Je! Alama za Ibada ya Hija ni katik...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je! Alama za Ibada ya Hija ni katika Mabaki ya Alama za Ibada za Masanamu?

Question

Asili ya shaka
Imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu:
{Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliye konda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali * Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya wanyama hoa alio waruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri * Kisha wajisafishe taka zao, na waondoe nadhiri zao, na waizunguke Nyumba ya Kale}[AL-HAJ: 27- 29].
 

Answer

Matendo haya ya ibada ya Hija hayakuwa isipokuwa ni katika alama za matendo ya ibada za masanamu, yameendelea kubakia kutoka zama za ujinga, mfano kama vile kutufu kurusha vijiwe kubusu jiwe jeusi kuchinja na mengine, hivyo ni kwa nini Mtume wa Uislamu aliendeleza alama hizi za ibada za masanamu baada ya kuwashinda watu wa Makka na kuvunja masanamu?

Kuondoa shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hija ni katika mila za Nabii Ibrahim A.S. ambayo Mwenyezi Mungu ametuamrisha kufuata mila yake, na Mwenyezi Mungu Ameamrisha watu kutangaziwa ibada ya Hija.
Inafahamika kuwa Manabii wote na Mitume dini yao ni moja nayo ni ulinganiaji kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu, pamoja na kuwepo kwa baadhi ya tofauti kati yao katika Sharia, isipokuwa zenyewe zinakaribiana sana na lengo ni moja. Mtume S.A.W. amesema: “Mitume ni ndugu wa baba mmoja mama zao tofauti na dini yao ni moja”( ).
Hija ni Ibada inayoshirikiana kati ya Sharia ya Nabii Ibrahim A.S. na Sharia ya Mtume wetu Muhammad S.A.W. Mtume wa mwisho, ibada ya Hija imeendelea kutekelezwa kwa mwenendo ambao Nabii Ibrahim ameufundisha kwa watu kwa muda mrefu, kisha mafundisho hayo yakaingiziwa baadhi ya ibada ambazo ziliharibu, miongoni mwa uharibifu huu ni pamoja na kuweka baadhi ya masanamu pembezoni mwa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu, na washirikina kutufu Nyumba hiyo wakiwa uchi. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:
{Na haikuwa ibada yao kwenye hiyo Nyumba (Al-Kaaba) ila ni kupiga miruzi na makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru} [AL ANFAAL: 35]. Ndipo ikaja Sharia ya Mtume Muhammad S.A.W. na kusahihisha yale yaliyoharibiwa na hawa makafiri na kurejea ibada ya Hija kwa usahihi wake.
Na matendo ya ibada ya Hija si katika matendo yaliyobuniwa na kuzushwa na Manabii bali ni amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na matendo haya yanasimama kwa kuitikia amri ya Mwenyezi Mungu, ibada ya kutufu kutembea kati ya Safa na Marwa kuchinja kubusu jiwe jeusi na zingine katika matendo ya Hija hayakusudiwi hayo yenyewe bali makusudio ni kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuonesha utiifu kwake, kwani ibada ya Hija ni sura miongoni mwa sura za kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alama za mahujaji ni: “Labbaika Allahumma Labbaika, Labbaika laa shariika laka Labbaika” hayo maneno ni dalili ya kumtenga Mwenyezi Mungu peke yake, na umar Ibn Al-Khatwab R.A. akasema wakati wa kulibusu jiwe jeusi: “Mimi ninafahamu kuwa wewe ni jiwe hauna madhara wala manufaa lau mimi nisingemuona Mtume S.A.W. anakubusu nisingekubusu”( ).
Matendo ya ibada ya Hija Mwenyezi Mungu hakuna chochote anachofaidika nacho katika hayo bali makusudio yake ni waja wa Mwenyezi Mungu wapate ucha-Mungu kwa kufuata na kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ngamia wa sadaka tumekufanyieni kuwa nikudhihirisha matukuzo kwa Mwenyezi Mungu; kwa hao mnakheri nyingi. Basi litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao wanapo simama safu. Na waangukapo ubavu kuleni katika hao na walisheni walio kinai na wanaolazimika kuomba. Ndio kama hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru * Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia ucha-Mungu wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa alivyo kuongoeni. Na wabashirie wafanyao mema} [AL-HAJ: 36, 37].

 

 

Share this:

Related Fatwas