Tofauti Nyingi kati ya Madhehebu ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Tofauti Nyingi kati ya Madhehebu ya Waislamu

Question

 Kwanini kumekuwa na tofauti nyingi kati ya madhehebu ya Waislamu mfano kuhusu ndoa ya Muta'a na Zaka, pamoja na watu wa madhehebu ya Shia wanasema kuwa wao ndio hasa watu wa Peponi na wasiokuwa wao ni watu wa Motoni ukweli upo wapi?

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Kuna kanuni maalumu zinapaswa kuzingatiwa zaidi katika akili ya Muislamu wa hivi sasa, kanuni hizo ni:
1- Kujitoa kwenye tofauti ni jambo lenye kupendeza.
2- Hupingwa mambo yaliyokubaliwa wala si yenye tofauti.
3- Mwenye kufikwa na lenye tofauti basi na amfuate Mwanachuoni aliyepitisha hilo.
Kanuni hizi kwa ufupi zinaweka wazi kwa Muislamu kuwa inapendaza kwake kuweka uzio kwenye Dini yake hivyo asifanye kile chenye tofauti kati ya Wanachuoni kwa maana baadhi yao wamekipitisha na wengine wakakichukiza, lakini wakati huohuo haifai kwa Muislamu kupinga kwa ndugu yake Muislamu kufanya jambo lisilopitishwa na Wanachuoni kuwa ni haramu, kwa maana Wanachuoni wametofautiana baadhi yao wakalichukiza na wengine wakalipitisha.
Hii haina maana kuwa inafaa kwa yeyote yule kuzungumza katika Dini vile atakavyo lakini ni lazima kauli yake hii iwe inakubaliana na dalili inayozingatiwa na Wanachuoni wa Sharia.
Sio kila tofauti inazingatiwa isipokuwa tofauti yenye mtazamo.
Ni lazima tofauti iwe imejengeka kwenye misingi na yenye dalili.
Hivyo Sharia ya Kiislamu haipo kama wanavyodhani baadhi ya watu kuwa hakuna nafasi ya kubadilishana rai na mitazamo, kwani tofauti katika Dini ya Uislamu si jambo lenye kukataliwa muda wote.
Ninakunasihi ndugu yangu mwenye kuuliza swali kuchukua elimu kutoka kwa Wanachuoni, hivyo ikiwa unataka kufahamu Dini yako basi ni lazima usome.
Masuala haya ambayo umeyataja kila suala moja lina hukumu kadhaa sambamba na kutofautiana na aina zake na sifa zake, kwa mfano Zaka zipo za aina nyingi na kila aina ina hukumu halikadhalika watu wa Shia wako katika makundi mbalimbali na kila kundi linakuwa na hukumu.
Na kuhusu ndoa ya Muta'a kuna aina nyingi za ndoa hiyo, basi ni aina gani unakusudia.

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas