Luqmani

Egypt's Dar Al-Ifta

Luqmani

Question

Imekuja katika Qur`ani: {Na tulimpa Luqman hikima, tukamwambia: Mshukuru Mwenyezi Mungu. Na mwenye kushukuru basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na aliye kufuru, basi Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifiwa} [LUQMAAN: 12-13] 

Answer

Imepokewa katika tafsiri: kwamba Luqman ni mtoto wa Baauraa katika watoto wa Aazar mtoto wa dada yake Ayoub, na pamesemwa ni mtoto wa mama yake mdogo au mkubwa , na ameishi mpaka kuonana na Dawud A.S. na amesoma kwake, na alikuwa anatoa Fatwa kabla ya kupewa Utume.
Iwaje Qur`ani inasema kuwa Luqmani Mtume? Na vipi kwamba yeye ameishi pamoja na Ayoub na Dawud na kati ya wawili hao kuna kitambo kikubwa miaka 900, na Ayoub amekulia miji ya Ausw na Dawud Palestina.
Kuondoa shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Qur`ani haikusema kwamba Luqman ni Nabii, bali imesema: Kwamba yeye ni mja Mwenyezi Mungu Amempa hekima, na jamhuri ya wanazuoni inasema: Kwamba yeye alikuwa ni mtu mwema mwenye hekima, Ibnu Atia amesema: kwamba Ibnu Umar amesema: Nimemsikia Mtume S.A.W. anasema: “Luqman hakuwa Mtume bali alikuwa mja mwenye fikra sana, mwenye yaqini nzuri aliyempenda Mwenyezi Mungu naye akampenda, Mwenyezi Mungu Akampa hekima” hili likabainisha kwamba Mwenyezi Mungu Amempa hekima tu na hakumpa Wahyi, na yaliyotajwa katika kumfundisha mtoto wake akiwa anampa mawaidha, hayo ni mafundisho kwa mtoto wake, si kufikisha sharia.
Ama kauli ya kwamba ameishi zama za Ayoub na Dawud, tunasema kwamba: Qur`ani haikusema haya, bali maneno haya yamekuja katika kauli za baadhi ya wafasiri, nazo ni jitihada zao wakipatia watapata malipo mara mbili, na wakikosea basi watapata malipo mara moja, na baadhi yao wamejishughulisha kwa kukusanya kila yaliyosemwa kuhusiana na Aya hii watimize faida.
Na ikiwa yaliyosemwa kwamba Luqma ni mtoto wa dada yake Ayoub ni kweli, basi hilo halizuii kuwa Luqman alionana na Ayoub wala halizuii kuwa Ayoub alionana na Dawud, vilevile hili halieleweki kuwa walikuwa sehemu moja; kwa sababu Ayoub anaweza kuwa ndugu wa Dawud, kisha akaenda miji ya Dawud kwa mfano.
Na kauli ya kwamba kati Dawud na Ayoub kulikuwa na tofauti ya mia 900, muulizaji hakuleta dalili ya kauli hiyo, na wala Qur`ani na tafsiri hazikulitaja, kwa hivyo, kutambua muda ulio kati yao ni vigumu kuthibitisha hilo.
Na maana ya kauli ya baadhi ya wafasiri kwamba “ alikuwa akitoa Fatwa kabla ya kupewa Utume” katika neno (kupewa Utume) anayezungumziwa hapa ni Dawud si Luqman, kwa maana Luqman alikuwa akitoa Fatwa kabla ya Dud kupewa Utume, kwa makusudio kabla ya Dawud A.S. kupewa Utume.

 

Share this:

Related Fatwas