Tulimuahidi Musa masiku thalathini
Question
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Tulimuahidi Musa masiku thalathini natukayatimiza kwa kumi; ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi masiku arubaini. Na Musa akamwambia nduguye Haarun: Shika mahala pangu kwa watu wangu nautengeneze wala usifuate njia ya waharibifu.} [AL AA'RAF 142]
Swali langu kama ifuatayo: Kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimuahidi Musa siku thelathini kwanini akaongeza siku kumi pamoja na kwamba Yeye Mtukufu aliyetukuka anajua kwamba muda wake na Musa utatimia ndani ya siku arubaini? Shukrani na Ninamwomba Mwenyezi Mungu Msamaha kama nimemvunjia adabu Mwenyezi Mungu kwa kuuliza swali kama hilo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Katika swali lako hili hakuna uvunjifu wowote wa adabu, na hakuna chochote lakini hili linakupatia sifa njema, na Uislamu unamtaka Muislamu atumie akili yake na afikirie katika Dini ya Mwenyezi Mungu.
Katika swali lako hili hakuna uvunjifu wowote wa adabu, na hakuna chochote lakini hili linakupatia sifa njema, na Uislamu unamtaka Muislamu atumie akili yake na afikirie katika Dini ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyetukuka ametaja katika Aya hiyo tukufu kwamba maagano yalikuwa na Bwana wetu Musa A.S, siku thelathini, kisha Mwenyezi Mungu akaongeza siku kumi zingine na jumla zikawa siku arubaini, na huu ndio uwazi wake, na hivi ndivyo Mtume Musa alivyokuwa anajua.
Na Aya ya Suratu AL BAQARAH imetaja kuwa maagano yalikuwa siku arobaini ya kwanza, na hayo yalikuwa katika Elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi hakuna upingano baina ya Aya zote mbili.
Basi Aya ya Suratu ALBAQARA huambia yaliyopo katika Elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Aya ya Suratu AL AA'RAF huambia yaliyoambiwa Bwana wetu Musa A.S. na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na kuhusu ni kwanini Mwenyezi Mungu Mtukufu Alimwambia Mtume Musa A.S, hivyo? na kwanini hakumwambia tangu mapema siku arubaini? Hiyo ni kwa njia ya kufanya ibada hatua kwa hatua. kama awafanyiavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu waja wake wote. Na akamjaalia muda wa kunong`ona naye uwe siku thelathini kwa ajili ya kumrahisishia, na akwambia hivyo, na baada ya kuukamilisha katika moyo wake uchamungu uliongezeka pamoja na mfungamano wake na Mola wake, kwani kwa kunongona na Mwenyezi Mungu na kumwabudu akaongeza siku kumi na jumla zikawa arubaini nao ni muda anaoujua Mwenyezi Mungu Mtukufu tangu Kale.