Kundi la Muslim Brotherhood (Ikhwan Muslimin) ni la kigaidi au Kundi la Khawariji wa sasa
Question
Je! Kundi la Muslim Brotherhood (Ikhwaan Muslimin) ni la kigaidi au Kundi la Khawariji wa sasa?
Answer
Kwa upande wa kifikra, inazingatiwa fikra za mwasisi wake Hassan Al-Banna, na tungo za muweka mitazamo Sayid Qutb imechukuliwa kutoka kwa Banna na imeungwa mkono na mitazamo ya makundi ya kigaidi ya mashariki na magharibi, hasa vitabu viwili vya (Maalim Fi Al-Tariq) na (Fidhilal Al-Qur’án). Hassna Al-Banna na Sayyid Qutb ni mababa wa kiroho wa makundi haya katika historia mpya.
Ama kwa upande wa kihistoria matendo ya kijanai ya kundi la Muslim brotherhood (Ikhawan Musilimin) ndio matukio ya kwanza ya kijinai ya kigaidi katika Historia mpya; miaka ya arubaini ya karne iliyopita wamewaua Mawaziri Wakuu wawili na mshauri wa Mahakama! Na miaka hamsini walijaribu kumuua Rais wa nchi hayati Jamal Abdunnasir walikaribia kufaulu katika hilo, na wanahusika kwa karibu na kifo cha hayati Rais Mohammad Anwar Sadat.
Na ikumbukwe kwamba waasisi kadhaa wa makundi ya kigaidi na wafuasi wake, walikuwa na mahusiano makubwa na kundi la Muslim brotherhood (Ikhawan Musilimin), kwa mfano: Shukri Mustafa, mwasisi wa (Ukufurishaji na Uhamaji) alikuwa mkwe wa mmoja wa wafuasi wa Muslim brotherhood (Ikhawan Musilimin), na alikamatwa mwaka 1965 A.D pamoja na wafuasi wa kundi hilo kabla ya kuanzisha kundi lake binafsi.