Je Mtume S.A.W Alimdharau Kipofu?

Egypt's Dar Al-Ifta

Je Mtume S.A.W Alimdharau Kipofu?

Question

Matni ya Shaka:
Imepokelewa ndani ya Quran kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Mtume alikunja pasi la uso na akageuka * Kwa sababu alijiwa na kipofu * Na nini kitakujulisha pengine yeye atatakasika? * Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? * Ama ajionaye hana haja * Wewe ndio unamshughulikia? * Na si juu yako kama hakutakasika * Ama anaye kujia kwa juhudi * Naye anaogopa * Ndio wewe unampuuza?} [ABASA: 1: 10].
 

Answer

Imepokelewa na mmoja wa Swahaba naye ni Ibn Ummu Maktoum siku moja alikwenda kwa Nabii wa Kiislamu akamkuta anazungumza na wakubwa wa Kikuraishi ndipo Swahaba huyu akamuambia Mtume: Nisomeshe na unifundishe kile alichokufundisha Mwenyezi Mungu, hapo Mtume hakumgeukia na akampuuza, kisha akasema ndani ya nafsi yake: “Hawa viongozi wanasema anasikilizwa na watoto wadogo watumwa na watu wajinga” hivyo akakunja uso wake na kumchukia kisha akaendelea na watu ambao alikuwa anazungumza nao.
Sisi tunauliza: Ni vipi Nabii wa Uislamu anawachunga sana watu wenye vyeo na kuwakataa watu mafakiri masikini na kukunja uso wake kwa mtu kipofu? Nafasi yake ipo wapi kwa upande wa Masihi ambaye pindi alipojiwa na mtu kipofu alimkumbatia kwa huruma yake na usimamizi wake na kumrejeshea macho yake?
Jibu la Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mazungumzo kuhusu Ibn Maktoum kama yalivyo kwenye vyanzo:
Wafasiri wa Qur`ani zaidi ya mmoja wamesema kuwa Mtume S.A.W siku moja alikuwa akizungumza na baadhi ya wakubwa wa Kikuraishi na alikuwa na matumaini ya kusilimu kwao, wakati anazungumza nao mara akatokea Ibn Ummi Maktoum – na alikuwa miongoni mwa watu waliosilimu zamani – akawa anamuuliza swali Mtume S.A.W kuhusu kitu na kumsisitiza, na Mtume S.A.W alipenda angenyamaza ili aweze kukamilisha mazungumzo yake akiwa na matarajio ya kuongoka kwao, ndipo alipomkunjia uso Ibn Ummu Maktoum na kumpuuza na kuendelea na wengine, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha Aya: {Mtume alikunja pasi la uso na akageuka * Kwa sababu alijiwa na kipofu * Na nini kitakujulisha pengine yeye atatakasika?} ( ).
Kama unavyoona katika kisa hiki hakuna maelezo yaliyopokelewa kwenye swali kuwa Mtume S.A.W aliipa nafasi zaidi kauli ya hawa viongozi: Hakika anasikilizwa na watoto wadogo watumwa na watu wajinga hivyo akakunja uso wake kutokana na hilo.
Kama vile ukute kwenye vyanzo vingi kuwa Ibn Ummu Maktoum alimsisitiza sana Mtume S.A.W kwenye ombi lake.
Mtume wa huruma na ulinganiaji:
Kisha tafasiri inayodai kitendo hiki cha Mtume S.A.W ni kumdharau mtu kipofu au kupendelea kwake watu matajiri kuliko watu masikini ni tafsiri ipo mbali na ukweli, na tafasiri hii inazidi kuwa mbali zaidi ikiwa tutaangalia nafasi yake Mtume S.A.W katika usimamizi wake kwa watu masikini miongoni mwa Maswahaba zake na wengine, angalia namna Mtume S.A.W alivyoshirikiana na Bilal Al-Habashy na kumuinua pamoja na kumteua kuwa muadhini wake, bali angalia ukarimu wake Mtume S.A.W kwa Ibn Ummu Maktoum mwenyewe ni mtu ambaye Mtume S.A.W alimuweka karibu na kumpa jukumu la kuongoza Madina mara kumi na tatu hivyo ni vipi inasemwa ( ) kuwa: Kumfanyia aina fulani ya dharau?
Kwani shime ya Mtume S.A.W ilikuwa ni kuwalingania watu kwenye dini na kuwangoza awe masikini au tajiri, vile vile katika wakati ambao masikini anakuwa na sehemu katika uongofu wa Mungu basi tajiri katika hili anakuwa na haki tofauit na inavyodhaniwa kuwa tajiri hawezi kuingia kwenye ufalme wa mbinguni ( ) na kuelekeza ulinganiaji kwa kundi bila ya kundi lingine si katika mwenendo wa waongofu.
Kuyapa uzito kati ya masilahi mawili:
Hivyo tukuio la kuwa Ibn Ummu Mkatoum alisisitiza – Si la kuzingatiwa kutokana na hali iliyokuwepo – katika kuomba ufafanuzi kuhusu jambo la dini yake ndani ya wakati ambao Mtume S.A.W alikuwa mwenye kushughulishwa na kazi ya ulinganiaji wa wengine miongoni mwa wale ikiwa itawezekana kuongoka basi hilo litakuwa ni linganio litakalo pelekea watu wengi kuongoka, kisha Mtume S.A.W akayapa nguvu masilahi ya Kisharia ya shime ya kuwangoa zaidi ya masilahi yanayopatikana kwenye kutoa jibu la swali la Ibn Maktoum, haswa ukizingatia uhusiano wa Mtume S.A.W na Ibn Ummu Maktoum ni endelevu, hivyo akaona kuwa kuleta uongovu kwa watu wa mbali ambao ni ngumu kuwapata ni bora zaidi kuliko kuleta uongovu kwa mtu wa karibu na kuna wepesi kumfikia, lakini hata hivyo Qur`ani ilitoa maelekezo kwa Mtume S.A.W kuwa huenda kukawa nyuma ya matukio mambo yasioonekana mwanzoni, hivyo ikateremka Sura hii ikimfundisha Mtume S.A.W uwiano kati ya viwango vya masilahi, na wajibu wa kusoma yaliyojificha ili asijepitwa na jambo muhimu kwa umuhimu mwingine, na Aya zikaelezea Swala la Imani na kuwa mwanadamu ambaye hamuamini Mwenyezi Mungu vyovyote utakavyofikia utajiri wake na nafasi yake ni mwenye sehemu ndogo sana kuliko Muumini hata kama ni masikini na kipofu ( ).
Kisha tusiachwe kuwa kuthibiti mfano wa Aya hizi za Qur`ani Tukufu hoja juu ya Qur`ani Tukufu kujitenga na haiba ya Mtume S.A.W kwani mtu anatunga kitabu kisichoendana na kuthibiti lawama zake ambazo atalaumiwa nazo na Mola wake.

 

Share this:

Related Fatwas