Yusuf Alifanya Nini Alipokutana na Ndugu Zake Katika Misri?
Question
Matini ya shaka:
Imetajwa katika Qur'ani Tukufu: {Wakaja ndugu zake Yusufu, na wakaingia kwake. Yeye akawajua na wao hawakumjua. Na alipo watengenezea tayari haja yao alisema: Nileteeni ndugu yenu kwa baba. Je! Hamwoni ya kwamba mimi ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa kukirimu?} [YUSUF 58-59]
Answer
Na hapa Qur'ani inaweza kwenda kinyume na yaliyokuja katika Kitabu kitakatifu, kwani Qur'ani Tukufu inasema: Hakika Yusufu aliwaambia nduguze: mleteni ndugu yenu. ama Kitabu kitakatifu kinasema: Hakika nduguze Yusufu walipokuja Misri ili wanunue ngano, Yusufu aliwaona na akawatambua lakini alijificha kwao.
Kisha baada ya hayo akawatuhumu kuwa wao ni majasusi, na wao wakajitetea kwa kusema: sisi sio majasusi bali ni ndugu, na idadi yetu ni kumi na mbili, na sisi hapa tuko kumi, na tuna ndugu yetu mdogo pamoja na baba yake, na tuna ndugu yetu aliyepotea. Yusufu akamchukuwa nduguye Mamuun kama rehani mpaka wamlete ndugu yao mdogo Benjamin; ili wadhihirishe kwamba wao sio majasusi.
Kujibu shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Aya hizo zinatusimulia: kisa cha Bwana yetu Yusuf A.S. baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomwokoza kutoka gereza, na alimwezeshea katika ardhi, na zinatusimulia kisa cha kuja kwa nduguze kwa Misri, na zinatutajia sababu ya kufika kwake Misri kwamba miaka ya usitawi (mavuno) ilipita, kisa kikafuatwa kwa miaka ya njaa, na njaa ilienea katika miji yote ya Misri, na ikafika nchi ya Kan'aan, na hizo ambazo Nabii wa Mwenyezi Mungu Yakub A.S. na wanawake wanaishi ndani yake. Basi Bwana wetu Yakub aliwatuma wanawe Misri ili kununua chakula, basi walipoingia Bwana wetu Yusuf aliwajua na wao hawakumjua, halafu akawaulizia hali yao, na juu ya idadi ya jamaa zao, basi walimjibu kwamba wana kaka yao mdogo, basi Bwana wetu Yusufu aliwaomba wamlete kwake.
Na kuhusu aliyoyataja Muulizaji ya kwamba Bwana wetu Yusufu A.S, aliwatuhumu nduguze kuwa ni majasusi, ukweli ni kwamba Qur'ani Tukufu haikutoa maelezo yoyote kuhusu suala hili, na kutotajwa hayo ndani ya Qur'ani Tukufu ni jambo lisilopingika; kwani Qur'ani Tukufu ni muongozo sio Kitabu cha simulizi, na Qur'ani Tukufu haizungumzii kisa chochote isipokuwa kwa kuwepo Mazingatio ndani yake na mawaidha, na wala haitoi maelezo marefu zaidi ya Simulizi mbalimbali ila yanapokuwa maelezo hayo ni yenye kuathiri katika udhihirishaji wa Mazingatio. Na yale aliyonukulu Muulizaji kutoka katika Kitabu Kitakatifu hatujakuta ndani ya Qurani Tukufu chochote kinachoyaunga mkono, na hakika sisi tunaishia hapo na wala hatumuamini na wala hatumkadhibishi. Basi katika Sahihi ya Bukhari kwamba Mtume S.A.W. anasema: "Msiwaamini watu wa Kitabu wala msiwakadhibishe, na semeni sisi tumemuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na yale tuliyoteremshiwa na yale mlioteremshiwa". [Kitabu cha: Fathu Al Bariy, Ibn Hajar Juzu ya 8, Uk. 170]
Na maana inayokusudiwa hapa katika Hadithi hii ni kwamba Maneno ya Watu wa Kitabu yanagawanyika migawanyiko mitatu: Mgawanyiko tunaouamini, nayo ni yale ambayo Sharia yetu imekuja kuyasadikisha, na mgawanyiko wa pili ni ule ambao tunaukadhibisha na kumekuja katika Sheria yetu kile kinachokadhibisha, na mgawanyiko wa tatu ni ule wa yale ambayo hakijapokelewa katika Sharia yetu chochote kinachoyakadhibisha au kinachoyasadikisha na sisi tunaishia hapo. Na matamko ambayo muulizaji aliyataja katika kisa cha Bwana wetu Yusufu A.S., hayo ni mgawanyiko wa tatu ni ule wa yale ambayo hakijapokelewa katika Sharia yetu chochote kinachoyakadhibisha au kinachoyasadikisha na sisi tunaishia hapo.