafiti, na Ubaguzi wa rangi unandani yake, wakati ambapo kwa upande mwingine, utamaduni wa waislamu una nafasi hasi.
8- Na katika vibanzi pia ni kibanzi cha kutoruhusu sehemu au nafasi yoyote kwa vyombo vya habari kuwapa nafasi Waislamu wajitangaze, kama walivyopewa kitu kama hicho – angalau kwa sura ya uchache – nchini Australia, ambako Waislamu waliruhusiwa kuanzisha Magazeti na Idhaa mbali mbali, na kuwa na nafasi kadhaa katika uwanda wa Habari kwa njia zake zote zinazowawezesha kujielezea, na jambo hili linawaandaa kwa ajili ya mchakato wa kuchanganyika na jamii, na linayaondosha matatizo mengi yanasababishwa na Kasumba na Ubaguzi wa rangi.
Hakika idadi ya Waislamu nchini Denmark ni zaidi ya Wadenmarki laki mbili, baadhi yao ni wadenmarki wa asili na wengi wao ni Wahamiaji, na kwa mujibu wa kumbukumbu za Azhar Shariif – tangu mwaka wa 2002 mpaka mwishoni mwa mwaka wa 2005 – katika nchi ya Denmarki peke yake, walisilimu zaidi ya watu arubaini wakiwa ni wadenmarki wa asili, na hii ni idadi kubwa sana kwa nchi ambayo idadi ya wakazi wake haizidi milioni tano.
9- Waislamu wanatakiwa kujinasua na mtihani huu, kwa mhamo wa aina yake unaopelekea maisha yao yawe katika sura ya kushiriki zaidi katika Ustaarabu wa Kibinadamu, na kwa Mbele yenye utulivu na usalama zaidi kwao na kwa Ulimwengu mzima, na kwa ajili hiyo – na kupitia kufikiri kwa akili ya kimantiki – wanapaswa wao kuzitumia njia zote walizonazo, na tuyakumbushe mashirika ambayo hivi sasa yanafanya majaribio ya kimataifa kwa ajili ya kuweka sheria na maamuzi ili kuwalinda Waislamu kutokana na mashambulizi, kwa namna kipengele cha sheria namba 20 cha Azimio la Umoja wa Mataifa la haki za kiraia na kisiasa kinasema: inakatazwa – kwa mujibu wa kanuni – kila wito wa chuki za kitaifa, kibaguzi au za kidini, na ambao unaweza kuleta uchochezi wa ubaguzi wa rangi au vurugu>>
Kamati kuu ya Umoja wa MAtaifa imethibitisha katika Maamuzi yake namba 59 (d -1) ya tarehe 14 Disemba mwaka wa 1946, kwamba: “Moja ya vipengele ambavyo havikwepeki kwa ajili ya uhuru wa Habari ni kuwepo kwa Idara na Uwezo wa kutotumia vibaya na kuwajibika kimaadili kwa kuchcunguza uhalisia bila ya uchochezi, na kusambaza Maelezo bila ya ubaya wa kusudio”. Hiki ndicho kibanzi, kwa hakika kibanzi hiki inahitaji kazikubwa, na je, gogo la mtende lililopo machoni mwetu ni lipi. Na tulichojifunza kutokana na Dini yetu ya Kiislamu ni kwamba Uislamu ni Wito wa Kimataifa, na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na hatukukutuma isipokuwa kwa watu wote, uwe mtoaji wa habari njema na mwonyaji. Lakini wengi hawajui} Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema: hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Je! Mmesilimu?
Na maana ya hayo yote ni kwamba sisi ni umma wa Ulinganiaji, na hali ya Ulinganiaji ni kuufikisha kwa sura inayoyavutia macho, na kuuonesha kwa watu, kwa masharti yaliyowekwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu; na la kwanza katika masharti hayo ni: Uhuru wa Akida na kutoilazimisha, na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na sema: Hii ni kweli kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye aamini na atakaye akatae},( )
Na anasema Mwenyezi Mungu: {Nyinyi mna dini yenu na mimi nina Dini yangu}. ( )
Na anasema Mwenyezi Mungu: {Hapana kulazimishana katika Dini. Kwani uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu } ( )
Na anasema Mwenyezi Mungu: {Wewe si mwenye kuwatawalia} ( ) Na anasema Mwenyezi Mungu: {Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye}. ( )
Na anasema Mwenyezi Mungu: {Na wakipuuza basi sisi hatukukupeleka ili uwe mwangalizi wao. Si juu yako isipokuwa kufikisha Ujumbe tu}. ( )
Na miongoni mwa masharti ya Ulinganiaji ni kwamba Ulinganiaji huo ufanyike kwa Hekima na Busara. Na anasema Mwenyezi Mungu: {Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hekima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora} ( )
Na miongoni mwa masharti ya Ulinganiaji ni kwamba Ulinganiaji huo uwe kwa mwono, Na anasema Mwenyezi Mungu: {Sema: Hii ndiyo njia yangu – ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua – mimi na wanaonifuata} ( )
Na miongoni mwa masharti ya Ulinganiaji ni kwamba Ulinganiaji huo uwe wazi unaonekana. Na anasema Mwenyezi Mungu: {Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha – nazo ni hoja zilizo wazi na uwongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni – hao anawalaani Mwenyezi Mungu, na wanalaaniwa kila wenye kulaani} ( )
Na Mwenyezi Mungu akajaalia kuficha uhsahidi na Uongofu ni katika madhambi makubwa yanayopelekea uvurugaji wa Dini, na adha pamoja na madhara kwa viumbe; na kwa ajili hii laana ya Mwenyezi Mungu imekuwa wajibu, kwa dalili ya kwamba hiyo ni katika madhambi makubwa, na laana ya wenyekulaani ambao wanaidhinisha hivyo katika maisha ya Duniani. Lakini kutokana na rehma za Mwenyezi Mungu Mtukutu aliye takasika ni kwamba amefungua mlango wa kurejea na kurudi kwake kwa ajili ya kurekebisha: Na anasema Mwenyezi Mungu: {Ila wale waliotubu na wakatengeneza na wakabainisha, basi hao nitapokea toba yao, na Mimi ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu} ( )
10- Mgogoro wa Denmark unafichua kwamba sisi tumezembea katika kuidhihirisha Dini yetu kwa sura ya kuvutia machoni, na jambo hili linatulazimu juhudi kubwa kielimu na kiulinganiaji, juhudi ambayo inapindukia ile tuliyo nayo kwa sasa kwa sura ya kimzizi. Katika Chuo Kikuu cha Azhar, na Mwenyezi Mungu ashukuriwe yeye Mola wa viumbe vyote, pameasisiwa kitivo cha lugha mbalimbali na Ufasiri, na wamehitimu wengi miongoni mwa vizazi mbalimbali lakini sisi tunahitaji ongezeko zaidi la mwelekeo huu kwa kuzituma jumbe kutoka Azhar Sharif kuelekea Magharibi, na sisi kuzipokea jumbe mbalimbali nalo ni jambo ambalo Chuo cha Azhar imekuwa ikilifanya.
11- Kuchangamsha mchango wa hawa wahitimu wa kutoka katika Vitivo hivyo ili wakavitumikie vituo vya kiislamu nje ya nchi, pamoja na kuwapatia fursa ya maisha katika nchi hizo katika hali endelevu; kwani lugha ni kama viumbe hai haipatikani na haikui isipokuwa kwa kuitumia kwa muda mrefu na kuishi nayo; na kuyaangalia mambo ya ndani ya akili zao na namna ya kuzungumza nao, na hapana budi pawepo na hali ya utulivu kwa maimamu hawa wanaowakilisha ndani ya nchi hizi kwa kuangalia hali yao kabla ya maneno yao ya Uislamu, na mara nyingi huwa tunawapeleka hawa maimamu kisha tunawaondosha baada ya miaka mine au mitano, na huo ni muda usiotosha kutangamana na kutekeleza vizuri kama tutakavyo.
Kuna ulazima wa kuanzisha Kituo cha Ufuatiliaji ambacho kazi yake itakuwa ni kufuatilia na kuchambua kila kinachoandikwa na kuchapishwa na kutangazwa kuhusu Uislamu katika nchi za nje kwa lugha mbalimbali, na kukijadili pamoja kuandaa taarifa iliyo wazi kuhusu masuala hayo na kutoyaacha mambo yarundikane mpaka yafikie kiwango cha kulipuka, na kuanzisha chaneli ya kimataifa kwa lugha ya kiingereza hasa, linaweza kuwa jambo muhimu mno, nalo ni jambo ambalo mpaka sasa halijatimia kwa sura inayoendana na zama hizi tunazoziishi.
12- Tunataka kufanya mikutano endelevu ya mazungumzo na ambayo wataitwa waandishi wa habari na vyombo mbali mbali vya habari kutoka kila sehemu, na patazungumziwa istilahi na sura za kiakili ambazo zinazouchukia Uislamu na waislamu kwa kile kinachoitwa (Chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia).
13- Kutengeneza Mitaala bobezi na tafiti za juu kwa ajili ya kudurusu tofauti ya Kistaarabu baina ya Mashariki na Magharibi, na kuipendekeza kwa ajili ya mazungumzo pamoja na taasisi zote za Kifikra, Kihabari, Kichuo na Kiutamaduni na kutoyazingira hayo upande wa kiakademia tu.
14- Kuchangamsha Makubaliano yaliyopo baina ya Chuo cha Azhar na vyuo vingine mbalimbali pamoja na taasisi za kimataifa, nayo ni mengi – Alhamdu lillaah – lakini yanahitaji kazi na juhudi zaidi.
15- Kuanzisha vituo vya Ufasiri na Uchapishaji kutoka na kwenda katika lugha ya Kiarabu, ili kusoma yaliyotolewa katika Urithi wa Kiislamu, vijenzi vya akili ya Mwislamu na namna ya kunufaika na na Urithi wa kibinadamu, na kuwasiliana baina yetu na baina ya Zama hizi – na hasa hasa katika Nyanja za tafiti za kielimu – na kubainisha maadili ya utafiti huu na mtazamo wa Kiislamu juu yake, na namna ya kuhamisha teknolojia kwa kugundua na kubuni, na sio kwa kutumia na kuiga, pamoja na kulinda utambulisho wakati huo huo,; na haya ni mambo ambayo yanahitaji kufikiri zaidi, na uboreshaji zaidi kanuni na kuongeza ushiriki wa kiutendaji zaidi.
Je siku moja tunaweza kuona jarida kwa lugha ya kiingereza linalosambazwa kimataifa ambalo ndani yake tunawashereheshea watu kuhusu Waislamu ni akina nani, katika historia yao na katika uhalisia wao na pia katika Itikadi zao?
Mpango huu unatugharimu kiasi gani cha fedha? Kazi hii inahitaji kiasi gani cha kikosi kazi chenye uwezo wa hali ya juu katika bobezi mbali mbali? Hakika kushughulishwa na mpango huu badala ya upuuzi mwingi tunaouendeleza, na katika mielekeo ya kifikra na sura zilizomo katika akili za waislamu wengi kuuhusu huu huu Uislamu – tunahitajika kuwa na mabadiliko ya kimsingi na mageuzi ya njia ya kufikiri na katika masuala yaliyopo ambayo yanaishughulisha akili ya Mwislamu na ambayo Dini imepotoshwa ndani yake? Tunalazimika kuwahi hivi sasa pamoja na hizi nukta chache kwamba gogo la mtende liko machoni mwetu, au ile kauli ya Imamu Shafi imetusema kweli pale aliposema:
Tunaziabisha zama zetu na hakika sisi ndio wenye kasoro
Na zama zetu hazina kasoro isipokuwa sisi
Na tunazishutumu zama hizi bila ya kuwa na hatia
Na lau zama zingetamka, basi zingetushutu
Na mbwa mwitu hali nyama ya mwenzake
Na sisi tunakulana wenyewe kwa wenyewe
Au hwenda tukawa tumeingia katika kauli ya Mutanabbi aliposema:
Je, lengo la Dini ni kufunga ndevu zenu
Enyi Taifa lililochekwa na mataifa kwa ujinga wake
Migogoro ya aina hii inahitjai Uongozi uliozinduka, tunaweza kuuzungumza kwa manrno machache, kasha tukafafanua ndani yake baadae; ni kuutambua uhalisia kwa jinsi ulivyo, Hekima katika kuyashughulika Mambo haya, na kuyazingatia Makusudio na Malengo, na kunufaika na Mgogoro kwa yale yajayo baada yake, na kuzuia usitokee tena, na kujipatia mazingira mapya kutokana na hali hiyo; ili mtihani uwe tunu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
Chanzo: Kitabu cha Simaatul Aswri, cha Mufti wa Misri, Dkt. Ali Juma

 

Share this:

Related Fatwas