Kumhama Mke "Al-Iylaa"
Question
Assalaam Alaikum. Nataka kuuliza kuhusu “AI-Iylaa” ambapo nimefahamu kuwa mwanamume anaweza kuapa kwa mke wake kutokuwa naye kiunyumba kwa muda unaoweza kufika miezi mitatu wakati ambapo Mtume S.A.W. anasema katika maana ya Hadithi kuwa mke ambaye anajizuia kukutana na mume wake anakuwa ni mwenye kulaaniwa na Malaika, mume na mke utashi wao ni mmoja, na Uislamu haukutenganisha kati ya mume na mke katika haki hizi, ni mategemeao yangu kupata ufafanuzi na Mwenyezi Mungu awalipe mazuri.
Answer
Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Aya za Qur`ani Tukufu ambazo zimezungumzia hukumu ya kumuhama mke kwa maana ya Al-Iylaa na vile vile Hadithi Takatifu lengo lake lilikuwa ni kumtetea mwanamke na kumzuia mwanamume kumfanyia uadui kwa kumzuilia haki yake ya kukutana kimwili kwa muda mrefu ikiwa ndani yake kuna kero na maudhi kwa mwanamke, desturi ya Waarabu ilikuwa ni pamoja na kuishi na wanawake bila ya kuwatekelezea haki zao hivyo Uislamu ukaharamisha kuwafanyia madhara wanawake kwa sura hii, kwani zama za ujinga mwanamume alikuwa pindi akiwa hampendi mke wake na wala hataki kuoa mke mwingine basi anaapa kuwa hatomgusa mke wake muda wote wa uhai wake au kwa muda wa mwaka au miaka miwili kwa lengo la kumfanyia madhira na madhara, hivyo anamwacha akiwa hewani si mke wake wala si mwenye kuachwa ndipo Mwenyezi Mungu akataka kuweka mpaka kwenye uovu huu, akaweka kikomo cha miezi minne na kubatilisha kipindi cha zaidi ya muda huo ili kuondoa madhara.
Ama kuhusu uharamu wa kujizuia mwanamke na hitaji la mume, hili ni kwa sababu kujizuia kwa mwanamke kunapelekea madhara mengi na kuenea kwa uchafu na mambo ya madhambi ndani ya jamii na Uislamu umeharamisha hilo.
Wasifu wa matamanio kama inavyotofautiana kati ya mwanamume na mwamake:
Jibu la swali lililoulizwa ni kwanini Uislamu haukumchukulia mwanamume kama ulivyomchukulia mwanamke katika jambo hili? Kwa sababu hali ya mwanamume ni yenye kutofautiana na hali ya mwanamke katika yafuatayo, mzunguko wa matamanio kwa wanaume ni wenye kutofautiana na mzunguko wa wanawake kwani matamanio ya mwanamume pindi yanapofikia kilele haiwezekani kuyapa muda, ama mwanamke inawezekana kupewa muda mpaka miezi miwili mitatu hadi minne kwa kiwango cha juu sana lakini baada ya muda huo hawezi kuongeza isipokuwa kwa ugumu mkubwa hivyo Uislamu ukaharamisha kwa mwanamume kumzuilia mwanamke kumaliza matamanio haya kwa zaidi ya muda wa miezi minne.
Imepokelewa kuwa Umar Ibn Al-Khattab R.A. siku moja usiku alikuwa anazunguka ndani ya mji wa Madina, akasikia sauti ya mwanamke anaimba:
Usiku umekuwa mrefu na kiza chake - na kunilaza bila ya mpenzi wa kucheza naye.
Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu si vingine – kingo za kitanda hiki zingetikisika.
Kwa kumuogopa Mola wangu na aibu inanitosha – na kwa heshima ya Aliyemtukufu kitanda kupata mpandaji wake.
Kulipopambazuka kesho yake Umar alimwita huyo mwanamke na kumuuliza: Mume wako yupo wapi? Akajibu: Nimemtuma Iraqi. Umar akawaita wanawake na kuwauliza kuhusu huyu mwanamke ni kwa muda gani amekuwa akimsubiri mume wake? Wakajibu: Ni miezi miwili na unapungua uvumilivu wake ndani ya miezi mitatu na kumalizika kabisa ndani ya miezi minne, ndipo Umar akafanya muda wa kupigana vita ni miezi minne pindi inapoisha huwarudisha wapiganaji na kuelekeza kundi lingine liende vitani - Mwenyezi Mungu Anajua zaidi - nguvu ya kuhusisha muda wa kuwa mbali na mke miezi minne.
Wasifu wa hali ya matamanio inatofautiana kati ya wanaume na wanawake:
Matamanio ya wanaume ni yenye kutofautiana na matamanio ya wanawake kwa upande wa kutosheka, yenyewe kwa wanaume yanafanana na mahitaji ya kifiziolojia ambapo mwanadamu hawezi kujitenga nayo kama vile chakula kinywaji na hasa kwa wanandoa, ama mwanamke matamanio yake si kama wanaume bali matamanio ya mwanamke yanashiba pindi anapohisi ujoto na upole wa mwanamume na hii huinua haraka matamanio kwa wanaume zaidi ya wanawake.
Pingamizi na Majibu:
Baadhi ya wapingaji wanaweza kupinga maelezo yaliyotangulia kuwa mwanamke katika hali ya matamanio au nyege uhitaji wake wa kutosheka kwa mfano ni zaidi ya uhitaji wa mwanamume, hali hii si sehemu ya utafiti ambapo utafiti ambao tunauelezea ni kuwa, ni kwanini Uislamu umetofautisha kati ya matamanio ya mwanamume na ya mwanamke katika hali za kawaida si katika hali ya kukutana kindoa.
Baadhi ya Wanachuoni wamesema kwa sura nyingine katika sura za ufahamu wa hekima ya Sharia ya Mwenyezi Mungu katika hali ya kuwa mbali wanandoa ikiwa ndani yake pia kuna hali ya kuwaadabisha wanawake waasi na malaya kwa waume zao, ikahalalishwa kwa mume kwa kiwango cha mahitaji nacho ni kipindi cha miezi minne au chini yake, ama zaidi ya muda huo ni haramu dhuluma na uovu, kwa sababu ni kuapa kuacha kilicho wajibu kwake.