Je! Kuna Zaituni huko Sinai? Na An...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je! Kuna Zaituni huko Sinai? Na Anwani ya Zamani je Zaituni Inatoka kwenye Mlima wa Sinai?

Question

 Je! Kuna Zaituni huko Sinai?
Na Anwani ya Zamani je Zaituni Inatoka kwenye Mlima wa Sinai?
 

Answer

Matni ya Shubha:
Imekuja ndani ya Qur`ani: {Kwa maji hayo tukakufanyieni bustani za mitende na mizabibu, mnapata humo matunda mengi, na katika hayo mnakula * Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao} [AL-MUUMINUN: 19, 20].
Wamesema Wafasiri: Kusudio la mti hapa ni mzaituni, sisi tunauliza: Jangwa la Sinai lililokavu halikuwa na umaarufu wa miti ya mizaituni, hivi haikuwa bora zaidi kutaja Palestina na miti yake ya mizaituni na wala sio Sinai ambayo ukame wake Mwenyezi Mungu aliteremsha kwa Nabii wa Waisraili chakula cha manna kutoka mbinguni?
Kuondoa shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hii ni katika neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuanzisha mabustani ya mitende na mizabibu, na mti huu ambao unaota mlima Sinai ni mti wa zaituni ambao unatoa mafuta yanayotengenezea chakula.
Kwanza: Ni katika makosa ambayo ameyaingia muulizaji ni kuwa amejaribu kutafsiri maandiko kwa mgawanyo wa kijiografia ya sasa baada ya kuteremka Qur`ani Tukufu kwa karne nyingi, wala hajafahamu kuwa mlima wa Sinai katika zama za kuteremka Qur`ani kusudio lilikuwa ni eneo la kaskazini Mashariki mwa Misri, linaingia eneo hilo la Sinai na sehemu kubwa ya Palestina, kisha Wanachuoni wamesema: Wala hakutegemea mgawanyo wa sasa wa kisiasa ambao umetenganisha nchi zenyewe kwa zenyewe bali Misri kwa asili ilikuwa ni eneo lote hili, ama mgawanyo wa Sykes Pico hauwezi kutafasiri maandiko matakatifu kwa maeneo hayo( ).
Pili: Muulizaji hajafahamu kusudio la utokao kwenye Aya Tukufu ambapo kusudio lake ni kuota kwa mti huu kwa mara ya kwanza, kisha baada ya hapo ukaenea maeneo mengine, na maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameuanzisha kwa waja wake mti huu uliobarikiwa kwa mara ya kwanza katika eneo la Sinai ambapo ilikuwa ndio sehemu ya kwanza kuanza kwake ni katika eneo hili, hivyo Mwenyezi Mungu ameumba mti wa kwanza wa zaituni katika eneo la mlima Sinai( ) lakini akaongeza neno “Shajarata” kwenye mlima huu, ni kwa sababu kutoka eneo hili ndio ulienea maeneo mengine ya nchi lakini mingi yake inapatikana eneo hilo( ).
Tatu: Hapa muulizaji hana ujuzi wa kijiografia, kwani mizaituni ya eneo la Sinai ni katika aina bora zaidi duniani, katika eneo hilo kuna mizaituni inayofahamika kwa makosa kwa jina la “Olea Europaea” mizaituni ya Ulaya, ambapo sahihi zaidi kuita kwa jina la “Olea Sinaensis” mizaituni ya Sinai, kwa sababu kulimwa kwake kwa asili kumetoka kwenye eneo la rasi ya Sinai na kwenda maeneo mengine ya ukanda wa bahari ya kati( ).

 

 


 

Share this:

Related Fatwas