Je! Nabii Ismail Alikuwa ni Mtu Mwo...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je! Nabii Ismail Alikuwa ni Mtu Mwovu?

Question

Je! Nabii Ismail Alikuwa ni Mtu Mwovu? 

Answer

Imekuaj ndani ya Qur`ani Tukufu: {Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii} [MATYAM: 54].
Hapa kunatofauti kati ya Qur`ani na Taurati, kwa sababu Qur`ani inaelezea kuwa Ismaili alikuwa ni Mtume Nabii, wakati Taurati inasema: “Naye atakuwa kama punda mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote” Mwanzo 16: 12.
Kuondoa shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ismaili A.S. Nabii katika Manabii wa Mwenyezi Mungu, naye ni mtoto wa Nabii Ibrahim A.S. ni mwenye ubora mkubwa na heshima kubwa, kwani alisubiri sana kwenye mtihani wa Mwenyezi Mungu, na hilo ni pale Nabii Ibrahim alipoona ndotoni kuwa anamchinja mwanawe Ismaili, na ndoto za Mitume ni kweli, hivyo alimpa habari mwanawe ya hilo ndipo Nabii Ismaili alipojisalimisha pamoja na baba yake kwenye amri ya Mola wake, na Mwenyezi Mungu akamuokoa kutokana na kuchinjwa na kuwapa fidia mnyama wa kuchinjwa. Nabii Ismaili alimsaidia baba yake katika kujenga nguzo za Msikiti Mtakatifu wa Makka, hii ni heshima kubwa pia, na miongoni mwa heshima kubwa kwake ni kuja kutokana na kizazi chake kitakatifu Mtume wetu Muhammad S.A.W.
Mwenyezi Mungu Amemsifu katika Aya hii Tukufu kuwa alikuwa ni mtu mkweli wa ahadi, na amemuhusisha na sifa hii – pamoja na kuwa ukweli ni sifa ya Manabii wote – ni kwa sababu alikuwa ni maarufu katika sifa hiyo, kwani aliahidi subira wakati wa kutakiwa kuchinjwa na alitekeleza ahadi hiyo, ambapo Mwenyezi Mungu Anasema Akimuelezea kauli yake kwa baba yake: {Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanaosubiri} [AS-SWAFFAAT: 102].
Na kauli yake Mola Mtukufu: {Na alikuwa Mtume Nabii} inaonesha wazi juu ya heshima ya Nabii Ismail A.S. na ubora wake kwa ndugu yake Is-hak A.S. kwani Mwenyezi Mungu Amemhusisha Utume na Ujumbe kwa pamoja kwani Mwenyezi Mungu Alimpeleka kwa Waarabu wa kabila la Jurham na ndani ya kabila hilo alioa na kupata mtoto, aliwaelezea kuhusu Mwenyezi Mungu Sharia zake ambazo Amewawekea. Ama Is-haka amehusishwa na Utume tu pasi ya kupewa Ujumbe. Mwenyezi Mungu Amesema: {Tulimpa Is-haq na Yaaqub, na kila mmoja tukamfanya Nabii} [MARAYAM: 49].
Ama yaliyokuja ndani ya Taurati wasifu kuwa ni mtu muovu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, kwa maana ni mtu dhalimu muovu anachukua kwa watu kwa njia batili na anabadilisha dini ya Manabii na anaongopa kwa Mwenyezi Mungu na mfano wa hayo.
Ni maelezo yanayopingana na yaliyokuja kwenye Kitabu Kitakatifu kwa sababu tunakuta kinamsifu Ismaili sifa tofauti na sifa hii, kinasema: “Na kwa habari za ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, name nitamwongeza sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, name nitamfanya awe taifa kuu”. Mwanzo: 17: 20.

 

 

Share this:

Related Fatwas