Kumuita Mtume Ahmad alipozaliwa

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumuita Mtume Ahmad alipozaliwa

Question

Kwa nini Bwana wetu Muhammad S.A.W, hakuitwa Ahmad wakati wa kuzaliwa kwake, kama Yesu alivyohubiri? Je, alijulikana kama Ahmad kabla ya kupata Utume wake, na je, kuna ushahidi wa hilo? 

Answer

 Jina mashuhuri zaidi la Mtume Mtukufu S.A.W, ni Muhammad, ingawa alikuwa na majina mengine mengi, likiwemo Ahmad. Ilitajwa katika Al-Muwatta’, kutoka kwa Muhammad Ibn Jubair Ibn Muti’im, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mtume S.A.W, kuwa amesema: “Mimi nina majina matano: Mimi ni Muhammad, mimi ni Ahmad, na mimi Al-Mahiy ambaye Mwenyezi Mungu humfutia ukafiri, na mimi ni Al-Hashir ambaye watu wote watafufuliwa kwa mila yangu, na mimi ni Al-A’aqib.”
Na majina mengine yamepokelewa, ambayo Abu Bakr Ibn Al-Arabiy aliyachunguza katika “Al-A’aridhah” na “Al-Qabas. ”
Na tutakupeni majibu marefu kwa swali lenu siku chache zijazo; ambapo Idara ya Utetezi wa Uislamu inayahariri.

Share this:

Related Fatwas