Mwingiliano wa Kiroho

Egypt's Dar Al-Ifta

Mwingiliano wa Kiroho

Question

 Imekuja katika Surat Aal-Imraan: 27 {Wewe huingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku}. Na katika Suratul-Baqarah: 28 {Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu}. Na katika Sura hiyo hiyo Aya ya: 64 na 74 {Na hakika mlikwisha yajua ya wale miongoni mwenu walio ivunja Sabato (siku ya mapumziko Jumaa Mosi) na tukawaambia: Kuweni manyani wadhalilifu}.
Na imekuja katika Injili kisa kinachofanana na haya, kuhusu nguruwe na watenda dhambi, kuongezea na hilo imekuja katika Injili kuwa Nabii Eliya alirudi akiwa mwenye kumuwakilisha Yohana mbatizaji, kisha wote wakawa wanasubiri kuja kwa Masihi kabla ya Siku ya Kiyama.
Na kupatikana habari kuwa Mwenyezi Mungu Alimfisha Uzair kisha Akamfufua baada ya miaka mia (Qur`ani: 2: 256) na wakawepo wengine wenye kupitisha kuwa Al-Khidhr ataendelea kuishi mpaka Siku ya Kiyama, na baadhi walikuwa wanapinga hilo, wakiegemea Aya ya Qur`ani: {Nasi hatukumjaalia mwanadamu yeyote kabla yako kuwa na maisha ya milele}. Maelezo yote haya si dalili ya mwingiliano wa kiroho?

 

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Aya ya kwanza maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu huushikanisha usiku na mchana na huushikanisha mchana na usiku pasi na kuwepo kitenganishi kati ya nyakati hizo mbili ni katika hali ya muujiza hakuna kiumbe kinachoweza kufanya mfano wake, hivyo basi inaonesha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Aya ya pili inathibitisha juu ya makafiri vitendo vyao viovu wakiwa wanampinga Mwenyezi Mungu naye ndiye Amewaumba kutokana na tone la manii litokalo kwenye uti wa mgongo wa baba zao na ndani ya mifuko ya uzazi ya mama zao.
Aya ya tatu inazungumzia kuhusu kundi la Mayahudi waliokiuka amri ya Mwenyezi Mungu na wakamuasi ndipo Mwenyezi Mungu Akawateremshia laana na Akaifanya miili yao mfano wa miili ya nyani pamoja na kubakia uelewa wa kibinadamu, au nyoyo zao na akili zao kama vile nyoyo za nyani na akili zao bila ya kuwepo mabadiliko katika maumbile yao ya nje, na hayo ni matokeo ya kukiuka maelekezo.
Na wala hakuna ndani ya Aya Tukufu kilichotajwa kinaonesha imani ya mwingiliano wa kiroho ambayo inaelezewa na watu wa dini za kutengenezwa na ambayo haina ukweli wowote ndani ya Dini za Mbinguni, kitabu cha At-Tahrir wa Tanwir, juzuu ya 1/ uk. 333.
Umbile la nyani linachukuliwa kuwa ni kubadilishwa miili yao na kuwa miili ya nyani na kubakia uelewa wa kibinadamu kama kawaida, na hii ndiyo kauli ya Wanachuoni na Wafasiri, na inachukuliwa pia kuwa akili zao zilikuwa ni kama akili za nyani na kubakia umbile la kibinadamu, na hii ni kauli ya Mujahid, na mazingatio yanapatikana katika kila mazingatio mawili, zingatio la kwanza lipo wazi zaidi kwa sababu ndani yake kuna maelezo yao wenyewe na maelezo ya watu kuhusu wao tofauti na zingatio la pili, na zingatio la pili lipo karibu zaidi kihistoria ambapo haijawahi kunukuliwa mwingiliano wa kiroho katika vitabu vya historia ya Waibrania, na uwezo upo kwenye hali zote mbili na hali zote ni muujiza wa Sharia kwa sababu hiyo amesema Fakhr: Kauli ya Mujahid haipo mbali sana lakini tofauti ya wazi ya Aya kwani Aya haipo wazi kwenye uingiliano wa kiroho.
Na maana ya kuwa kwao nyani ni kuwa wao hawakupokea Sharia kwa uelewa unaokusudiwa na maana zake bali wakaichukua kwa sura ya maneno tu wakajifananisha kama wageni katika kusimama kwao vinavyohusika na hawakutenganika na sura hiyo ya kujifanya wageni, na huyu nyani anashiriki nao katika mfanano huu na hii ndiyo maana ya kauli ya Mujahid ni mwingiliano wa nyoyo na wala si mwingiliano wa kiroho.
Kisha wasemaji wanaosema uwepo wa mwingiliano wa mwili wamekubaliana au walikuwa karibu kukubaliana kuwa mwenye kuveshwa mwingiliano wa roho haishi zaidi ya siku tatu na kuwa hana kizazi kwani limepokelewa hilo na Ibn Mas,ud kutoka kwa Mtume S.A.W. kuwa amesema: “Mwenyezi Mungu haangamizi watu au kuwaadhibu na kuwabakishia kizazi”, kuna badhi ya Wanachuoni wamepitisha kuwepo kizazi cha mwenye kuvishwa roho na wakasema kuwa mnyama kama tembo, nyani, kenge na nguruwe ni katika jamii ya watu walioveshwa roho na Waarabu wanaamini hilo kwenye mnyama kama kenge.
Hata baadhi ya Wanachuoni wa Fiqhi wamesema uharamu wa kuliwa nyama ya tembo na mfano wake ni kutokana na uwezekano wa kuwa asili yake ni kizazi cha mwanadamu, amesema Ibn Hajib “Ama yanayosemwa kuwa ni mwenye kuvishwa roho kama vile tembo, nyani na kenge katika baadhi ya madhehebu wamepitisha kwa sababu ya ujumla wa Aya na uharamu kwa kutajwa” au kwa ujumla wa Aya za mambo ya vyakula, amesahihisha mwenye kitabu cha Tawdhih, na Imamu Muslim amepokea Hadithi nyingi mbalimbali katika kitabu chake cha Sahihi Muslim kutoka kwa Abi Huraira kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Ulipotea umma wa Wana wa Israeli hawajui nini wamefanya wala hawaoni isipokuwa panya, hivi hamuoni pindi anapowekewa maziwa ya ngamia hanywi na anapowekewa maziwa ya mbuzi anakunywa”. Imejengewa maelezo na Ibn Atiya pamoja na Ibn Rushd katika kitabu cha Bayan na Wanachuoni wengine kuwa haya aliyasema Mtume S.A.W. kuhusu jitihada kabla ya Mwenyezi Mungu kusimamisha kuwa mwenye kuvishwa roho haishi zaidi ya siku tatu wala hawezi kuwa na kizazi kama lilivyokuwa hilo wazi kwenye Hadithi ya Ibn Mas’ud, nikasema: Linakubalika hili kuwa amezungumzia kuhusu jitihada kwenye kauli yake: “Wala sioni”.

 

Share this:

Related Fatwas