Kudhoofisha mamlaka ya kiongozi wa ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kudhoofisha mamlaka ya kiongozi wa kundi la kigaidi la Daishi

Question

Je, ni mambo gani yanayodhoofisha mamlaka ya kiongozi wa kundi la kigaidi la Daishi?

Answer

Kiongozi mhalifu wa kundi la kigaidi la Daishi – aliyejisindika kwa jina la dini - si halali kwa yeye kuwa na mamlaka yoyote, bali si sahihi yeye kuwa Imamu mwenye kutambuliwa.

Na hiyo ni kwa sababu hakuna shaka kuwa kilichojengwa juu ya ujinga hakiwezi kuwa sahihi, na kinachukuliwa kuwa ni batili na kinabomolewa msingi wake, basi kuna jambo gani ikiwa hali hii ni kwa kiongozi wa kikundi kinachodai kufanikiwa ukhalifa wa Kiislamu, lakini hadhi yake na utambulisho wake haujulikani na wasifu wake haujulikani mpaka achaguliwe kwa mujibu wake!

Ukhalifa  kwa namna hii si sahihi katika tukio la kupewa cheo hiki. Anakaribia kuwa kiongozi wa kundi la siri, la kigaidi, la kihalifu ambalo halina uhusiano wowote na Sharia ya Uislamu, kwa karibu au mbali. Bali, Uislamu hauna uhusiano naye.

Kuasisi Ukhalifa wa Kiislamu kuna masharti ambayo ni lazima yatimizwe mpaka iwe Sharia ni yenye kutekelewa, na miongoni mwa masharti muhimu zaidi ni kwamba msingi wake unatokana na elimu kamili kwa anayepewa dhamana ya kuuwakilisha ukhalifa huu ambao ni ukhalifa unaowajibika mbele ya Mwenyezi Mungu na watu.

Wanachuoni wa Fiqhi waliweka masharti kuwa Khalifa ni  lazima awe muadilifu katika Historia ya maisha yake, na awe na uwezo wa kufahamu masuala ya kisharia na kifiqhi, na awe salama kimwili, na masharti yote hayo hayajulikani kwa kiongozi wa Daish.

Share this:

Related Fatwas