Je, Mwenyezi Mungu Mtukufu Aliwatak...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je, Mwenyezi Mungu Mtukufu Aliwataka Ushauri Malaika Kisha Wakapinga Kusudio la Mungu?

Question

Matni Yenye Shaka:
Ndani ya Qur`ani Tukufu imekuja kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Kiongozi, wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua} [AL BAQARAH: 30].
Hivyo ni kwanini Mwenyezi Mungu aliwataka Malaika wake ushauri hali ya kuwa Yeye ni tajiri kuliko kutaka ushauri kwa yeyote? Na je inaingia akilini kuwa Malaika wema wanaasi na wanapinga utashi wa Mwenyezi Mungu, na wanadai kuwa na elimu ya mambo yasiyooneana kinyume na ukweli, na wanapinga kuhusu Adamu kabla ya kuumbwa kwake na wakizitaka nafsi zao kwa ndimi zao.
 

Answer

Jibu lake:
Kituo cha tafiti za Kisharia Ofisi ya Mufti wa Misri.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Shaka hii si mpya bali yenyewe ina asili ya zamani katika imani za baadhi ya makundi ambayo yaliitwa kwa jina la “Al-Hashwiyah” makundi haya yalipinga suala la Malaika kuzuiliwa kufanya dhambi jambo ambalo Waislamu wamekubaliana kuwa Malaika hawatendi dhambi.
Kutokana na shaka hii ni kuwa mwenye shaka alidhania kuwa Aya inatoa habari kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwataka ushauri Malaika, lakini Aya haipo kwenye maana ya ushauri bali yenyewe inaelezea habari itokayo kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Malaika ili wapate maarifa na uelewa wa ubora wa mwanadamu kwa sura ambayo inaondoa kile alichokifahamu Mwenyezi Mungu kuwa kwenye nafsi zao kumekuwa na dhana mbaya kuhusu huyu mwanadamu, habari hii imekuja katika sura ya Malaika kutakiwa ushauri ikiwa ni sehemu ya kuwakirimu na inakuwa ni mafunzo ndani ya kuwakirimu, mfano wa mwalimu kumpa faida mwanafunzi kwa sura ya swali na jibu, na katika hukumu ya hilo pia ni pamoja na Mwenyezi Mungu kutengeneza sura ya ushauri katika mambo mbalimbali na kuwazindua Malaika juu ya undani na usiri wa hekima ya kuumbwa kwa Adam.
Ama kufahamika kwa Aya kupitia jibu la Malaika kuwa ni kumpinga Mwenyezi Mungu Mtukufu si sahihi, bali kusudio la kuuliza Malaika ni katika hali ya mshangao unaofungamana na uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu Naya ni mbora wa hekima kwa kumuumba kiumbe huyu ambaye watatoka katika mgongo wake watu watakaofanya uharibifu duniani na kumwaka damu na hili ni kutokana na elimu yao ambayo Mwenyezi Mungu amewafundisha, baada ya Mwenyezi Mungu kuwabainishia kuwa kuna hekima aliyoitaka Yeye Mola Mtukufu katika hilo na kuwaelezea hekima ndipo kwa haraka sana Malaika wale walisema:
{Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hekima} [AL BAQARAH: 32]. Katika haya yote hakuna maana ya kumpinga Mwenyezi Mungu Mtukufu kama wanavyodhania wadhaniaji.
Kwa sababu hiyo Imam Razy R.A anasema: Kauli yao kuwa Malaika wamempinga Mwenyezi Mungu Mtukufu ni katika madhambi makubwa, na tunasema kuwa si lengo lao kwa swali hilo kumzindua Mwenyezi Mungu na kitu alichokuwa amejisahau nacho kwani mwenye kuamini hivyo huyo atakuwa amekufuru, na si kumpinga Mwenyezi Mungu katika kufanya jambo lake, bali makusudio ya swali hilo ni mambo mengi:
La Kwanza: Ni kuwa mwanadamu anapokuwa hajafahamu hekima ya mwenzake kisha akamuona mwenzake anafanya kitendo mbali na hekima zake huwa anauliza: Vipi unafanya hili? Kana kwamba anashangaa kutokana na ukamilifu wa hekima yake na elimu yake, na anasema: Kumpa neema hii mtu mwenye kuharibu mambo ambayo akili haiwezi kuongoka kwenye hekima ya jambo hili ikiwa utalifanya, na ninafahamu kuwa wewe hulifanyi isipokuwa ni kwa ukina zaidi na siri iliyofichika ambapo wewe unaiona ni ukubwa wa aina gani wa neema yako na ukubwa wa elimu yako, jibu ni kusema kauli yake Mola Mtukufu:
{Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo} kana kwamba ameshangaa kutokana na ukamilifu wa elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na wigo wa hekima yake iliyojificha na akili zote.
La Pili: Kupatikana kwa swali lenye kutaka jibu si jambo lililokatazwa.
Ama ufahamu na uelewa wa muulizaji kuwa Malaika wamedai elimu ya kufikirika kwa maana ya mambo yasioonekana kwa sasa pasi na haki nalo hilo pia si sahihi, kwa sababu katika kazi za Qur`ani ni pamoja na kufupisha maelezo na kuleta makusudio muhimu, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye ambaye aliwapa habari Malaika ya hilo na kauli hii imepokelewa kutoka kwa Ibn Masoud na Maswahaba wengine wengi.
Kama vile haijawahi tokea kwa mtu yeyote kugundua kuumbwa kwa Malaika wala namna ya muundo wao ufahamu wao na uelewa wao, lakini kuamini uwepo wa Malaika na sifa zao ni katika Imani za lazima ambazo wamekubaliana Waislamu, miongoni mwa sifa za Malaika ni kuwa wao ni waja wema, wala kwa hali hiyo hawawezi kuwekwa mbali na kufahamu baadhi za sifa za viumbe kwa kule kuwaona kwao, hivyo Shaikh Twahir Ibn Ashuur R.A anasema: Kitendo cha Malaika kumuona kiumbe huyu wa ajabu anayekusudiwa kuwa kiongozi katika ulimwengu ulitosha ujuzi wao unaojumuisha sifa za kushangaza kwa sura ambayo itaonekana kwa nje, kwa sababu ufahamu wao ni wa hali ya juu sana uliosalimika na matirio ya akili ya kawada, ikiwa wanadamu wanatofautiana kwenye ufahamu wa mambo yaliyojificha, na katika muelekeo wa nuru ya nafsi kwenye ufahamu kwa kiwango cha tofauti zao katika sifa za nafsi, je waonaje kwa upande wa nafsi za Malaika!
Ama uelewa wa muulizaji kuwa Malaika walijitakasa kwa nafsi zao pamoja na kuleta ubishi kuhusu Adamu na kizazi chake pia hilo nalo si sahihi, kwa sababu waliyoyasema Malaika ni kuleta habari kuhusu elimu iliyotokea kwao kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutaja mema ya nafsi si jambo baya kwa hali yeyote ile bali inakuwa ni sifa njema wakati wa kuzungumzia neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo Amesema Mwenyezi Mungu: {Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie} Adhuhaa: 11. Inawezekana kusudio likawa si kusifu nafsi bali kuonesha ukamilifu wa unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kueleza maelezo haya.

 

Share this:

Related Fatwas