Roho za Mashahidi Zipo Katika Umbi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Roho za Mashahidi Zipo Katika Umbile la Ndege wa Kijani.

Question

 Aya yenye kuleta shaka:
Imekuja ndani ya Quran:
{Wala usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali wapo hai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi} [AAL-IMRAAN: 169].
Na imepokelewa Hadithi na Ibn Abbas kuwa Mtume S.A.W amesema: “Roho za mashahidi zitakuwa kwenye umbile la ndege wa kijani zinaruzukiwa vinywaji vya mito ya Peponi na kula matunda yake na zinakwenda kwenye taa iliyotundikwa chini ya Arshi”.
Tunauliza: Ikiwa Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu katika umbile zuri hivi inakuwaje anapokwenda peponi anamshusha na kuwa katika umbile la ndege? Na watu waovu motoni wanakuwa na miili ya nyani na nguruwe, na waja wema peponi wanakuwa kwenye maumbile ya ndege?

Answer

 Aya Tukufu imeelezea yale yaliyoandaliwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya wale waliouwawa katika njia yake kuwa malipo yao kutokana na kujitoa kwao muhanga kwa maisha yao katika njia yake kuwafanyia maisha ya kudumu yasiyokuwa na kifo, zingatia kauli yake Mola Mtukufu:
{Bali wapo hai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi} [AAL-IMRAAN: 169. Ambapo inakuonesha kuwa uhai huu ni maalumu usiofuata mfumo wa uhai ambao watu wanaishi, “Sio uhai unaofahamika kwenye ulimwengu huu, ninamaanisha maisha ya miili na utembeaji wa damu kwenye mishipa pamoja na mapigo ya moyo, wala si uhai wa roho zilizothibiti kwenye roho za watu wote, vile vile riziki inapaswa kuwa sawa na uhai wa roho nayo ni riziki ya neema za peponi” ( ).
Kisha inakuja Hadithi Takatifu kutaja kuwa roho za mashahidi zinaneemeshwa kwenye matumbo wa kijani wa peponi, na hii ni ufafanuzi wa hali katika hali za uhai huu unaohusiana na roho za mashahidi, na ulimwengu wa roho ni ulimwengu usioonekana kwa macho na wala haufuati kanuni za ulimwengu wetu.
Kama vile hii imepokelewa katika upokezi wa kukirimiwa kwa mashahidi na wala si kudharau ubinadamu wake ila ni ukarimu ambao Mwenyezi Mungu ameufanya bali ni ukarimu juu ya ukarimu.
Kwa vile hilo si makusudio ya Hadithi kuwa roho zinahama kutoka kwenye mwili ili mwisho zipate kutulia, jambo hili ndio kauli ya mwili kuvaa roho na hii si katika imani za Waislamu, bali makusudio yake ni yale yaliyokuja katika Hadithi ya Mtume S.A.W: “Hakika roho za Waumini zimekuwa umbile la ndege zinazoruzukiwa kwenye miti ya Peponi mpaka Mwenyezi Mungu atapozirudisha siku ya Kiyama kwenye mwili wake……” ( ).
Imeonesha kuwa roho zitakuwa ni kama mfano wa ndege wa kijani katika kuishi na haraka ya kutembea na kuruka wala sio zenyewe ni ndege wa kijani, hivyo inakuwa ni ufananishaji wa roho na ndege ( ).

 

 

 

Share this:

Related Fatwas