Mitume na Kufanya Makosa

Egypt's Dar Al-Ifta

Mitume na Kufanya Makosa

Question

 Je, Mitume wanakosea?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili akae naye kwa utulivu. Na anapo muingilia hubeba mzigo mwepesi, akitembea nao. Anapo kuwa mja mzito, wote wawili humwomba Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wao: Kama ukitupamwana mwema tutakuwa katika wanao shukuru} [ALAARAF 189].
Je, Mitume wanakosea? Katika Aya hii kuna Mazungumzo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kisa cha Kuumbwa Baba wa Walimwengu Adamu A.S, na Mke wake Mama Hawa kwa uwezo wake kuna dalili juu ya ulazima na upweke wake, kisha baada ya hapo anazungumzia sababu za uwepo wa Wanaadamu wote kwa uhusiano huu ambao ameujaalia baina ya Mwanaume na Mwanamke na ukashereheshwa na Aya Tukufu ukipitia hatua zote za Ujauzito.
Kisha kwa Maombi yao kwa Mwenyezi Mungu ili mtoto awe mzima mwilini mwake na katika maumbile yake, na imekuwa vyema kwao kwa yote hayo kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hayo na wasimshukuru mwingine yeyote katika viumbe vyake wao na watoto wao lakini amewajaalia watoto wao ni washirika kwa mtoto aliyowapa Mwenyezi Mungu Mtukufu na yeye Mwenyezi Mungu ametakasika na yote hayo. [Tazama kitabu cha: At Tasheel 57/4, na kitabu cha: Nadhmu Ad Durer 191/8]
Imamu Al Baidhawiy alisema: {Basi anapo wapa mwana mwema, wanamfanyia washirikina Mwenyezi Mungu katika kile kile alichowapa. Mwenyezi Mungu ametukuka na huko kushirikisha kwao} [ALAARAF 190] Yaani walijaalia watoto wao ni washirika na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika aliyowapa watoto wao, basi waliwaita majina ya Abduluza, na Abdumanaf, na dalili kwa hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu ametukuka na huko kushirikisha kwao. Ati wanawafanya viumbe kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu, nao hawaumbi, bali wao ndio wanaumbwa?} [ALAARAF 191] Yaani masanamu. [Tazama kitabu cha: Anwaaru At Tanzeel 180/1]
Imamu Al Qasimiy amesema: "Na Wanachuoni wa Tafsiri ya Qur'ani hapa wamezitaja Hadithi na Athari zinazoonesha kuwa anaekusudiwa hapa ni Adamu na Hawa na sisi hatuna haja yeyote kuelekea katika Mapokezi yake kwani yana Isnadi ya kufikirika yenye makosa, vilevile Ibnu Kathiir katika Tafsiri yake ameweka wazi" [Tazama Kitabu cha: Mahasen At Ta'weel 2921/7]
Na Imamu Ibnu Kathiir ametaja ya kwamba Haidithi hii imetiwa kasoro kwa pande tatu:
Ya kwanza: Kwamba Omar bin Ibrahim huyu ni Mbuswiri na aliaminiwa na Ibnu Muiin lakini akasema Abu Hatimul Raazi kwamba hiyo Hadithi haichukuliwi kama ni hoja lakini ameipokea Ibnu Marduwiya kutokana na Hadithi ya Muutamar kutoka kwa baba yake kutoka kwa Hasan kutoka kwa Samurat katika hukumu ya Marfuu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mjuzi zaidi.
Na ya Pili: Kwamba amepokea kutoka kauli ya Samrah yeye mwenyewe sio katika hukumu ya Marfuu, kama alivyosema Ibn Jarer alituzungumzia Ibn Abdu Al Ala, alituzungumzia Al Muutamar kutoka kwa baba yake, alituzungumzia Bakr Bin Abdullahi kutoka kwa Sulaimaan At Tamimiy kutoka kwa Abi Al Alaa Bin Ash Shakheer kutoka kwa Samrah Bin Jandab alisema kuwa Adam alimwita mwanae Abdulhareth.
Ya Tatu: Kwamba Hassan yeye mwenyewe ameifasiri Aya bila ya maelezo hayo na kama ingekuwa kwa Hadithi hii kutoka kwa Samurat katika Hukumu ya Marfuu basi asingeiacha. Ibn Jareer amesema: Ibn Wakee' ametuzungumzia, Sahl Bin Yusuf ametuzungumzia kutoka kwa Amru kutoka kwa Al Hassan, {Ati wanawafanya viumbe kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu} Alisema: hayo yalikuwa katika baadhi ya watu wa Mila, na hayakuwa na Adam. Ibn Abdul Al A'la alituzungumzia, Muhammad Bin Thaur alituzungumzia kutoka kwa Muammar alisema: Al Hassan aliikusudia nayo vizazi vya Adam, na walioshirikisha miongoni mwao baada yake, yaani {Ati wanawafanya viumbe kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu}.
Na Bishr alituzungumzia, Yaziid alituzungumzia, Said alituzungumzia, kutoka kwa Qatadah alisema: Al Hassan alikuwa akisema wao ni Mayahudi na wakristo, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaruzuku watoto basi waliwaingizia dini ya Uyahudi na Ukristo.
Na Isnaadi hizi ni Sahihi kutoka kwa Hasan R.A, kwamba yeye aliifasiri hii Aya kwa maelezo hayo nayo ni Tafsiri bora zaidi katika Tafsiri nyingi kuhusu yaliyomo ndani ya Aya hii, na kama Hadithi hii ingelikuwa kwake imehifadhiwa kutoka kwa Mtume S.A.W, asingeliiacha yeye au wengine na hasa hasa kwa uchamungu na unyenyekevu alionao yeye na hili linaonesha wazi kwamba Hadithi hii inaishia kwa Swahaba wa Mtume na kuna uwezekano mkubwa akawa Swahaba huyo ameipokea kutoka kwa Watu wa Kitabu miongoni mwa wale walioamini kama vile Kaabu au Wahab bin Munabih na wengine wengi kama ufafanuzi wake utakavyokuja akipenda Mwenyezi Mungu isipokuwa sisi tuko mbali na Jukumu la hukumu ya Marfuu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Anasema Bin Aadil katika Tafsiri yake Al-Lubaab baada ya kutaja kisa kinachofanana na hiki: Tambua kwamba Ufasiri huu ni potofu kwa namna mbalimbali, na akataja vipengele sita vinavyobatilisha Tafsiri hiyo. [Kitabu cha: Al lubab katika Uluumu Al Kitab 419/9, na tazama kitabu cha: At Tasheel kwa Uluumu At Tanzeel 57/2].
Tafsiri Sahihi ni ile iliyonukuliwa na Hasan Buswiiry aliyopokea kutoka kwa Ibnu Jurair kwamba Aya imekusudiwa kizazi cha Adam A.S, na yeyote baada yake atakayemshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na katika mapokezi kutoka kwake, hii ilikuwa katika baadhi ya Dini na hakuwa Adamu A.S. Ibnu Kathiir amesema: Na Isnadi zinazoelekezwa kwa Hasan katika Hadithi hii ni Sahihi, nayo ni Tafsiri bora ya yaliyomo ndani ya Aya hii.
Na miongoni mwa aina Sahihi katika kuifasiri Aya hiyo ni ile iliyotajwa na Al Qafaal Mwenyezi Mungu Amrehemu: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amekitaja Kisa hiki kwa maana ya kupigia Mfano na kubainisha kwamba Hali hii ni sura ya Washirikina katika Ujinga wao na Tamko lao la Ushirikina na kuyakubali kwao maneno haya kama vile Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Yeye ndiye aliyemuumba kila mmoja wenu kutokana na nafsi moja na akakujaalieni kutokana na umbile hilo Mke wake mwanadamu anayelingana naye katika Ubinadamu.
Na Mume alipokutana na Mke wake na Mimba ikatuga, Mume na Mke wake wakamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu wakisema: Ikiwa utatujaalia mtoto mwema aliye mzima tutakuwa ni wenye kukushukuru kwa neema zako mbalimbali na Mwenyezi Mungu alipowajaalia mtoto mwema aliye mzima mume na mke wakamshirikisha Mwenyezi Mungu na washirika mbalimbali kwa yale aliyowajaalia, na baadhi ya nyakati wanamnasibisha mtoto huyo na Maumbile kama isemavyo kauli ya Wafuasi wa Itikadi ya Maumbile na baadhi ya nyakati wanamnasibisha na Sayari kama ilivyo kauli na Wanajimu na baadhi ya nyakati wanamnasibisha na masamu na Upagani kama isemavyo kauli ya Wanaoyaabudu Masanamu. [Tazama kitabu cha: At Tasheel kwa Uluumu At Tanzeel 2922/7]
Ama Swali la Pili: Kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika tumekufungulia Ushindi wa dhaahiri. Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika Njia Iliyo Nyooka. Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu.} [AL FATH 1-3]
Manabii ni Alama za Ukamilifu:
Manabii na Mitume wao ni vilele vya Utu ambao watu wameamrishwa kuwafuata na kuzifuata nyendo zao. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basifuata hidaya yao. Sema: Mimi sikuombeni ujira. Hayahayakuwa ila ni mawaidha kwa walimwengu wote.} [AL ANA'AM 90] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Sisi tumewakhusisha wao kwa sifa ya ukumbusho waAkhera. Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora.} [Swaad 46-47].
Hii ni katika haki za Manabii kwa ujumla, na inakuwaje kwa yule aliyehitimisha Utume na Risala zote na akawa Mfano wa Kuigwa ambao watu wote wameamrishwa wamfuate katika kuabudu kwao na katika kufika kwao kwa Mwenyezi Mungu, je, unaona inaingia akilini kuinasibisha Qur'ani Tukufu na kosa lolote? Nacho ni Kitabu chake alichofunuliwa na Mwenyezi Mungu, akawasomea wafuasi na maadui wake Wafuasi wake wakamwamini na wasiomwamini hawakuweza kukinyanyua vichwa vyao? Au suala la Ufuasi na Uongozwaji linasihi pamoja na uwepo wa makosa kwa kiwango fulani?
Hapana budi kwamba mfahamiko huu ulionasibishwa kwa Mtume S.A.W, kitu kama hiki ni mfano ulioenda kombo na hauendani na mtiririko wa maisha yake ya heshima wala hauendani na Mazungumzo ya Qur'ani Tukufu yanaoyahusu maisha hayo wala hauendani na akili iliyosalimika ambayo inawatazama Manabii kwa mtazamo wa Heshima na Unyenyekevu.
Wizru ni Mzigo mzito na siyo Dhambi:
Na kwa namna ambayo imeamuliwa hivyo, hakika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukutu {Na tukakuondolea mzigo wako} ina maana tumekuondoshea uzito ulioteremshiwa, iwe alinyongea kwa kutojibiwa baadhi ya maombi yake au tumekuondoshea Shida mbalimbali ambazo zimeikwaza njia yako ya Ulinganiaji. na Hili neno "Wizru" kwa Kiarabu lina maana ya Uzito. Na maana ya kuliweka ni kumtua aliyeubeba mzigo. Na maneno haya yanaelezea hali ya Matatizo na Shida kwa hali ya yule aliyetumiwa mzigo kutokana na ubebaji wake ili ampumzishwe kutokana na uzito huo. [Tazama kitabu cha: At Tahreer Wa At Tanweer 307/16]
Msamaha Kupanda Cheo na Wala sio Kufuta Makosa:
Na Kadhalika Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika Njia Iliyo Nyooka,} Msamaha, kupanda cheo na kuondosha vinavyokwamisha kulifikia lengo la Ukamilifu na wala sio kufuta makosa yaliyotokea hapo kalba.
Na kuomba msamaha ni kufanya yale yanayouhusu uja ambao Mja hupandishwa cheo kwayo na kuwa katika viwango vya Ukamilifu na Cheo bila kikomo; na kwa ajili hii, hakika Kuomba Msamaha ni Ibada anayoitekeleza Mja hata kama hajafanya kosa lolote analoliombea Msamaha kwani kuhisi Upungufu ni alama ya Wafanyaibada vyovyote wafikiapo katika ibada zao.
Na kwa ajili hiyo tunamuona Mtume S.A.W, anasimama Usiku mpaka miguu yake inavimba kwa ajili ya kuutekeleza wajibu huu na kutambua neema ya kuwafikishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kutoka kwa Mughiira bin Shuuba R.A, kwamba yeye amesema: Mtume S.A.W, alikuwa anasimama mpaka miguu yake inamvimba na akaambiwa wewe umesamehewa na Mwenyezi Mungu madhambi yako yote yaliyotangulia, akasema: (nisiwe mja mwenyekushukuru). [Tazama kitabu cha Swahihi Al Bokhari 131/16]
 

Share this:

Related Fatwas