Je, Kuleta Takbira Kuna Asili na Za...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je, Kuleta Takbira Kuna Asili na Zama za Ujinga?

Question

Matni Yenye Shaka:
Kuleta takbira – Ni kawaida ya Kiislamu – limechukuliwa kutokana na asili ya zama za kijinga, Waarabu katika zama za ujinga walikuwa wanaleta takbira kisha wakachukuwa Waislamu kwa sura iliyokuja ndani ya Qur`ani:
 

Answer

{Na sema: Alhamdulillah, Himidi zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye hana mwana, wala hana mshirika katika ufalme, wala hana rafiki wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa} [AL ISRAA: 111].
Na katika mengine yaliyokuja ni kauli yake Mola Mtukufu:
{Na alipo liona jua linachomoza akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Huyu mkubwa kuliko wote. Lilipo tua, alisema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayo fanyia ushirikina} [AL AN'AAM: 78].
Uislamu umenukuu ibada hii kutoka kwa Waarabu wakati ambapo Waarabu walikuwa wakimtukuza Mwenyezi Mungu baadhi ya nyakati wakisema: “Allahu Akbar” kutokana na imani yao ya uwepo wa mungu wa mbinguni, au kuwa Mwenyezi Mungu ni kati miungu yote yeye ndiye mungu wao na miungu mingine wasaidizi wake na wafanya kazi wake duniani,
Jibu la hilo:
Kituo cha tafiti za mambo ya Kisharia ofisi ya Mufti wa Misri.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Maana ya neno Takbira lipo kinyume na ibada za masanamu:
Kwanza: Kinyume kabisa na madai haya, kwani takbira hii ambayo wanaitumia Waislamu asubuhi na jioni ambayo ni: “Allahu Akbar” na katika masikukuu yao na adhana zao hazikuwa isipokuwa ni moja ya nyiradi ambazo zinaonesha Uislamu kupinga maana ya ibada zisizokuwa za Mwenyezi Mungu na kuthibitisha upekee wa Mola wa viumbe vyote.
Al-Aluusy R.A anasema: Baadhi yao wamesema kumtukuza Mola Mtukufu ni kufahamu kuwa wewe hauwezi kumtukuza isipokuwa kwa kutumia hiyo takbira, na Ibn Atwaa amesema: Kumtukuza Mola Mtukufu kwa kutukuza neema zake na wema wake moyoni kwa kufahamu upungufu katika kumshukuru, ni vipi mtu anaweza kutekeleza shukurani zake kwa Mola Mtukufu na neema zake hazihesabiki!!
Imamu Razy R.A amesema: Kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu kuna maana za aina nyingi:
Ya kwanza: Kuitukuza nafsi yake, nako ni mja kuamini kuwa ana wajibu wa lazima kwa Mwenyezi Mungu.
Ya pili: Kumtukuza katika sifa zake kwa kuamini ukamilifu wa sifa zake na kumuepusha na kila upungufu, na kuamini kuwa kila moja katika sifa hizo inafungamana na elimu isiyo na mwisho, na uwezo wake unahusiana na kutokuwa na mwisho, na kuamini kuwa sifa zake ni za enzi na kuendelea bila kikomo zimeepukana na hali ya kubadilika kwisha na kuondoka.
Ya tatu: Kumtukuza katika matendo yake kwa mja kuamini kuwa hakuna jambo linalopita duniani isipokuwa kwa kupitishwa na hukumu zake utashi wake na uwezo wake.
Ya nne: Kumtukuza katika hukumu zake nako ni mja kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mfalme wa kutiiwa ni kwake hutekelezwa amri zake na makatazo.
Ya tano: Kumtukuza katika majina yake nako ni kutomtaja isipokuwa kwa majina yake mazuri, wala kusifiwa isipokuwa kwa sifa zake takatifu zilizoepukana na upungufu.
Ya sita: Mja kufahamu baada ya kufikia kiwango hiki cha utukuzo kuwa ni kiwango cha akili yake na ufahamu wake, na yote hayo hayatoshelezi kumtukuza Mola Mtukufu, na kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mkubwa zaidi ya yote hayo, na haya ni makadirio ya juu anayokadiriwa mja mnyonge katika kumtukuza Mola Mtukufu, ni maana ipi ya ibada za kisanamu au za kishirki baada ya kufahamu maana hii katika utajo huu mzuri, maana ya kauli yake Mola Mtukufu: {Na mtukuze kwa utukufu mkubwa} ni maneno mapana zaidi kuliko kauli ya: Allahu Akbar.
Pili: Na kauli yake Mola Mtukufu katika Aya hii: {Na mtukuze kwa utukufu mkubwa} sio kusudio lake kama inavyofahamika kuwa semeni: “Allahu Akbar” ambapo kusudio lake ni kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ujumla.
Imamu Twahir Ibn Ashuur R.A anasema: Na maana ya {Mtukuze} nina imani kuwa Yeye ni Mkubwa, kwa maana ya mkubwa wa ukubwa unaojumuisha wajibu wa uwepo na kujitosheleza, na sifa zote za ukamilifu ni zenye kukamilika kwa sababu kusifika kwa sifa hizo zote ni ukamilifu, na kusifika kinyume na hivyo ni upungufu na maana ndogo.
Uislamu unatufundisha kukubali haki msemaje wake hata awe vipi:
Tatu: Tukichukulia kwa mfano wa utajo huu ulikuwepo kwa Waarabu kabla ya kuletwa kwa Mtume - Amani iwe kwake – likiwa linafahamika kwa maana ya kuepukana Mwenyezi Mungu na mapungufu pamoja na kumpwekesha, hivyo hakuna ulazima wa kuharamisha hilo katika Sharia ya Kiislamu kwa vile hili linakubaliana na yaliyokuja kwenye Sharia ikiwa ni pamoja na kumpwekesha Mola Mtukufu na kumuepusha na mapungufu na kumtukuza.
Kulieneza hilo kwa Waarabu wote halikubaliki:
Nne: Waarabu kabla ya Uislamu kuhusu kadhia ya dini walikuwa wanatofautiana kwa tofauti kubwa, wakati huo miongoni mwao walikuwa na dini sahihi ambao walimfahamu Mwenyezi Mungu Mtukufu na walikuwa maarufu katika hilo, miongoni mwao pia walikuwepo wanaotengeneza mungu asubuhi kwa kutumia tende kisha jioni wanamla, hivyo si wepesi kuainisha dini ya Waarabu wote kwa kina zaidi na taswira zao kuhusu mungu, pamoja na uwazi ni kuwa wengi wao walikuwa wanaabudia masanamu, kisha akaletwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W ili kuleta marekebisho ya imani hii chafu, kama vile kufanya marekebisho ya yale yaliyoharibiwa na imani za wengine.

 

Share this:

Related Fatwas