Maana ya Maneno ya Mwenyezi Mungu:...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maana ya Maneno ya Mwenyezi Mungu: “Wamewafanya Makuhani Wao na Wamonaki Wao Kuwa Ni Marabi.”

Question

 Imetajwa katika suala la “Je, inajuzu kuswali makaburini, na ni ipi hukumu ya kuswali katika misikiti yenye makaburi, na je, hii inachukuliwa kuwa ni aina ya kulichukua kaburi kama msikiti?”

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Mayahudi na Manasara walikuwa wakiwaabudu makuhani wao na wamonaki wao badala ya Mwenyezi Mungu kwa kuwasujudia, kama alivyosema mwandishi katika kauli yake, “Ni kwamba kaburi lenyewe ni mahala pa kusujudu, na asujudiye anasujudu juu yake kwa waliomo makaburini ili kumwabudu, kama walivyofanya Mayahudi na Manasara, ambapo Mwenyezi Mungu alisema: {Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipo kuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo.}
Na nikataja katika matini niliyoyanukuu kutoka katika tafsiri ya Ibn Kathir kwamba makuhani wao na wamonaki wao walikuwa wakiwahalalishia na kuwakataza wanachotaka.
Hakuna mgongano baina ya maana hizo mbili, kwa sababu inajuzu kuzichanganya, kundi la Mayahudi na Wakristo lilikuwa likiwasujudia makuhani wao na wamonaki wao kama lilivyo na linaonekana hadi leo, kama alivyosema mwandishi wa suala hilo lililotajwa hapo juu, na makundi mengine yanafuata yale waliyohalalishiwa na makuhani wao na wamonaki wao, kama nilivyonukuu kutoka katika tafsiri ya Imam Ibn Kathir, kwa hiyo hakuna mgongano au upinzani baina ya maana hizo mbili, kama ilivyodhihiri kwako.

 

 

Share this:

Related Fatwas