Je! Mtume S.A.W. Alikuwa na Shaka katika Wahyi?
Question
Answer
Asili ya shaka
Imekuja ndani ya Qur`ani kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka} [YUNUS: 94].
Na kauli ya Mola Mtukufu: {Kitabu kilichoteremshwa kwako - basi isiwe dhiki kifuani kwako kwa ajili yake, upate kuonya kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini} [AL A'ARAAF: 02].
Ni wazi kwa Nabii huyu wa Uislamu alikuwa na shaka katika chanzo cha Ufunuo wake mpaka chanzo cha Ufunuo wake kikamnasihi kuwauliza katika hilo Mayahudi na Wakristo ambao wamesoma Kitabu kabla yake, ikiwa Mtume anashaka katika Ujumbe wake na mfikishaji anashaka katika ukweli wa ufikishaji wake ni vipi anategemewa kwa msikiaji wake kumuamini?
Kuondoa shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Imani ya Mtume S.A.W. katika yale aliyoshushiwa Ufunuo:
Kwa mtazamo jumla juu ya hali za Mtume S.A.W. na kwa maelezo ya Qur`ani Tukufu kwake inabainika kwa uwazi ni kiwango gani alikuwa na imani na kile alichokuwa akipokea katika Wahyi na chanzo chake ni kutoka kwa Mola wa viumbe vyote.
Kwa – mfano – angalia msimamo wa Mtume S.A.W. kwa wale waliokuwa wanamfanyia uadui wakati wote wa uhai wake hivyo akapigana nao na akiwa ni mwenye subira kwenye kupigana nao kwa kipindi chote cha miaka ishirini na mitatu akiwa ni mwenye kuthibiti kwenye ulinganiaji wake kuwa Yeye ni Nabii aliyetumwa na kuwa amefunuliwa, hivi inaingia akilini kwa binadamu kusubiri subira hii kwenye jihadi na ndugu zake wa baba mdogo miongoni mwa Waarabu hali ya kuwa Yeye anashaka na Wahyi aliyofunuliwa nao?
Angalia ni vipi alipata taabu katika kazi ya kufikisha alichoamrishwa na kufikisha kwa watu pindi alipopingwa na kufanyiwa maudhi kwa kupigwa na wakati mwingine kutukanwa na kutengwa, yote haya Yeye akiwa thabiti hayumbiyumbi kwenye ulinganiaji wake, hivi unaona anafanya hayo hali ya kuwa ana shaka – hapana – hata kidogo kuwa na shaka kwenye chanzo anachokipokea.
Angalia vile vile maisha yake kufikwa na hatari kwa kuisha ulinzi ambao ulikuwa unamlinda kutokana na hatari za maadui wanyemeleaji na hilo ni baada ya kuteremka kauli ya Mola Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu} [AL MAIDAH: 67], kutoka kwa Bi. Aisha R.A. amesema: Mtume S.A.W. alikuwa analindwa mpaka ilipoteremka Aya hii Tukufu: {Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu} ndipo Mtume S.A.W. alipotoa kichwa chake kutoka kwenye Kubba na akasema: “Enyi watu ondokeni kwani Mwenyezi Mungu atanilinda”( ).
Je inaingia akilini maisha yake kufikwa na hatari akiwa anapigania kitu alicho na shaka nacho? Na yasiyokuwa hayo mengi miongoni mwa matukio yaliyopelekea kuthibiti kwenye kazi yake ya ulinganiaji kwa sura ambayo wala haihiitaji nafasi ya kuwa na shaka.
Maana ya Aya mbili:
Haingii akilini kuwa katika Aya maana ndani yake ina kitu kinachothibitisha shaka katika chanzo cha Wahyi hasa pindi inapokuwa shaka hii – inayodaiwa – kwa upande wa sehemu ya majukumu yake ya ufikishaji wa Ufunuo, kwani chanzo cha kukinaisha watu ni kutoonekana anachopewa msikilizaji hoja ya kumletea shaka katika kazi ya ufikishaji wake, na namna gani anafanya hivyo na pembezoni mwake kuna maadui ambao lau wangefahamu hili wangemfanyia ubaya kwa maana ya ubaya bali pembezoni mwake kuna Maswahaba na wafuasi ambapo lau wangeangalia kwa maana hii basi wangemuuwa badala ya kupigana naye hasa baada ya kuuza vitu vyao kwa ajili ya jambo hili ghali na tukufu na wakaacha ndugu na watoto, hakuna ubaya kwani katika Aya hizi kumekuwa na muundo wa lugha unaofahamika na mwenye kuifanyia mazoezi miundo ya lugha ya Kiarabu inashambulia ndimi za wapingaji na kulainisha nyoyo za wafuasi.
Ama kauli ya Mola Mtukufu: {Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka} [YUNUS: 94].
Ni ufafanuzi utokao kwa Mwenyezi Mungu juu ya ukweli wa ulinganiaji wa Mtume S.A.W. kuwa Kitabu hiki ni Ufunuo wa Mwenyezi Mungu ambapo Aya imekuja baada ya kuelezea visa vya baadhi ya Manabii Nuh na Musa, na hilo kwa kuanzia na kauli ya Mola Mtukufu: {Wasomee habari za Nuhu alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Ikiwa kukaa kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu kunakutieni mashaka basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikane kwenu. Kisha nihukumuni, wala msinipe muhula} [YUNUS: 71].
Aya imeelezea kuwa mwenye kutaka kuaminisha usahihi wa chanzo cha Kitabu hiki – Na kuthibitisha ni haki ya mwenye kuzingatia – basi ni juu yake moja ya dalili hizi nazo ni kuwa yaliyotangulia na kusikika katika visa vya Qur`ani kuna kiwango cha ushirikiano na Vitabu vilivyotangulia, na kiwango hiki ni dalili kuwa nafasi ya vitabu hivi viwili ni moja ambapo ni namna gani Mtu asiyejua kusoma kilichoandikwa – Naye ni Mtume Muhammad S.A.W. – kuja na habari hizo wala hakusoma chochote kwenye Vitabu hivi.
Al-Khaadimy anasema: Ama kauli yake Mola Mtukufu: {Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu} si uwepo wa shaka kwa Mtume S.A.W. kama walivyodhani baadhi ya Wafasiri, bali kusudio ni: Sema Muhammad kumwambia mwenye shaka ikiwa unashaka mpaka mwisho wake, kwa dalili kauli yake Mola Mtukufu: {Sema: Enyi watu ikiwa muna shaka katika dini yangu} Aya, na ikasemwa: Anayeambiwa sio Mtume sawa na kauli nyingine: {Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu matendo yako mema yataanguka}( ).
Imamu Twahir anasema kuhusu maana ya Aya Tukufu na upande wa mfungamano wake na Aya iliyopita: “Kuchambua muundo wa visa ambayo Mwenyezi Mungu amevifanya kuwa mfano kwa watu wa Makka na mawaidha kwa watu wa mfano wao, uchambuzi huu umehama kutoka mfumo kwenda mfumo mwingine ambapo mifumo yote miwili ni kuwaelezea wapingaji, mfumo uliopita ni kuelezea tahadhari ya wao kuwa sawa na umma zinazofanana na wao, na mfumo huu ni sawa na kuwaelezea ushahidi wa watu wa Kitabu kwenye matuko hayo, na yaliyomo ndani ya Vitabu vilivyotangulia miongoni mwa habari za Ujumbe wa Muhammad S.A.W.( ).
Ama kauli yake Mola Mtukufu: {Kitabu kilichoteremshwa kwako - basi isiwe dhiki kifuani kwako kwa ajili yake, upate kuonya kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini} [AL A'ARAAF: 02].
Hakuna ndani yake – kwa karibu wala mbali – kinachoeleza kutokea shaka yeyote katika chanzo cha Ufunuo bali ni maelekezo kwa mwenye kuamini Kitabu hiki kutojali uwezekano wa kuwa na dhiki kwenye kifua chake kutokana na upingaji wa mpingaji au mfano wa shaka, tatizo la kuhisi dhiki na shida sio shaka.
Imamu Razy amesema: Ni Kitabu kilichoteremshwa kwako basi kuwa na kifua kipana kwani chenyewe kimeteremshwa kwako ili kuwaonya makafiri na kuwakumbusha Waumini, na makusudio: Kuituliza nafsi ya Mtume S.A.W. na chuki za makafiri, na kuwaliwaza Waumini, kwa maana ni Kitabu kimeteremshwa kwa faida na faida imepatikana hivyo usihisi taabu kwenye kifua chako ikiwa watapinga, na kwa maelezo haya na kukosekana kwa kupishana yenyewe kwa yenyewe yanabeba maneno ya utashi wa maelezo yote, na hilo ni miongoni mwa sura za ajabu za ufafanuzi. Kisha akasema: Na maana ni kuwa Mwenyezi Mungu amekiteremsha Kitabu kwako ili isijekuwa kifuani kwako tatizo bali lengo ni kufungua kifua chako( ).