Piga Jiwe kwa Fimbo Yako

Egypt's Dar Al-Ifta

Piga Jiwe kwa Fimbo Yako

Question

Aya yenye kuleta shaka:
Imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu:
{Na Musa alipo omba maji kwa ajili ya watu wake, tulimwambia: Lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikachimbuka chemchem kumi na mbili; kila kabila likajua mahali pake pa kunywea} [AL-BAQARAH: 60].
Na ikasema tena:
{Na tuliwagawanya katika makabila kumi na mbili, mataifa mbali mbali. Na tulimfunulia Musa walipomuomba maji watu wake kumwambia: Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako. Mara zikachimbuka humo chemchem kumi na mbili, na kila watu wakajua mahali pao pa kunywea} [AL-AARAAFaaf: 160].
Na imekuja katika Kitabu Kitakatifu: “Wakafikilia Elimu palipokuwa na chemchem kumi na mbili, na mitende sabini, wakapanga hapo, karibu na maji.
Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama Bwana alivyowaagiza, wakatua Refidimu napo hapakuwa na maji, watu wanywe.
Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe, Musa akawambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu Bwana?
Watu wakawa na kiu huko, nao wakamnung’unikia Musa, wakasema. Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu? Musa akamlilia Bwana akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe. Bwana akamwambia Musa, pita mbele ya watu, ukawachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe, na ile fimbo yako ambayo uliupiga mto kwayo, uitwae mkononi mwako, ukaenda.
Tazama nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu, nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli”. Kitabu cha Kutoka 15: 27 na 17: 1 – 6.
Hapa kuna tofauti kati ya Qur`ani Tukufu na Kitabu Kitakatifu, wala sio chemchem kumi na mbili ambapo kipo Elimu ni jabali ambalo lipo Horebu.
 

Answer

Kauli yao: Katika eneo la Elimu kuna chemchem kumi na mbili za maji na mitende sabini, haioneshi kwa ukaribu wala kwa umbali yaliyokuja kwenye Aya, wala Aya haikusudii, kwa sababu ni wazi kuwa chemchem hizi ni visima vya zamani vya maji, na wala sio chemchem ambayo ilichimbuka pale Musa alipopiga jiwe, dalili ni yaliyokuja kwenye Kitabu Kitakatifu chenyewe kuwa wao walifika Elimu na hapo kuna chemchem kumi na mbili za maji na mitendo sabini wakapanga hapo karibu na maji, hivyo visima vipo kabla ya kuja kwa Nabii Musa Amani ya Mungu iwe kwake sehemu hiyo.
Ama jabali ambalo lilipasuka na kutoa chemchem Qur`ani Tukufu wala haikuelezea sehemu ya jabali hilo bali imetaja muujiza huu ambao Mwenyezi Mungu aliufanya kupitia mikononi mwa Nabii wake Musa A.S ili kuwakumbusha wana wa Israeli neema ambazo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha baba zao, ili hilo liwe msukumo kwenye imani na kumuamini Mtume wetu Muhammad S.A.W. Mwenyezi Mungu akawakumbusha hali ya Nabii wa Mungu Musa A.S pindi alipotakiwa kuwanywesha maji watu wake Mwenyezi Mungu akamuamrisha kupiga jiwe kwa fimbo yake, baada ya kupiga ikachimbuka kwenye jiwe hili chemchem kumi na mbili sawa na idadi ya makabila ya wana wa Israeli, na mgawanyo huo ni kutokana na kuwafanyia kwake huruma ili wasisongamane kwenye kunywa maji kwa uwingi wao na wakauwana, na akawaamrisha kula na kunywa katika riziki za Mwenyezi Mungu na kuwatahadharisha vitendo vya kueneza uharibifu duniani.
Imebainika kupitia maelezo yaliyopita kuwa Qur`ani haikusema sehemu hii ya jabali ni Horebu au sehemu nyingine lakini yamesemwa hayo kwenye Kitabu Kitakatifu.
Kisha Kitabu Kitakatifu hakijatuambia kuwa jabali ambalo Musa alilipiga na kwa fimbo yake ndio lililochimbuka chemchem za maji au hapana? Lakini Qur`ani ndio ambayo imetuambia kuwa jabali au mwamba ulichimbuka visima vya maji na idadi yake ni visima kumi na mbili, hakuna kizuizi chochote kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwatolea visima kumi na mbili huko Horebu kama vile visima kumi na mbili vilivyopo Elimu ili wapate kukumbuka neema za Mwenyezi Mungu kwao.
Na mwisho kabisa, tunakuta kuwa kisa cha Musa kupiga jiwe na kutoa maji ili wapate kunywa wana wa Israeli ni jambo limekubalika na Qur`ani sawa na jumla iliyokuja kwenye Kitabu Kitakatifu, na kwa hali hii hapa hakuna shaka inayoelekezwa kwenye Qur`ani.


 

Share this:

Related Fatwas