Utume Kuhusika kwa Wana wa Israeli ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Utume Kuhusika kwa Wana wa Israeli

Question

Aya yenye shaka:

Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu imekuja ndani ya Qur'ani:

{Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote}([1]).

 

[1] Al-Jaathiyah: 16.

Answer

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena:

{Na tulimtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaqub. Na tukajaalia katika kizazi chake Unabii na Kitabu, na tukampa malipo yake katika dunia; naye Akhera bila ya shaka ni katika watu wema} ([1]).

Haya ni maelezo kutoka ndani ya Qur'ani kuwa Utume umehusishwa kwa wana wa Israil bila ya wengine, na haya yanakubaliana na mtazamo wa Torati ambayo imewatahadharisha wana wa Israel kumkubali yeyote mwenye kudai kuwa ni Nabii kutoka kizazi cha Ismail, ikiwa Utume umehusika kwa wana wa Israil kwa mujibu wa ushahidi wa Torati Injili na Qur'ani basi vipi Nabii wa Uislamu anakuwa Nabii hali ya kuwa si katika kizazi cha Yakubu? Na vipi Qur'ani inasema:

{Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii} ([2]).

Na Ismail hakuwa kabisa katika kizazi cha wana wa Israil mpaka awe na Utume.

Qur'ani imeelezea ubora wa wana wa Israil kwa walimwengu wote:

{Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni zile neema zangu nilizo kuneemesheni, na nikakuteuweni kuliko wote wengineo} ([3]).

Na imetaja mara kwa mara kuwa Isaka mtoto wa pili wa Ibrahimu na Yakubu ni mjukuu wake hao wawili ni zawadi ya Mwenyezi Mungu kwa Ibrahimu bila ya kumtaja Ismail pamoja na kuwa ni mtoto wa kwanza wa Ibrahimu.

Jibu la Shaka:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Aya zilizotajwa hakuna inayokubaliana na madai:

Aya hizi zilizotajwa hazioneshi – kwa ukaribu wala kwa umbali – kupinga watoto wa Ismail Amani ya Mungu iwe kwake wala kukana Utume kwa mbora wa viumbe S.A.W

Kwani kauli ya Mola Mtukufu:  {Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote}([4]).

Inaelezea ukubwa wa neema zake Mola Mtukufu kwa waja miongoni mwa waja wake – Nao ni wana wa Israil – ambapo amewapa Kitabu hukumu Utume na kuwaruzuku vilivyovizuri na kuwafanya bora zaidi ya walimwengu wote wa zama zao, kisha wana hawa wa Israil hawakuwa wenye kushukuru neema ya Mwenyezi Mungu, na Aya hii Tukufu haina kabisa kinachoelezea kuhusika Utume kwa wana wa Israil tu kama anavyodai muulizaji, bali Aya ambayo inayofuata inaashiria tofauti zao katika jambo la dini na hukumu ya hilo siku ya Kiyama itarejea kwa Mwenyezi Mungu kwani Mola wako atawahesabu bila ya dhuluma kwa yeyote. Mola Mtukufu Amesema:

{Na tukawapa maelezo wazi ya amri. Basi hawakutafautiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa ajili ya uhasidi uliyo kuwa kati yao. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu kati yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyokuwa wakitafautiana}([5]).

Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema baada ya Aya iliyopita:

{Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu * Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika wenye kudhulumu ni marafiki wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni rafiki wa wamchao} ([6]).

Kwa maana ni juu yako ewe Mtume kulazimika na Ufunuo wa Mwenyezi Mungu kwako katika mambo ya Sharia na haki pasi ya kuwageukia wale wasiojua kitu.

Ama Aya ya pili nayo ni kauli yake Mola Mtukufu:

{Na tulimtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaqub. Na tukajaalia katika kizazi chake Unabii na Kitabu, na tukampa malipo yake katika dunia; naye Akhera bila ya shaka ni katika watu wema} ([7]).

Yenyewe inaonesha kuwa hakuna kizuizi cha kutokea Utume kwa ujumla katika kizazi cha Ibrahimu – Na Ismail miongoni mwao – kwa sababu Aya baada ya kuzungumzia zawadi ya Mwenyezi Mungu – Mtukufu – kwa Ibrahimu Amani ya Mungu iwe kwake kwa kumpa Isaka na Yakubu Utume na Kitabu vimekuwa kwa kizazi cha Ibrahimu moja kwa moja, ni sawa sawa katika hilo kizazi chake katika watoto wa Isaka au kizazi cha watoto wa Ismail.

Ismail Amani ya Mungu iwe kwake ndani ya Qur'ani Tukufu:

Maelezo ya utangulizi kuhusu Ismail Amani ya Mungu iwe kwake na kutambulika Utume wake ni maelezo ya Qur'ani kwenye Aya nyingi. Mwenyezi Mungu Anasema:

{Na tukamtunukia (Ibrahim) Isaka na Yakubu. Kila mmoja wao tulimuongoa. Na Nuhu tulimuongoa kabla. Na katika kizazi chake tuliwaongoa Daud na Suleiman na Ayub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema * Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyas. Wote walikuwa miongoni mwa watu wema * Na Ismail, na Al-Yasaa, na Yunus, na Luut. Na wote tuliwafadhilisha zaidi ya walimwengu wote} ([8]). Kisha Mola Mtukufu Akasema baada ya hayo:   {Hao ndio tulio wapa Vitabu na hukumu na Unabii. Ikiwa hawa watayakataa hayo, basi tumekwisha yawakilisha kwa watu wasio yakataa} ([9]). Na Mwenyezi Mungu Akaendelea kusema:

{Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema * Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote * Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yakubu: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu * Je! Mlikuwepo yalipo mfikia Yakubu mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Isaka, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake} ([10]).

Uwongo wa shaka dhidi ya Torati na Injili:

Ndani ya Kitabu Kitakatifu hakuna dalili hata moja ya kuhusishwa wana wa Israil peke yao na Utume wala pingamizi la Utume kwa watoto maalumu wa Ismail.

Yanayodaiwa katika shaka kuwa Torati na Injili zimetaja kuhusisha Utume kwa wana wa Israil tu, na kuwa Torati imetahadharisha kukubaliwa mtu yeyote mwenye kudai Utume kutoka kizazi cha Ismail, ni madai yasiyo na maana yeyote wala hayana dalili, na wala hakuna ndani ya Torati au Injili yanayoelezea hivyo.

Ni kwanini utenganisho huu kati ya kizazi cha Isaka na Ismail? Je kuna jinai yeyote Ismail ameifanya anastahiki adhabu Yeye peke yake bali na kizazi chake nyuma yake? Uadilifu wa Mungu upo wapi kuwajumuisha watoto kwenye jinai – Ikiwa tutakiri kuwa Ismail amefanya makosa pamoja na kuwa hajafanya hayo makosa – hali ya kuwa hawahusiki? Au ni muendelezo wa msingi wa kurithi makosa ambayo haikubali akili yenye yakini uadilifu na huruma ya Mungu, kuongezea pia hata kukubalika na dini za mbinguni, kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu Anajua zaidi pale anapoweka Ujumbe wake, ikiwa atateua – Naye ndio mteuzi – kwishilizia Utume kwa kizazi kinachotokana na Ismail Amani ya Mungu iwe kwake basi hakuna kinachozuia uteuzi wake na matakwa yake.

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: 

{Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri - yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao!} ([11]).

Akaendelea tena kusema:  {Na alipo wajia Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mwenye kuthibitisha yale waliyo nayo, kundi moja miongoni mwa wale walio pewa Kitabu lilitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui} ([12]). Kusudio la kupendelewa wana wa Israil zaidi kulito watu wengine:

Ama kupendelewa kwa wana wa Israil kuliko watu wengine hilo ni kwa vile Mwenyezi Mungu amewapa asichowapa wengine miongoni mwa kupasuka bahari kufunikwa na kiwingu na mengine yasiyokuwa hayo, na ikasemwa kuwa kusudio la walimwengu: Ni wasomi wa zama zao ([13]).

 

[1] Al-Ankabuut: 27.

[2] Mariam: 54.

[3] Al-Baqarah: 47.

[4] Al-Jaathiyah: 16.

[5] Al-Jaathiyah: 17.

[6] Al-Jaathiyah: 18, 19.

[7] Al-Ankabuut: 27.

[8] Al-Anaam: 84 – 86.

[9] Al-Anaam: 89.

[10] Al-Baqarah: 130 – 133.

[11] Al-Baqarah: 89.

[12] Al-Baqarah: 101.

[13] Tafsiri ya Imamu Aluusy 25/148.

Share this:

Related Fatwas