Ni vipi Shetani Anaweza Kutawala Uf...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ni vipi Shetani Anaweza Kutawala Ufalme wa Suleiman?

Question

Asili ya shaka
Ndani ya Qur`ani Tukufu imekuja: {Na Tulimtia mtihani Suleiman, na Tukauweka mwili juu ya kiti chake, kisha akarejea kwa kutubu * Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na Unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji}[SWAD: 34, 35].
 

Answer

Wafasiri wametaja kisa cha pete ya Nabii wa Mwenyezi Mungu Suleiman ambayo ilikuwa na ufalme wake, siku moja aliivua na ndipo shetani akaichukua na kupitia pete hiyo ndipo alipoweza kuutawala ufalme wa Suleiman na kujifananisha na sura ya Suleiman mpaka pale ilipomdondoka maeneo ya baharini na Nabii Suleiman akaipata kwenye tumbo la samaki kisha akaivaa na kurudi tena katika ufalme wake.
Ni vipi shetani alitawala ufalme wa Suleiman, na nini maana ya hii pete ya kichawi ambayo mwenye kuivaa miongoni mwa wanadamu au majini anakuwa mfalme?
Kuondoa shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hapa muulizaji anaelezea kisa cha habari za Wasraili kuhusu Nabii Suleiman kisichokubaliana kwa hali yeyote na nafasi ya Unabii na kuzuiliwa kwa Manabii kutofanya maasi.
Kisa hiki kimetajwa na baadhi ya wanatafsiri wakinukuu kutoka vyanzo vya Kiyahudi, na wanatafsiri wameelezea chanzo cha kisa hiki( ).
Miongoni mwa wanatafsiri wapo wanaokusudia kunukuu kila wanachokuta kuhusu Aya wakiacha uchunguzi wa kiumakini kwa msomaji, wakitosheka na yanayopewa nguvu na akili zao, wengine ni wenye kufanya uchambuzi wa yale aliyoyapokea na kuyapata, kisa hiki ambacho amekielezea muulizaji kimekuwa na ukosoaji na uchambuzi mwingi wa wanatafsiri, na wakaweka wazi kuwa kimetengenezwa na Mayahudi pamoja na wanafalsafa wazushi( ).
Shetani hawezi kujiweka katika sura ya Manabii, na haiwezekani kuchanganyika kwenye familia ya kifalme Nabii wao na shetani( ).
Ama kuhusu pete ya Nabii Suleiman A.S. ambayo imefungamana na ufalme wake ni jambo lisilokubalika kabisa, ambapo akili inakataa na wala Qur`ani haijatuelezea hilo( ) pamoja na kwamba kawaida ya Qur`ani Tukufu kuelezea umaalumu wa baadhi ya mambo kama ilivyoelezea kuhusu fimbo ya Nabii Musa A.S. ni vipi Qur`ani Tukufu ielezee umaalumu wa fimbo bila kuelezea suala la pete?
Na kwa vile imethibiti kudondoka kwa kisa hiki, hivyo kumethibiti kudondoka kila alichokieleza muulizaji ikiwa ni katika ufafanuzi wa kisa hicho kuongezea swali la muulizaji limechanganya ndani yake vitu vya kushangaza visivyoaminika wala kukubalika na akili.
Tafsiri sahihi ya Aya Tukufu
Ni kuwa Nabii Suleiman A.S. alisema: Usiku huu nitawazungukia wanawake sabini na kila mmoja atazaa mtoto atakayepigania njia ya Mwenyezi Mungu, wala hakusema In shaa Allah kwa maana Mwenyezi Mungu akipenda, hivyo aliwazungukia na hakuna aliyepata ujauzito isipokuwa mwanamke mmoja, na akajifungua mtoto wa kiume, maelezo haya yamepokelewa na Masheikh wawiil “Bukhari na Muslim” na wengineo kutoka kwa Abi Huraira, na ndani yake kuna maelezo yanayosema: Ninaapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad ipo mikononi mwake lau angesema In shaa Allah kwa maana ya Mwenyezi Mungu akipenda basi wangepigania njia ya Mwenyezi Mungu kwa kutumia farasi.
Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka kumfundisha jambo la kutanguliza neno “Mwenyezi Mungu akipenda” nalo ni jambo muhimu sana alilifanya kama hilo Mtume S.A.W. pindi alipoulizwa kuhusu kisa cha vijana wa Kahfi “Pangoni” akaahidi majibu na akasema: Nitakuelezeeni kesho kile mlichoulizia, wala hakusema In shaa Allah, ndipo ikateremka Aya ndani ya Qur`ani Tukufu: {Wala usisema kamwe kwa jambo lolote lile: Hakika nitalifanya hilo kesho * Isipokuwa Mwenyezi Mungu akipenda}[ALKAHF: 23, 24].
Kusudio la mwili ni ule upande ambao amezaliwa, na maana ya kuwekwa juu ya kiti chake: Ni hali ambayo inayokubaliana na yeye kuonekana( ). 

Share this:

Related Fatwas