Hatua za Kuumbwa kwa Mwanadamu

Egypt's Dar Al-Ifta

Hatua za Kuumbwa kwa Mwanadamu

Question

 Ni hatua zipi za kuumbwa kwa mwanadamu ndani ya Qur`ani Tukufu?

Answer

  Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Hatua za kuumbwa kwa mwanadamu zilizotajwa ndani ya Qur`ani Tukufu zimetangulia sayansi ambapo haikugundua hayo isipokuwa ni baada ya kuteremka Qur`ani Tukufu kwa muda mrefu. Wasomi wa elimu ya kiinitete baada ya maendeleo ya sasa ya elimu wamegundua kuwa kutengenezwa kwa mifupa kunakuwa ndani ya kipindi cha wiki ya saba ambapo huanza mfumo wa mifupa cartilaginous kuenea mwilini na mtoto tumboni huanza kwa umbo la mifupa, kujitengeneza mifupa ndiyo hatua kubwa ya kuanza ambapo hubadilika kikamilifu kutoka umbo la mfinyanziko ambalo hatuoni sura ya mwanadamu na kuanza umbo la mifupa ndani ya kipindi kifupi, na umbo hili la mifupa ndilo ambalo humpa mtoto tumboni mwonekano wa mwanadamu.
Kisha baada ya hapo huja hatua za uvishaji wa nyama kipindi cha mwishoni mwa wiki ya saba na kuendelea mpaka mwishoni mwa wiki ya nane baada ya hatua ya kukua mifupa kama vile Qur`ani Tukufu ilivyoeleza kwenye kauli ya Mola Mtukufu: {Tukavisha mifupa nyama} kipindi hiki kina sifa ya kusambaa pia misuli pembezoni mwa mifupa na kuizunguka kama vile inavyozunguka nguo kwa mvaaji, baada ya kukamilika kwa uvishaji wa misuli kwenye mifupa ndipo sura ya mwanadamu huanza kuwa sawa na kuanza kutengenezwa maeneo mbalimbali ya mwili kwa mahusiano yenye kuendana sana, baada ya kukamilika kutengenezwa kwa misuli hapo mtoto ndio anaweza kucheza tumboni.
Utaratibu huu wa hatua za kuumbwa ndio uliothibitishwa zama za sasa na kuchukuliwa picha za rangi hatua ya kupandikizwa mifupa mtoto aliyetumboni na kuanza kuvishwa nyama kwenye mifupa, hivyo ukweli huu umethibitishwa kisayansi.
Aya hizi Tukufu zimekuwa ndiyo sababu ya Wasomi wengi wa Magharibi kuingia katika Uislamu, na wakazingatia mazungumzo ya Qur`ani Tukufu kuhusu hatua za kuumbwa kwa mwanadamu ni muujiza mkubwa wa kisayansi, miongoni mwao ni pamoja na Profesa Keith Moore ni msomi kutoka nchini Canada ni miongoni mwa wasomi wakubwa duniani wa mambo ya upasuaji wa mtoto, naye ni mkuu wa kitengo hiki ndani ya Chuo Kikuu cha Toronto nchini Canada, na ndiye mwenye kitabu cha “The Developing Human” nacho ni kitabu maarufu kinafundishwa vitivo vingi vya masomo ya tiba duniani na kimefasiriwa kwa zaidi ya lugha 25, katika kitabu hiki amezungumzia hatua za kuumbwa kwa mwanadamu kwa hatua hizi zilizotajwa ndani ya Qur`ani, na katika kila somo katika masomo yaliyomo kwenye kitabu ambayo yanazungumzia hatua za kuumbwa kwa mtoto tumboni na kubainisha ukweli wa kisayansi aliunganisha na Aya pamoja na Hadithi zinazohusiana na hilo na kusherehesha pamoja na kuzitolea maelezo.
Na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas