Kuhusu Kuuwawa Mtu Aliyeritadi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhusu Kuuwawa Mtu Aliyeritadi

Question

 Mtu mmoja ambaye ni Mkristo ameukosoa Uislamu kwa kuwa mtu anayeritadi kwa maana ya kuacha Uislamu baada ya kuwa Muislamu anapaswa kuuwawa ambapo jambo hili amelizingatia lipo kinyume na misingi ya uhuru kwa upande wa mtazamo wake na Mkristo anaingia kwenye Uislamu bila ya matatizo yeyote.
Mimi sifahamu nimwambie nini huyu mtu...Ni matarajio yangu kulipa uzito hili.

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Uislamu unatambua uhuru wa kuteua dini, kwani Uislamu hautenzi nguvu mtu yeyote kufuata dini yeyote, kwani Anasema Mola Mtukufu:
{Hapana kulazimisha katika Dini} [AL BAQARAH: 256].
Mwisho ni kuwa Uislamu haukubali kumshirikisha Mwenyezi Mungu wala haukubali ibada kinyume na kuabudiwa Mwenyezi Mungu, na huu ni msingi wa kweli wa Uislamu kwa kuzingatia kuwa ni dini ya itokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, pamoja na hayo Uislamu unakubali Ukristo na Uyahudi wala haupambani na wao kwa hali waliyonayo, lakini unawalingania kuja kwenye Uislamu, kama vile Uislamu hauhalalishi kutoka kwa mtu aliyeingia kwenye dini ya Mwenyezi Mungu wala haumlazimishi yeyote kuhama kwa ajili ya kuutetea Uislamu, lakini haukubali kwa yeyote kuudhalilisha Uislamu, mtu ambaye ameritadi na kuuhama Uislamu kwa kufanya hivyo basi huyo anakuwa ni adui wa Uislamu na anatangaza vita dhidi ya Uislamu na Waislamu, hakuna la ajabu au la kushangaza Uislamu kulazimisha kuuwa mtu mwenye kuritadi au kuuacha Uislamu, kwani kila mfumo duniani hata ule ambao hauna uhusiano na dini yeyote kanuni zake zinaeleza kuwa mtu kutoka kwenye mfumo mkuu na miiko yake ana adhabu ya kifo na si vyingine, ni kile wanachokiita ni usaliti mkubwa.
Na huyu anayeritadi kwa kuuhama Uislamu kwa uwazi kuonesha kuritadi kwake, kwa kweli kwa kitendo hiki anatangaza vita kwa Uislamu na kuinua bendera ya upotofu na kuwalingania watu wasiokuwa waislamu, na kitendo hiki ni mpiganaji vita dhidi ya Waislamu na anazingatiwa kama wanavyozingatiwa wapiganaji vita dhidi ya dini ya Mwenyezi Mungu.
Jamii ya Kiislamu inasimama kwa hatua ya kwanza kwenye Akida na Imani, kwani Akida ni msingi wa Muislamu na muhimili wa maisha yake lakini pia ndio roho ya uwepo wake, kwa sababu hii Muislamu hawezi kuruhusu mtu yeyote kugusa msingi huu, hivyo kuritadi kwa kutangaza wazi kumekuwa ni uhalifu mkubwa katika mtazamo wa Uislamu kwa sababu ni hatari kwa haiba ya jamii na mjengeko wake kimaana, ni hatari kwa jambo la kwanza katika mambo makuu matano ya makusudio ya Sharia: “Dini nafsi kizazi akili na mali”.
Uislamu haukubali dini kuwa kufanyiwa mchezo mtu anaingia leo na kesho anatoka kama vile baadhi ya Mayahudi ambao wamesema:
{Yaaminini yale waliyo teremshiwa wenye kuamini mwanzo wa mchana, na yakataeni mwisho wake; huenda wakarejea} [AALI IMRAAN: 72].
Kuacha Uislamu sio tu tukio la kiakili bali pia ni kubadilisha uaminifu na kubadili utambulisho lakini pia kugeuza ufuasi, mwenye kuritadi huhamisha uaminifu wake na ufuasi wake kutoka uma kwenye uma mwingine huwa anaivua nafsi yake kutoka kwenye uma wa Kiislamu ambao alikuwa sehemu ya umma na kuwa mgomvi wake, na linaelezewa hilo na Hadithi kwa kauli ya Mtume S.A.W:
“Mwenye kuacha dini yake ni mwenye kutengana na jamaa”. [Imepokelewa Na Muslim]
Vyovyote utakavyo kuwa uhalifu wa mwenye kuritadi Waislamu hawafuatilii aibu za yeyote wala kuvamia nyumba ya yeyote wala hawamzingatii mtu isipokuwa yule mwenye kujitangaza wazi kwa ulimi wake au kwa maandishi yake au kitendo chake kinachopelekea kuwa kafiri wa wazi bila ya kuwepo sababu ya kujengea hoja au uwezekano, hivyo shaka yeyote katika hilo hufasiri masilahi ya mtuhumiwa wa kuritadi.
Kitendo cha kupuuza adhabu ya mwenye kuritadi kwa kutangaza kuritadi kwake kuna sababisha kwa jamii yote kukutwa na hatari na kunafungua mlango wa fitina hakuna anayejua mwisho wa fitina hii isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, wala asipate nafasi mwenye kuritadi ya kumpotosha mwingine, na hasa wale watu dhaifu na masikini, na kutengeza kundi dhidi ya Umma linalojihalalishia lenyewe kutafuta msaada kwa maadui wa Umma na kupelekea kuibuka mvutano na mpasuko wa kifikra kijamii na kisiasa, na huenda ikapelekea mvutano wa kumwaga damu bali vita vya wenyewe kwa wenyewe vitakavyo kula kibichi na kikavu.
Jamhuri ya Wanachuoni wamesema, ni wajibu kwa murtadi kutakiwa kwanza kutubu kabla kutekelezwa adhabu kwake bali amesema Sheikh wa Uislamu Ibn Taimiya ni makubaliano ya Maswahaba - Radhi za Mungu ziwe kwao – na baadhi ya Wanachuoni wameainisha siku tatu, na baadhi yao wakasema chini ya siku tatu na wengine wamesema zaidi ya siku tatu na wengine wamesema muda wote atatakiwa kutubia, wakaondoa katika hilo kwa mtu zindiki, kwa sababu zindiki huwa anaonesha tofauti na kile anachokificha hivyo hana toba kwake, vile vile ni mwenye kuukashifu utukufu wa Mtume S.A.W na heshima yake hivyo haikubaliki kwake toba, na Ibn Taimia ametunga kitabu katika hilo na amekiita “Msimamo mchafu juu ya kumkashifu Mtume”.
Na kusudio la kutakiwa kutubu ni kumpa nafasi ili kurudi, kwani huenda ikaondoka hali hii ya shaka na kuwepo hoja, na Wanachuoni wanampa jukumu la kuipatia majibu shaka iliyo ndani ya nafsi yake ili mpaka asimamishiwe hoja ikiwa anautaka ukweli kwa nia safi, na akiwa na hali ya kufuata tu au anafanya kwa ajili ya mwingine basi Mwenyezi Mungu ndiye atasimamia anachosimamia.

Share this:

Related Fatwas