Uhalisia - Namna ya Kuudiriki na Vinavyoujenga na Jinsi ya Kuishi nao.
Question
Mara nyingi sisi huwa tunataja katika maneno yetu ibara isemayo ((Kuudiriki Uhalisia)), je ni upi huo Uhalisia? Na vitu gani vinavyoujenga? Na tunaishi na vipi kwa sehemu zake ndogo ndogo na kubwa kubwa? Na ni ipi misingi ambayo Mwislamu kwa sifa ya ujumla na Mwanachuoni kwa sifa Maalumu anaweza kuichunga na ili aweze kuitumia katika kuudiriki?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hakika sisi tunaishi katika zama ambazo zimebadilika mno katika mfumo wa maisha ya mwanadamu ukizilinganisha za zilizopita, na zimekuwa na ugumu zaidi na kasi na maendeleo, na inawezekana ikawa katika baadhi ya pande zake zinaporomoka zaidi, na hapana budi kwa Muumini mwenye mwerevu atambue nafasi yake, na azijue zama zake.
Maana hii imepokelewa katika Sunna za Mtume S.A.W; na kutoka kwa Wahab bin Munabbih kutoka katika Hekima ya Jamaa wa Daudi: Mwenye akili anatakiwa kutojishughulisha katika masaa manne: Saa moja ni ya kunong'ona na Mola wake, na saa moja ni ya kujitathmini, na saa moja ni ya kuwa na ndugu zake wanaomwamini na kasoro zake, na kumnasihi kwa hali yake, na saa ya vilivyo halali kwake na vizuri, hakika saa hii ni msaada kwa masaa mengine, na kuzistarehesha nyoyo na wema pamoja na kujitosheleza. Na mtu mwenye akili anatakiwa asiwe mkali isipokuwa katika mambo matatu: kujiandaa na Akhera, au kujikimu kimaisha au kujiburudisha na visivyo haramu. Na mtu mwenye akili anatakiwa azijue zama zake, aulinde ulimi wake na ayaelekee yanayomuhusu. (1)
na tuyazungumzie hayo kwa mtazamo jumla juu ya uhalisia, kwa Alama za Zama hizi, na tutajaribu katika suala hili kugusia jambo hili la uhalisia kwa kupendekeza na kushughulikia pamoja na kunufaika na pande mbalimbali za kheri, na kujaribu kujiepusha na Shari, na kujaribu kuulinda utambulisho wa Ulimwengu wenye mawimbi makali ujulikanao kama ulimwengu wa Mac, nacho ni kipande cha kwanza cha maneno mengi yaliyozagaa katika utamaduni wa Zama hizi kama vile: (MacDonald, McKintosh na Microsoft) na ambayo yanaonekana kama alama ya maendeleo na mageuzi katika chakula, ufundi na mawasiliano.
1- Uhalisia kwa mujibu wa uchambuzi wa Malik bin Nabiy, una aina nne za Ulimwengu: Ulimwengu wa Vitu, Ulimwengu wa Watu, Ulimwengu wa Matukio, na Ulimwengu wa Fikra mbalimbali. na kila mmoja kati ya aina hizi nne za Ulimwengu una vinavyoujenga, na kila mmoja una njia yake maalumu ya kutangamana nao, na mfumo tofauti wa kuufahamu.
2- Kwa hivyo, Ulimwengu wa Vitu una uhalisia wake unaopaatikana kwa hisia za kawaida, na una uhakika wake unaofikiwa na mwanadamu kwa darubini, na kisha akauwekea hukumu zake na mfumo wake ambao ni mfumo wa kufanya majaribio waliouridhia Waislamu, kisha ukahamia katika Ulimwengu wote bila ya kukanwa na wenye akili ambao walijikomboa kutoka katika akili za ngano za kale na wakashikamana na Elimu pamoja na Uhalisia, na baadhi yao walifupishia hapo, bila ya kufungamanisha na Mwenyezi Mungu Mtukufu, fikra yake ikawa ya kina zaidi lakini haiangazi ipasavyo, bali bila ya kuhisi kwamba amekanusha sehemu ya ukweli ambayo ni muhimu katika yaliyomo, nayo ni kumwamini kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu Muumba wa Ulimwengu wote.
Na tunaweza kuufafanua Uhalisia kama ni: Ni ule alioudiriki Mwanadamu kwa hisia zake za kawaida, nao kwa maana hii kuna kiasi cha ushirikiano baina ya Adamu na Mtu wa zama hizi. Wakati ambapo jambo hilo hilo linalohusiana na uhakika wa vitu linatofautiana jinsi mwanadamu anavyolidiriki kupitia nyakati, na kwa mujibu wa kiwango kikubwa cha maelezo aliyonayo, na mwanadamu analigundua kwa njia ya vyombo - kama Darubini - hatua kwa hatua, kwani mwanadamu analiona Jua likitembea angani, wakati ambapo Jua hilo hilo limetulia na Dunia ndiyo inayolizunguka Jua.
Na katika jambo hilo pia ni kwamba Maji yaliyochanganyika na gesi yanawaka moto, na hicho cha pili kinasaidia maji kuwaka moto, kwani huo ni Moto wa Mwenyezi Mungu uwakao, na kwamba haidrojeni inajengeka kutokana na chembe na ilektroni moja tu, na chaji ya elektroni ni hasi, na uhalisia ni kwamba maji ni kinywaji kizuri kinachotegemewa na maisha ya mwanadamu. Kila siku - na wala sio kwa sura ya ujumla kwa Muda Sehemu na Watu - kwamba mtu anaudiriki ukweli mpya unaowez kwenda kinyume au unapindukia uhalisia.
kama Jambo liko hivyo, basi hakika Maandiko ya Kisharia yanapaswa kuhusishwa na uhalisia katika lengo lake kuu kwa wote na kwa sura ya asili, na wala hayahusiani na jambo hilo hilo isipokuwa kwa sura ya pili, na ninahisi ya kwamba kufahamu huku kunatatua ((Tatizo la Elimu na Dini)), lililoanza pale mgongano wa Maandiko ya Ufunuo yaliyovurugwa ulipojitokeza katika nchi za Magharibi pamoja na Ukweli unaofuatana na tambuzi kwa kufanya majaribio na kwa kuhisi, kwa maana ya kwamba: ((Tatizo la Dini na Elimu)) kama lilivyoitwa.
Bali utangulizi huu unaweza kutatua - unaponyambuliwa kwa mapana zaidi - tatizo baina ya Wanachuoni wa Fiqhi na wa Sufi wanaouzungumzia ukweli na kwenda kwake kinyume na Sharia, na jaribio la kupatanisha baina yake, nalo ni jambo linalofaa kutajwa kwa kuzingatia zaidi Tafiti.
3- Na Ulimwengu wa Watu umeendelea pia, na pamekuwepo Utu wa Kimaumbile, Utu wa Kimazingatio ambao haukuacha kuendelea kujitenga na ule Utu wa Kimaumbile, na kuwa huru mpaka kujitenga kwake kukakamilika na ukawa ni kiumbe kinachojitegemea chenyewe, kina hukumu zake zinazotofautiana na zile na Utu wa Kimaumbile; ambapo ndani yake hakuna nafsi inayotamka maneo na inayohitaji hisia na upendo, na inaogopewa kwa maadili mabaya na tabia chafu, na kutangamana na aina hii ya Utu wa Kimazingatio kunakaribia kuwa maudhui iliyo mbali na Dhati ambayo imeathiri masuala mengi katika kutangamana na Mtu wa Kimaumbile.
4- Kwa upande wa Matukio, yenyewe yanajengeka kutokana na mwingiliano wa Vitu mbalimbali na Watu, na vinahitaji uchambuzi wa yaliyomo na kuelekea katika makisio ya Siku za Usoni na kuelekea katika kudhibiti na kuelekeza katika baadhi ya nyakati, na kuelekea katika kujua Matokeo ya baadaye, na kuleta Masilahi, kupangilia Vipaumbele na kuchukua hatua za kuvitekeleza kwa mujibu wa Wakati.
5- Na kuzihusu Fikra, hapana budi pawepo Kigezo kinachotumika kutathmini kinakubali kilicho kizuri na kukikataa kilicho kibaya, na kigezo hiki kinafungamana kwa Waislamu na Mfumo wa Maarifa wanaoufuata, na ambao wameuchukua kutoka katika Qurani na Sunna na Uelewa wa Maswahaba wa Mtume S.A.W, na Jaribio la Kihistoriaa, Akida,Mtazamo Mkuu wa Mwanadamu,Ulimwengu na Maisha, na Misingi ya Qurani na Alama za Mwenyezi Mungu na mfumo wa Maadili, na Makusudio ya Sharia katika uwekaji wa Sharia, Utoaji wa Majukumu, na kila kipengele miongoni mwa vipengele hivi kina maana na mijengeko yake katika Vigezo vinavyozinyoosha Fikra.
6- Na Uhalisia ni tunaouishi umebadilika, kwani tangu mwaka wa (1830) mpaka mwaka wa (1930) Mwanadamu aligundua na kutengeneza vitu vilivyowwezesha kubadilisha mfumo wa maisha yake ya kila siku. Na wataalamu wa Ustaarabu waliutenga mwaka wa (1830) kwa kuuzingatia kama ni kipindi tenganishi, na kipindi tenganishi hiki ndani yake kuna tukio linalochukuliwa kama anuani ya kuanza hatu au kumalizika kwake, na tukio hilo linakuwa ni alama, na katika mwaka huo Waingereza waliingiza chuma melini, na hapakuwepo kinachofanana na Mhimili wa Kusini au kwa maana sahihi Mhimili wa Uislamu (Twanja - Jakarta, Ghana - Farghana) kinachofanana na Uvumbuzi huo, au huo ufichuzi ambao uliwezesha kukifanya chuma kielee baharini, Wataalamu wa Uingereza wakafanikiwa kuiga na kuingiza chuma katika meli zao, lakini Hisia za Ubunifu na Uanzishaji wake na Kujiamini, pamoja na Mwingine huhisi anahitaji na kungojea Ubunifu ili aufuate na kuuiga, ndicho kilichokifanya kipindi hiki kiwe kipindi tenganishi baina yake na yale yajayo baadaye, na wengi walifanya bidii ya kutaka kulinganisha baina ya Mashariki na Magharibi, baada ya kuondoka kwa hisia za Ukuu nyakati za Vita vya Msalaba.
na katika miaka hii mia moja, zilijitokeza Elimu mbalimbali za mwanadamu, na zikaanza kukua, na pakadhihirika fikra zingine zisizokuwa ongozi, na ukaja wito wa Kuelimisha na Usasa, na Papa wa Vatican akatoa hotuba yake mashuhuri ijulikanayo kama (Parcent) akitangaza Elimu sabini na kuziharamisha; kwa sababu zinajenga fikra hii mya ijulikanayo kama Usasa kutokana na ielewavyo na jinsi mfumo wake ulivyo. Usasa ambao ulikuja kutokana na Uzao wa Mwinuko wa Ulaya hapo kabla, kuvikwa taji la Karne nne ambazo ndani yake palifanyika gunduzi nyingi za Kijiografia na Mapinduzi ya Kiviwanda pamoja na Mapinduzi ya Ufaransa... na kuendelea. Mwanadamu hivi sasa amekuwa akiishi kesho yake kama anavyoiishi leo yake, na wala sio siku yake kama alivyoiishi jana yake, na magazeti yameenea, na yametokea mapinduzi makubwa katika Njia za Usafiri, Mawasiliano na Teknolojia. Mwanadamu amefanikiwa kusafiri kutoka ardhini na kuelekea angani kwa ndege.
Na baada ya mwaka wa (1930) mpaka leo hii, Mwanadamu amefanikiwa kuboresha alichokigundua, na na kutumia alichokifichua, na akafanikiwa kukusanya Falsafa zote hizi na Mitazamo inayomtumikia, na pakadhihirika nadharia kadhaa:
Kwanza: Nadharia ya Kukua, ya Darwin.
Pili: Nadharia ya Kiwango cha Kifalsafa, ya Nitcher, kisha Kimahesabu ya Ainshtein.
Tatu: Nadharia ya Uchambuzi wa Kifalsafa, ya Froid.
Nne: Nadharia ya Ubepari ya Markas
Na nadhari hizi zote imeijenga akili inayotawala Duniani, na kuzalisha kutokana nazo na kutokana na wasifu wa Zama hizi alama za Zama zetu ambazo tunataka kuzijua.
Chanzo: Kitabu cha Simaatul Aswri, cha Mheshimiwa Mufti wa Misri, Dkt Ali Juma.