Ni Kwa Sababu Gani Uislamu Huhalali...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ni Kwa Sababu Gani Uislamu Huhalalisha Ndoa kwa Wanawake Wakristo?

Question

Matini ya Shaka:
Imetajwa katika Qur'ani Tukufu: {Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa waliopewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anaye kataa kuamini bila shaka a'maliyake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwawenye khasara.} [AL MAIDAH 5]
 

Answer

Qur'ani inawaruhusu wanaume waislamu kuwaoa wanawake wa kikristo wakati ambapo Bibilia inaharamisha kabisa wanawake wakristo kuolewa na wanaume wasio wakristo, na inasema: {Mwanamke yuko huru kuolewa na mtu yeyote ampendae, katika Bwana tu} [Ujumbe wa Paulo kwa Wakorinto 7:39]. Na hilo ni tangazo la Qur’ani kuheshimu imani ya ukristo na kuukubali, kwani mke wa mkristo atawalea watoto wa mume Muislamu.
Kujibu shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Swali hilo lina sehemu mbili:
Ya Kwanza: Kwamba muulizaji alifahamu kwamba baina ya Aya Tukufu ambayo ilithibitisha, na baina ya kauli ya Paulo katika risala yake kuna ukinzani na jambo si kama muulizaji alivyofahamu, basi Aya Tukufu haipingani na maneno ya Paulo, kwani Waislamu wanamwamini Mola, na wanawaamini Manabii wote wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hasa Nabii wa Mwenyezi Mungu Musa, na Isa A. S. Basi kusudio la Paulo, anawaagiza wasioe makafiri, au watu wasio na dini. Ama Waislamu wanaamini mitume wote wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kwa ufahamu huo si kusudio kuoa kwa Waislamu kama alivyofahamu muulizaji.
Na kwa kuyaangalia maandiko haya kama yalivyo na ambayo muulizaji ameyathibitisha ni kwamba hayapingani maneno ya Qur'ani Tukufu na ya Paulo, na ukamilifu wa maandiko ni kama ulivyopokelewa katika Risala ya Paulo: “Mwanamke ana mfungamano na Malaika kwa kuwa tu mume wake ataendelea kuwa hai, lakini atakapofariki mume wake basi mwanamke huyo atakuwa huru kuolewa na mwanaume mwingine kwa jina la Mungu tu [Wakorinto 7:39
Na inawezekana ikawa inafahamika kutokana na matini hiyo, kwamba Kitabu kitakatifu hakizingatii isipokuwa ndoa inayosajiliwa kanisani. Yaani hakizingatii ndoa ya kienyeji, kwa hiyo, kuna jambo linalojulikana katika siri ya ndoa, na hiyo ni moja miongoni mwa siri saba za ndoa kanisani.
Ya Pili: Muulizaji anasema ndani yake kwamba hakika Aya Tukufu inawakilisha uwazi wa kuheshimu Imani ya Kikristo, na wala katika hili hakuna upinzani wowote, kwani Waislamu wanaheshimu viumbe vyote vya Mwenyezi Mungu na wanaheshimu kwa sifa maalumu yule aliyekuwa anamwamini Mwenyezi Mungu, na kasoro iliyopo ni kwamba anakuwa nayo yule asiyemheshimu mtu anayemwamini Mwenyezi Mungu na wala haamini Mitume wote wa mwenyezi Mungu. Na kwa Mtume wa Mwisho Mohammad S.A.W.
Upeo wa jambo hili ni kwamba Waislamu wanatofautiana katika Imani zao na imani inayoona baadhi ya Itikadi nyingine kuhusu Mtume Isa A.S, kwani Waislamu wanaamini ya kwamba Mtume Isa A.S, ni mja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na ni Mtume wake, ingawa wanatofautiana kiimani na imani za wale wanaoamini kwamba Isa A.S, ni zaidi ya alivyo, na jambo hili halivurugi heshima ambayo Waislamu wanawapa Viumbe wengine, kwani Waislamu wanaanzia kwa kiasi kikubwa na watu wengine katika suala hili
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu na yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake}. [AL ANKABUT 46]
Na Muislamu huenda katika matendeano yake pamoja na watu, juu ya misingi miwili ikikamilishana; Wa Kwanza: kushika kwake kwa imani zake, maelezo yake, na wa Pili: kumuheshimu mwanadamu kama yeye ni mwanadamu.

 

Share this:

Related Fatwas