Kisa cha Nabii Ayub na Mke wake
Question
Shaka:
Imekuja katika Qur`ani Tukufu: {Na shika kincha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo} ni namna gani inafaa kwa Nabii Ayub ambaye Vitabu Vitakatifu vimezungumzia wema wake na uwingi wake wa kusubiri amkasirikie mke wake na kumuahidi kumpiga fimbo mia eti kwa sababu tu ya kumchelewesha?
Na ni vipi kwa Mwenyezi Mungu Muadilifu inafaa kukubalika hasira zake kwa kukusanya fimbo mia moja ili kumpigia mkewe kwa pigo moja, hivi hukumu hii ni yenye uadilifu?
Na ni vipi inaingia akilini baadhi ya tafsiri zilizopokelewa kuwa mke wa Nabii Ayub alikuwa ni binti wa Nabii Yakub au mjukuu wa Nabii Yusuf, wakati zama za Nabii Ayub zimetangulia zaidi zama za Manabii hao wawili?
Answer
Jibu la Shaka:
Kituo cha tafiti za Kisharia Ofisi ya Mufti wa Misri.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hasira za Nabii Ayub:
Inapaswa mwanadamu kutafautisha kati ya hasira ambayo inatokana na asili ya mwanadamu ambayo inakusanya Manabii na watu wengine wa kawaida na kati ya hasira ya kulaumiwa ambayo inatoka kwa mtu husika kutokana na tabia nzuri, ama hasira asili ya mwanadamu ni jambo la kawaida mwanadamu yeyote hawezi kuepukana nalo hata wale viongozi wa tabia njema miongoni mwa Manabii, kwani mwanadamu ni mwenye hisia zake na jazba zake ambazo Mwenyezi Mungu amezifanya ni katika asili aliyomuumbia, ama hasira za lawama ni mwanadamu kwenda mbali zaidi katika hasira zake na kupelekea kwenye tabia inayomtoa kwenye tabia njema.
Na hali hii ya Nabii wa Mwenyezi Mungu Ayub amani ya Mungu iwe kwake ni hali ya kawaida haiondoshi uwezo wake wala kupunguza sehemu ya subira yake, na kauli ya Manabii wamezuiliwa kutenda dhambi haina maana kabisa kuwa wao hawapitiwi na mambo ya kibinadamu, wao ndio wamefanywa na Mwenyezi Mungu kuwa ni alama ya uongofu wa viumbe ili wapatwe kuigwa na vitendo vya wanadamu, pindi anapochukuwa maamuzi mtu anapaswa kuiga mfano wa Nabii Ayubu pindi mmoja wetu anapofikwa na hasira kuto kwenda mbali zaidi katika hasira zake na kupelekea mambo yenye madhara kwa mwingine, ikiwa ameapa katika hali ya hasira kufanya kitu fulani kisha akataka kufanya jema kwa kiapo chake linalofungamana na haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu basi na ashikamane na kimbilio litakalo mfikisha kwenye hilo, hivyo aitulize nafsi yake kutokana na maumivu kutomfanyia mtu yeyote jambo lenye madhara kwake.
Kiapo cha Nabii Ayub:
Ama njia ambayo Qur`ani Tukufu imezungumza kuwa Nabii Ayub alifanya wema kiapo chake, yenyewe ikiwa ina maanisha kitu basi ina maanisha huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye alitaka kwa Nabii Ayub kutovunja kiapo chake, vile vile haijapokelewa kwa mke wake kwamba amemsababishia maudhi na kumpiga pigo lenye maumivu, lakini mjenga hoja hafahamu maana hizi hivyo hajui maana ya huruma ya Mwenyezi Mungu.
Je Nabii Ayub alioa binti wa Nabii Yakub au mjukuu wa Nabii Yusuf?
Ama mgongano uliopatikana kupitia baadhi ya tafasiri kuhusu nasaba ya mke wa Nabii Ayub ifahamike kuwa tafauti za mitazamo ya Wanachuoni haitaisha – hata waliozungumzia kwa upande wa Kitabu Kitakatifu – kuhusu zama za Nabii Ayub Amani ya Mungu iwe kwake wapo wenye kusema kuwa aliishi kati ya zama za Nabii Nuuh na Nabii Ibrahimu, na wapo wenye kusema kuwa aliishi kati ya zama za Nabii Isa na Nabii Yakub, na wapo wenye kusema kuwa hao ni watu wawili waliishi ndani ya zama mbili, kwa zote kadhia hii itabaki ni yenye tofauti mbali na andiko la Qur`ani Aya haikuzungumzia kitu chochote katika hivyo wala haikuashiria kabisa nasaba ya mke wa Nabii Ayub, ikiwa hii ni jitihada za baadhi ya wafasiri katika kuainisha haiba ya mke wa Nabii Ayub au kuainisha zama za Nabii Ayub kutokana na mapokezi ya kihistoria, hivyo kupinga jitihada hizo hakukugusi chochote Aya ya Qur`ani, wala hautuletei madhara utafiti kufikia kiwango cha kuainisha zama za Nabii Ayubu Amani ya Mungu iwe kwake au kuainisha nasaba ya mke wake na kuwa sawa na yaliyofikiwa na tafiti za kielimu.