Adamu na Kizazi chake Kutuhumiwa U...

Egypt's Dar Al-Ifta

Adamu na Kizazi chake Kutuhumiwa Ukafiri

Question

 Adamu na Kizazi chake Kutuhumiwa Ukafiri 

Answer

Matni yenye shaka:
Ndani ya Qur`ani Tukufu imekuja kauli ya Mwenyezi Mungu: {Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili akae naye kwa utulivu. Na anapo muingilia hubeba mzigo mwepesi, akitembea nao. Anapo kuwa mja mzito, wote wawili humuomba Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wao: Kama ukitupa mwana mwema tutakuwa katika wanao shukuru * Basi anapo wapa mwana mwema, wanamfanyia ushirikina Mwenyezi Mungu katika kile kile alichowapa. Mwenyezi Mungu ametukuka na huko kushirikisha kwao} [AL-AARAAF: 189, 190].
Imepokewa katika tafairi yake kuwa Adamu na Hawa walipoteremshwa kwenye ardhi Adam alifikwa na matamanio ya nafsi ndipo alipomwingilia Hawa na kushika ujauzito, pindi mimba ilipokua alijiwa na iblisi akiwa kwenye umbile la mwanadamu akamwambia: Kuna nini ndani ya tumbo lako? Hawa akajibu: Sifahamu: Iblisi akasema, ninahofia asije kuwa ni mnyama au mbwa au nguruwe. Hawa akasema: Mimi ninaogopa baadhi ya wanyama hao, iblisi akauliza: Ni kitu gani kitakujuza atatokea wapi kwenye tupu yako au mdomoni au atapasua tumbo lako kisha kukuuwa? Hawa lilimtia wasi wasi sana hilo na akamwambia Adam, waliendelea kuwa katika hali ya shida kisha iblisi akarudi tena na akasema: Mimi ni mungu ikiwa utamwomba mungu kilichokuwa tumboni akifanye kiumbe kama wewe na atoke kwa wepesi basi huyo mtoto utamwita Abdul-Harith – na iblisi kwa Malaika alikuwa anafahamika kwa jina la Harith – ndipo Hawa akamwelezea Adam na iblisi akajizoesha kwenda kwa Hawa, hakuwaacha mpaka akawazamisha baada ya Hawa kujifungua mtoto walimpa jina la Abdul-Harith.
Katika tafasiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu: {Mwenyezi Mungu ametukuka na huko kushirikisha kwao * Ati wanawafanya viumbe kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu, nao hawaumbi, bali wao ndio wanaumbwa} [AL-AARAA: 190, 191]. Kwa maana ya masanamu.
Kisa hiki cha kushangaza kimekuja kutoka wapi, na ndani ya Aya kuna kinachofahamisha ukafiri wa Adam?
Kuondoa Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ubatilifu wa vigezo vya mapokezi ya hii shaka:
Sio yote yaliyopokelewa ndani ya kitabu cha tafsiri yanakuwa ni sahihi na kutegemewa kwa sababu baadhi ya wafasiri wanategemea njia ya kukusanya yaliyosemwa pasi na kuangalia yaliyokuwa sahihi na dhaifu katika lengo la kukusanya mapokezi, na kwa vile mwangaliaji wa vitabu vyao ni lazima awe mtu mwenye weledi ili kubainisha kilicho sahihi kutoka kisicho sahihi, na athari zilizotajwa katika shaka hazifai kwa hali yoyote kuzitegemea kwani zenyewe ni dhaifu na msingi wake umechukuliwa katika maelezo ya kutengenezwa.
Imamu Ibn Katheer amesema baada ya kutaja mapokezi haya: “Lengo ni kuwa Hadithi hii ina kasoro kwa pande tatu:
Upande wa Kwanza: Umar Ibn Ibrahim – Mpokezi wa Hadithi – ni mtu kutoka Basra na kuthipitishwa hilo na Ibn Muiin, lakini Abu Haatim Ar-Razy amesema sio hoja, lakini imepokelewa na Ibn Mardawy Hadithi kutoka kwa Muutamir kutoka kwa baba yake kutoka kwa Hassan kutoka kwa Samrah ni Hadithi iliyoinuliwa mpaka kwa Mtume. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi.
Upande wa Pili: Ni kuwa imepokelewa kutoka kauli ya Samrah yeye mwenyewe sio Hadithi iliyounganishwa moja kwa moja kwa Mtume kama alivyosema Ibn Jariir, alituambia Ibn Abdil-Aalaa ametuzungumzisha Muutamir kutoka kwa baba yake ametuambia Bakri Ibn Abdillah kutoka kwa Suleiman Taimiy kutoka kwa Abi Al-Alaa Ibn Shakhiir kutoka kwa Samrah Ibn Jandab amesema Adamu mwanawe alimpa jina la Abdul-Harith.
Upande wa Tatu: Hassan mwenyewe amefasiri Aya tofauti na hivi, lau kama hii imetoka kwake akipokea kutoka kwa Samrah kuwa imetoka kwa Mtume basi asingeifanyia marekebisho. Ibn Jariir amesema ametuambia Ibn Wakiii ametuambia Sahli Ibn Yussuf kutoka kwa Amr kutoka kwa Hassan: {Wanamfanyia ushirikina Mwenyezi Mungu katika kile kile alichowapa} Aaraaf: 189, 190.
Na ametuambia Bashar ametuambia Zaid ametuambia Said kutoka kwa Qatadah amesema, Hassan alikuwa anasema, hao ni Mayahudi na Wakristo Mwenyezi Mungu aliwapa watoto alafu wao wakawafanya Wayahudi na Wakristo.
Mapokezi haya ni sahihi kutoka kwa Hassan R.A kuwa amefasiri Aya hivyo nayo ni katika tafasiri nzuri zaidi na mambo bora yaliyobeba Aya, lau Hadithi hii ingekuwa kwao imehifadhiwa kutoka kwa Mtume S.A.W basi asingeifanyia marekebisho yeye wala mtu mwengine na hasa wacha-Mungu wao na watu wema, hii inaonesha kuwa Hadithi hii imesimama kwa mmoja wa Masahaba na inachukuliwa kuwa ameipokea kutoka baadhi ya watu wa kitabu wale walioamini mfano wa Kaab au Wahab Ibn Minmbah na wengine….. Isipokuwa sisi kwa mtazamo wetu ni katika Hadithi iliyopandishwa kwa Mtume S.A.W. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi.
Na kuna mapokezi sahihi kutoka kwa Hassan R.A kuwa amefasiri kauli ya Mola: {Wanamfanyia ushirikina Mwenyezi Mungu katika kile kile alichowapa} Aaraaf: 189, 190.
Kwa kauli yake: “Hii ilikuwa kwa baadhi ya mila na wala haikuwa kwa Adam” nayo ni tafsiri bora inayobeba maana ya Aya, lau ingekuwa Hadithi ni yenye kuunganishwa hadi kwa Mtume S.A.W. kuwa huyo ni Adam na Hawa ikiwa imehifadhiwa kwake ni upokezi kutoka kwa Mtume S.A.W. basi asingeingiza marekebisho yeye wala mtu mwingine hasa wale wacha-Mungu wao na watu wema, na hii inaonesha kuwa yenyewe ni sahihi imesimama kwa Sahaba na wala sio yenye kunyanyuliwa kwa Mtume S.A.W.
Kubatilika mapokezi ambayo yametumiwa na muulizaji kwa upande wa maana:
Maelezo haya – ambayo yametajwa katika tafsiri ya Aya – si sahihi kwa pande mbalimbali:
Upande wa Kwanza: Maana ya kauli yake Mola: {Mwenyezi Mungu ametukuka na huko kushirikisha kwao} ni kuwa hao ambao wamekuja na shirki hii ni kundi.
Upande wa Pili: Kauli ya Mwenyezi Mungu baada ya hapo: {Ati wanawafanya viumbe kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu, nao hawaumbi, bali wao ndio wanaumbwa} nayo inaonesha kuwa makusudio ya Aya: Kumjibu yule anayewafanya masanamu washirika wa Mwenyezi Mungu iblisi aliyelaaniwa wala hajatajwa kwenye Aya hii.
Upande wa Tatu: Lau kusudio lingekuwa ni iblisi basi angesema: Ati wanamshirikisha na asiyeumba Kwa sababu akili inataja kwa muundo wa herufi ya “Man – Nani”.
Upande wa Nne: Ni kuwa Adam A.S. alikuwa ni mtu mwenye uelewa sana kuhusu iblisi na alikuwa ni mwenye uelewa wa majina yote kama Mwenyezi Mungu Alivyosema: {Adam alifundishwa majina yote} hivyo ni lazima atakuwa amelifahamu jina la iblisi ni Harith pamoja na kufahamu uadui wake mkubwa uliopo kati yao na kulifahamu jina la iblisi ni Harith vipi mtoto wake ampe jina la Abdul-Harith? Na vipi abanwe na haya majina ambapo hakupata jina isipokuwa jina hili?
Upande wa Tano: Mmoja wetu akiwa amepata mtoto kisha akaja mtu na kumtaka ampe jina mtoto wake kwa jina hili basi mwenye mtoto atakataa na kupinga vikali sana, Nabii Adamu A.S. pamoja na Utume wake na elimu kubwa ambayo ameipata kwa kauli ya Mola: {Adam alifundishwa majina yote} na majaribio yake mengi ambayo aliyapata kwa sababu ya kuteleza kulikotokana na kutiwa wasi wasi na iblisi ni vipi Nabii Adam A.S. asigundue kiwango hiki cha uovu?
Upande wa Sita: Ikiwa tutakubali kuwa Adam A.S. alimpa jina mwanawe la Harithi, haitokuwa nje ya kutajwa jina hili limefanywa jina maarufu au sifa yake, kwa maana alimpa habari ya jina hili kuwa ni Abdul-Harith, ikiwa ni sababu ya kwanza basi si katika shirki kwa sababu majina maarufu na ya utani hayana faida yoyote kuitwa kwake, hakuna ulazima kwenye kuita majina haya kuwepo ndani yake shirki, ikiwa ni sababu ya pili basi kauli hii inakuwa Nabii Adamu A.S. ameamini kuwa Mwenyezi Mungu ana mshirika katika kuumba, na hilo linapelekea moja kwa moja kukufuru Nabii Adam, hivyo mwenye akili hawezi kusema hilo, imethibiti kauli hii si sahihi( ).
Faida ya kisa ni kupiga mfano:
Kimetajwa kisa hiki kwa ajili ya kutolea mfano tu wa hali ya hawa washirikina kwenye ujinga wao na kauli zao za shirki na kukubali maneno haya kana kwamba Mola Anasema: Yeye ndiye ambaye amemuumba kila mmoja miongoni mwenu kutokana na nafsi moja na akatoa kwenye nafsi hiyo hiyo mke wake ambaye ni mwanadamu aliyesawa na yeye katika ubinadamu, pindi mume alipokutana na mke wake na kupatikana ujauzito mume na mke walimwomba Mola wao ikiwa utatupatia mtoto mwema wa kiume basi tutakuwa ni wenye kukushukuru kwa neema zako, lakini Mwenyezi Mungu alipowapa mtoto mwema wa kiume mume na mke wakamfanyia Mungu mshirika katika kile alichowapa kwa sababu wakati mwingine huyo mtoto wanamhusisha na maumbile kama ilivyo kauli ya watu wa maumbile, na wakati mwingine wanamhusisha na sayari kama ilivyo kauli ya watu wa nyota, na wakati mwingine wanamhusisha na masanamu kama ilivyo kauli ya waabudu masanamu( ).
 

Share this:

Related Fatwas