Kiwakilishi jina cha Kiume kwenye ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kiwakilishi jina cha Kiume kwenye Habari ya Jina la Kike

Question

 Aya ya Qur'ani:
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema} {AL-AARAF: 56} na Akasema pia: {Mwenyezi Mungu ndiye aliyeteremsha Kitabu kwa Haki, na Mizani. Na nini kitakacho kujulisha kuwa pengine Saa ya Kiyama ipo karibu?} {AS-SHUURA: 17}.

Answer

 Maana kwa ujumla:
katika Aya ya kwanza Mwenyezi Mungu Mtukufu Anabainisha kuwa waja wake wema wapo karibu zaidi na rehema zake, na katika Aya ya pili Mwenyezi Mungu Anabainisha kuwa kuteremka kwa Qur'ani kulikuwa ni kwa ajili ya haki na uadilifu na Kiyama kinaweza kuwa hivi karibuni.
Nini mjenga hoja amesema?
Ilikuwa inapasa habari ya herufi ya “Inna” ya Kiarabu kufuata jina lake katika kiwakilishi jina cha kike na badala yake neno liwe “Karibah badala ya Karib” kama ilivyokuja kwenye Qur'ani Tukufu ( ). Na akasema sehemu nyingine kuhusu Aya ya pili, ni kwa nini habari ya Herufi “Laalla” ya Kiarabu haikufuata jina lake katika kiwakilishi jina cha kike na neno likawa Karibah? ( ).
Yanayochukuliwa kwenye Shaka
Ni kuwa habari ya herufi ya Kiarabu “Inna” katika Aya ya kwanza, na habari ya herufi ya Kiarabu “Laalla” katika Aya pili zipo kinyume na kanuni inayofahamika ambayo habari inakuwa sifa ya Kima katika maana, na kwa hili Aya mbili Takatifu zimekwenda kinyume na kanuni ya lugha ya Kiarabu ambapo imekuja ndani ya Aya hizo mbili sifa ya kike kwa muundo wa kiume na inafahamika kuwa sifa inapaswa kukubaliana na kinachosifiwa katika kiwakilishi jina cha kiume na kike.
Kuondoa shaka
Tofauti kati ya ukaribu na umbali ni kiasilimia na sehemu:
Wanachuoni katika shaka hii wametaja kauli nyingi za kujibu( ) kwa kweli amenitangulia Dkt. Abduladhim Al-Muity katika kuelezea na yeye pia akatanguliwa na Mwanachuoni Tahir na hiyo ndiyo kauli ya Furaa na Abi Ubaidah: “Neno Karibu au Mbali pindi linapotumika kwenye ukaribu wa kinasaba au umbali wa kinasaba basi linapaswa kuwa na kiwakilishi jina cha kike kwa herufi ya Kiarbu ya Taa, na pindi likitumika kuelezea ukaribu wa masafa au umbali wake basi inafaa kuendana na kinachosifiwa na inafaa pia kiwakilishi jina cha kiume kwa kuelezea sehemu, na hiyo ndiyo imetumika zaidi. Mwenyezi Mungu Amesema: {Na haya hayako mbali na wenye kudhulumu wengineo} {HUUD: 83} na akasema tena: {Na nini kitakujuvya? Pengine hiko Kiyama kipo karibu} {AL AHZAAB: 63} pindi ulipotumika kwenye Aya hii muundo wa kuazima neno ukaribu wa masafa imekuwa ni kawaida iliyoenea kutumika kwa maana ya halisi ( ).
Na katika Aya Tukufu ukaribu uliotajwa sio kusudio ukaribu wa kinasaba hivyo ikalazimika uwepo wa kiwakilishi jina cha kike bali kusudio ni ukaribu wa muda, na Waarabu hupitisha hali mbili kutumika kiwakilishi jina cha kike na kiume.
Ni kwa nini kanuni hii
Mara nyingi imekuwa ikisikika masikioni mwa wanaosoma kuwa katika ujumbe huu elimu ya sarufi ni elimu inayoweka wazi na wala si elimu ya awali, lakini hii haina maana ya kubatilisha hukuu ya kisarufi kama inavyodhaniwa na baadhi, lakini nasema kukubalika kwa hukumu ya kisarufi na kuzingatiwa hukumu hii ni kivuko cha kufahamu roho ya elimu hii na kisha jibu linakuja la swali lililotolewa ikiwa ni mfululizo wa majibu majibu ya maswali, ikiwa itasemwa ni kwanini kanuni hii imekuwa, jibu la kwanza ndio hivi Waarabu wamenukuu kwenye lugha yao, na swali lifuatalo ni kwa nini lugha ya Waarabu imekuwa kwenye namna hii hutenganisha kati ya ukaribu na umbali Katika unasaba na katika sehemu, Imamu Tahir Ibn Ashuur amejibu swali hili ambapo amesema: “Hii ni katika tafauti ndogo za Kiarabu katika matumizi ya pamoja kuondoa sintofahamu kadiri inavyowezekana ( ), na maana hii ni kuwa tamko la karibu na mbali pindi liliposhirikiana kwa upande wa nasaba na sehemu Waarabu wakalifanya kuwa na hali katika maana yake kwenye nasaba nayo ni kukubaliana kwa kinachofisiwa, pamoja na sehemu wakafanya kuwa na hali nyingine inatofautiana na kinachosifiwa, na hii inafanana na kujengea hoja kwa sababu, na busara ya Wanachuoni wa elimu ya asili ya Sharia au yenyewe ni katika upande wa sababu nyingi au hukumu na kuzingatiwa

Share this:

Related Fatwas