Juju-wa-Maajuju

Egypt's Dar Al-Ifta

Juju-wa-Maajuju

Question

 Na vipi kuhusu Yajuja-wa-Maajuja katika Qur'ani Tukufu?

Answer

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kutajwa kwa kisa cha Yaajuja na Maajuja katika Qur'ani Tukufu katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya Dhul-Qarnaini (Mwenye pembe mbili):
{Hata alipo fika matokeo ya jua aliliona linawachomozea watu tusio wawekea pazia la kuwakinganalo. Ndio hivyo hivyo. Na Sisi tulizijua vilivyo khabari zake zote. Hata alipo fika baina ya milima miwili, alikutanyuma yake watu ambao takriban hawakuwa wanafahamu lolote. Wakasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Hakika Yaajuuja-wa-Maajuja wanafanya uharibifu katika nchi. Basije, tukulipe ujira ili utujengee baina yetu ngome? Akasema: Yale Mola wangu aliyo niwezesha ni bora zaidi. Lakini nyinyi nisaidieni kwa nguvu zenu.Nitakujengeeni kizuizi baina yenu na wao. Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipo ijaza nafasi iliyo kati ya milima miwili, akasema: Vukuteni.Hata alipo kifanya (chuma) kama moto akasema: Nileteeni shaba iliyo yayuka niimwagie. Basi hawakuweza kuukwea, wala hawakuweza kuutoboa.} [AL KAHF.90-97]
Mwalimu Sheikh Ahmad Hassan Al Baqoriy Waziri wa Waqfu aliyepita – Mwenyezi Mungu amrehemu- alitoa kitabu anuani yake ni: "Wanakuulizia Dhul-Qarnaini!" na hiyo ni tafsiri kwa utafiti ulioandikwa na Maulana Sheikh Abu Al Kalam Azad kwa lugha ya Kiurdu, juu ya kuainisha uhusiko wa mja huyo mwema –Mwenye pembe mbili- na kuelezea safari yake. Kitabu hicho kilichapishwa katika maktaba ya uchapishaji ya Ash Sha'ab mwaka wa 1970.
Na Sheikh Daktari AbdulMune'm An Nemr – Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu- Waziri wa waqfu pia, aliandika kitabu juu ya Abu Al Kalam Azad, na aliunga kwa juzu yake ya kwanza tafsiri ya utafiti huo, pia ilikuja kwamba mfumo sahihi katika mtazamo wa sheikh huyo –Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu- ni ufuatano sababu ya kuteremka Aya hiyo katika Qur'ani Tukufu, na katika sababu ya kuteremshwa inafahamika kuwa waulizaji ni mayahudi au washirikina kwa amri ya mayahudi.
Na juu ya hivyo, Kisa hiki kinaanzia hapa, na Sheikh alielekea katika Agano la Kale akitafuta utajo wa mtu huyu Dhul Qarnaini (Mwenye Pembe Mbili) na kukuta kuwa alitajwa ndani yake mara tatu katika sehemu tofauti katika Agano la Kale, na Sheikh - Mola amrehemu - akakuta kwamba sifa hizi zilizotajwa na Qur'ani Tukufu na kutakaswa na Taurati zinaendana na Mfalme Ghorshi au Korshi wa pili wa kiajimi, ambao alitawala kutoka mwaka wa 550-529 kabla ya kuzaliwa Nabii Issa.
Na Sheikh hakusita hapo bali alirejea katika yale yaliyoandikwa na Wanahistoria wa Kigiriki kisha akaenda yeye Mwenyewe kuyatembelea Mabaki (magofu) ya Kale ya Irani ya Kale na akasoma vitabu vya Wanachuoni na Mabaki ya kale ndani yake, kisha akajua kwamba imedhihiri kutokana na kuchimbwa kwa Mabaki ya Sanamu lililochongwa kwa jiwe la Korshi ni mwenyewe na juu ya kichwa chake kuna taji ambalo katika pembe zake kuna Mapembe, hapo ndipo alipopata uhakika kamili kwamba huyu Korshi ndiye anayekusudiwa na Qur'ani Tukufu kuwa Mwenye Pembe Mbili .
Na Sheikh Mola amrehemu baada ya hapo akaamua kulinganisha baina sifa zilizoandikwa na Historia kuhusu mfalme huyu na yale yaliyotajwa ndanio ya Qur'ani Tukufu na Historia.

 


Bwawa la Yaajuja wa Maa'juja:
Kwa kukamilisha utafiti Sheikh aliona kwamba ni lazima kuainisha sehemu la Bwawa hili na kwa kusoma kwa umakini historia na kurejea maandiko ya Taurati na yaliyomo ndani yake kuhusu Yaajuja na Maajujaa na alifikia ya kwamba Bwawa hilo lilijengwa katika Mlango wa Bahari wa Kaukas nao ni Mlango wa Bahari ambao hao walitokea hapo katika Eneo lililopo kati ya Bahari ya Caspian upande wa Mashariki na Bahari Nyeusi upande wa Magharibi.
Kisha Sheikh anaiunga mkono rai yake kwa kutumia maandishi ya Kiarmenia ya Kale, akisema: Hakika maandishi ya Kiarmenia yana Umuhimu wake kwani ni ushahidi wa ndani, na ukuta huu uliitwa kwa jina la Kiarmenia tangu zama za kale zilizopita kwa jina ya "Bahaak Ghuraa'i".
Na neno Kabat Ghuraa'i lina maana ya Mlango wa Bahari wa Goresh, au njia ya Goresh, na anaongeza ushahidi mwingine kutoka kwa Watu wa Jojia ambao waliupa jina Mlango huu tangu Kale kama Lango la Chuma. [Tazama kitabu cha: "Wanakuulizia Mwenye Pembe Mbili" Uk. 79 na kurasa zinazoifuatia. Na Tazama kitabu cha: Abu Al Kalam Azad, juzu ya kwanza, Uk. 174 na kurasa zinazoifuatia kwa kueleza Zaidi].
Na miongoni mwa walioshughlikia kisa cha Mwenye Pembe Mbili, ni Dkt. Ezz Edeen Abdulqader, na aliandika utafiti wa kisaikolijia, ulitangazwa na Sheikh Abdullah Bin Asw Swdeeq katika kitabu kimoja kutika vitabu vyake.
Basi alitaja kwanza: Mikanganyo ya Kisa hiki na Muulizaji ni kwamba wao ni katika Mabwana wa Kikureshi na nyuma yao kuna Wayahudi wa Yathrib kisha Aya za Qur'ani Tukufu kisha kunafuatia utajo wa Dhul-Qarnaini (Mwenye Pembe Mbili) katika vitabu vya Wayahudi na katika Kitabu cha Nabii Isaya na katika ndoto ya Nabii Danyeli aliyoiona ndotoni baada ya kupita miaka hamsini ya Familia ya Babiloni na ndoto hii kwa ufupi ilikuwa inasema kwamba yeye alimuona kondoo mwenye nguvu ndotoni ana pembe mbili ndefu anapiga kwazo upande wa Magharibi na Mashariki kisha akaliona beberu la mbuzi likitokea upande wa Magharibi huku likiwa na pembe moja, na macho yake yamejitokeza kwa mbele na lilipomjongelea Kondoo yule, Kondoo akalipiga pembe na kuivunja pembe yake moja na kisha akaliua.
Na Kitabu hicho kinasema kwamba Jiburilu A.S, alimfafanulia Mtume Danyeli ndoto yake kwamba yule Kondoo ni Mwenye Pembe Mbili nayo ni alama ya muungano wa Falme mbili zilizo jirani ambazo ni Midia na Uajemi, huko Irani, Mfalme mmoja anazimiliki na Nchi haina uwezo wa kupambana naye, na kwa upande wa Beberu, mwenye pembe moja, Jiburilu alimfasiria kwamba hiyo ni alama inayoonesha Mfalme wa Ugiriki.
Na Wayahudi katika Babilon walikuwa wanayahitaji mno matumaini haya ambayo yangeinua kiwango cha ari yao na hivyo ndivyo alivyotajwa Dhul-Qarnaini katika ndoto hii kama Ishara na alama ya jambo hili, na Sheikh -Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu – anaona ya kwamba aliyekusudiwa kwa swali la Makureshi hakika mambo yalivyo ni Goresh Mwajemi kisha ikasemwa kwamba ana yeye katika Taurati utabiri na tatu ni katika Kitabu cha Primiya kisha akalinganisha baina ya Alexandra na Goresh na akapitisha kwamba kinachokusudiwa katika Aya hizi ni Goresh.

Kundi la Mashubha ya Posta ya Dar Iftaa


1- Kitenzi Ata “Kimekuja” kwa Jina la Mtendaji
badala ya Kitenzi Kisokikomo
Aya ya Qur'ani: {Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi. Bali wema ni anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi, na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanaovumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao} [AL BAQARAH: 177].
Maana za kijumla
Katika Aya Tukufu kuna ufafanuzi wa maana ya neno wema ambalo halina maana ya kuelekea nyuso pande za Mashariki na Magharibi bali wema wa kweli ni katika kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuamini Siku ya Mwisho pamoja kuamini Malaika, Vitabu Sahihi vya Mbinguni pamoja na kuamini Mitume, na katika sura za imani ya kweli ni kutoa mali katika kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwapa watu wa karibu pia mayatima, masikini, wasafiri wenye kuomba na kumkomboa mtumwa, kudumisha ibada ya Sala pia kutoa Zaka na kutekeleza ahadi na kusubiri katika shida, hizi ndizo alama za ukweli na ucha-Mungu.
Nini amesema mjenga hoja?
Kilicho sahihi ni kusema: lakini wema ni kumwamini Mwenyezi Mungu kwa sababu wema ni imani na si Muumini( ).
Asili ya shaka
Aya imeelezea kuhusu wema nao unabeba maana ya kiakili kwa Muumini “Mwenye kuamini” ambaye ni nafsi, hii kilugha haifai kwa sababu kuelezea maana ya kiakili haifai isipokuwa kwa maana ya kiakili inayofanana nayo.
Kuondoa shaka
Katika mifumo ya ufikishaji zaidi wa lugha ya Kiarabu:
Muulizaji kutokujua sifa za lugha ya Kiarabu ambayo Qur`ani Tukufu imekuja kwa lugha hiyo, nayo ni sifa ya ufikishaji zaidi kimaana, na katika mifumo ya ufikishaji kimaana ni kuleta habari kwa jina la nafsi “Mwenye kuamini” kwa maana ya Muumini badala ya kuleta kitenzikisokikomo “Imani” kwa maana ya kuamini, ikiwa unataka kufikisha sifa ya uadilifu wa mwanadamu basi kauli yako kusema fulani adilifu ni sahihi zaidi kuliko kusema fulani mwadilifu au anafanya uadilifu, na katika hilo kuna kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Mwaonaje, yakiwa maji yenu yanapokauka}[AL MULK: 30], wala hakusema maji yenu yamekauka au yana kauka bali amesema “Kukauka” nayo ni kitenzikisokikomo ili kuelezea ufikishaji zaidi wa kukauka maji.
Miongoni mwa maneno ya Waarabu yanayokubaliana na hilo
Ama watu wa Farraa wamefanya “Mwenye kuamini” imekaa sehemu ya imani na wakasema: Waarabu hufanya jina kuwa habari ya kitenzi, na wakaleta ushahidi wa hilo kwenye kauli ya mshairi:
Umri wako ujana si kuota ndevu bali ujana ni kila kijana aliyeitwa. Ambapo mshairi amefanya kuota ndevu ni habari ya kijana. Na maana yake: Umri wako ujana si kuota ndevu.
Kauli ya Nabigha.
Niliogopa na kuongezeka woga wangu .. juu ya kuogopa katikati ya mwenye akili timamu
Kwa maana wema ni kuamini au mwema inamaanisha kuelezea maana na wala si kuwepo kiwango cha wema. Na kutoka kwa Al-Mubarrad: Lau ningekuwa katika wasomaji ningesoma lakini wema kwa silabi ya fat’ha kwenye herufi ya Baa ya neno Birra kana kwamba anataka kuachana na makadirio katika habari ya kuhusu wema kwa jumla “Mwenye kuamini” kwa sababu mwenye kuamini huyo ndio mwema na wala si wema wenyewe, ni vipi anasoma hivyo na neno “Birra” limeungana na neno lakini ambapo haiwezikuwa isipokuwa ni wema wenyewe hivyo hakuna yeyote aliyesoma isipokuwa ni kwa kutamka “Al-Birra” kwa silabi ya kasra kwenye herufi ya Baa, kwa kuwa visomo vimepokewa wala sio vitu vya hiyari na huenda hili si sahihi kwa Mubarrad.
Kauli nyingine inayofahamisha maana ya Aya Tukufu
Kauli ya Kwanza: Katika melezo ya Aya kuna maneno yaliyoondolewa ambayo yanakadiriwa kuwa. Lakini wema ni kwa mwenye kuamini.
Hii ni kauli ya Siibawayh na msukumo wake wa kuipa nguvu ni kuwa imekuja baada ya kufahamika, na ambalo linafahamika linapaswa kuwa katika aina ya iliyetokewa na hali ya ukanushaji hapa ni neno “Wema”.
Kauli ya Pili: Maelezo ya neno “Wema” kwa maana ya “Mwema”.
Kauli ya Tatu: Kitenzikisokikomo nacho ni neno Birra kwa maana ya “Wema” kiwe sehemu ya jina la mtendaji katika hali ya ufikishaji.
{Na wewe ni mkazi wa Mji huu}[AL BALAD: 2].
{Je, mnafanya kuwanywesha maji Mahujaji … ni sawa na mwenye kumuamini}[AT TAWBAH: 19].
Kitabu cha Tahrir wa Tanwir – 2/ 110.
Na kuali yake: {Bali wema ni mwenye kuamini} ni habari kuhusu kitenzikisichokikomo kwa jina la nafsi kwa lengo la uzidishaji wa ufikishaji.
Hakuna la ajabu kwenye hali ya “Mwenye kuamini” kuwa ni habari ya neno “Wema” ni sawa sawa ikiwa tumechukua kwa maelekezo ya Sheikh wa mambo ya sarufi Siibawayhi, kuwa katika maelezo kuna yaliyoondoshwa ambayo yanakadiriwa kuwa “Lakini wema wema wa mwenye kuamini” au tumechukua kwa maelezo ambayo yamepitishwa kuwepo kwa kitenzikisokikomo sehemu ya jina la mtendaji au mtendaji mwenyewe … hii yote ni mifumo ya lugha fasihi ya Kiarabu inayotumika, miongoni mwa ushahidi wake ndani ya Qurani ni pamoja na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na wewe ni mkazi wa Mji huu} kumekuwepo na kitenzikisokikomo ambacho ni neno Hillu kwa maana ya “Mkazi” sehemu ya jina la mtendaji “Haalu” kwa maana ya mkazi wa mji huu.
Ikiwa tutaelekeza sura zetu upande wa fasaha baada ya sarufi na lugha basi balagha ni pana zaidi kuliko sarufi na lugha, ambapo tunatazama maelezo ya Qur`ani “Lakini wema ni anayeamini” ni maana ya kina zaidi yenye faida kubwa kwa sababu “Mwenye kuamini” inaonesha wenye imani ndani ya nyoyo zao kwani imani ni “Mkazi” katika nyoyo hizo, ikiwa kutasemwa: “Bali wema Imani” ingekuwa hii imani ni ibara ya fikra tu isiyo na sehemu, bali yenyewe imetengwa na nafsi, kwa maana imani ya kimtazamo na wala si ya vitendo na hii si sawa, lakini pindi ilipofanywa hii imani sifa ya nafsi iliyoelezewa na neno “Man” kwa maana ya “mwenye” kushikamana imani na Muumini, Muumini na imani na kubadilika kuwa imani ya vitendo iliyojikita kwenye nyoyo, ikikabiliana na imani ya umbo ambayo haijaridhiwa na Qur`ani, nayo ni kuelekeza nyuzo upande wa Mashariki na Magharibi.
Jibu: Anasema Imamu Razy kuwa katika Aya hii yameondolewa maneno ya ziada kama vile angetaka kusema “Bali wema wote ambao unapelekea kwenye thawabu nyingi wema wa aliyemuamini Mwenyezi Mungu” na Aya inayofanana na hiyo na inakadiriwa:
Hivi watu wanaonywesheleza maji mahujaji ni sawa na mwenye kuamini? Au mnafanya kuwanywesheleza mahujaji sawa na imani ya mwenye kuamini? Na kuwepo uwakilishi kati ya vitenzi viwili visokikomo au kati ya watendaji wawili, ambapo hakuna uwakilishi kati ya kitenzikisokikomo na mtendaji.
Na huenda akakusudiwa mtu mwenyewe na kuwa neno Birri “Wema” hapa maana yake “Mtenda mema” mfano wa Aya inayosema: {Na mwisho mwema ni kwa mcha-Mungu} [TWAHA: 132]. Kwa maana ya wacha-Mungu, na mfano wa Aya hii kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je mwaonaje, yakiwa maji yenu yamekauka} [AL MULK: 30], kwa maana yenye kukauka.
Na huenda maana yake ikawa “Bali mwenye wema” kama vile kauli yake Mola Mtukufu: {Hao wana vyeo mbalimbali kwa Mola wao} [AAL IMRAAN: 163], kwa maana ya wenye vyeo.
****



2- Kitenzi Ata “kimekuja” kwa Jina la Wingi
badala ya Jina la Wawili
Aya ya Qur`ani: {Kama nyinyi wawili hamkutubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwisha elekea huko. Na mkisaidiana dhidi yake (Mtume), basi hakika Mwenyezi Mungu ndiye kipenzi chake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia} [AT TAHREEM: 4].
Swali: Ni kipi alichokisema mjenga hoja?
Na maelezo hayo kama anavyosema Al-Baidhawiy, yanaelekezwa kwa Bi Hafwa na Bi Aisha, basi ni kwa nini hakusema, nyoyo zenu nyinyi wawili zimeshaelekea badala ya imeshaelekea nyoyo zenu ambapo haikuwa kwa wawili kuwa na zaidi ya nyoyo mbili ( ).
Kuondoa shaka
Muulizaji hafahamu kuwa miongoni mwa sifa za lugha ya Kiarabu ambayo Qur`ani Tukufu imeteremka kwa lugha hiyo ni kuwepesisha katika utamkaji wakati wa kutumika matamshi, miongoni mwa uwepesishaji huu ni kutorudia dhamiri ya watu wawili kwani muundo wa uwili ni mzito kutokana na uchache wa matumizi yake katika maneno ya Waarabu, pindi ilivyoondoka hali ya kutofahamika, maelezo yakaja kwa muundo wa wingi badala ya uwili, na hii ni kawaida ya Qurani kwani imekusanya Aya nyingi ndani ya Qurani Tukufu miongoni mwake Aya Takatifu ambayo ameithibitisha muulizaji, na pia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mwizi mwanamme na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyo ya chuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hekima} [AL MAIDAH: 38].
Na matumizi zaidi ya Waarabu na yaliyofasihi zaidi katika hayo ni pamoja na kuelezea tamko la uwingi kwa kuongezea jina la uwili kwa sababu muundo wa uwingi hutumika pia kwa wawili katika maneno ambapo kwa upande wa hao wawili yanafanana. Na matumizi haya kwa Waarabu hayana kipimo, hivyo katika kila jina la wawili lililoongezwa jina la wawili kinachoongezwa kinakuwa uwingi kama vile katika Aya hii.
Tafasiri
Hii ni kwa upande wa matamshi, ama kwa upande wa maana na dalili katika Aya mbili kuna maana nzuri sana na muujiza nao ni kuchunga tamko pamoja na maana yake.
Kuchunga tamko katika uwili ulioongezewa neno “Kumaa” katika neno “Kuluubikumaa” kwa maana ya nyoyo zenu wawili.
Kisha kuchunga maana katika uwingi wa mikono na nyoyo.
Na uwingi wa mikono na nyoyo umekuja ukiwa umebeba maana yenye kufahamika katika vidokezo vya sehemu kwa upande wa ukweli katika wingi wa mikono.
Na sababu katika uwingi ndani ya Aya Tukufu ni kuwa kila mmoja kati ya Mabibi wawili Hafswa na Aisha kulikuwa nyuma yao na idadi ya wake wa Mtume S.A.W. ( )

****

 

 

Share this:

Related Fatwas