Qur'ani Imechangaya Baina ya Kisa c...

Egypt's Dar Al-Ifta

Qur'ani Imechangaya Baina ya Kisa cha Hajar na Kisa cha Mariamu A.S.

Question

Matni ya shaka:
Imetaja katika Qur'ani Tukufu: {Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali. Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya, na nikawa niliyesahaulika kabisa! Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji! Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu. Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Napindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu}. [MARIAMU 22-26]
Na katika hayo kuna kuchanganya baina ya Mariamu Mwali na Bibi Hajar: Mama wa Ismaili, kwani Hajar yeye ndiye ambaye alienda kuishi jangwani na mwanae Ismaili, na alipoona kiu, Mwenyezi Mungu alimtayarishia chemchem ya maji na akanywa. Ama Mariamu Mwali hakusafiri kuelekea jangwani, na wala hakuhitajia maji, na wala hakuwa chini ya mtende.
 

Answer

Kuirudi Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Tofauti baina kisa cha Mariamu na kisa cha Hajar:
Muulizaji hakutoa dalili yoyote kwa yale aliyoyadai ya kuwepo mchanganyiko katika Qur'ani Tukufu baina ya Simulizi mbili za Hajar na Maryam, bali ameenda mbali zaidi kwa tuhuma za kufikirika ili kuthibitisha kile anachokidai, na utamwona akisema kwamba Hajar alikimbia na kuelekea mwituni wakati ambapo Marya hakukimbilia mwituni.
Na Qur'ani haikusema kamwe kwamba Maryam ametoroka kwenda mwitu, kama ilivyotajwa katika kisa cha Hajar, bali Qur'ani ilisema: {Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali} [MARYAM 22]. Yaani Hakika kwamba sehemu aliyokimbilia Maryam ilikuwa mbali na ni nje ya mji na watu wake, na Qur'ani Tukufu haikutaja kwamba ilikuwa mwituni kama anavyodai muulizaji.
Ama kuhusu rafiki huyu mwenye hijabu kuhitaji maji kutoka kwa jamaa zake katika mfano wa hali hii ambayo aliingia nayo ile sehemu ya kujihifadhi, na jambo hili ni katika misingi ya maisha ya mwanadamu,. Na wala sijui inakuwaje kwa mtu mwenye akili timamu anaweza kusema kwamba Bi Maryam hakuwa anahitaji maji? Je, Maryam sio binadamu anayepatwa na kiu inayowapata wanawake wengine na watoto wake? Je Qur'ani inapotaja ya kwamba Maryam alikunywa hii inamaanisha kwamba yeye alichanganya mambo mawili?
Na kwamba Bibi Hajar pia hakuelekea jangwani, bali Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka kuimarisha Nyumba Tukufu kupitia Bibi Hajar na mwanae bwana wetu Ismael, basi akaamuru Bwana wetu Ibrahim A.S. kwamba awachukue na awaache katika mahali hapo kuimarisha Nyumba Tukufu na nguzo za Dini Tukufu,
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


 

Share this:

Related Fatwas