Misri Haikuwa Miongoni mwa Mirathi ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Misri Haikuwa Miongoni mwa Mirathi ya Wana wa Israel

Question

Matini ya Shaka:
Imetajwa katika Qur'ani Tukufu: {Musa akawaambia watu wake: Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu. Naye humrithisha amtakaye katika wajawake. Na mwisho ni wa wachamngu. Wakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia, na baadaya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamhilikisha adui wenu, na akakufanyeni nyinyi ndio wa kufuatia kushika nchi, ili atazame mtakavyo kuja kutenda nyinyi}. [AL ANFAAL 128-129] Imetajwa katika Tafsiri yake: Kwamba Misri ilifunguliwa katika zama za Nabii Dawud A.S. Basi kilichobainika kwamba Qur'ani katika Aya hizo ilitofautiana na uhalisi na imetofautiana na yaliyotajwa katika Kitabu Kitakatifu, kwani Watu wa Isra'el walirithi ardhi ya Kan'aan, na hawakurithi ardhi ya Misri.
 

Answer

Kuirudi shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Aya hizi zinafafanua kwamba Musa A.S, aliwaamuru watu wake wavumilie na kumtaka msaada Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya vitimbi vya Firauni na watu wake, na hakika Firauni amewaamuru wasaidizi wake wawauwe watoto wa kiume wa kizazi cha Israeli na wahalalishe wanawake zao, na hii ilikuwa kabla ya kuja Musa A.S, na baada ya Imani yao kwa Musa Firauni aliwapatia vitisho vya kuwaadhibu na kuwaua.
Basi wakaudhiwa kabla ya wao kuwajia na baada ya kuwajia pia, na Mwenyezi Mungu akawabashiria wao Ushindi na urithi wa Ardhi, na urithi hapa sio matumizi ya kheri za ardhi na kuwadhalilisha watu wake katika masilahi yao, lakini ni urithi wa Kisharia, nao ni kuifikisha Taurati kwa Mataifa mbalimbali. Na hiyo Aya haiongelei kuainishia mahali pa ardhi hiyo, ama yaliyosemwa na wanazuoni wa tafsiri katika kuainisha ardhi hiyo kwamba hiyo ni ardhi ya Misri, basi hiyo ni kauli inayothibitishwa na historia na haikanushi, kwani Watu wa Israel walikuwa makhalifa katika zama za bwana wetu Musa A.S. Baada ya Mwenyezi Mungu kumwokoa Firauni na wale walioamini na kuwa naye, wakaelekea katika mlima wa Turi, na Mwenyezi Mungu akawawezesha kuishi katika ardhi hiyo na akawaruzuku chakula cha Manna na Salwaa, na Mlima Turi ni sehemu ya ardhi ya Misri, na kwa hivyo Watoto wa Israeli Mwenyezi Mungu aliwawezesha kuishi Misri, na wakapewa tena uwezo wa kuijenga ardhi wakati wa Dawud A.S, na Suleimani A.S.
 

Share this:

Related Fatwas