Wanafunzi "Ar-Rusul"

Egypt's Dar Al-Ifta

Wanafunzi "Ar-Rusul"

Question

Wanafunzi ni wale wafuasi wa Nabii Isa pindi waliposema: je, Mola wako Anaweza kututeremshia meza kutoka mbinguni? Na nini maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu inayosema: {Na Tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi} ikiwa ndiyo hivyo basi ni nini hekima ya Mwenyezi Mungu kutotaja idadi yao? 

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Kwanza: Imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wanafunzi waliposema: Ewe Isa bin Maryamu! Je, Mola wako Mlezi Anaweza kututeremshia chakula kutoka mbinguni? Akasema: Mcheni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini * Wakasema: Tunataka kukila chakula hicho, na nyoyo zetu zitue, na tujue kwamba umetuambia kweli, na tuwe miongoni mwa wanaoshuhudia * Akasema Isa bin Maryamu: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshie chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku * Mwenyezi Mungu Akasema: Hakika Mimi Nitakuteremshieni hicho. Lakini yeyote katika nyinyi atakaye pinga baadaye, basi hakika Mimi nitampa adhabu nisiyopata kumpa yeyote katika walimwengu} Al-Maidah: 112 – 115.
Aya hizi zinatukumbusha mazungumzo yaliyofanyika kati ya Nabii wa Mwenyezi Mungu Isa A.S. na watu wake, walikuwa wanamuuliza kuhusu uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu wa kuteremsha meza kutoka mbinguni, na Nabii Isa A.S. alikuwa anawataka wawe na Imani kwa Mwenyezi Mungu nao wakiwa wanamjibu kuwa kusudio lao ni kutaka kulia chakula na kuona kwa macho yao, na waweze kutolea ushahidi kwa wengine, baada ya Nabii Isa kujiridhisha na ukweli wa maelezo yao na makusudio yao ndipo alipomwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Awateremshie meza kutoka mbinguni iwe ni ishara kwao wote lakini pia ni kumbukumbu kwa watakao kuja baada yao mpaka Siku ya Kiyama, ndipo Mwenyezi Mungu Akajibu maombi ya Nabii wake Isa A.S. na Akasema: {Hakika Mimi Nitakuteremshieni hicho. Lakini yeyote katika nyinyi atakayepinga baadaye, basi hakika Mimi Nitampa adhabu nisiyopata kumpa yeyote katika walimwengu}.
Ombi la wanafunzi wa Nabii Isa halikutokana na shaka pamoja na upungufu wa imani bali ni kama ombi la Nabii Ibrahim A.S. pale aliposema: {Mola wangu Mlezi! Nioneshe nikutazame}.
Pili: “Au” katika Aya Tukufu ni ya kuhiyarishwa, kwa maana hawa watu ambao Mwenyezi Mungu amewapelekea Nabii wake Yunus A.S. pindi wanapoonwa na mwonaji hushangaa kwa kutoa kauli mbili, kwa kusema: Wao ni laki moja, au kwa kusema: Wanazidi laki moja, kama kwamba Aya Tukufu imeleta taswira ya hali ya hawa watu wakati wanapoangaliwa na watu idadi yao inatofautiana kwa tofauti ya mtazamo wa wanaowatazama.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas