Mbalamwezi ni Kama Karara Kongwe

Egypt's Dar Al-Ifta

Mbalamwezi ni Kama Karara Kongwe

Question

 Mbalamwezi ni Kama Karara Kongwe 

Answer

 Matni yenye Shaka:
Ndani ya Qur`ani Tukufu imekuja kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe * Haliwi jua ni lenye kuufikia mwezi, wala usiku ni wenye kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao} [YASIN: 39, 40].
Imekuja kwenye tafasiri ya Imamu Baidhawy: “Pindi mwezi unapokuwa kwenye kituo chake cha mwisho” nao unakuwa hivyo kabla ya kufika na kufanya upinde {Mpaka unakuwa kama karara kongwe} ukweli wa wasifu huu upoje “Mwezi kuwa kama karara kongwe”
Jibu Fupi:
Hii ni alama katika alama za Mwenyezi Mungu ambayo ipo wazi kwa waja wake ni dalili ya uwezo wake, nayo ni dalili ya usahihi wa Vitabu na kutuma Mitume pamoja na ukweli wa imani ya siku ya mwisho, ambapo yenyewe ni alama iliyowazi kila mwanadamu anaona na wala hawezi kupinga.
Maana ya Aya ni kuwa mbalamwezi Mwenyezi Mungu ameitengenezea vituo na hali tofauti, una malizikia kwa kuwa kama karara kongwe, kufananisha ni katika sifa tatu: Ulaini kujikunja na unjano, kwa sifa hii ambayo watu wa Makka wanaijua na wengine miongoni mwa Waarabu na ambayo inakubaliana na viwango vya watu wote anaoambiwa.
Jua linazunguka na mbalamwezi pia inazunguka wala haifai mwezi kukutana na jua katika mzunguko wake wala usiku kuutangulia mchana bali hufuata( ).
Jibu la Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza: Ufananishaji huu mkubwa unakubaliana na viwango vya watu wote wanaoambiwa na Qur`ani Tukufu kipindi chote kutokana na mfungamano wake na jambo la kihisia linaloonekana na wote.
Pili: Katika Aya hii kuna muujiza wa kinafsi nao ni kuambiwa Waarabu kile wanachokifahamu, kwani unaposikia kwa watu wa lugha nyingine wakizungumza na kusikika kwenye lugha yao neno litokanalo na lugha yako au wakiwa wanazungumza kwa lahaja isiyokuwa lahaja yako na kusikika kwenye lugha yao neno lenye asili ya lahaja yako basi neno hili kwako litaleta uelewa na furaha ya moyo wako, na kutokana na hilo yamekuja matumizi ya maneno mengi yanayotangatanga katika mazingira ya Waarabu, mfano wa neno Qatmir kwa maana ya kokwa ya tende, na neno Fateel ni nyuzi ya kwenye kokwa ya tende( ), na hapa Mwenyezi Mungu amesema ni kama karara kongwe.
Maneno haya ambayo yanakubaliana ya mazingira ya Kiarabu na si mazingira mengine msomaji na msikilizaji atahisi uelewa wa Qur`ani Tukufu na kisha nafsi yake haimiliki isipokuwa ni kukubali kwa shukrani na kutakasika kwa Mteremshaji wa Qur`ani.
Kwa nini mbalamwezi umeelezewa kwa mfano wa karara kongwe
Kusudio la Aya Tukufu la kuielezea mbalamwezi kwa sifa hii iliyokaribu na akili za Waarabu ili iwe kielelezo kikubwa cha hali hii kwa mtazamo wa Waarabu wa hii hali, kana kwamba Mwenyezi Mungu ametaka kuwaonesho sura hii ya hali ya mbalamwezi katika mwonekano wake unaoonekana kila siku, na mfumo huu unafahamika na kutambulika kwa Waarabu, kisha zimekuja Aya nyingi kwenye hilo Mwenyezi Mungu Amesema: {Jee huwaoni wale wanao dai kuwa ati wametakasika! Bali Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye. Na hawatadhulumiwa hata kwa kiwango kidogo cha kijiuzi kilichomo ndani ya uwazi wa kokwa ya tende} [AN-NISAA: 49]. Neno Fateela ni nyuzi ndani ya tunda ya tenda, imekuwa ni kawaida kutumia neno hili kwa Waarabu kuashiria udogo au kitu kidogo sana ambapo chenyewe hakinufaishi wala kuonekana kwa wazi( ).
Hali za Mbalamwezi:
Mwezi huanza kuzaliwa kwa hatua ya kuwa upinde mwembamba, kisha unakua kidogokidogo mpaka unakuwa duara kamili la mwezi, kisha unaanza kupungua kiwango mpaka unakuwa kama karara kongwe la mtende au mnazi, kisha unajificha kwa maana ya kutoonekana kwa muda wa siku moja au mbili, na hujirudia huu mzunguko kila mwezi muandamo mpaka mwisho wa dunia.
Katika muujiza huu wa Qur`ani ambao hauwezi kabisa kuisha huongezeka sifa ya hatua ya mwisho katika hatua za mzunguko wa mwezi wa mbalamwezi na kuwa kama karara kongwe, nalo ni kole la tende mbichi pindi linapokauka na kuinama, rangi yake inakuwa ya njano nalo wakati wa kukauka kwake juu ya mtende huinama kuelekea mti wa mtende, vilevile mbalamwezi ya siku ya pili huinamia pande zake kuelekea ardhini, wakati ambapo mbalamwezi inaozaliwa huinamia pande zake na ardhi ... uzuri ulioje wa ufananishaji huu wa Qur`ani.
Haya ndiyo matukio ya mbalamwezi hayakufahamika na elimu ya kusoma isipokuwa baada ya juhudi kubwa zilizochukua maelfu ya wanachuoni kwa karne nyingi, na kuelezea kwenye Aya moja ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho amekiteremsha kwa Mtume wake S.A.W. na kwa Umma ambao watu wake wengi walikuwa ni wasiojua kusoma wala kuandika, kiasi cha miaka elfu moja na mia nne kipindi ambacho kimeonesha kuwa Qur`ani Tukufu ni maneno ya Mwenyezi Mungu Muumba ambaye amekiteremsha kwa elimu yake kwa Mtume wake wa mwisho, na ameahidi kukilinda na amekilinda kwa lugha yake ile ile iliyoteremkia, amekilinda kikamilifu herufi kwa herufi neno kwa neno Aya kwa Aya Sura kwa Sura, kama vile kilivyopangiliwa kwenye kopi nyingi zilizochapishwa na kurekodiwa kwenye mikanda ya sumaku na vyombo vyengine miongoni mwa vyombo vya kurikodi, na ikinukuliwa na wengi ndani ya kipindi cha miaka elfu moja na mia nne, ikiwa imehifadhiwa kwenye vifua vya mamilioni ya watu kwa utaratibu ule ule wa Msahafu Mtakatifu, imeendelea kuhifadhiwa kwa utukufu wa Mungu ambao unaonekana kati ya Aya zake na kwa kuchomoza kwake nuru, na kusema ukweli katika kila kadhia miongoni mwa kadhia zake, shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu kwa neema hii ya Uislamu, shukrani anastahiki Mwenyezi Mungu kwa neema ya Qur`ani. Sala na salamu zimuendee Nabii wa mwisho na Mtume wa mwisho, na kwa Watu wake na Masahaba zake, na kwa kila mwenye kufuata uongofu wake na kulingania kwa ulinganiaji wake mpaka Siku ya Mwisho, na mwisho wa maombi yetu tunasema shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote.
Mbalamwezi ndani ya Qur`ani:
Utajo wa mbalamwezi ndani ya Qur`ani Tukufu umekuja mara ishirini na saba, kama ilivyokuja ishara ya hatua zake mbalimbali chini ya jina la Ahillah mara moja, na inafanya jumla ni mara ishirini na nane nayo ndiyo masiku ya mbalamwezi ndani ya kila mwezi, na ndiyo idadi ya vituo vyake vya kila siku, wala haiwezekani kukubaliana huku kwa undani zaidi kukaja kwa bahati tu kwa sababu mfano wa maelezo haya ndani ya Qur`ani Tukufu ni mengi zaidi yasiyohesabika, na yenyewe lau yatatumika kwa takwimu ya kina basi yatakuwa wazi zaidi kwa upande wa miujiza ya kielimu na kisayansi ndani ya Qur`ani Tukufu.

 

Share this:

Related Fatwas