Kutenzwa Nguvu Kutoa Zaka

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutenzwa Nguvu Kutoa Zaka

Question

Imekuja kwenye kitabu cha historia ya Waislamu kuwa Abubakri Swiddiq alimtuma Khalid Ibn Waliid ili kupambana na watu wanaozuia utoaji zaka, akakusudia kwenda Batwah ili kupigana na Malik Ibn Nuwairah, akaendelea mpaka akamshambulia na watu wake wakarudi kutoa zaka.
Tunauliza: Ikiwa zaka ni nguzo katika nguzo za dini na dini ya Mungu je dini inaweza kuzingatiwa ni dini iliyonyooka ikiwa inaendesha mambo si kwa utashi na kujitolea bali na nguvu na kutenza nguvu! Zaka inakusanywa na upanga wa Khalid Ibn Waliid na watu wa mfano wake. Mwenyezi Mungu anapinga kwa sababu si katika wema.
 

Answer

 Zaka ni nguzo katika nguzo za dini ya Kiislamu, kwani Mwenyezi Mungu ameilazimisha kwa kila Muislamu mwanamme au mwanamke kwa sharti maalumu limeletwa na Sharia ya Kiislamu nalo ni, Uhuru, Kufikia kiwango, Kutimiza mwaka kamili wa Kiislamu wa kumiliki kiwango, hivyo zaka ni haki iliyowekwa kwa mtu aliyetimiza masharti haya, na wala si jambo la wema la kujitolea kwa hiyari, kwani Amesema Mola Mtukufu: {Na katika mali zao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba} [ADHARIYAT: 19].
Hukumu za Kisharia zipo zisizofungamana na maslahi ya waja zenyewe ni kati ya mja na Mola wake kama vile ibada ya funga kwa mfano, na hukumu zingine zinafungamana na maslahi yao kama vile zaka, na huonekana umuhimu wa zaka kwa upande wa kiuchumi kwa jamii ya Kiislamu, kwani yenyewe husaidia watu masikini wagonjwa mayatima na wengine, ikiwa watu watasimama au kusitisha kutoa zaka na akazembea mtawala au kiongozi mkuu katika kukusanya, hilo linapeleka kukwamisha Sharia katika Sharia za Uislamu, na hupelekea pia uharibifu mkubwa wa kiuchumi kwa jamii, kwa sababu hawa watu hawapati wa kuwasaidia hivyo ima wafe kwa njaa au waende kinyume, na huu ndio uharibifu tuliokatazwa na Uislamu kuufanya au kuandaa mazingira ya sababu zake, hivyo Sharia imemlazimisha kiongozi mkuu kukusanya zaka kwa wale waliowajibikiwa kutoa ili kuepuka kutokea uharibifu huu, na kiongozi mkuu anapaswa kuwataka watubie wale wenye kujizuia kutoa zaka, ikiwa waterejea na wakatoa zaka basi hakuna tatizo lolote, lakini wakiendelea na msimamo wao wa kuzuia kutoa zaka basi kiongozi atambana nao, ama adhabu yao siku ya Kiyama imetajwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwenye kauli yake:
{Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie habari ya adhabu iliyo chungu * Siku zitapotiwa moto katika Moto wa Jahannamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mlio jilimbikizia nafsi zenu, basi onjeni mliyo kuwa mkilimbikiza} [AT-TAWBAH: 34 – 35].
Tunakuta kuwa aliyoyafanya Swahaba Abubakri Swiddik Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe kwake katika kupigana vita na wanaojizuia kutoa zaka si jambo geni lenye kupingwa, kwa sababu serikali nyingi hutangaza vita kwa wenye kwenda kinyume na sheria za nchi ambazo zinandesha maisha ya watu na kujaribu kutoka kuharibu, na hili ndilo alilolifanya Abubakri R.A kwa hawa waliotoka kwenye Uislamu na kuwa nje ya mfumo wa dola ya Kiislamu, wakiwa wenye kukusudia kuharibu.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas