Msimamo wa wema waliotangulia juu y...

Egypt's Dar Al-Ifta

Msimamo wa wema waliotangulia juu ya Khawariji

Question

Ni upi Msimamo wa wema waliotangulia kwa Khawarij?

Answer

Wema waliotangulia wakiongozwa na Masahaba wa Mtume S.A.W. waliamiliana na Khawariji kwa maamuzi thabiti. Tangu kudhihiri kwao rasmi na kuleta athari kama kundi la Kiislamu zama za Imamu Ally bin Abi Talib Allah Amwie radhi, mwanazoni wetu bwana wetu Abdillah bin Abbas ili kuwabainishia upotevu wao na kujibu tatizo lao la kifikra ambalo limewafikisha walipofikia, theluthi yao wakatoka katika fikra hii isiyo ya kawaida, waliobaki wakang’ang’ania msimamo wao, Imamu Ally akawapiga vita kwa sifa yake kama kiongozi wa kisharia na kiongozi wa Umma wa Kiislamu kipindi hicho, na kwa kufanyia kazi wasia Mtume S.A.W. aliposema: “Wao ni viumbe washari, anastahiki pepo mwenye kuwaua na kuuwawa nao, wanalingania katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na hawalewi chochote, mwenye kupigana nao atakuwa bora kwa Mwenyezi Mungu kuliko wao….” [ ameipokea Abou Dawoud], pamoja na hivyo halikupokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. au kutoka kwa Masahaba tamko la wazi linalojulisha ukafiri wao na kutoka katika Dini ya Uislamu.

Share this:

Related Fatwas