Kuwachukia watu wote

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwachukia watu wote

Question

 Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema:
{Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a'mali zao}. [MOHAMMAD 4]
Na pia Amesema: {Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki, na kuwa mgumu kwao! Na makaazi yao ni Jahannamu. Na hayo ni marejeo mabaya}. [AT TAHREEM 9]
Maana ya Jumla:
Mdai amesema nini?
Katika Aya Tukufu kuwa: Muhammad alipokuwa Makkah, alikuwa na amani na watu wote na akiwaheshimu Mayahudi, Wakristo na Masabiina, na akasema kuwa: Wao wapo Peponi [Suratul AL MAIDAH 5: 69]. Lakini alipokuwa na nguvu zaidi hapo Madina kwa wasaidizi wake (Al-Ansaar), aliamuru kuwaua wote wasiokuwa Waislamu, au kulipa kodi (jizyah), au kusilimu. Hii ina maana ya kujiwekea mipaka katika udugu wa Kiislamu, kuharibu nguzo za udugu wa jumla, na kukata mafungamano ya upendo na kutendeana mema baina ya matabaka ya watu. Hivyo Waislamu wakakataza makazi katika nchi zote za Hijaz kwa kila asiye Muislamu.

Answer

Mizani kati ya udugu wa kibinadamu na udugu wa Kiislamu
Udugu wa kibinadamu: kiunganishi cha ubinadamu
Ubinafsi:
Tatu: Upendo wa Muislamu kwa asiyekuwa Muislamu.
Je, inajuzu kwa Muislamu kuwa na hisia za upendo kwa wasiokuwa Waislamu? Sikilizeni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hivyo basi nyinyi ndio mnawapenda watu hao, wala wao hawakupendeni. Nanyi mnaviamini Vitabu vyote. Na wanapo kutana nanyi husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao wanakuumieni vidole kwa chuki. Sema: Kufeni kwa chuki yenu}.
Kinachokusudiwa na Aya hii ni Mayahudi kwa rai ya wengi wa Wafasiri; na Makafiri kwa rai ya baadhi yao. Na At-Tabariy anasema katika kuitafsiri Aya hii:
(..Basi ikiwa nyinyi Waumini mnaviamini Vitabu vyote, na mnajua ya kwamba niliyowakataza kuwafanya wasaidizi wasiokuwa nyinyi, ni hao Makafiri katika kukanusha hayo yote, kutokana na ahadi za Mwenyezi Mungu, na kuyabadili yale yaliyo katika amri na katazo la Mwenyezi Mungu, hao ndio wanastahiki zaidi uadui, chuki, na ulaghai wenu, kuliko uadui na chukio lao..).
(..na katika Aya hii ubainifu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu hali ya makundi mawili, yaani Waumini na Makafiri, rehema ya watu wa imani na huruma yao kwa watu wanaotofautiana nao, ugumu wa nyoyo za makafiri na ukali wao kwa watu wa imani.
Kama alivyotuambia Bishr... kutoka kwa Qatadah: kauli yake: {Hivyo basi nyinyi ndio mnawapenda watu hao, wala wao hawakupendeni. Nanyi mnaviamini Vitabu vyote}. Wallahi! Muumini anampenda mnafiki na anamtengenezea hifadhi - yaani ni mpole kwake - na anamrehemu, na ikiwa mnafiki ana uwezo wa kile ambacho Muumini anakiweza, angeharibu nafasi zake za kijani kibichi.
Bwana Muhammad Rashid Rida, katika tafsiri ya Aya hii anasema: (Qur'ani inatamka usemi ulio fasihi zaidi na ulio wazi kabisa, ikiwaelezea Waislamu kwa maelezo haya, ambayo ni moja ya athari za Uislamu: kuwa Waislamu wanapenda watu wenye uadui zaidi kwao, ambapo wale hawachelewi katika kufisidi mambo yao na kuwatakia shida kwao, na hali ya kuwa chukio lao kwa Waislamu liko dhahiri, na yaliyofichika humo ni makubwa kuliko yanayodhihirika..
Je, siyo mapenzi ya Waumini kwa wale Mayahudi mahaini na wadanganyifu, na Qur'ani kuwaidhinisha juu ya hilo, kwa sababu ni moja ya athari za Uislamu katika nafsi zao, ni ushahidi wenye nguvu zaidi kwamba dini hii ni dini ya mapenzi, rehema, na msamaha, ambayo akili haiwezi kugeuza macho yake juu zaidi ya kuliko hayo).
Na baada ya mazungumzo marefu, Bwana Rida anasema: (Na kutokana na hayo yote: mtu anakuwa katika uvumilivu, upendo na huruma kwa wanadamu wenzake ni kwa kadiri ya kushikamana kwake na imani ya kweli, na ukaribu wake na ukweli, na yaliyo sahihi ndani yake.
Na vipi haiwezekani, na Mwenyezi Mungu anawaambia waumini walio bora zaidi: {Hivyo basi nyinyi ndio mnawapenda watu hao, wala wao hawakupendeni},
Hivyo, tunawapinga wale wanaodai kuwa dini yetu inatushawishi kuwachukia wanaotupinga..).
Hivyo usielewe kutokana na hilo kuwa mapenzi yako kwa Muislamu ni sawa na mapenzi yako kwa asiyekuwa Muislamu, kuna tofauti kubwa, na wewe unapenda Muislamu kwa ajili ya imani yake kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kushikamana kwake na imani iliyo safi na iliyo sahihi, hata usipokutana naye, na hakuna maslahi baina yenu, kwa sababu unampenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu ambaye aliyeunganisha baina yenu kwa kiunganishi cha imani, hata ikitokea hitilafu baina yenu, hiyo haiondoi mapenzi yake kabisa kutoka ndani ya moyo.
Vile vile haiwezekani kwako kuwa na mapenzi kwa asiye Muislamu kwa sababu ya ukafiri wake, hili haliwezekani, lakini unaweza kuwa na mapenzi naye moyoni mwako kwa mazingatio mengine. Anaweza kuwa mkweli na ukapenda ukweli wake, na anaweza kuwa mwaminifu na ukapenda kutimiza agano, na akawa mwaminifu kwako katika biashara na ukaipenda amana hii, na ukapenda uwongofu kwa ajili yake katika hali zote.
Hisia hizi zinaweza kuwepo baina yako na asiyekuwa Muislamu, na zinatofautiana na mapenzi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ambayo hayawezi kuwepo isipokuwa kwa Muislamu tu, na ambayo hayana mazingatio mengine yote, wakati mapenzi ya kafiri yanapokuwepo lazima kuhusishwa kwa sababu zingine. Imetajwa kuhusu washirikina watekwa katika Vita vya Badr, Hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., isemayo: “Lau Al-Mutiim Ibn Adiy angekuwa hai kisha akaniambia kuhusu wabaya hawa, ningewaachilia kwake”. Ni ushahidi wa uaminifu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., kwa Al-Mutiim Ibn Adiy, kwa jukumu lake la kumlinda yeye aliporejea kutoka Taif, na kwa jukumu lake la kuichana Sahifa ya Kususia, wakati alipokuwa mshirikina katika hali zote mbili. Hisia hii kutoka kwa Mtume S.A.W., mbele ya Al-Mutiim inabeba aina ya upendo wa asili kwa maadili ya uungwana na ujasiri, na kamwe sio aina ya upendo wa kiitikadi.
Hatua za uhusiano kati ya Muislamu na asiye Muislamu - Mahusiano ya kijamii kati ya wanadamu - Mapenzi ya Muislamu kwa asiye Muislamu - Mapenzi ya Muislamu kwa mke wake wa Kitabu - Mapenzi yaliyokatazwa – Mapenzi ya asili na mapenzi kiitikadi.

Sura ya kwanza: Hisia
Je, unaweza kufikiria kuzuka kwa mapenzi baina yako kama Muislamu na asiyekuwa Muislamu - katika nchi hizi - huo ungekuwa msingi wa ulinganiaji?
Je, unaweza kumuita mtu huku una kinyongo naye? Na unamchukia? Na unapanga kupigana naye? Je, unaweza kumuita katika kesi hii kwa hekima na ushauri mzuri?
Ukitaka kumuita mtu, na ukakataa kumsalimia mwanzoni, kwa kufuata yale tunayoyajua kutoka katika Hadithi ya Mtume S.A.W., na huko ni kuipotosha Hadithi isemayo: “Msianze kutoa salamu kwa Mayahudi na Wakristo”.
Hadithi hii ni maalumu aliyoisema Mtume Mtukufu S.A.W., katika hali maalumu, Mayahudi wa Madina walipokuwa wanafanya njama na kuwachukia Waislamu, na Waislamu wakiwaanza kwa salamu, walikuwa hawajibu salamu za amani, bali waliitikia kwa chuki na fitina zaidi, wakisema: (Assamu Alaikum) maana yake ni kifo kiwe juu yenu. Katika mazingira haya Mtume S.A.W alisema: Msiwaanze kwa salamu”.
Na kwa hiyo Hadithi hii ikawa katika vitabu vyetu msingi wa uhusiano kati ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu katika hali zote, na tumesahau makumi ya Aya Tukufu na mamia ya Hadithi Sahihi zinazoamrisha kutoa salamu, na kuitikia salamu kwa mfano wake au kwa ubora zaidi, n.k.
Nasema: Vipi Muislamu awe mlinganiaji wa mtu ambaye anaona aibu kumwanzia kwa slamu, au kusema naye neno la fadhili, ili asiyekuwa Muislamu afikirie kuwa hakuna mapenzi katika moyo wa Muislamu kwa asiye Muislamu.
Swali tena: Je, inawezekana kuanzisha uhusiano wa upendo kati ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu?
Kwanza: Hatua za uhusiano kati ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu:
Ili kujibu swali hili, nitajikita katika kubainisha uhusiano kati ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu katika hatua tatu ambazo zote zimetajwa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, nazo ni:
Hatua ya kwanza: Kujuana:
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi watu, tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke, na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari}.
Kwa hivyo mimi siwezi kumuona asiyekuwa Muislamu, na ishara yangu ya kwanza ni kumpa kisogo na kumkimbia, bila ya sababu nyingine isipokuwa yeye si Muislamu, hivyo simzungumzie na hali ya kuwa hakuna tatizo kati yetu.
Ikiwa wewe Ewe ndugu yangu Muislamu ni mlinganiaji, basi ardhi hii ya Mwenyezi Mungu ina rutuba kwa ulinganiaji wako, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameitiisha kwako ili utekeleze wajibu wa kulingania na Mwenyezi Mungu, na upate kufaulu na ufanisi humo, kwa ajili ya kurimdhisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Basi mwelekee asiyekuwa Muislamu, na umjue yeye na matatizo yake ikibidi, pengine kujuana huku kutausogeza moyo wake kwako, na pengine atakuwa na raha kwako, hivyo itakuwa ni fursa ya kumuita kwa Mwenyezi Mungu.
Kujuana kati ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu ni hatua muhimu, na ni lazima.
Hatua ya pili: kuishi pamoja:
Je, inajuzu kwa Muislamu kuishi na wasiokuwa Waislamu?
Jibu: Ndio..
Hili ni suala la msingi, ambalo linashuhudiwa na maandiko mengi, Aya, Hadithi Tukufu, na uhalisia. Sio busara kwa Muislamu kuishi katika mazingira ya Kiislamu tu. Hili halitakiwi katika Sheria ya Mwenyezi Mungu isipokuwa pale Muislamu anapoogopa yeye mwenyewe au kwa ajili ya dini yake. Waislamu hawakufanya hivyo, bali walifanya kinyume, na walisafiri katika nchi zisizokuwa za Kiislamu na kukaa pamoja na watu wake kwa maadili ya Kiislamu, na hii ndiyo ilikuwa sababu ya kuingia kwa watu wengi katika Uislamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amebainisha msingi wa kuishi pamoja kwa kusema: {Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu}.
Asipoanza vita asiyekuwa Muislamu, wala hakukutoa nyumbani kwako, wala hakusaidia adui kukutoa, basi huyu ni mtu ambaye unaweza kuishi naye, na wakati huo lazima ushikamane naye kwa wema na uadilifu. Kwa sababu uadilifu ndio kiwango cha juu kabisa cha tabia njema.
Tazameni maana hii kubwa ya Qur'ani (wema), ambao ni daraja ya juu kabisa ya tabia njema, na miongoni mwa sura zake ni heshima ya mtu kwa mama yake na baba yake, kwani ni daraja ya juu kabisa ya tabia njema. Kinachotakiwa kwetu sisi Waislamu ni kukabiliana na wema huu na wasiokuwa Waislamu, na kuwashughulikia pia kwa uadilifu ambao ni haki. Haijuzu Ewe Muislamu kumdhulumu asiye Muislamu, lakini lazima usimame naye ikiwa haki iko kwake, hata kama mpinzani ni ndugu yako Muislamu.
Haya ni maadili makubwa na masuala ya kimsingi ya kisheria ambayo tunaishi nayo na wasio Waislamu. Na Mwenyezi Mungu hakutulazimisha kufanya hivyo ili kuwapa kisogo kwa wasiokuwa Waislamu, au tusiwashughulikie, bali alituwekea sisi ili iwe ndio msingi wa kuishi pamoja kunakohitajiwa na uhalisia.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaumba wanadamu namna hii ya mbali mbali na ya tafauti, na lau Mwenyezi Mungu angelitaka angewafanya umma mmoja, {.. lakini hawaachi kukhitilafiana, isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba ..} Kisha akawataka kujuana wenyewe kwa wenyewe, na kuambatana na wema huu na uadilifu.
Hatua ya tatu: ushirikiano:
Kujuana Kwanza na wasiokuwa Waislamu.
Kisha unaishi pamoja nao kwa upendo na uwazi.
Kisha .. Je, huna masuala maalumu ya kisheria? ..
Je, ni vigumu kuona baadhi ya masuala haya ya kisheria yanaleta maslahi yako, na wakati huo huo, maslahi ya wasio Waislamu?
Upatanifu ukitokea katika jambo moja, ushirikiano unaweza kutokea pia, pingamizi gani kwa hilo? Na Mtume S.A.W., - kama tunavyojua sote - alizungumza juu ya (Hilf Al-Fudhuul, yaani Muungano wa fadhila), na huu ulikuwa katika zama za Jahiliyah, wakati Wakuu wa Quraishi na Viongozi wake walipokutana na kufanya mazungumzo baina yao kuwa: wanasaidia wanyonge, wanasaidia wenye dhiki, wanasaidia wenye shida, na mfano wa hayo ya maadili mema, na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., akahudhuria, na akasema baadaye katika zama za Uislamu:
“Nilishuhudia katika nyumba ya Abdullah bin Judaan Muungano kwamba ningependa kuwa na ngamia wekundu, na lau ningeitwa katika Uislamu, ningejibu.”
Basi, inajuzu kwetu kuitikia mwaliko kwa wasiokuwa Waislamu, ikiwa ni kwa msingi unaomridhisha Mwenyezi Mungu. Na iwapo tuna masuala tunayoyaona kuwa ni kisheria, na wasiokuwa Waislamu wakayapitisha kwa sababu nyinginezo, basi tunaweza kushirikiana nayo kuyafanikisha maadamu sisi tunayaona kuwa ni kisheria, na masuala kama hayo ni mengi sana.
Kwa hivyo, hatua zinazobainisha sifa za uhusiano kati ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu ni: kujuana.. kisha kuishi pamoja kwa misingi ya Sheria.. kisha ushirikiano katika mambo yaliyokubaliwa ambayo ni kisheria katika dini yetu.
Pili: Mafungamano ya kijamii kati ya wanadamu:
Kisha nakwenda kwenye kipengele kingine katika kuainisha uhusiano kati ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu:
Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaumba wanadamu na kuweka baina yao mafungamano mengi, ambayo kupitia haya wanashirikiana katika mambo ya maisha, na karibu nayo wanakutana.
Miongoni mwa mafungamano haya:
Kwanza: Fungamano la kibinadamu:
Ni kile kinachounganisha na kila mwanadamu aliyeko juu ya uso wa ardhi, upende usipende, kwani wewe unatokana na kizazi cha Adam na yeye anatokana na kizazi cha Adam, na wewe ni binadamu na yeye ni binadamu tu. Na mwanadamu amelazimishwa kwa agizo moja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, iwe anafuata agizo hili au la. Ndio maana unakuta Aya nyingi za Qur'ani Tukufu zikiwahutubia watu wote: {..Enyi watu..}. Na neno (watu) limetajwa zaidi ya mara mia mbili katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, pamoja na maneno mengine yanayoeleza umoja wa jinsi ya wanadamu, na hivyo kuonesha kuwepo mafungamano baina ya watu hawa, kile tunachoita kiunganishi cha wanadamu, Kwa sababu ni kuwepo kwa mwanadamu yeyote mbele ya watu wote.
Kwetu sisi Waislamu, kiunganishi hiki kinahusisha wajibu na haki za kisheria ambazo unazipata kwa undani katika vitabu vya Fiqhi, Maadili na Ulinganiaji, na hakuna haja ya kuzitaja hapa.
Pili: Fungamano la kitaifa:
Nalo lina nguvu zaidi kuliko kiunganishi cha kwanza, kwa maana mtu hukutana na watu wake – nao ni kikundi cha watu - juu ya mambo zaidi kuliko kiunganishi cha kibinadamu tu. Kwa kawaida anaishi na watu wake, anazungumza kwa lugha yao, na ana maslahi ya kawaida nao, na yeye na wao mara nyingi wana mambo mengi ya kawaida. Na bila shaka, kiunganishi hicho kipo na kina athari katika uhalisia wa mtu binafsi na ulimwengu wa watu. Kwa hiyo, istilahi ya (watu) na viasili vyake vimetajwa ndani ya Qur'ani Tukufu zaidi ya mara mia tatu na arobaini.
Tatu: Fungamano la familia:
Inaenea zaidi ya miduara mitatu:
Ya kwanza: Inajumuisha wazazi, watoto, mke na jamaa wanaoishi nao katika nyumba moja.
Ya pili: Inajumuisha jamaa wengine wote wa karibu zaidi, wanawake na jamaa.
Ya tatu: Inajumuisha jamaa wengine wote wanaohusiana na babu mmoja, hata awe mbali kiasi gani.
Kiunganishi hiki kina athari kubwa zaidi katika maisha ya mwanadamu, na kwa hiyo Sharia imeihusisha kwa idadi kubwa ya hukumu, ikiwa kwa wazazi, mke na watoto, au ndugu wa karibu, au urithi, au jamaa wa karibu zaidi (ni jamaa waliolazimika kumsaidia mmoja wao katika kulipa pesa ya damu ikiwa atafanya mauaji yasiyokusudiwa), au kitu kingine.
Nne: Fungamano la maslahi:
Ndiyo kinachounganisha kundi la watu wenye maslahi ya pamoja ambayo kila mmoja wao anataka kuyahifadhi na kuyaunga mkono, kama vile vyama vya wafanyakazi vinavyounganisha wafanyakazi katika nyanja moja, na huenda wasiwe na kiungo kingine.
Uhusiano huu wa kudumu na maslahi ya pande zote huzalisha uhusiano kati yako na watu hawa.
Tano: Fungamano la makazi:
Mtu anayeishi katika nchi anahisi uhusiano na nchi hiyo unaomvuta kwenye makao yake mapya.
Kwa hivyo ikiwa Muislamu anaishi katika nchi isiyokuwa ya Kiislamu, na Mwarabu anapoishi katika nchi isiyokuwa ya Kiarabu, na Mkristo anapoishi katika nchi ya Kiislamu - isiyo nchi yake - watu wote hawa wanahisi uhusiano maalumu na nchi mpya ya makazi, ambayo inaweza kuwa na upendo na heshima, na inaweza kuwa aina ya kinyongo na chuki kutokana na matendeano anayopata katika nchi hii mpya, na viunganishi hivi ni hisia za asili za kibinadamu.
Sita: Fungamano la Kiislamu:
Ama kiunganishi cha Kiislamu ndiyo kinachounga Muislamu kwa ndugu yake Muislamu, na inajumuisha kila anayesema: Hapana Mungu ila Mwenyezi Mungu tu, na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ni kiunganishi cha kiitikadi ambacho hutawala mahusiano mengine yote na kuyashinda katika mzozo, lakini hata hivyo hakifuti hata moja kati ya viunganishi vingine.
Tatizo hapa ni kwamba baadhi ya Waislamu wanafikiri kwamba kiunganishi hiki kinafuta viunganishi vingine na wala hawatambui isipokuwa hicho tu, ingawa hii si kweli hata kidogo.
Kwani mwenyezi Mungu anasema: {Sema: Ikiwa baba zenu, na wana wenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu}.
Al-Qurtubiy anasema katika tafsiri ya Aya hii: (Na katika Aya hiyo kuna ushahidi wa wajibu wa kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na hakuna hitilafu ya hilo katika umma, na kwamba hili linatangulia juu ya vipenzi vyote). Hii ina maana kwamba upendo wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake haukufuta aina nyingine za upendo, bali unachukua tu kutanguliza juu yao.
Aya Tukufu imeonesha viunganishi vya: ubaba, uana, udugu, ndoa, ukoo (utaifa), masilahi yanayowakilishwa na pesa, biashara, na kiunganishi cha nyumbani, yaani makazi.
Na kutumiwa neno (ni vipenzi zaidi kwenu kuliko) kwa sababu Mwenyezi Mungu hakutunyima mafungamano haya na mapenzi yanayotokana nayo, bali alitukana kuwa mapenzi haya ni makubwa kuliko mapenzi yetu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Basi kinachohitajika ni kwamba upendo wa Mungu ni mkubwa kuliko upendo wa mwingine yeyote. Na inapotokea mgongano, Muislamu hushinda mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu na kujitolea kwake kwa masharti ya sheria yake juu ya matakwa ya mafungamano mengine yote.
Lakini ikiwa hakuna mgongano, basi unaishi na ndani ya moyo wako uko upendo wa mambo haya ya kidunia, maadamu hayapingani na mapenzi yako kwa Mwenyezi Mungu au mapenzi yako kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW. Kwa hiyo, kutokana na mafungamano haya aliyoyataja Mola Mlezi wa walimwengu wote, lazima utokee upendo, kwa sababu mtu anaishi na binadamu mwingine ima kwa mapenzi au kwa chuki. Na upendo una ngazi mbali mbali mfano wa Chuki.
Na upendo unaweza kuwa katika ngazi ya chini zaidi au ya juu zaidi, na chuki ni vivyo hivyo, na hakuna mwanadamu anayeweza kuhusishwa na mwingine isipokuwa katika mojawapo ya hisia hizi mbili kwa namna fulani.
Hapa naona ni muhimu kurejea ili kubainisha suala jingine muhimu sana hasa kwa wale wanaoishi na wasiokuwa Waislamu. Naweza kusema:
Tatu: Upendo kwa Muislamu kwa asiyekuwa Muislamu.
Je, inajuzu kwa Muislamu kuhisi upendo na wasiokuwa Waislamu? Sikilizeni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hivyo basi nyinyi ndio mnawapenda watu hao, wala wao hawakupendeni. Nanyi mnaviamini Vitabu vyote. Na wanapo kutana nanyi husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao wanakuumieni vdiole kwa chuki. Sema: Kufeni kwa chuki yenu}.
Kinachokusudiwa na Aya hii ni Mayahudi kwa rai ya wengi wa Wafasiri; na Makafiri kwa rai ya baadhi yao. Na At-Tabariy anasema katika kuitafsiri Aya hii:
(..Basi ikiwa nyinyi Waumini mnaviamini Vitabu vyote, na mnajua ya kwamba niliyowakataza kuwafanya wasaidizi wasiokuwa nyinyi, ni hao Makafiri katika kukanusha hayo yote, kutokana na ahadi za Mwenyezi Mungu, na kuyabadili yale yaliyo katika amri na katazo la Mwenyezi Mungu, hao ndio wanastahiki zaidi uadui, chuki, na ulaghai wenu, kuliko uadui na chukio lao..).
(..na katika Aya hii ubainifu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu hali ya makundi mawili, yaani Waumini na Makafiri, rehema ya watu wa imani na huruma yao kwa watu wana nao, ugumu wa nyoyo za makafiri na ukali wao kwa watu wa imani.
Kama alivyotuambia Bishr... kutoka kwa Qatadah: kauli yake: {Hivyo basi nyinyi ndio mnawapenda watu hao, wala wao hawakupendeni. Nanyi mnaviamini Vitabu vyote}. Wallahi! Muumini anampenda mnafiki na anamtengenezea hifadhi - yaani ni mpole kwake - na anamrehemu, na ikiwa mnafiki ana uwezo wa kile ambacho Muumini anakiweza, angeharibu nafasi zake za kijani kibichi.
Bwana Muhammad Rashid Rida, katika tafsiri ya Aya hii anasema: (Qur'ani inatamka usemi ulio fasihi zaidi na ulio wazi kabisa, ikiwaelezea Waislamu kwa maelezo haya, ambayo ni moja ya athari za Uislamu: kuwa Waislamu wanapenda watu wenye uadui zaidi kwao, ambapo wale hawachelewi katika kufisadi mambo yao na kuwatakia shida kwao, na hali ya kuwa chuki yao kwa Waislamu iko dhahiri, na yaliyofichika humo ni makubwa kuliko yanayodhihirika..
Je, siyo mapenzi ya Waumini kwa wale Mayahudi mahaini na wadanganyifu, na Qur'ani kuwaidhinisha juu ya hilo, kwa sababu ni moja ya athari za Uislamu katika nafsi zao, ni ushahidi wenye nguvu zaidi kwamba dini hii ni dini ya mapenzi, rehema, na msamaha, ambayo akili haiwezi kugeuza macho yake juu zaidi ya kuliko hayo).
Na baada ya mazungumzo marefu, Bwana Rida anasema: (Na kutokana na hayo yote: mtu anakuwa katika uvumilivu, upendo na huruma kwa wanadamu wenzake ni kwa kadiri ya kushikamana kwake na imani ya kweli, na ukaribu wake na ukweli, na yaliyo sahihi ndani yake.
Na vipi haiwezekani, na Mwenyezi Mungu anawaambia waumini walio bora zaidi: {Hivyo basi nyinyi ndio mnawapenda watu hao, wala wao hawakupendeni},
Hivyo, tunawapinga wale wanaodai kuwa dini yetu inatushawishi kuwachukia wanaotupinga..).
Hivyo usielewe kutokana na hilo kuwa mapenzi yako kwa Muislamu ni sawa na mapenzi yako kwa asiyekuwa Muislamu, kuna tofauti kubwa, na wewe unapenda Muislamu kwa ajili ya imani yake kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kushikamana kwake na imani iliyo safi na iliyo sahihi, hata usipokutana naye, na hakuna maslahi baina yenu, kwa sababu unampenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu ambaye aliyeunganisha baina yenu kwa kiunganishi cha imani, hata ikitokea tofauti baina yenu, hiyo haiondoi mapenzi yake kutoka kwa moyo kabisa.
Vile vile haiwezekani kwako kuwa na upendo kwa asiye Muislamu kwa sababu ya ukafiri wake, hili haliwezekani, lakini unaweza kuwa na upendo naye moyoni mwako kwa mazingatio mengine. Anaweza kuwa mkweli na ukapenda ukweli wake, na anaweza kuwa mwaminifu na ukapenda kutimiza agano, na akawa mwaminifu kwako katika biashara na ukaipenda amana hii, na ukapenda uwongofu kwa ajili yake katika hali zote.
Hisia hizi zinaweza kuwepo baina yako na asiyekuwa Muislamu, na zinatofautiana na mapenzi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ambayo hayawezi kuwepo isipokuwa kwa Mwislamu tu, na ambayo hayana mazingatio mengine yote, wakati mapenzi ya kafiri yanapokuwepo lazima huhusishwa kwa sababu zingine. Imetajwa kuhusu washirikina watekwa katika Vita vya Badr, Hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., isemayo: “Lau Al-Mutiim Ibn Adiy angekuwa hai kisha akaniambia kuhusu wabaya hawa, ningewaachilia kwake”. Ni ushahidi wa uaminifu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., kwa Al-Mutiim Ibn Adiy, kwa jukumu lake la kumlinda aliporejea kutoka Taif, na kwa jukumu lake la kuichana Sahifa ya Kususia, wakati alipokuwa mshirikina katika hali zote mbili.
Hisia hii kutoka kwa Mtume S.A.W., mbele ya Al-Mutiim inabeba aina ya upendo wa asili kwa maadili ya uungwana na ujasiri, na kamwe sio aina ya upendo wa kiitikadi.
Mapenzi ya Muislamu kwa mke wake wa Kitabu:
Wazo hili linaungwa mkono na ukweli kwamba Mwenyezi Mungu, amewaruhusu Waislamu kuoa wanawake wa Kitabu, kama inavyojulikana. Mwenyezi Mungu ameumba aina ya upendo na mapenzi kati ya wanandoa ambayo yanahakikisha kuendelea maisha ya ndoa, licha ya matatizo yote.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri}.
Mwanamume Muislamu anampenda mke wake wa Kitabu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliyeumba mapenzi haya ndani ya moyo wake, basi je, inajuzu kwake kumkataza nayo? Namaanisha, je inajuzu kwa Muislamu kuoa mwanamke wa Kitabu kisha kuombwa asimhurumie na asimpende? Hii haifahamiki, na lau isingejuzu kwake kumpenda, basi Mola Mtukufu angemkataza kumuoa.
Kwa hivyo kunaweza kuwa na mapenzi baina ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu, lakini si kwa sababu ya ukafiri wake na upotofu wake – kinga kwa Mwenyezi - bali kwa mazingatio mengine ya halali, ikiwa ni pamoja na kifungo cha ndoa, na mke hata ikiwa ni wa kitabu, anashiriki mume katika hisia nyingi, na wanaweza kuelewana pamoja.
Kunaweza pia kuwa na hisia za asili na mahusiano ya kijamii kati ya Muislamu na asiye Muislamu, ikiwa mazingatio hayo ya halali yapo, kama vile ahadi, ujirani, shughuli, na mengineyo. Ikiwa hakuna aina ya upendo, heshima, au tabia njema kati yako na asiye Muislamu, kamwe huwezi kufanikiwa katika ulinganiaji wako.
Akasema Mwenyezi Mungu: {Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora..}.
Huu ni msingi mmojawapo wa ulinganiaji ambao ni kwamba kuwe na mazungumzo kwa namna iliyo bora zaidi, na kuwe na hekima na ushauri mzuri. Yote haya hayapatikani bila kuwepo hisia kati ya anayelingania na anayelinganiwa, unaweza kuuita upendo kwa uzingatio mmoja, na unaweza kuuita huruma kwa uzingatio mwingine. Bila shaka haitokani na mapenzi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na wala haitokani na mapenzi ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha katika Kitabu chake Kitukufu.
Mapenzi yaliyokatazwa:
Anasema Mwenyezi Mungu: {Hauwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, na watoto wao, na ndugu zao, au jamaa zao}.
Mapenzi ambayo Mwenyezi Mungu ameyaharamisha katika Aya hii ni kwa yule aliyekufuru na kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wala si kwa aliyekufuru tu, bali anayezidisha ukafiri wake kwamba anampinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na anaupiga vita Uislamu na Waislamu.
Lakini tukidhania kuwa yupo kafiri ambaye hapigani na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hampingi Mwenyezi Mungu na Mtume wake - na akawa na sifa njema na maadili ya hali ya juu - basi hakuna ubaya kwetu kuthamini sifa hizi, maadili au mazingatio ndani yake, kwa sababu ni mabaki ya akiba yake ya asili, na zinakubalika kwa mtazamo wa kisheria, na Mtume S.A.W, anayafanya maadili haya kama msingi wa ujumbe wake anaposema: “Nimetumwa kwa ajili ya kutimiza maadili mema”.
Al-Shawkaniy kataja katika tafsiri yake kuwa Aya hii {Huwakuti watu wanaoamini..} Imemteremkia Abu Ubaidah Ibn Al-Jarrah alipomuua baba yake katika Vita vya Badr, na hili limepokelewa na Ibn Abi Hatim, At-Tabariy, Al-Hakim na Abu Nuaim katika Al-Hilyah na Al-Bayhaqi katika Sunan yake.
Al-Qurtubiy aliitaja kauli kama hii kutoka kwa Ibn Masoud. Vile vile ametaja kuwa Aya hii imeteremshwa kumuhusu Hatib Ibn Abi Balta’ah alipowaandikia watu wa Makkah kuhusu safari ya Mtume S.A.W, kwao katika mwaka wa Kufungua Makkah. Akataja kutokana na sababu ya kuteremshwa kwake au kwa maelezo yake msimamo wa Abu Bakr pale alipomwita mwanawe Abdullah kwenye pambano, na msimamo wa Musa’ab Ibn Umair alipomuua kaka yake Ubaid Ibn Umair. Na msimamo wa Umar Ibn Al-Khattab alipomuua mjomba wake Al-A’as Ibn Hisham, na msimamo wa Ali na Hamza walipowaua Uqbah, Shaibah na Al-Waliid.
Hali zote hizi zinathibitisha kwamba mapenzi, ambayo yameharamishwa katika Aya hii, ni kwa mwenye kuchanganya ukafiri na vita. Hili linaungwa mkono na yale tuliyotangulia kuyataja kuhusu kuruhusiwa kwa mapenzi ya Mwislamu kwa mke wake wa Kitabu kwa mujibu wa maandishi ya Qur'ani Tukufu, kwa sababu hawezi kuwa mpiganiaji kwa sababu ya kufunga ndoa. Na ikiwa yeye atasababisha vita kutokea, basi mapenzi yanapaswa kukomwa, kwa sababu yatakuwa haramu.
Tunahitimisha kutokana na hili kwamba hisia inaweza na inapaswa kuwepo kwa mwanadamu unayetaka kumlingania kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na hisia hii ni sehemu ndogo ya hisia ya upendo ambayo Mwenyezi Mungu alitaka iwe safi kwa ajili yake, na alitaka pawepo upendo na chuki kwa watu wengine pia kuwa safi kwa ajili yake Mtukufu. Huu ndio msingi unaozingatiwa kuwa na nguvu zaidi kuliko kila kitu kingine, na unashinda kila kitu kingine.. lakini inaweza kuwa ndani ya upendo huu mkubwa kuna sehemu ambayo hutolewa kwa wasio Waislamu, ndani ya mipaka ya kile kinachomridhisha Mwenyezi Mungu, ama kama mapenzi au mazungumzo kwa njia iliyo bora zaidi, au mawaidha, au huduma, au kujitolea au ushirikiano katika jambo la halali, hayo yote ni machache, lakini ni lazima yapo kwa sababu yanaeleza ukweli wa ujumbe wa Kiislamu kwamba Mungu aliufanya (Rehema kwa ajili ya walimwengu) na kusaidia kwa kufanikisha ulinganiaji kwa Mwenyezi Mungu.
Uislamu ulikuja kama rehema kwa watu wote.
Kafiri akinitangazia vita, siwezi kuwa na chembe ya kumpenda moyoni mwangu, lakini tunaishi - katika Nchi za Magharibi - leo katika mazingira ya amani, hata ikiwa ni tofauti na sisi katika dini, na sisi tuna wenzi na majirani wasio Waislamu, na wanaweza kuwa miongoni mwa hawa walio karibu sana Kutoka kwetu, na wewe ndugu Mwislamu, unaweza kuhisi aina fulani ya uhusiano kati yako na watu hawa, na unaweza kuona haya au aibu kuuita upendo au mapenzi.
Hakuna ubaya katika hilo kwa mujibu wa ufahamu sahihi wa Aya zilizotupita kwa sababu za kuteremshwa kwake, na pia Hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW. Hizi ni hisia ambazo hazina uhusiano wowote na imani, lakini ni hisia zinazohusiana na mazingatio halali kwa sisi Waislamu.
Mazingatio hayo ya halali yanaweza kusababisha hisia za asili, na hizi haziwezi na hazifikiriwi kuwa kupingana na upendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, licha ya kuwa kuushinda upendo huo ambao unachukuliwa kuwa mojawapo ya misingi ya imani.
Vifungo vyenye nguvu zaidi vya imani ni: kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na chuki kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kinachothibitisha uhalali wa hisia hizi ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimtuma Mtume wake Muhammad S.A.W., kuwa ni rehema kwa walimwengu wote, na kwamba Mtume S.A.W., alisema: “Hamtaamini mpaka muwe ni wenye kuhurumiana! Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi sote ni wenye kuhurumiana, akasema: Sio kumhurumia mwenzie bali ni kuwahurumia watu wote, huruma ya jumla”. Na akasema pia: "Wahurumieni waliomo ardhini, na Yeye aliye mbinguni atakuhurumieni”. Je, rehema kwa watu wote si kitu isipokuwa aina fulani ya hisia?!
Upendo wa asili na upendo wa kiitikadi:
Kutoka kwa yote hapo juu inakuwa wazi kwetu kwamba kuna aina mbili za upendo. Upendo wa asili na upendo wa kiitikadi.
Mapenzi ya Asili: Ni miongoni mwa athari za matamanio, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na wana, na mirundi ya dhahabu na fedha, na farasi asili, na mifugo, na mashamba. Hayo ni starehe ya maisha ya duniani; na kwa Mwenyezi Mungu ndio kwenye marejeo mema}.
Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW: “Mimi nimependezewa katika dunia yenu: Manukato, na wanawake, na faraja yangu ni katika Sala”.
Imam Al-Ghazaliy anasema kuhusu aina hii ya mapenzi: (Ni mapenzi kutokana na hulka na matamanio ya nafsi, na yanatazamiwa kutoka kwa mtu asiyemwamini Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, ikiwa yakiunganishwa kwa kitu chenye ubaya basi yakwa mabaya, ama yakiunganishwa kwa kitu chenye uzuri, basi yakawa mazuri, na hapo hayawezi kuelezwa kwa uzuri wala ubaya).
Mapenzi tunayoyazungumza na wasiokuwa Waislamu ni ya aina hii tu ya asili. Unaweza kumpenda mwanamke asiye Mwaislamu kwa uzuri wake au tabia nzuri yake, hili ni jambo la kiasili. Ni jambo la kulaumiwa ikiwa kuna jambo lililoharamishwa kwake, kama vile faraghani, kuchanganywa haramu, au zinaa, na inajuzu ikiwa imeunganishwa na lengo linaloruhusiwa kama ndoa.
Unaweza kumpenda asiye Muislamu kwa sababu ya tabia zake njema, ukamilifu wa akili yake, au undugu baina yako na yeye, au kwa ajili ya maslahi yako naye, au kwa kufahamiana kati yenu wawili au kitu kingine. Iwapo mapenzi haya hayahusiani na kitu cha kulaumiwa, basi inajuzu, na Muislamu anapaswa kufaidika na upendo huu katika kumwita mtu huyu kwa Mwenyezi Mungu.
Kama ilivyopokewa kutoka kwa Abdullah bin Abdullah bin Ubayi, yule Sahaba mwema ambaye baba yake alikuwa mnafiki, na alimpenda kwa sababu ni baba yake, na anampenda uwongofu kwake, na Mtume anamuamuru kumtendea mema baba yake, pamoja na unafiki wake, lakini upendo huu wa asili haukumsukuma kupata ushindi kwa baba yake dhidi ya Waislamu, na kama hilo lingetokea, angekuwa na mapenzi ya kulaumiwa, bali aliushinda Uislamu dhidi ya baba yake, kama ilivyotokea baada ya Vita vya Banil Mustalaq.
Upendo wa kiitikadi:
Ni upendo wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na upendo kwa Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Ni mojawapo ya matunda ya imani, na sehemu ya imani ya Muislamu. Na kwake Inahusisha taklifu ya kisheria, kwa sababu wajibu wa Muislamu ni kumpenda ndugu yake Mwislamu, hata kama hakuna uwiano, maelewano, ujamaa, au maslahi baina yao, bali ampende kwa sababu yeye ni Muislamu.
Ndiyo maana Mjumbe wa Mwenyezi Mungu S.A.W., aliona kuwa ni miongoni mwa utamu wa imani kwamba “mtu anampenda menzake si kwa ajili ya kitu isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee”. Na akasema kuhusu wale Watu Saba ambao Mwenyezi Mungu anawatia kivulini mwake, na miongoni mwao: “Watu wawili wanapendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wanakusanyika juu yake na wanafarakana juu yake”. Na akasema: Msiingie Peponi mpaka muamini, na wala msiamini mpaka mpendane. Na Hadithi kama hizi ni tele.
Je, wasiokuwa Waislamu wanazingatiwa (ndugu):
Baadhi ya Waislamu wanaweza kuona haya kuwaona wasio Waislamu kuwa ni ndugu zao, na ikiwa wengine wanatumia neno (ndugu zetu Wakristo), unaona vijana wengi wa Kiislamu wanakasirika na kupaaza suti, wakisema: Vipi mnawaitaje Wakristo ndugu zetu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Hakika Waumini ni ndugu}.
Wao wanaelewa kutokana na aya hii kwamba udugu umewekewa mipaka kwa waumini, na hauwezi kuwajumuisha wengine, na hii si sahihi, kwa dalili zifuatazo:
1- Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaeleza Mitume kuwa ni ndugu kwa watu wao
walio makafiri, Akisema Mwenyezi Mungu:
- {Na kwa kina A'di tulimtuma ndugu yao Hud}.
- {Na kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shua’ibu.}
- {Na kina Thamud tuliwapelekea ndugu yao Saleh.}
Na Mwenyezi Mungu alisema:
- {Alipowaambia Ndugu yao Nuh: Je! hamchimungu}?
- {Alipo waambia ndugu yao Hud: Je! hamchimungu}?
- {Alipo waambia ndugu yao Saleh: Je! hamchimungu}?
Mitume hawa: Nuh, Hud, Saleh na Shua’ib, Mwenyezi Mungu aliwahesabu kuwa ni ndugu kwa watu wao, na hii ni kauli ya Qur'ani kwamba kuna udugu wa kitaifa licha ya tofauti za dini.
2- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amehifadhi sifa ya udugu hata kwa kafiri aliye adui, nayo ni katika kauli yake Mtukufu: {Hauwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, na watoto wao, na ndugu zao, au jamaa zao}.
Udugu wa kibinadamu upo, udugu wa kitaifa upo, udugu wa jamaa upo, na unaweza kuwa udugu wa Kiislamu nao, ambapo huzidisha nguvu na nguvu zaidi, na hauwezi kuwa na udugu wa Kiislamu nao, kwa hivyo aina zote za udugu huu hubaki karibu na kila mmoja, na ikitokea mzozo Muislamu ataushinda udugu wake wa Kiislamu juu ya kila kitu kingine.
Ama Aya Tukufu {Hakika Waumini ni ndugu} ina maana kuwa uhusiano baina ya Waumini unaweza tu kuwa uhusiano wa udugu kwa Mwenyezi Mungu, lakini hauwekei mipaka udugu baina ya waumini tu. Kwa kuwa udugu unaweza kuwa na sababu nyingine kati ya Waumini na wasio Waumini, unaweza kuwa udugu wa kitaifa au udugu wa kibinadamu, au unaweza kuwa urafiki unaotegemea masilahi ya halali.
Kwa upande mwingine, uhusiano kati ya Waislamu na wasio Waislamu unaweza kuwa vita, uadui, au chuki, ama kwa Waislamu, uhusiano huo daima unapaswa kuwa na msingi wa udugu kwa Mwenyezi Mungu.
Tukiitazama Aya hii katika mwangaza wa Aya nyingine, tunafikia hitimisho lifuatalo kwamba: Mafungamano haya yote ya kibinadamu ni ya kiasili, lakini mafungamano yenye nguvu zaidi yanayonifunga mimi na mwanadamu ni mafungamano ya udugu kwa Mwenyezi Mungu, na haiwezi kuachwa, kupuuzwa, au kuona haya kutoka kwake.
Lakini mshikamano huu wenye nguvu hauko peke yake na haunizuii mimi na wasio Waislamu kuwa na udugu wa aina nyingine, ambamo ninathamini udugu wa jamaa, utaifa, au ubinadamu, na kila aina ina thamani yake, na linaloshinda aina moja juu ya nyingine ndio ni utaratibu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Sheria yake.

Je, kila kafiri anazingatiwa adui? – Wote hao si sawa sawa - Sababu ya mapigano ni uadui, sio ukafiri - Amani ni kanuni.
Sura ya Pili: Fikra
Zaidi ya theluthi moja ya Waislamu wanaishi leo katika nchi zisizo za Kiislamu, na kati yao zinaenea jumla ya fikra walizozirithi kutoka katika urithi tajiri wa Uislamu, lakini baadhi yao waliathiriwa na hali ya kihistoria ya taifa hilo, na leo fikra hizo zinahitaji uhakiki ukosoaji mwingi na marekebisho, ili kuendana na kanuni zilizowekwa za kisheria.
Miongoni mwa dhana hizo ni kwamba kila kafiri anahesabiwa kuwa ni adui, na kwa hiyo damu yake na fedha zake zimeruhusiwa, na kutendana naye kwa maadili ya kivita, kunaruhusiwa kutokana na uwongo na ulaghai, pamoja na chuki na kinyongo. Maneno ya namna hiyo niliyasikia mimi mwenyewe kutoka kwa mmoja wa mashekhe aliyeigwa na kundi la watu.
Ninaharakisha kusema kwamba wanazuoni wengi wa Fiqhi, ingawa wanamchukulia kafiri kuwa ni mtu wa vita kimsingi - na hili ndilo tutakalolijadili baadaye - lakini hawaoni kuwa: Inajuzu kutendana naye kwa maadili ya vita isipokuwa vita vinapotokea kikweli kati yetu na yeye. Na maandishi yote yaliyotajwa kuhusu kuruhusiwa kwa uwongo na ulaghai katika vita yamewekewa mipaka kwenye kutokea vita halisi.
An-Nawawiy ametaja katika maelezo yake ya Sahih Muslim wakati akizungumzia Hadith “Vita ni hadaa” akisema: (Wanazuoni wameafikiana juu ya uhalali wa kuwahadaa makafiri katika vita jinsi udanganyifu unavyowezekana, isipokuwa unahusisha kuvunja agano au usalama, ambapo haijuzu), pamoja na ukweli kwamba Mujahid wa Kiislamu bado anashikamana na maadili ya Uislamu, hata wakati wa mapigano, hairuhusiwi kwake kuua watoto, wanawake wasiopigana, wazee wasiopigana, watawa katika kibanda zao za ibada, vibarua, au wafanyabiashara.
Katika haya yote kuna maandishi ya wazi, na wengi wa wanazuoni wa Fiqhi wamehusisha kila asiyewezi kupigania, au asipiganie kikweli, kama vile kipofu, magonjwa wa kudumu, mjinga, na mkulima.
Haijuzu kwa Mujahidina kukeketa maiti za adui isipokuwa ni kutendeana sawa kwa sawa, na ni bora kwao kusamehe na kutokeketa. Haijuzu kufanya uharibifu na uchomaji moto isipokuwa ni lazima ya kupigana. Amri ya Abu Bakr kwa jeshi la kwanza lililotoka Bara Arabu kwenda kupigana na Warumi, inajumlisha maana hizi zote: (Msikate viungo, msiue mtoto mdogo au mzee, au mwanamke, na msikate mitende au kuichoma moto, msikate mti wenye matunda, wala msichinje kondoo, ng'ombe au ngamia ila kwa ajili ya chakula, na mtapita karibu na watu ambao wamejinyima katika vibanda vya ibada, waacheni na yale waliyoyanyima nafsi zao za faragha).
Na kwa vile hali halisi ya vita haipo kwa Waislamu waishio katika nchi zisizokuwa za Kiislamu, wawe ni raia au wakaazi, kila mazungumzo juu ya uhalali wa damu na fedha - kwa mtu mmoja au serikali - ni kinyume cha kanuni na maadili ya Uislamu, na hairuhusiwi hata kidogo na ye yote miongoni mwa wanazuoni.
Je, kila kafiri anazingatiwa adui?
1. Kafiri siyo adui, isipokuwa yeye - au dola yake - kutangaza vita dhidi ya Waislamu, au ikiwa Waislamu watatangaza vita dhidi yake au dola yake, kutokana na sababu za halali. Hapo ndipo tunaweza kutumia Sheria za Vita katika matendeano naye.
2. Iwapo tangazo la vita halitafanyika kama tulivyotaja katika ibara iliyopita, basi kila kafiri hawezi kuwa mpiganaji wa vita, na hivi ndivyo wanavyomaanisha Wanazuoni wa Fiqhi wanapomzungumzia kafiri kuwa ni mtu wa vita, na kwa hiyo Waislamu lazima kumuogopa mpaka vita vyake viishe kwa ahadi, basi Waislamu wanapaswa kushikamana na masharti ya ahadi.
3. Inawezekana kwamba ahadi ya mtu binafsi inaweza kutokea baina ya kafiri na Muislamu, na ni lazima ifuatwe baina yao.
Agano linaweza kuwa kati ya kafiri na dola ya Kiislamu, na ni lazima litekelezwe na Waislamu wote, ambao ni raia wa nchi hii. Ikiwa ni pamoja na mkataba wa dhimma, ambao ni agano la kudumu; na mkataba wa usalama ambao kafiri huingia kwa mujibu wake kwenye makazi ya Uislamu, nalo ni agano la muda.
Huenda likafanyika baina ya Muislamu na dola ya kikafiri, kwa hiyo Muislamu lazima aitimize vilevile, kana kwamba Muislamu aliingia kwenye nyumba ya ukafiri kwa ajili ya biashara zamani, na anapoingia hivi leo kwa Visa.
Na inaweza linafanyika kati ya dola ya Kiislamu na dola ya kikafiri, kwa hiyo ni lazima ifuatwe, kama vile Mkataba wa Al-Hudaybiyyah huko zamani, na Azimio la Umoja wa Mataifa hivi leo.
Na vitabu vya Wanazuoni wa Fiqhi vina wingi wa kutaja maelezo ya kadhia hizi tatu, ambazo zote zinatawaliwa na kauli yake Mola Mtukufu: {..na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa..}. Mwenyezi Mungu Mtukufu alizingatia kuvunja ahadi miongoni mwa maadili ya Mayahudi {..Je! Ati ndio kila wanapo funga huwapo kikundi kikaivunja..?} na miongoni mwa maadili ya washirikina {..Wale ambao miongoni mwao umepatana nao ahadi, kisha wanavunja ahadi yao kila mara na wala hawamchi Mungu}. Ama Waislamu miongoni mwa maadili yao ni kutimiza ahadi {..na wanao timiza ahadi yao wanapo ahadi..} {Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao}.
Wote hao si sawa sawa..
Kwa hiyo, kwa mtazamo wa kisheria, wasiokuwa Waislamu wanakuwa mbele ya Waislamu katika mojawapo ya hali tatu: Vita halisi, uwezekano wa vita, au agano.
Hatuwezi daima kuwachukulia kama wapiganiaji wa kweli hadi tuhalalishe kuwatendea kwa masharti ya vita.
Bali kuwa Qur'ani Tukufu iliwatofautisha wasiokuwa Waislamu, hata kwa ukaribu wao au umbali wao kutoka katika Uislamu kama dini, na kutoka kwa Waislamu kama taifa. Akasema Mwenyezi Mungu: {Hakika Utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi}. Na akasema Mwenyezi: {Wote hao si sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo watu walio simama barabara, wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu...}.
Katika tafsiri ya Aya hii, Sheikh Muhammad Rashid Rida ametaja kauli ya Imam Muhammad Abduh kwamba Aya hii (ushahidi wa kuwa Dini ya Mwenyezi Mungu ni moja katika ndimi za Mitume wote, na kwamba kila mwenye kuichukua kwa unyenyekevu, na kufanya kazi ndani yake kwa ikhlasi, na kuamrisha mema na kukataza maovu, ni miongoni mwa watu wema..).
Na akaongeza hilo kwa kusema: (Na inaonekana kuwa haya ni kama yale ya kabla yake, katika hali ya Watu wa Kitabu wanaposhikamana na dini yao, kinyume cha Mfasiri wetu “Al-Jalal” na wengineo, ambao walihusisha kusifu kwa wale waliosilimu miongoni mwao. Maana Waislamu hawakusifiwa kama Watu wa Kitabu, bali wanasifiwa kuwa ni Waumini).
Na Sheikh Rida akamalizia kwa kusema: (Uadilifu wa baadhi ya Watu wa Kitabu juu ya ukweli wa dini yao haupingani na yale tuliyoyapata katika tafsiri ya Taurati na Injili mwanzoni mwa Surah hii ya kuwa: upotevu wa vitabu vyao na upotoshaji wa baadhi ya waliyo nayo mikononi mwao).
Hii inamaanaisha kwamba hata kwa mtazamo wa kihisia, Mwislamu anahisi kwamba Mkristo yuko karibu naye zaidi kuliko Myahudi. Anahisi kwamba Mtu wa Kitabu kwa ujumla ni karibu naye zaidi kuliko yule Majusi au Mpagani.
Na Qur'ani ilieleza hili kuonyesha furaha ya Waislamu siku ya Warumi wangeshinda, nao ni Watu wa Kitabu, juu ya Waajemi Mamajusi. Na Mwenyezi Mungu amesema: {Alif Lam Mim. Warumi walishindwa, katika nchi iliyo karibu, nao baada ya kushindwa kwao watashinda. Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu, Humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu}.
Sababu ya mapigano: Uadui, sio ukafiri
Wanazuoni wa Fiqhi walichunguza katika masuala ya Jihad kuhusu sababu inayowaruhusu Waislamu kuua maadui. Wengi wao miongoni mwa wafuasi wa Malik, Hanafi na Hanbal walisema kuwa sababu ya kupigania ni kutangaza vita - yaani kupigania vita- na hujuma, na sio ukafiri tu, wakati Shafiy anaona katika mojawapo ya kauli zake kuwa: Sababu ya kupigania ni ukafiri. Na maoni ya wengi wa wanazuoni juu ya suala hili ndiyo sahihi zaidi, na waliijenga juu ya shahidi zifuatazo:
1- Aya nyingi zilizo wazi zinathibitisha kwamba sababu ya Waislamu kupigania na wengine ni hujuma inayotoka nao. {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui} {Je hamtapigana na watu walio vunja viapo vyao na wakawa na hamu ya kumfukuza Mtume, nao ndio walio kuanzeni mara ya kwanza}? Na piganeni na washirikina wote kama wao wanavyo pigana na nyinyi nyote..} {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigana vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu}.
Wachunguzi wengi wamekubali kwamba Aya hizi ni thabiti na hazijafutwa.
2- Hadithi nyingi Sahihi zinazoharamisha kuwauwa makafiri wengi kwa sababu hawakupigana au hawakuweza kupigana, zikiwemo Hadithi inazoharamisha kuwauwa wanawake kwa kuwa hawapigani na wavulana kwa sababu hawapigani, na maana hii ilitajwa na Bukhariy, Muslim, Abu Daawuud, Ibn Majah na wengineo.

Abu Daawuud na Ibn Majah walitaja uharamu wa kumuua Al-A’siif, na Al-Albaniy akazisahihisha mapokezi mawili (Sahih Sunan Abi Dawuud Na. 2324 na Sahih Sunan Ibn Majah 2294).
Maana ya Al-A’siif ni: Mtu wa kuajiriwa katika mambo yasiyokuwa na mapigano, kama vile wakulima na wafanyakazi katika viwanda, wasafishaji wa barabara, madaktari, wauguzi, na wafanyakazi wa hospitali.

Na imepokewa katika Sunan Abi Dawuud kwamba: Kumuua mzee mkongwe kumeharamishwa; vile vile kuna amri ya kuwaua wazee wa washirikina, na Ash-Shawkani akaunganisha mapokezi mawili kuwa: Mzee aliyeharamishwa kumuua ndiye ni mwanaadamu ambaye bado hana manufaa yoyote kwa makafiri, na mzee aliyeamrishwa kumuua ni yule mwenye manufaa ya makafiri, hata kama kwa maoni kama vile: Duraid Ibn As-Simmah ambaye alikuwa mwenye maoni juu ya vita, ambapo aliuawa wa umri zaidi ya miaka mia moja.
Na kwa kuwa sababu ya kuua ni kupigana, sio ukafiri, Abu Bakr akaliusia jeshi lake lisiwashambulie wale waliojifungia kwenye vibanda vya ibada, na lisiwaue mwanamke, mvulana au mzee mkongwe. Ingawa Imam Shafiy anaruhusu kuwaua wasiokuwa wanawake na watoto hata kama hawatashiriki katika mapigano, lakini haoni kuwaua watawa, kwa kumfuata maoni ya Abu Bakr. Na imetajwa katika Musannaf Ibn Abi Shaybah kwamba: (hawakuwaua wafanyabiashara wa washirikina).
Wanazuoni wa Fiqhi - ambao wanaona kuwa: Sababu ya kupigana ni uadui na sio kufuru – wamelinganisha maandiko haya kila mtu ambaye hakuweza kupigana, kama vile kiwete, kipofu, aliyepooza, mwenye mguu na mkono liliyokatwa kutoka kinyume. Mwenye mkono wa kulia uliokatwa, kichaa, mtawa katika kibanda chake, na mtalii asiyechanganyika na watu, na watawa ndani ya makanisa na nyumba za watawa.
Na wafuasi wa Malik wanaona kuna uharamu wa kuua watu wa aina saba: mwanamke, mvulana, kichaa, mzee mkongwe: mwenye ugonjwa wa kudumu - kipofu na mtawa aliyejitenga katika nyumba au kibanda cha watawa. Na wafuasi wa Hanbal wanaona kuwa: haijuzu kuua mvulana, mwanamke, mkongwe, mwenye ugonjwa wa kudumu, kipofu, na mtawa.
3- Ikiwa kuua kwa ajili ya ukafiri tu kuliruhusiwa, hii ingepingana na kutolazimishwa katika dini. Hili ni suala ambalo halina hitilafu baina ya wanazuoni wote, na maandishi yaliyo wazi na yakinifu ndani ya Qur'ani Tukufu yanathibitisha hilo. Anasema Mwenyezi Mungu: {Hapana kulazimisha katika Dini..} Akamwambia Mtume wake {Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini}? {Basi atakaye, aamini, na atakaye, akataye..} {Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu}.
Pia imethibiti katika Sunna ya Mtume S.A.W., kwamba aliwakamata washirikina wengi, lakini hakumlazimisha yeyote kusilimu. Baadhi yao waliuawa kwa sababu zisizokuwa za ukafiri, baadhi yao walikombolewa, na wengine wakaachiliwa. Lau kuua kungekuwa ni wajibu kutokana na ukafiri tu, isingeliruhusiwa kuwaacha. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu, alipotaja hukumu ya wafungwa, alisema: {Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe..}.
Hii ni mojawapo ya Aya za mwisho zilizoteremshwa kutoka katika Qur'ani, na haikuamrisha ndani yake kuwaua wafungwa, bali haikufanya jambo hili kuwa miongoni mwa mambo yanayowezekana kimsingi, kwa maana ya kutengwa, isipokuwa pale inapokuwa kuna hali maalumu inayolihalalisha.
Kwa hiyo, wanazuoni walio wengi walikubaliana juu ya chaguo la imamu wakati wa kuainisha hatima ya wafungwa kati ya kuwaachilia, kuwakomboa, au kuwaua, kwa mujibu wa maslahi ya Waislamu, kwa kuzingatia hilo, Mtume S.A.W., akaamuru kuwaua baadhi ya wafungwa kwa sababu maalumu zinazohusiana na jinai na matendo waliyoyafanya, na si kwa ukafiri tu, la si hivyo, angeamuru kuwaua wote, na hapo chaguo lisingekuwa na maana tena.
Amani ni kanuni
Ipo Mitazamo mingi ya wanazuoni wa Fiqhi kuhusu hukumu za vita, na ni vigumu kupata kitabu cha fiqhi ambacho hakishughulikii na suala hili kwa undani. Tunaangalia kwamba maoni yote ya Wanazuoni yanatokana na maandishi thabiti ndani ya Qur'ani Tukufu au Sunna Takatifu, lakini yanahusu uhalisia maalum wa kihistoria. Pamoja na kuwa: maandishi yenyewe ni ya aina mbili:
- Baadhi yake yanahusiana na uhalisia ambao maandishi haya yametajwa, kwa kuwa ni ufumbuzi kwao, na sio lazima kueleza hukumu kamili.
- Na baadhi yake yanahusiana na kanuni na maadili ya Kiislamu ambayo
Qur'ani iliteremshwa ili yaenezwe baina ya watu, na kuweka maisha ya
wanadamu kwa mujibu wa kanuni hizo. Kwa hiyo zinazingatiwa hukumu kamili.
Uhalisia wa wanadamu ambao ndani yake yalitajwa maandishi ya Qur'ani Tukufu na Sunna Takatifu zinazohusiana na mapigano, kisha maoni ya wanazuoni yakaja kuishughulikia, kuanzia zama za kwanza hadi kuporomoka kwa Ukhalifa wa Uthmani mwanzoni mwa karne hii. una sifa zifuatazo:
1- Utawala wa Serikali za Udikteta juu ya watu wote waliopo.
Serikali hizi ziliwazuia watu kuchagua kwa uhuru dini wanayoitaka, na hata kuwalazimisha kufuata fundisho rasmi la serikali, na kuruhusu kumuua mpinzani, hata kama ni raia. Jambo hili halikuwa tu kwa Nchi za Warumi na Waajemi katika zama za mwanzo za Kiislamu, bali lilienea hadi kujumuisha Nchi za Ulaya hadi karne hii.
Na ikiwa shuruti ya kidini haipo tena dhidi ya raia wa nchi moja kwa sababu ya kuenea kwa fikra za Usekyula, chuki ya kidini bado inaunda msingi wa fikra za Ulaya na Magharibi – ikiwa kwa watu au kwa watawala - dhidi ya Uislamu na Waislamu hasa. Na inaonekana mara kwa mara katika matendo dhidi ya Uislamu na Waislamu ambayo yanavuka hata masuala ya uhuru wa mtu binafsi na haki za binadamu, kama vile suala la Hijaab.
2- Utawala wa wazo la vita, mauaji na vurugu kwa ujumla.
Na dhidi ya Uislamu na Waislamu hasa. Tunaangalia hivi mwanzoni mwa Utume wa Mtume S.A.W., wakati wa kipindi cha Makkah, na jambo liliendelea namna hii wakati wa kipindi cha Madinah, kisha uvamizi dhidi ya Bara Arabu ulianza na Warumi na Waajemi, na msisitizo wa watawala ukaonekana kuwazuia watu wao kuingia Uislamu, hivyo vita vyote vya Kiislamu vilikuwa ni kupambana na uvamizi halisi, au kuzuia uvamizi unaotarajiwa, au kutaka kuwaokoa watu katika tawala dhalimu ili waweze kuchagua wanachokitaka kwa uhuru kamili.
Mazingira haya yanayotawala duni nzima; mazingira ya vita, njama, uovu na kuzuia uhuru yalikuwa na taathira kubwa kwa hukumu nyingi za kifiqhi zinazohusiana na Jihad.
Licha ya mashinikizo makubwa ya hali hizi za kihistoria juu ya fikra za kifiqhi ya Kiislamu, daima tunapata kuwa wanazuoni wetu wana dhamira ya kuzingatia maadili kamili ya Kiislamu, kushikamana nayo, na kutanguliza kwake katika hali zote.
Zaidi ya hayo ni kile ambacho Uislamu kulingania kutokana na heshima ya mwanadamu, awe ni Muumini au kafiri, wakati wa uhai wake na baada ya kufa kwake. Na imethibiti kutoka kwa Mtume S.A.W, katika yale waliyoyapokea Bukhari na Muslim, kwamba alisema kuhusu Myahudi aliyesimama Mtume kwa ajili ya mazishi yake, akimjibu mtu aliyemwambia kuwa alikuwa Myahudi, basi Yeye, Rehema na Amani ziwe juu yake, akasema: “Je, huyu si nafsi”? Na hebu! Vipi ikiwa ni nafsi ya baba, mama, au jamaa wa kizazi?


 

Share this:

Related Fatwas