Maneno Yasiyopangika

Egypt's Dar Al-Ifta

Maneno Yasiyopangika

Question

Aya ya Qur'ani:

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na Qur'ani tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kidogo kidogo} ([1]).

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema tena:

{Na wakasema walio kufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur'ani kwa jumla moja? Hilo ili tuuthibitishe moyo wako, na ndio tumeisoma kwa mafungu} ([2]).

Anasema nini mwenye madai?

 

[1] Israa: 106.

[2] Furqan: 32.

Answer

Imamu Baidhawy amesema: Na Qur'ani tumeitenganisha kwa maana tumeiteremsha kidogo kidogo kwa muda wa miaka ishirini, lengo upate kuwasomea watu kwa vituo utulivu na ufanisi, kwani yenyewe ni nyepesi kuhifadhi na kusaidia zaidi kwenye kufahamu….tumeiteremsha kwa mafungu kutokana na matukio.

Imamu Baidhawy amesema: Na wakasema wale waliokufuru kwa nini haikuteremshwa Qur'ani mara moja, kwa maana imeteremshwa kwake kama habari.

Neno: Kuteremshwa mara moja, kwa maana ya fungu moja kama vile vitabu vitabu, huo ni upinzani usio na maana kwa sababu muujiza hauna tofauti kuteremka kwake mara moja au kwa nyakati tofauti, pamoja na kwamba kushuka kwa nyakati tofauti kuna faida nyingi miongoni mwazo ni kama iliyoashiriwa na kauli ya Mwenyezi Mungu: Kufanya hivyo ili tukithibitishe kifua chako, kwa maana tumeiteremsha ndani ya nyakati tofauti ili kukipa nguvu kifua chako kwenye kuihifadhi, ambapo Mtume S.A.W alikuwa si mwenye kujua kusoma wala kuandika na walikuwa wanaandika, hivyo lau angeshushiwa Qur'ani yote mara moja basi ingekuwa ngumu kuhifadhi na kutotulia, na ikiwa atapokea basi haiji isipokuwa kidogo kidogo, na kwa sababu kuteremka kwake ni kutokana na matukio kunahitaji muono zaidi na kuzamia kwenye maana, na kwa vile pindi inapoteremka kidogo kidogo hupelekea kushinda wasomi hivyo wanashindwa kuipinga na hilo hupelekea nguvu na kuimarika moyo wake, na kwa vile pindi Malaika Jibril anapoiteremsha wakati baada ya wakati moyo wake huthibiti, na kutokana na ushukaji wa muundo huo hufahamika Aya iliyofutwa na iliyofuta pamoja na sifa ya chanzo cha Aya iliyofutwa, na ishara ya kuteremshwa kidogo kidogo ina dalili kauli yake: Kwa nini Qur'ani haikuteremshwa mara moja, na huenda ikawa ni ukamilifu wa maneno ya makafiri kwa sababu hiyo wamesimamia hapo ili kuwa hali ya ishara ya Vitabu vilivyotangulia.

Sisi tunauliza: Ni namna gani Qur'ani inakuwa ni Ufunuo au Wahyi nayo ni yenye kukatika na kutengana, baadhi ya Aya zake zinakuja wakati fulani na zingine zinachelewa na kuja wakati mwingine? Muhammad alikuwa anaipangilia pindi Waarabu au Wayahudi au Wakristo walipokuwa wanamuuliza, na wakati mwingine alikuwa analalamika kuwa Jibril amechelewa kwa sababu ya kuwepo maneno ([1])

Yatokanayo na Shaka:

  1. Kuteremka kidogo kidogo kunapingana na muujiza hivyo basi vipi Kitabu hiki kinakuwa Ufunuo?
  2. Mtume wa Uislamu alikuwa anapangilia Qur'ani pindi anapoulizwa na Waarabu Wayahudi na Wakristo, wakati mwingine alikuwa analalamika kuwa Mtume wa Ufunuo “Jibril” amechelewa kuja na Ufunuo kwa sababu ya maneno.

 

Kuondoa Shaka:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Kwanza: Shaka hii iliyotajwa na washirikina tokea kuteremka kwa Qur'ani Tukufu Mwenyezi Mungu Mtukufu amesimamia majibu ndani ya Kitabu chake Kitukufu akathibitisha shaka ya washirikina na makafiri wapingaji wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, vile vile alithibitisha majibu ya shaka hii na hekima ya kuteremshwa Qur'ani Tukufu kidogo kidogo lakini muulizaji yote haya hajafahamu au ubishi ambao wako nao washirikina na makafiri ni sawa kati ya muulizaji na hawa watu, pindi akili zao na nyoyo zao zilipofanana katika kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi kauli zao na sifa zao vimefanana:

{Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia} ([2]).

Hapa muulizaji pia amenukuu Aya katika tafsiri ya Imam Baidhawy Mungu amrehemu inabainisha ndani yake hekima ya kuteremshwa Qur'ani Tukufu kidogo kidogo na faida zake na kuelezea upuuzi wa kauli ya mwenye kusema:

{Kwa nini hakuteremshiwa Qur'ani yote mara moja?}

Muulizaji amenukuu nukuu hii ambayo inaleta jibu la analouliza na wala hajaweza kufahamu kile kilichonukuliwa au inasemwa kuwa ubishi wake kwenye haki na ukweli umemzunguka kati yake na ufahamu wa anachonukuu.

Pili: Nani anayeleta habari kuhusu mambo ya Mungu:

Je Mwenyezi Mungu anashindwa kuteremsha Kitabu kidogo kidogo katika vifungu vyenye kuungana katika maana yake? Kauli hii ameitoa wapi? Je Mwenyezi Mungu amemteremshia Ufunuo akamuambia kuwa: Kila Ufunuo utokao kwangu kuteremka kwake kunakuwa ni mara moja, na kila Ufunuo unaokuwa kinyume ya utaratibu huo hauwi Ufunuo? {Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli} ([3]).

Tatu: Qur'ani Tukufu ambayo imeteremshwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu yenyewe inatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa utaratibu huu tokea ilipoumbwa mbingu na ardhi ikiwa imepangiliwa kwenye muundo wa Sura na Aya kwenye “Lauhil-Mahfuudh” Ubao uliyohifadhiwa.

Nne: Ni kipi kipimo cha maneno kuelezwa kuwa hayajapangika?

Meneno yasiyopangika kwa watu wenye akili ni maneno ambayo hayakubaliani yenyewe kwa yenyewe, si kwa upande wa maneno yake moja moja mpangilio na wala si kwa upande wa maana na makusudio, kipimo hiki ndicho kipimo jumla hakina tofauti kati ya maneno na maneno mengine ([4]).

Kukatika kwa muundo na kuungana kwake hakuna uhusiano mkubwa wa kuungana maneno wala kutengana kwake kwani baadhi ya watu hutunga kitabu kwa muda mrefu wala hilo haliwi sababu ya kutopangika kitabu chake, vile vile mtu anaweza kutunga kitabu akachukuwa mwaka mmoja na bila ya kuwa na athari yeyote katika muunganiko wa kitabu chake, kwa ujumla ni kuwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu “Qur'ani Tukufu” si katika utunzi wa mwanidamu mpaka aweze kuijadili kwa kanunu hizi hali ya kuwa kimeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu: {Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hekima Msifiwa} ([5]).

{Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye kujua} ([6]).

Qur'ani ambayo imeteremshwa kidogo kidogo ndani ya kipindi cha miaka ishirini na mitatu, haina mfano wake wala ukaribu katika mfumo wake wa hukumu na utunzi wa muundo wake na usahihi wa maana zake na ubora wa ibara zake, pia usalama wa lugha yake iliyoepukana na kila aina za kasoro au upungufu.

Kitabu kimeishi miaka mingi ni karibu ya miaka elfu na mia tano, pamoja na hayo ni kitabu cha zama zote kina maneno mazuri kutokea kusemwa baada yake au kabla yake au katika zama za kuteremshwa kwake, na maana zake zinazovumbuliwa na watu ndani ya zama zote zilizopita kwenye maeneo ya kimaarifa ni yenye kushangaza, na inatosha ubora uliotanguliwa na staarabu za sasa katika maeneo mbalimbali ya maarifa ya anga na ardhi na kati ya mbingu na ardhi na yaliyomo kwenye vina vya mito bahari na bahari kubwa, na yaliyomo ndani ya vina vya ardhi.

Yote haya ni utekelezaji wa ahadi ya Mwenyezi Mungu ambayo imepokelewa ndani ya Qur'ani:  {Tutawaonesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli} ([7]).

Qur'ani ambayo wanaizushia ni Kitabu cha uwepo wa vyote, wangapi miongoni mwa wenye chuki walijaribu kabla yenu pamoja na nyinyi kuleta ufa wakapofuka macho yao, na neno la Mwenyezi Mungu likabakia kuwa juu likiogelea katika anga likivuka vikwazo vya zama mbalimbali, nayo ni mnara mwangaza wake unawake na kufuta giza: 

{Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu ambaye amemteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kina upogo * Kimenyooka sawa, ili kitoe onyo kali kutoka kwake, na kiwabashirie Waumini watendao mema kwamba watapata ujira mzuri * Wakae humo milele * Na kiwaonye wanao nena Mwenyezi Mungu ana mwana * Wao hawana ujuzi wa jambo hili, wala baba zao. Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu} ([8]).

Ama yanayohusu kuchanganyikiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu wakati wa kuulizwa na Wayahudi Wakristo na Waarabu, maelezo haya ni kumtengenezea uwongo Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na muulizaji hakutaja dalili yeyote inayotuondeshea taarifa ya makosa yake isipokuwa sisi tunaeleza ukweli ili kuonesha batili. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema:

{Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na  mara ukatoweka. Na ole wenu kwa mnayo yazua} ([9]).

Ni vipi mja anayeungwa mkono na Mwenyezi Mungu Mtukufu akaogopa waja wa Mwenyezi Mungu na Aya nyingi za Qur'ani Tukufu zinabainisha kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameteremsha kwa Mtume wake S.A.W Aya nyingi zikiwa ni jibu la maswali yaliyoelekezwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mola Mtukufu Amesema:                                                    

{Na wanakuuliza habari za Dhul-Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake} ([10]).

Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema tena:

{Na wanakuuliza habari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo tu} ([11]).

Na Mwenyezi Mungu Akasema:

{Watu wanakuuliza habari ya Kiyama. Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu. Na nini kitakujuvya? Pengine hiyo Saa iko karibu} ([12]).

Mola Mtukufu Akasema tena:

{Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha mtaka Musa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuoneshe Mwenyezi Mungu wazi wazi. Wakapigwa na radi kwa hiyo dhuluma yao. Kisha wakamchukua ndama kumuabudu, baada ya kwisha wajia hoja zilizo wazi. Nasi tukasamehe hayo, na tukampa Musa nguvu zilizo wazi} ([13]).

Bali wakati mwengine Mwenyezi Mungu Mtukufu alikuwa anateremsha kwa Mtume wake S.A.W majibu ya maswali kabla washirikina makafiri na wengine hawajauliza:

{Wapumbavu miongoni mwa watu watasema: Nini kilicho wageuza kutoka Kibla chao walicho kuwa wakikielekea? Sema: Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu; Yeye humuongoa amtakaye kwenye njia iliyo nyooka} ([14]).

Pia akasema:

{Watakuambia mabedui walio baki nyuma: zimetushughulisha mali zetu na watu wetu, basi tuombee msamaha. Wanasema kwa ndimi zao yasiyo kuwamo katika nyoyo zao. Sema: Ni nani awezaye kukusaidieni chochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka Yeye kukudhuruni au akitaka kukunufaisheni? Bali Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayo yatenda} ([15]).

Kauli nyingine ya Mola Mtukufu:

{Walio baki nyuma watasema: Mtapo kwenda kuchukua ngawira, tuacheni tukufuateni! Wanataka kuyabadili maneno ya Mwenyezi Mungu. Sema: Hamtatufuata kabisa. Mwenyezi Mungu alikwisha sema kama hivi zamani. Hapo watasema: Bali nyinyi mnatuhusudu siyo, bali walikuwa hawafahamu ila kidogo} ([16]).  Na Aya nyengine nyingi za Qur'ani, na hii ni katika hekima ya kuteremshwa Qur'ani Tukufu kidogo kidogo kutokana na matukio, na zingine ni kutokana na maswali ya waulizaji miongoni mwa Wayahudi Wakristo na washirikina Waarabu.

 

 

[1] Ukurasa wa 195 – 205 ndani ya kitabu cha je Quran imezuiliwa kuwa na makosa?

[2] Al-Swaff: 08.

[3] Al-Baqarah: 111.

[4] Kitabu ha Haqaaiq Al-Islaam ukurasa 74.

[5] Fussilat: 42.

[6] Ghaafir: 02.

[7] Fussilat: 53.

[8] Kitabu cha Haqaiq Al-Islaam ukurasa wa 53, na Aya za Suratul-Kahfi: 1 – 5.

[9] Al-Anbiyaa: 18.

[10] Al-Kahfi: 83.

[11] Al-Israa: 85.

[12] Al-Ahzaab: 63.

[13] An-Nisaa: 153.

[14] Al-Baqarah: 142.

[15] Al-Fath: 11.

[16] Al-Fath: 15.:

Share this:

Related Fatwas