Mtume S.A.W. Na Kufuru ya Washirik...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mtume S.A.W. Na Kufuru ya Washirikina.

Question

Aya yenye shaka:
Ndani ya Qur`ani imekuja kauli ya Mwenyezi Mungu:
{Na hakika walikaribia kukushawishi uache tuliyokufunulia ili utuzulie mengineyo. Na hapo ndio wangelikufanya rafiki.* Na lau kuwa hatukukuweka imara ungelikaribia kuwaelekea kidogo * Hapo basi bila ya shaka tungeli kuonjesha adhabu maradufu ya uhai, na adhabu maradufu ya kifo. Kisha usinge pata mtu wa kukunusuru nasi * Na walitaka kukukera ili uitoke nchi. Na hapo wao wasingelibakia humo ila kwa muda mchache tu * Huo ndio mwenendo kwa Mitume tulio watuma kabla yako. Wala hupati mabadiliko katika mwenendo wetu} [AL ISRAA 73-77].
Sisi tunauliza: Hivi Aya hizi hazioneshi kumili na kuelekea kwa Nabii wa Kiislamu kwa washirikina na kuwafuata kwenye kusifu miungu yao, kisha kutaka kwake msamaha kwenye hili kwa sababu Mwenyezi Mungu amemkataza hilo na kumkemea?
 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Aya haioneshi - kwa ukaribu wala kwa umbali – kuwa Mtume S.A.W alikuwa anamili na kuegemea kwa wale wanao waabudu hilo hapana kwa Mtume S.A.W – bali ni kinyume kabisa Aya inakanusha madai ya muulizaji, na kwa maelezo mepesi ya Aya utakuta kuwa yenyewe imetuonesha kwa uwazi kuwa Mtume kuegemea kwao hakupo, wala hakuna ukaribu wa kufanya hilo, na hilo kwa namna nne:
1- Neno “Laula” kwenye Aya ambalo linaonesha kuwa jibu lake limezuilika na maana yake: Kujiegemeza kwao ni jambo lililozuilika kutokea kwa sababu sisi tumekuimarisha.
2- Na kitendo cha ukaribu ambacho ni: “Kidta” chenye kuonesha kuwa hakuingia kwenya uegemezi.
3- Na maana ya kudharau inaonekana kwenye Silabi ya Tanwiin kwenye kauli yake Mola Mtukufu “Shaian”.
4- Na uchache unaonekna kwenye maana ya neno “Kaliilan”.
Na katika hayo maana jumla ya Aya ni: Lau isingekuwa kukufahamisha kwetu upande wa haki ingehofiwa kujiweka karibu na kujiegemeza kidogo sehemu dhaifu lakini hilo halikutokea ( ).
Na zaidi ya inayokuangazia Aya ni ulinzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake na kumuimarisha kutokana na jaribio la watu waovu wasimdanganye Mtume S.A.W na lau isingekuwa uimarishaji wake Mwenyezi Mungu Mtukufu basi udanganyifu wao na vitimbi vyao vingemuongopea na kuingia kwenye yale yanayokwenda kinyume na ufunuo aliofunuliwa, lakini Mwenyezi Mungu ni Mlinzi ambaye anamlinda kwa ungalizi wake na kumkinga na madhambi – hasa katika yanayohusu ufunuo – usimamizi wake ulikuwa ni zaidi ya akili yao.
Hii ndio hali yao ya udanganyifu na upigaji chenga, kama Mwenyezi Mungu Alivyosema akielezea hali yao hii:
{Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wange kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia Haki. Basi sameheni na wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atapo leta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu}[AL BAQARAH 109].
Na akaendelea kusema:
{Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie} [AL QALAM 9]. Na kazi ya Mwenyezi Mungu kwake ni kumlinda na kumsimamia.

Share this:

Related Fatwas