Ndoa ya Bibi Aisha kwa Mtume

Egypt's Dar Al-Ifta

Ndoa ya Bibi Aisha kwa Mtume

Question

 Hapo awali tumelishughulikia suala hili katika utafiti huru uitwao: "Inakuwaje Mtume anamuoa Bibi Aisha akiwa na umri wa miaka tisa?" Huu ndio muhtasari wake.

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kutokana na tofauti asili za mazingira:
Sababu halisi ya swali hili ni ukosefu wa ufahamu wa tofauti kubwa kati ya mazingira tofauti na ustaarabu ambao umetenganishwa kwa mamia ya miaka. Kutumia mila na desturi za zama za kisasa kwa zama za kale, huku tukipoteza tofauti kubwa iliyotokea kutokana na wakati na mila na desturi.
Ni mila na desturi ngapi zilienea kwa baadhi ya watu na kubadilika miongoni mwa wengine, na ni tabia ngapi ambazo baadhi ya watu huzizoea na hazina athari ya kubadilisha mila na desturi kutoka zama moja hadi nyingine.
Nia mojawapo ya swali hilo pia ni kutofahamu tofauti alizoziumba Mwenyezi Mungu watu kutokana na tofauti za umbo la muundo na saizi ya mwili hasa kwa mazingira fulani, na hasa katika masuala ya wanawake. Je, tunaona wanawake wangapi, hata katika wakati wetu huu, ambao wamevunja ungo na kuimarika wakati bado wana umri wa miaka kumi au zaidi.
Maadui hawakushangazwa na ndoa hii
Kwa hiyo, Makkah haikushangaa ilipotangazwa habari ya kufunga ndoa kati ya marafiki wawili wakubwa na marafiki wawili waaminifu zaidi, bali iliipokea kama jambo la kawaida, kuzoeleka na kutazamiwa. Na hakuna hata mtu mmoja katika maadui wa Mtume SAW, aliyejipatia jambo hili kuwa ni gumzo kwake, bali kwamba mmoja wa wapinzani wake wakubwa hakuwahi kufikiri kwamba angeichukulia ndoa ya Muhammad SAW na Aisha kuwa ni kashfa au njia ya kashfa na tuhuma, na hao ndio ambao hawakuacha njia yoyote ya kumpinga Mtume ila waliitumia, hata kama njia hiyo ni kashfa ya Uongo.
Na wangeweza kusema nini?
Je, wanakataa kwamba msichana kama Aisha, ambaye hana zaidi ya miaka saba, ameposwa?
Lakini alichumbiwa kabla ya “Muhammad bin Abdullah” kumposa kwa “Jubair bin Mut’im bin Adiyy” ili kwamba Abu Bakr asingeweza kutoa neno lake kwa Khawla binti Hakiim, mpaka akaenda na kuvunja ahadi yake kwa Abu Jubair. Je, wanakanusha kuwa kuna ndoa kati ya msichana wa rika lake na mwanamume aliyefikia umri wa miaka hamsini na tatu? Ni ajabu gani katika jambo kama hilo, na ni msichana gani wa kwanza kuolewa katika mazingira hayo na mwanamume wa rika la baba yake, na hatakuwa wa mwisho kati yao? Na Mzee Abdul-Muttalib, alimuoa Halah Az-Zuhriyyah, binamu yake Amina, siku ambayo Abdullah mdogo wa wanawe alimuoa msichana wa rika lake Halah, naye ni “Amina binti Wahab”.
Na Umar Ibn Al-Khattab akamuoa Binti ya Ali Bin Abi Talib, wakati Umar yuko katika umri ulio juu ya umri wa baba yake Ali!
Umar anamwambia Abu Bakr amuoe binti yake mdogo, Hafsa, na kati yao kuna tofauti ya umri kama ile iliyo baina ya Mtume na Aisha...
Lakini kikundi cha Mustashrikuna walikuja baada ya karne kadhaa za ndoa hiyo, wakizipuuza tofauti za nyakati na mazingira, na kurefusha kile walichoeleza kuwa “mchanganyiko wa ajabu kati ya mume mzee na msichana bikira asiye na ujuzi,” nao wanapima kwa jicho la matamanio ndoa ambayo ilifanyika Makka kabla ya Kuhama, na kile kinachotokea leo katika nchi za Magharibi, wakati msichana haolewi kabla ya umri wa miaka ishirini na tano, umri unaozingatiwa hadi leo kuchelewa sana katika Bara Arabu, pia katika mashamba na majangwa ya Mashariki na Magharibi. Na hivi ndivyo alivyojaalia mmoja wa hao Mushtashrikina, mwenye haki, ambaye alitembelea Bara Arabu na akarudi na kusema:
"Aisha, katika umri wake mdogo, alikuwa akikua kwa kasi ya ukuaji wa wanawake wa Kiarabu, ambayo inawafanya wazeeke mwishoni mwa miaka ya ishirini ...
Lakini ndoa hii iliwashughulisha baadhi ya Wanahistoria wa Bwana wetu Muhammad SAW, ambao waliitazama kwa mtazamo wa jamii ya kisasa wanayoishi, kwa hiyo hawakuzingatia kuwa ndoa kama hii ilikuwa na bado ni mazoeo ya wakazi wa Asia, na pia mazoeo haya bado yapo katika eneo la Mashariki ya Ulaya, na ilikuwa ni jambo la kawaida nchini Uhispania na Ureno hadi miaka michache iliyopita, na si ajabu leo, katika baadhi ya maeneo ya Marekani”.
Ni kama vile mtu ana umri wa aina mbili: Umri wa kiwakati na umri wa kiakili, na huenda nyakati hizi mbili ziko mbali zenyewe kwa zenyewe. Unaweza kukuta mtu ambaye umri wake ni miaka kumi, wakati umri wake wa kiakili ni miaka kumi na tano, na unaweza kukuta mtu ambaye umri wake ni miaka ishirini, na umri wake wa kiakili ni miaka kumi na tano, hivyo akili haikui kwa kukua kwa mwili, bali ina makuzi yake ya pekee, na Bibi Aisha R.A, ingawa alikuwa mdogo wa kiwakati lakini alikuwa na akili timamu, mwangavu wa mawazo, na mwangalifu sana. Ushahidi wa hayo ni kwamba alikuwa na jukumu kubwa katika Ulinganiaji wa Kiislamu.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas